#Habari Watoto 67 wilayani Tarime mkoani Mara wamekataliwa na familia zao baada ya kukataa kukeketwa na kukimbilia kwenye kituo cha kuhifadhi wasichana wanaokataa kutekeleza mila hiyo.
#Habari Msemaji wa Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa amesema kuwa hali ya kifedha ya umoja huo ni mbaya hivyo kuna mpango wa kuwafuta kazi maafisa wake 131 kama njia ya kubana matumizi.
#Habari Meya wa Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, Raymond Mboya amekanusha tetesi za kujivua wadhifa wake huo na kuhama chake cha Chadema na kuhamia CCM.
Shukrani kwa @salim_alkhasas @abbykirahi @patnanyaro@issamwamba@hmbwambo@d33dat, ambao kwa pamoja wamewasiliana na familia ya Msafiri, wamekidhi ombi lake na kumnunulia kiti cha magurudumu pamoja na vifaa vya shule, ambavyo aliomba kusaidiwa.
#Habari Wanawake watatu wamemtuhumu rais Donald Trump kwamba aliwafanyia ukatili wa kijinisa miaka iliyopita kabla hajawa rais.Hivyo baraza la Congress kumchunguza trump kutokana na kashfa hizo.
#Habari Mchungaji Ambikile Mwasapile maarufu kama ‘Babu wa Loliondo’ amesema ameoteshwa kuwa maelfu ya watu watafuata tiba yake maarufu ya ‘Kikombe cha Babu’ anayoamini inatibu magonjwa mengi.
Leo nchi ya #Kenya inasheherekea maadhimisho ya miaka 54 tangu ilipopata uhuru wake Disemba 12, 1963 kutoka kwa wakoloni Waingereza.
#JamhuriDay#HappyJamhuriDay
#Habari Juvenal Munubo, mwakilishi wa Kivu Kaskazini katika Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ametahadharisha kuhusiana na vitisho vya waasi wa ADF-Nalu wa Uganda wanaoendesha harakati zao mashariki mwa DRC.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imeamuru kurudishwa rumande aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na Mbunge wa Donge, Zanzibar, Sadifa Khamis hadi Disemba 19, mwaka huu.
#Habari Klabu ya Yanga inajiandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayoanza mapema mwakani huku mmoja wa wapinzani wake katika kusaka taji hilo ni mshambuliaji wake wa zamani, Simon Msuva anayecheza Difaa El Jadidi ya Morocco.
Mkurugenzi Mtendaji wa tume ya Ukimwi Zanzibar Dkt. Ahmed Mohmaed Khatibu amesema pamoja na Zanzibar kujitahidi kushusha kiwango cha idadi ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi bado idadi inaongezeka kila mwaka huku vijana wakiwa ndio wahanga wakubwa.
#Michezo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameshinda nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika Baraza la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. @HKigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza bandarini Dar es Salaam na kuagiza Katibu Mkuu wa atangaze kujitokeza kwa wamiliki wa magogo 938 yaliyokaa bandarini kwa zaidi ya miaka 10 vinginevyo yatakua mali ya Serikali.
#Habari Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe jana aliwafuta kazi mawaziri wake wawili zikiwa zimepita siku mbili tu tangu awateuwe siku ya Alkhamisi.
Serikali mpya ya Zimbabwe imesema kuwa, mawaziri hao wamefutwa kazi kama sehemu ya kuheshimu katibu ya nchi hiyo.
#Habari Kinara wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema ataapishwa kuwa rais 'halali' wa Kenya Disemba 12, wakati nchi hiyo itakuwa inaadhimisha Siku ya Jamhuri.
#Habari Serikali ya Zimbabwe imetangaza siku kuu mpya ya kukumbuka mchango wa Robert Mugabe ambaye aliondolewa madarakani wiki iliyopita.
Gazeti la serikali la Herald limesema sikukuu hiyo itakuwa ikiadhimishwa siku ya kuzaliwa kwa Bw Mugabe kila mwaka.
#Habari Rais Uhuru Kenyatta amemualika 'ndugu yake' Raila Odinga katika sherehe za kuapishwa kwake zikatazofanyika katika mji mkuu Nairobi Jumanne ijayo ya Novemba 28.