‼️DEREVA WA MHE. HECHE AKUTWA AMEKUFA DAMU DAMU ZIMETAPAKAA SAKAFUNI.‼️
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinasikitika kuwatangazia kifo Suez Dani Maradufu ambaye ni dereva wa Makamu wa Mwenyekiti Bara, Mheshimiwa John Heche
Suez amekutwa amefariki leo asubuhi Jumatano, Julai 01, 2026 chumbani kwenye nyumba ya wageni aliyofikia, mjini Kigoma.
Mwili umechukuliwa na Polisi kuupeleka hospitali ya mkoa wa Kigoma kwa ajili ya taratibu nyingine za uchunguzi.
Chama kinatoa pole kwa familia ya marehemu, wanachama, ndugu jamaa na marafiki kwenye msiba huu mzito.
Taarifa zaidi tutaendelea kuzitoa.
Bwana alitoa. Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina
#TANZANIA: LISSU KUWAKAANGA KAMISHINA WA MAGEREZA NA MKUU WA GEREZA LA UKONGA
Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Taifa, Tundu Lissu atawahoji kwa maswali ya dodoso Kamishina Mkuu wa Magereza pamoja na Mkuu wa Gereza la Ukonga kuanzia leo Julai Mosi hadi Julai 03, 2026 katika Shauri la Kikatiba Na. 7300 la Mwaka 2026 mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu Dodoma. Shauri hilo lilifunguliwa na Mawakili Paul Kisabo, Kulwa Maduhu na Nashon Nkungu dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamishna Mkuu wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ukonga.
Katika shauri hilo, Mahakama inaombwa kuamua kuhusu masuala mbalimbali ya kikatiba yanayohusu vikwazo vya Jeshi la Magereza dhidi ya Tundu Lissu, mawakili wake, ndugu, viongozi na wanachama wanaomtembelea gerezani.
Kulingana na Wakili Paul Kisabo miongoni mwa masuala yanayolalamikiwa ni pamoja na kuzuiwa kwa viongozi na wanachama kumuona Lissu gerezani, pamoja na vitendo vya askari wa magereza vya kusikiliza mazungumzo kati ya Lissu na mawakili wake wanapofanya mashauriano ya kisheria jambo ambalo linakiuka haki ya faragha na haki ya mawakili kufanya kazi yao kwa mujibu wa Katiba na Sheria.
Katika shauri hilo, Mhe. Tundu Lissu ni miongoni mwa wajibu maombi (Respondents, huku Chama cha Wanasheria Tanganyika kitashiriki kama mdau mwenye maslahi katika shauri (Interested Party) baada ya Mahakama kukubali maombi yake.
Aidha, kutokana na uzoefu wao wa kukumbana na changamoto hizo wanapomtembelea Mhe. Lissu gerezani kwa ajili ya mashauriano ya kisheria, Lissu anatarajiwa pia kuwahoji mawakili waliofungua shauri hilo ili waweze kuieleza Mahakama kuhusu mazingira halisi wanayokumbana nayo wanapotekeleza wajibu wao wa kitaaluma.
Shauri hilo litasikilizwa kwa njia ya Mtandao mbele ya Jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu; Mhe. Jaji Mruma, Mhe. Jaji Dkt. Rumisha na Jaji Dkt. Longopa. Shauri hili ni miongoni mwa mashauri muhimu ya kikatiba yanayoweza kuweka mwelekeo wa kisheria kuhusu haki ya mawakili kufanya mashauriano ya faragha na wateja wao waliopo mahabusu au gerezani, pamoja na kulinda misingi ya haki ya kupata msaada wa kisheria na usiri wa mawasiliano kati ya wakili na mteja.
WACHIMBAJI WADOGO WATAANDAMANA.
Leo Kijiji Cha Nyaburundu wilaya ya bunda Kuna mgodi ambao wananchi wanachimba wanapata kipato sasa hii serikali haramu imemuuzia mchina mgodi wetu sasa wananchi wamesala wanasema wataandamana Tarehe 7-7.
Wakati CHADEMA tumezuiwa kufanya Mikutano ya hadhara, kesho Mwenyekiti wa UVCCM atakuwa Mikutano huko Chato.
Ushaidi huu hapa someni wenyewe barua ya Mkurungenzi wa Wilaya ya Chato.
TAARIFA KWA UMMA
Kwa wale ambao mnataka kufuatilia kesi ya Mhe. Lissu dhidi ya Mkuu wa Gereza la Ukonga na Kamishna Mkuu wa Magereza itakuwa LIVE kupitia link hii 👇
https://t.co/xgXlc9zyAD
Before Hon. Mruma,
Dr Rumisha ,Dr Longopa,JJJ’s
Miscellaneous Civil Cause 7300/2026
Kulwa William Maduhu and 2 others
VS
The Attorney General and 4 others
Mention
at 09:00 am
DATE: 01/7/2026
Neema Chozaile mkt wa chadema Geita vijijini inasemekana tangia jana 29.6.026 hajaonekana
Tunatoa wito kwa vyombo vinavyomshikilia Neema kumwachia mara moja ili kuondoa hii taharuki ambayo hahitajiki kuwepo katika Taifa letu
Huyu ni mama wa watoto wanamhitaji
Free Neema Chozaile
Mh. TUNDU LISSU KUMUHOJI MKUU WA GEREZA LA UKONGA NA KAMISHNA MKUU WA MAGEREZA KATIKA SHAURI LA KIKATIBA NAMBA 7300/2026*
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Mhe. Tundu Lissu, atawahoji kwa maswali ya dodoso (cross-examination) Kamishna Mkuu wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ukonga hapo kesho tarehr 1 Julai 2026.
Shauri hilo lilifunguliwa na Mawakili Kulwa Maduhu na wenzake 3 dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamishna Mkuu wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ukonga.
Mawakili hao walifungua shauri wakilalamikia vitendo vya Jeshi la Magereza kuwazuia kutekeleza majukumu ya uwakili kwa mteja wao akiwa Gerezani, vikiwemo vitendo vya kuwanyima privacy ya mashauriano ya kisheria na vitendo vya kuzuia wanachama na viongozi kumtembelea gerezani.
Mhe Lissu aliunganisgwa katika shauri kama upande mhimu Katika shauri hilo na hivyo kuwa miongoni mwa wajibu maombi . Aidha Chama cha wanasheria nchini (Tanganyika Law Society ) nao wanashiriki shauri hili kama mdau mwenye maslahi katika shauri (Interested Party) kufuatia maombi ya kuunganishwa kwenye kesi hii kukubaliwa na mahakama kuu.
Wengine watakaohojiwa na Mhe Lissu ni wahanga wa vitendo hivyo vya magereza ambao ni mawakili waliofungua kesi hii kwa lengo la kupata au kuieleza Mahakama mazingira halisi wanayokumbana nayo wanapotekeleza wajibu wao wa kitaaluma.
Shauri hilo litasikilizwa na Majaji watatu ambao ni Mhe. Jaji Mruma, Mhe. Jaji Dkt. Rumisha na Mhe. Jaji Dkt. Longopa kuanzia saa tatu asubuhi kupitia link ya:
https:/virtualcourt.judiciary.go.tz/7300
Wapenda haki na Demokrasia ya kweli, mnaombwa kuingia online kusikiliza sgauri hilo.
‼️HABARI MBAYA KUTOKA GEITA‼️
Huyu Dada anaitwa Neema Chozaile ni Mwenyekiti wa CHADEMA wa Jimbo la Geita, June 29, 2026 aliaga watoto wake kwamba anaenda Sokoni kununua mahitaji ya nyumbani.
Kwa mujibu wa mashuhuda wanasema Neema akiwa njiani alivamiwa na Mapolisi kutoka Central Mkoa wa Geita walimkamata na kumuingiza kwenye gari yao kisha wakaondoka mpaka muda huu haijulikani wamempeleka wapi.
#FreeNeemaChozaile
Serikali haram ya Nduli Idd Amin Mama imeagiza Petrol Station zote za Dar es salaam kuanzia usiku huu wasitishe kuwauzia mafuta madereva wa Bodaboda mpaka Julai 7 ipite.
Mnaogopa nini nyie wauaji kwamba mkiwauzia bodaboda mafuta ndo watafanyaje?
Umepiga risasi na kuuwa kikatili maelfu ya watu pasipo sababu zozote za msingi.
Badala ya ukatili wako kukuletea mafanikio na furaha, umegeuka kuwa mtumwa wa hofu.
Maisha yako yote unalazimika kufake kuanzia tabasamu mpaka support.
What a terrible life to live!!🙌
Kuna tofauti kubwa kati ya Wabunge waliochaguliwa na Wananchi na Wabunge waliojiweka madarakani baada ya kumwaga damu za Watanganyika zaidi ya elfu kumi.
SHAURI LA KIKATIBA LA MHE. TUNDU LISSU KUSIKILIZWA JULAI 1–3, 2026
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinawataarifu wanachama wake, vyombo vya habari na umma kuwa kuanzia tarehe 1 hadi 3 Julai 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu Dodoma, itaendelea na usikilizwaji wa Shauri la Kikatiba Na. 7300 la Mwaka 2026.
Katika hatua hiyo ya usikilizwaji, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Tundu Lissu, anatarajiwa kuwahoji kwa maswali ya dodoso Kamishna Mkuu wa Magereza pamoja na Mkuu wa Gereza la Ukonga kuhusu vikwazo vinavyodaiwa kuwekwa dhidi yake akiwa gerezani, ikiwemo haki ya kupata mashauriano ya faragha na mawakili wake na haki ya kutembelewa na viongozi pamoja na wanachama.
Shauri hili linahusu tafsiri ya Katiba na linatarajiwa kuwa na mchango muhimu katika kulinda haki za wafungwa na mahabusu, hususan haki ya kupata msaada wa kisheria na usiri wa mawasiliano kati ya wakili na mteja.
CHADEMA kinawahimiza wanachama, wadau wa sheria na Watanzania wote kufuatilia kwa karibu mwenendo wa shauri hili muhimu.
Hi guys, I need a huge favor. Naomba msaada wenu mkubwa.
Hili tangazo ni la maana sana, siwezi kuelezea kwa kina sasa hivi ila baadae nitawaelezea. Ila ni process ya kupata account zangu za meta (instagram na Facebook)
Naomba mnitumie posti yoyote ile ya Mmarekani yoyote yule, mweusi au Mzungu ambae kawahi kuandika posti yoyote ile akiikosoa serikali ya Tanzania na posti hiyo haikufutwa au kuchukuliwa hatua na meta, posti lazma iwe kwenye mitandao ya instagram au facebook sio humu X.
Sio lazma awe Mmarekani au mzungu, hata awe mweusi ila sio Mtanzania ila awe anaishi hapa Marekani au hata nje ya Marekani.
Yani kwa kifupi posti za foreigners haswa wazungu wakiikosoa serikali ya Tanzania.
Naomba mnitumie kupitia whatsapp +1 424-537-3057
TUNDU LISSU KUMUHOJI MKUU WA GEREZA LA UKONGA NA KAMISHNA MKUU WA MAGEREZA KATIKA SHAURI LA KIKATIBA NAMBA 7300/2026
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Mhe. Tundu Lissu, atawahoji kwa maswali ya dodoso Kamishna Mkuu wa Magereza pamoja na Mkuu wa Gereza la Ukonga tarehe 1 hadi 3 Julai 2026 katika Shauri la Kikatiba Na. 7300 la Mwaka 2026 mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu Dodoma.
Shauri hilo lilifunguliwa na Mawakili Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu na Paul Kisabo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamishna Mkuu wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ukonga.
Katika shauri hilo, Mahakama inaombwa kuamua kuhusu masuala mbalimbali ya kikatiba yanayohusu vikwazo vya Jeshi la Magereza dhidi ya Mhe. Tundu Lissu, mawakili wake, ndugu, viongozi na wanachama wanaomtembelea gerezani.
Miongoni mwa masuala yanayolalamikiwa ni pamoja na kuzuiwa kwa viongozi na wanachama kumuona Mhe. Lissu gerezani, pamoja na vitendo vya askari wa magereza vya kusikiliza mazungumzo kati ya Mhe. Lissu na mawakili wake wanapofanya mashauriano ya kisheria, jambo ambalo linakiuka haki ya faragha na haki ya mawakili kufanya kazi yao kwa mujibu wa Katiba na Sheria.
Katika shauri hilo, Mhe. Tundu Lissu ni miongoni mwa wajibu maombi (Respondents, huku Chama cha Wanasheria Tanganyika kitashiriki kama mdau mwenye maslahi katika shauri (Interested Party) baada ya Mahakama kukubali maombi yake.
Aidha, kutokana na uzoefu wao wa kukumbana na changamoto hizo wanapomtembelea Mhe. Lissu gerezani kwa ajili ya mashauriano ya kisheria, Mhe. Lissu anatarajiwa pia kuwahoji mawakili waliofungua shauri hilo ili waweze kuieleza Mahakama kuhusu mazingira halisi wanayokumbana nayo wanapotekeleza wajibu wao wa kitaaluma.
Shauri hilo litasikilizwa kwa njia ya Mtandao mbele ya Jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu; Mhe. Jaji Mruma, Mhe. Jaji Dkt. Rumisha na Mhe. Jaji Dkt. Longopa.
Shauri hili ni miongoni mwa mashauri muhimu ya kikatiba yanayoweza kuweka mwelekeo wa kisheria kuhusu haki ya mawakili kufanya mashauriano ya faragha na wateja wao waliopo mahabusu au gerezani, pamoja na kulinda misingi ya haki ya kupata msaada wa kisheria na usiri wa mawasiliano kati ya wakili na mteja.
Imetolewa na:
Wakili Paul Kisabo
Dar es Salaam
30 Juni 2026
Malasusa kapewa ahadi na Nduli Idd Amin Mama kwamba Uchaguzi ujao maccm yatasimamisha mgombea uRais mKKKT ambae ni Mwigulu so haya ambayo anafanya sasa ni katika kupalilia ahadi 😂😂😂😂
Sikilizeni nyie VIKARAGOSI kila mpango mnaopanga dhidi ya @ChademaTZ2 lazima utashindwa, chadema ni mpango wa Mungu na yeyote anayepanga uovu huo hashindani na chadema anashindana na Mungu mwenyewe. Aluta continua!
7/7 maandamano loading in #Tanzania as flyers are flying everywhere 😅
#KeepEyesOnTanzania
We will be posting all plots and plans of Samia Suluhu’s murdeeous cabal heading to the 7/7 mega protest
Yaani watajaza wanajeshi, polisi , goons wa Mwaipopo ila nguvu ya umma haijawahi kushindwa! Madhulmat wanajichosha!
#TutaelewanaTu lakini
Yaani dar es salaam askari wamejazana kila kona ya mtaa utazani maandamano yapo Dar tu!
Kwa taharifa yenu @tanpol mahandamano ni yaamani na siyo kosa kisheria kwenda kudai haki zetu sisi hatuna shida ila shida mlete nyie?