#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 229
Anasimama Mhe. Lissu.
Anasema baada ya kusikiliza hoja za Wakili wa mleta maombi naomba nianze kwa kunukuu maneno ambayo Mahakama hii iliyasema kwenye kesi ya Commissioner General of TRA Criminal case namba 62/2022 pale ambapo maombi ya mdaawa yamezuiliwa na sheria, hawezi kufanya drafting ya kuhadaa Mahakama.
Wanasema uamuzi ulifanyika bila wao kusikilizwa, mgogoro ulianza 19 February 2026 ukurasa 391 wa record, Ugomvi ambao umetuleta hapa ulianza siku Tano kabla ya maamuzi ya Mahakama.
Wakili wa Serikali mkuu Renatus Mkude alisema "waheshimiwa Majaji tuko tayari kuendelea na mashahidi 3 lakini kabla ya kuendelea tuna notice of additional substance of evidence, ambayo imejazwa electronically siku ya Jana"
Katika ukurasa wa 392 Mahakama ikaamua kuwa tuendelee na mashaidi kwanza baadae tutarudi kwenye hoja za notice.
February 20, 2026 ukiangalia ukurasa wa 405-419 utayaona maneno niliyoyasema.
Mahakama ikaamua tumesikiliza sehemu zote kesi hii anahairishwa hadi jumatatu ilikuwa 23 February 2026 kuanzia ukurasa 420 unaonesha hayo.
Mkude akasema wako tayari kuendelea na Katuga akafanya submission in chief pg 421, 423 Katuga akajibu PO, nikafanya rijoinder, pg 428 kuna ruling of the court.
Baada ya submission ya Renatus, submission in chief ya Katuga, rejoinder yangu na reexamination in chief ndipo Mahakama ilitoa uamuzi.
Kwa record hiyo yote nguvu ya kusema hawakusikilizwa wanaitoa wapi?
Kwasababu ya maombi haya leo ni siku ya 139 kesi haiendelei kwa sababu ya uongo wao kwamba hawakusikilizwa.
Haki ya kusikilizwa ni haki ya kikatiba ni kweli sasa kwa ushaidi huu wanawezaje wakasema hawakusikilizwa?
Mmemsikia Wakili Katuga akisema Mahakama ilikosea ilipaswa iangalie reasonablity ya hiyo notice, ipokee ushaidi, iangalie competence kisha iamue.
This is an appeal under 6.3 wanayoitaja, it's only clever drafting inayolenga kuiadaa Mahakama.
Iangalie TRA vs New Musoma textile industry kwenye orodha yangu ni kesi namba 7 hawaruhusiwi kuleta malalamiko kuhusiana na hiyo notice kwenye Mahakama hii. Kifungu 6.3 cha AJA mamlaka ya Mahakama hii siyo hiyo wanayoiomba wao.
Ukurasa wa 21 unaonesha mjadala mpana wa ninachokisema sasa na inamaliza huu mjadala, hamuwezi kuanza kuangalia hiki kilicholetwa ni kitu gani mnapaswa kutazama je huu uamuzi ni legal.
Wanasema hawakusikilizwa mnaangalia kwenye record, Je ni kweli hawa watu hawakusikilizwa, hamuendi kwenye huu usikilizwaji ulikuwaje, Mahakama hii haiangalii mambo superficial.
Waheshimiwa Majaji mleta maombi alisikilizwa hivyo ruling ya mahakama ni legal, imeandikwa na Majaji wenye mamlaka baada ya kusikiliza pande zote hata kama hauwafurahishi wanapaswa kukubaliana nao.
Waheshimiwa Majaji waleta maombi hawana hoja yeyote ya maana on the basis of this record. Section 308 ya CPA imetajwa kwa lengo la kuwaalika mtengue kilichoamuliwa na Mahakama kuu nawaombeni msiende huko.
Nitasema kwa kifupi sana juu ya section 308 ya CPA na nini Mahakama ilisema inakataa kuongezwa kwa ushahidi mpya inadeal na Shaidi mpya tu.
Inazungumzia ni katika mazingira gani shaidi ambaye hakutajwa kwenye commital proceedings anaweza kuongeza kwenye trial, mleta maombi hapa analeta ushahidi mpya wa shaidi ambaye ametajwa kwenye commital na siyo shaidi mpya kama Sheria inavyotaka.
Anaendelea Mhe. Lissu
Kwenye uamuzi huu hakuna sehemu ambayo Mahakama imesema ushaidi huo haufai bali imesema ni ushahidi mpya na haufai kisheria.
Hii clever drafting in order to avoid the legal power, kama wanataka kupinga uamuzi huo wasubiri kesi iishe kisha wakapinge uamuzi huo.
Part 230 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 228
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba nimalizie nisiwachoshe.
Hoja yangu inahusika na maamuzi ambayo hayamalizi kesi, kesi bado ipo na tutakapoenda kwenye substance nitawaoneshe Majaji kwenye hicho walichokileta wao wenyewe ambavyo kesi bado inatusubiri.
Kwa bahati mbaya wametupotezea muda sana hivyo nawaombeni Waheshimiwa Majaji mkatae maombi hayo.
Anasimama Katuga anasema Waheshimiwa Majaji maombi yetu yameletwa chini ya kifungu cha 6 kifungu kidogo cha 3 cha Sheria ya mamlaka ya rufaa ya mahakama hii na kanuni ya 65 kanuni ndogo ya 1. Waheshimiwa Majaji ukisoma notice yetu inataja kifungu cha 6 cha Sheria ya mamlaka ya rufaa ya mahakama hii, Waheshimiwa Majaji lalamiko la mjibu maombi lisingekuwepo kama angeipitia kanuni ya 48.
Jaji anamwambia Katuga ulishamaliza usilete jambo jipya nenda moja kwa moja kwenye maombi.
Katuga anaendelea
Waheshimiwa Majaji maombi yetu yamejikita kuiomba Mahakama hii tukufu iweze kuangalia uhalali na usawa wa muenendo wa shauri lililoko mbele ya Mahakama kuu.
Maombi haya yametokana na mzizi wa upande wa Jamhuri kuleta notice ya kuongeza ushaidi ambao haukusomwa wakati wa commital na upande wa Jamhuri ulifanya vile kuendana na kifungu cha 308 cha CPA, kifungu hiki Waheshimiwa Majaji kinaweka zuio kwamba hakutakuwa na ushahidi ambao utaongezwa Mahakamani kama ushahidi huo haukusomwa hautaruhusiwa kuongezwa unless upande wa Jamhuri utatoa notice ya kuongeza ushaidi huo.
Tunatakiwa kutoa notice ili mshitakiwa asikutane nayo by surprise, kifungu hicho kinaitaka Mahakama wakati inafanya reasonablity ya notice ifanye vitu gani.
Mahakama wakati inatakiwa kutambua reasonablity ya notice inapaswa kuzingatia kifungu cha 308 kifungu kidogo cha 3 inatakiwa kuuchambua ushaidi wenyewe.
Naona Job Mrema ni kama kambonyeza Katuga ameinama sijui wanaongea nini na wenzake,
Halafu sio mara moja kila baada ya sentence kadhaa vikao vinakuwa vingi.😤
Anaendelea Katunga
Mahakama ilienda kuangalia huo ushahidi katika ukurasa wa 431 wa muenendo wa Mahakama kuu na kuita ni ushaidi mpya umekusanywa baadae na hivyo wamekataa.
Ushaidi unakatakiwa pale ambapo unakuwa umefikishwa Mahakamani baada ya kuwa umepimwa ndipo Mahakama inaamua uingie au usiingie, upokelewe au usipokelewe lakini hauwezi kuamuliwa wakati unakuwa introduced.
Kifungu cha 308 kimetoa nini Mahakama inafanya, ndo maana kwenye maombi yetu tunasema tumenyimwa haki ya kusikilizwa in relation na huo ushahidi.
Haki ya kusikilizwa ni haki ya kikatiba, maana ya hii haki ya kusikilizwa ni kumpa mtu haki ya kumsikiliza full kwa utimamu ndo maana Mahakama ina vitu vitatu vya kupima.
Ushaidi unapimwa unapokuwa umefika Mahakamani, kusema ushaidi ni mpya usiletwe ni kuukataa ushaidi kabla hata haujafika Mahakamani.
Mahakama hata haikuusikia ushaidi lakini ikaenda kusema ushaidi huo ni irrelevant.
Utaratibu wa proceeding ulikuwa umekiukwa na ukiukaji ambao unaenda kwenye shauri yenyewe na ndiyo maana upande wa Jamhuri tukaona kwa busara zenu muangalie hizo proceedings hatuwezi kuendelea na hizo illegalities.
Anaendelea Katuga
Tunataka Mahakama iangalie ni kwa namna gani kwa muda gani ushaidi unaangaliwa na kuwekwa kama ushaidi.
Kwenye kifungu hakuna sehemu tuliposema Mahakama iende ikaupime huo ushahidi ilikuwa ni notice tu, ushaidi kuja Mahakamani na kufukuzwa kabla ya kusikilizwa huko ni kutunyima haki.
Ni vigumu kupima ushaidi ambao hauko hata mahakamani.
Ukurasa wa 431 wa proceedings naomba muuangalie waheshimiwa Majaji, jambo hili lilikiuka taratibu za mienendo ya proceedings.
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya rufani tunaomba maombi yetu yaangaliwe na yakubaliwe.
Waheshimiwa Majaji ya kwetu ni hayo tu.
Part 229 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 227
Anasimama Wakili wa Serikali Mrema
Anasema naomba kuongeza kidogo kwenye mawasilisho yaliyofanywa na Wakili mkuu wa Serikali Katuga, naomba kuongeza yafuatayo.
Waheshimiwa Majaji hii obligation inayowasilishwa mbele ya mahakama ya rufani lazima iwe na uwezo wa kuondoa shauri hilo lililoko mbele ya Mahakama hii, nikirejea shauri alilolilejea, shauri la DPP dhidi ya Mohammed Ussi naomba kuialika Mahakama hii kwenye kifungu cha 5 kifungu kidogo cha 2.
Mleta maombi amefanya reference kwa kifungu ambacho kimepitwa na wakati it's not applicable.
Kifungu hiki kukihusianisha na kesi ya Mohammed Ussi na kukileta kwenye Sheria ya sasa it's not applicable.
Kifungu cha 8 kinazungumzia mashauri ya madai, swali la kujiuliza ni je shauri hili ni la madai.
Jaji anawasha kipaza anauliza. Katuga ulisema Mrema anaongezea sasa mbona anarudia yaleyale.
Watu wanacheka😂😂😂😂😂
Jaji anamwambia Mrema aendelee ila asirudie mambo ambayo tayari Katuga ameongea.
Mrema anasimama anasema waheshimiwa Majaji ni hayo tu.
Watu wanacheka maana ni kama alichosema Jaji kimemto kabisa Mrema kwenye mood.😂😂😂😂
Anasimama Mhe. Lissu
Waheshimiwa Majaji naomba mniruhusu nijibu hoja za waleta moambi.
Wanacholalamikia siyo order wanalalakikia findings.
Waheshimiwa Majaji wanacholalamikia wamekileta wenyewe kwenye hati yao ya maombi hicho kiko kati ya ukurasa wa 428-431 wanalalamikia rulling, uamuzi.
Uamuzi wanaoulalamikia unajadili ushaidi wanaotaka kuuingiza, na Mahakama ikajadili ushaidi huo kwamba ni kinyume na Sheria hautaingizwa.
Kama wasingekuwa wanalalamikia hii ruling wasingeileta mbele ya Mahakama yako. Finding is not similar to a decision.
Waheshimiwa tuasume Mawakili hawa wako sahihi finding is similar to decision, tuangalie Mahakama inasema nini juu ya aina hii ya ushaidi, Mahakama ikasema ni kinyume na Sheria hauruhusiwi kuingia.
Mawakili waleta maombi wameleta kesi muhimu sana kesi ya Peter Michael Madeleka, kuna mahali katika kesi hiyo ambako Mawakili wa Serikali wamepakimbia kama ukoma, ukurasa wa 9 Mahakama ilisema hivi kuhusiana na hicho kifungu hayampi mamlaka ya kuimove Mahakama.
Mhe. Lissu anawambia Mawakili wa Serikali ahsanteni sana kwa kuleta kesi ya Madeleka.
Watu wanacheka 😂😂😂😂 maana akina Katuga wameleta kesi ambayo badala ya kuwasaidia kumkandamiza Mhe. Lissu yenyewe ndo imekuwa msaada kwa Mhe. Lissu.
Anaendelea Mhe. Lissu
Mamlaka ya Mahakama ya rufani kuitisha Suo moto ni mamlaka yake yenyewe haiwezi kuwa moved na waleta maombi.
Kama Mahakama haijaiona yenyewe haiwezi kuletewa maombi.
Wanasema nisiwafundishe lakini mkiangalia record waliandika barua, walileta maombi kisha wakaandika barua wanataka kuimove Mahakama.
Katuga amesema maombi yao wameyaleta under 6.3, Waheshimiwa Majaji nawaomba muangalie maombi hayo kama kuna sehemu wametaja kifungu hicho. In their notice of motion hakuna sehemu wametaja ni 6 ipi kati ya vifungu 6 vya Sheria hiyo hawawezi kuja hapa kuzungumza kitu tofauti na maombi yanavyozungumza.
Nirudi kwenye hoja ya Job Mrema, mmealikwa Majaji kukubaliana na hoja kwamba Sheria imeshabadilika ni vifungu tofauti, Waheshimiwa Majaji mimi nina revised Act of 2023 inasema section 5 haina marekebisho ya kabla ya 2023 kwa hiyo hii hoja ya kwamba kuna Sheria imebadilika ni vitu tofauti ni hoja ambayo nachelea kusema haina mashiko.
Waheshimiwa Majaji wakili ametaja rule 48.1,
Waheshimiwa Majaji inazungumzia PO must have a capacity to dispose of application na kwa maana hiyo anasema pingamizi langu halina uwezo wa kumaliza madai,
Je kwenye hoja ya kwangu hii kwamba maombi haya hauruhusiwi kwasababu hayana uwezo wa kuyafuta maombi kama inasema imeletwa chini ya kifungu cha 8.2.d? hakuna hoja hapo.
Part 228 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 226
Anaendelea Mhe. Lissu.
Waheshimiwa Majaji uamuzi uliotolewa na Mahakama ya rufani katika kesi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA na bodi ya wadhamini wa CHADEMA vs Saidi Issa Mohammed na wenzake inasema kwamba kama mdaawa (Mleta maombi) analeta maombi mwenyewe ni yale yaliyoko kifungu cha 6 kifungu kidogo cha e, maombi mengine ni Mahakama yenyewe ndiyo inaamua bila kusukumwa na yeyote au kuletewa maombi yenye hati ya kiapo.
Waheshimiwa Majaji kwa vyovyote vile maombi hayo hayako halali mbele ya mahakama hii kwani hayakuletwa katika utaratibu wa kisheria kwani Mahakama hii haijaamua maombi haya yaje yenyewe Suo moto kwa hiyo Mahakama isikubali kusikiliza maombi hayo kwasababu ambazo nimezisema.
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa waheshimiwa Majaji sijui kama mnaniruhusi niendelee au wajibu kwanza.
Jaji anasema Jamhuri wajibu kwanza PO kisha tutaendelea.
Anasimama Wakili Katuga anasema Waheshimiwa Majaji tukirejea mapingamizi yake ya awali yameletwa chini ya kifunga cha 8.2.d hiki ni kifungu mahususi kwa mashauri ya madai.
kifungu hiki kilikopwa kikatumika kwenye madai kwenye mashauri ya rufaa, hata kama Mahakama yenu tukufu kwa rejea hizo za Mahakama hii ikakikopa kitumike kwenye maombi yetu haya bado tunasema kwamba maombi yetu yako sahihi mbele ya mahakama hii tukufu tofauti na kile ambacho mjibu maombi amekileta kama pingamizi la awali.
Maombi yetu yameletwa chini ya kifungu cha 6 specifically kifungu kidogo cha 3 cha Sheria ya mamlaka ya Mahakama. Kanuni ya 65 na kanuni ya 45 ya kanuni za Mahakama ya Rufani inasuport maombi yetu.
Anaendelea Wakili wa Serikali Katuga
Waheshimiwa Majaji ukiyasoma maombi yetu kwenye notice of motion hakuna sehemu yeyote tunayoiomba Mahakama hii tukufu ipitie order ya Mahakama au uamuzi wa Mahakama, pale mwisho tunasema Mahakama idiscuss kukataa ushahidi hatujazungumzia kukataa notice, sisi tunazungumzia kuuchambua na kuukataa ushahidi.
Hakuna sehemu kwenye maombi haya tunalalamikia order, Mahakama yenu itaona kwamba pingamizi la mjibu maombi limekuwa mislead hakuconsue sawasawa maombi yetu.
Pale ambapo neno or litatumika kwenye Sheria yeyote maana yake maneno haya hayako similar yanatumika tofauti, Waheshimiwa Majaji nimewarejesha humu muweze kukitafsiri kifungu cha sita. Haya maneno yanatakiwa yatafisiriwe tofauti hayaendi pamoja ama hayategemeani, inaweza kuwa kimoja wapo kati ya haya.
Kama mahakama yenu imekikopa kifungu cha 8.2.d kinazungumzia katazo la decision or order ndo hauwezi kuziombea appeal or revision.
Sasa tunapata wapi nguvu za kuleta pingamizi kwa tafsiri hiyo tunaiomba Mahakama hii ikaangalie maana ya maneno haya.
Waheshimiwa nawarejesha kwenye kamusi kwa sababu nayo ni kati ya vitu vinavyopaswa kutumika kutafsiri Sheria. Katika ukurasa wa 129 kamusi inadefine order ni nini?
Kwenye application yetu hakuna sehemu tumeombea decision or order, kwenye kifungu cha 8 hata kama kimekopwa hakiwezi kucocer maombi yetu.
Mahakama yenu ilishawahi kuiamulia hili kwenye kifungu 394 cha CPA, katika kesi ya Peter Michael Madeleka dhidi ya jamhuri.
Kutaja kitu fulani means exclusion ya kitu kingine, kitendo cha kifungu cha 8 kutaja findings and order means haijatuzuia kwa maana hiyo findings hapa haijazuiwa kwa maana hiyo tunachotaka kuiambia Mahakama yako ni kwamba ule ushahidi ulikataliwa kabla ya wakati wake.
Anaendelea Wakili wa Serikali Katuga
Waheshimiwa naomba niishie hapo kwenye hilo ili tusiende mbali kwa kuyasema hayo mtaona kwamba kesi ambazo mshitakiwa amewapitisha ni distinguishable kwenye mazingira yetu.
Hii kauli ya kwamba hatuna mamlaka ya kuomba Mahakama iitishe ‘Suo moto’ sisi tunasema mamlaka tunayo.
Katiba anasema naomba Mrema anisaidie anayo nyongeza.
Anasimama Wakili wa Serikali huyu anaitwa Job Mrema anakipara kama Mrema wa ubwabwani, sijui na yeye huwa anakunywa visungura kama mwenzake, anyway
Part 227 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo July 3, 2026
Last time kwenye ya Uhaini dhidi ya Mhe. Lissu tuliishia part 224 so leo tunaendelea na -;
Part 225
Mheshimiwa Tundu Lissu anaingia ndani ya chumba cha mahakama, ukumbi namba 01 wa Mahakama Kuu.
Anaonekana mwenye tabasamu na furaha usoni kwake kama ilivyo siku zote.
Upande wa Jamhuri wapo kama kawaida yao
Inapigwa Court…..
Jopo la Majaji watatu wanaingia,
Kesi inatajwa
Anasimama Wakili wa Serikali anajitambulisha jina lake Ajuaye kisha anatambulisha Mawakili wenzake.
Jaji anaamuliza Mhe. Lissu kama yupo tayari
Mhe. Lissu anasema yuko tayari kuendelea.
Kama kawaida yao anasimama Wakili wa Serikali Katuga kuweka pingamizi.
Mhe. Lissu anapendekeza maombi yake ya sikilizwe kwanza ndo pingamizi lao lijibiwe.
Majaji wanasema tuanze kwanza kusikiliza PO, kisha taratibu nyingine zitafuata.
Anaanza Mhe. Lissu Waheshimiwa Majaji kesi hii inatokana na maombi namba 19065 ya mwaka 2025, Juu ya maombi ya kuongeza ushahidi katika muendelezo wa kesi, uamuzi wa tarehe 24 February 2026 wa Mahakama Kuu wa kukataa kuingizwa kwa ushahidi mpya.
Waheshimiwa Majaji uamuzi wa February 24, 2026 ni uamuzi mdogo, uamuzi ambao haujamaliza shauri na kwa mantiki hiyo kisheria kabisa haupaswi kukatiwa rufaa au pingamizi.
Waheshimiwa Majaji wa rufaa, Mahakama hii katika kesi ya Mkurugenzi wa Mashitaka dhidi ya Mohammed Mussa Ussi criminal appeal namba 521 ya mwaka 2023 Mahakama ikiwa imeketi Zanzibar ilisema msingi wa kukataza rufaa ama mrejesho (revision) ya jinai msingi wa hiyo hoja ni kifungu cha 8.2.d kutokana na marejeo ya mwaka 2023 mahakama hii ilisema uamuzi huo hauwezi kukatiwa rufaa kwani ni uamuzi usiomaliza shauri.
Anaendelea Mhe.Lissu
Kesi ambazo nimeziwasilisha mbele yenu waheshimiwa Majaji zinazungumzia uamuzi mdogo ni wa aina gani na uamuzi unaoweza kutolewa kama uamuzi wa mwisho unaoweza kuombewa revision ni wa aina gani.
Uamuzi unaomaliza kesi na kunyima haki za wadaawa ndiyo unaopaswa kukatiwa rufaa, uamuzi unaokuwa treated as the final order ndiyo unaomaliza haki za msingi za wadaawa lakini kama uamuzi haufanyi hivyo hauwezi kukatiwa rufaa.
Sasa waheshimiwa Majaji baada ya kuwapitisha kwenye kesi hizo nirudi kwenye hoja yangu ya msingi je uamuzi wa February 24 mwaka huu ulimaliza kesi hii?
Kama ni hivo ulimaliza kesi hii na kwamba Sasa hivi sina kesi ya uhaini basi hoja yangu haina msingi na maombi haya hayawezi kusikilizwa.
Hoja yangu waheshimiwa Majaji ni kwamba uamuzi wa Mahakama Kuu wa February 24, 2026 haukumaliza kesi namba 19065/2025 na kwasababu haukumaliza maombi haya ya revision yanakatazwa kuletwa Mahakama ya Rufaa.
Anaendelea Mhe.Lissu
Waheshimiwa Majaji uamuzi huo unasema nini, ili tujue kama ulimaliza kesi lazima tuusome huo uamuzi unasema nini.?
Rulling yenyewe iko ukurasa wa 405-432, kwenye ukurasa wa 431 paragraph ya mwisho waheshimiwa Majaji mtaona Mahakama ilichokiamua.
Kilichokataliwa kupokelewa na Mahakama ni notice of additional substance of evidence, Mahakama Kuu haikusema kesi haitaendelea. Mahakama kuu ilitoa Mwongozo haikutoa uamuzi wa mwisho wa kesi, uamuzi wao ulikataa subodinate issue.
Waheshimiwa Majaji ushaidi mwingine huko kwenye maombi yenyewe yaliyoletwa. Mahakama inasema ilijadili na kukataa notice yao ya kuongeza ushahidi haisemi kesi ilifia hapo kutokana na uamuzi huo.
Mahakama imekata notice of additional substance of evidence, kwahiyo wanalalamikia uamuzi wa notice kukataliwa.
Jambo la pili ni Je mleta maombi anayo mamlaka ya kuiambia Mahakama itumie mamlaka yake ya kupitia kumbukumbu ili kuridhisha matakwa yake mwenyewe?
Jibu ni hapana hiyo siyo haki yao kisheria kwani wajibu wa kuangalia record ni wa mamlaka yenyewe.
Part 226 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
@Sisimizi3 Hata akichukua miaka 10 haina shida bado tuna imani nae na sababu za kuongeza mda zipo umri wa kugombea miaka 45 wakati zamani ilikuwa 35 so wajibu na ni haki yake
Nakumbuka kipindi hicho ndio nimeanza kazi, nimepanga kageto kangu Kachumba na kasebule. Sebuleni kuna TV tu na kakochi flani kakisela na nilikuwa na tabia ikifika mida ya saa tatu kwenda mbele nahamishia TV yangu chumbani Ili vibaka wasije Kuniibia.
Eneo nililokuwa naishi kulikuwa kuna wapangaji wengi sana, na kati ya hao wapangaji kulikuwa na mpangaji mmoja mbulu. Mtoto ni mzuri, sio mrefu sana lakini ana unywele kutoka Balazir , pua kutoka India na rangi kutoka Uturuki, chuchu ndogo kama za mtoto wa form 2. Kiufupi huyo mwanadafada kila kitu amepata kutoka Iraq, kasoro tako tu ndio ameiba kutoka usukumani ama kwa wahaya wazee wa katelelo.
Huyu mtoto alikuwa ni wale mabinti ambao wapo mjini wamepanga chumba, na unakuta weekend flani inakuja njemba kwake, halafu siku za kazi huioni tena. Kiufupi mimi nilikuwa namchukulia kama hawara wa jamaa kwani huyo jamaa pia kuna baadhi ya weekend alikuwa haji pale tunapoishi.
Huyu binti alikuwa anaringa kiaina, nadhani ni kutokana na uzuri wake na huduma anazopatiwa na jamaa yake, kwani nilikuja kujua baadae kwamba huyu mchiz anafanya kazi kwenye mashirika ya kiserikali na mpunga anao wa kutosha.
Huyu binti alikuwa ni mzuri mno na mwanaume yoyote mzima angemtamani, lakini kwa jinsi nilivyo mimi huwa hata kama natamani demu huwa si mshobokeaji sana, kwa hiyo hata mazoea kati yangu mimi na yeye yalikuwa ni salamu tu, kuchangiashana hela ya umeme na stori mbili tatu.
Siku moja nipo geto mida ya saa 3 usiku nacheki TV chumbani, nikasikia hodi ya sauti ya kike inagongwa nikasema karibu, nikaona kimya mtu haingii, nikatoka sebuleni nikasogea hadi mlangoni, nilipochungulia nje ili kujua ni nani huyo, Sikuamini macho yangu.
Story Inaendelea next post ....
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 222
Katuga anasema kifungu cha 308 ni mlinzi wa kifungu cha 263 cha CPA ni kumfanya mshitakiwa awe aware na ushahidi wote anaokutana nao Mahakama kuu.
Ushahidi upo wa aina nne, real, documentary, testimonial na nyingine nimesahau nitaikumbuka.
Kwahiyo kwa maana ya aina ya shahidi nne zinatakiwa zioneshwe kwa mshitakiwa kabla ya kuwa committed kwenda High Court na kwakuwa kuna takwa hili la 263 kukawekwa kifungu cha 308 ambacho ni mlinzi sasa.
Kwamba hakutakuwa na ushahidi utakaoingia hadi uwekwe wazi basi prosecution wampe notice kuhusiana na ushahidi huo ni lini prosecution wamegundua huo ushahidi. Je mshitakiwa alikuwa na reasonable time kuupitia.
Kif. 308(4) kinazungumzia substance or witness.
Kesi ya Remina Omary Abdul vs Jamhuri CA 189/2020 Mahakama ya Rufaa ilisema, INASEMA IF PART OF THE EVIDENCE IS NOT DISCLOSED.
Mahakama ili quote with approval maneno kuwa additional evidence is allowed.
Sisi tunasema mbali na statement yake kusomwa tunataka kuleta mambo mengine ambayo hayakujumuishwa.
Notice hii ina comply na tafsiri ya sheria na sio tafsiri ya mtu. Iko sheria na tunaomba ikubaliwe.
Katuga kuna maneno pia yamesemwa kuwa notice hii ikiachwa hizo sio hoja. Unamtisha nani? Naona kama anatutisha ni hoja ambayo itafungua pandora na hiyo pandora ni ipi?
Tunaomba mapingamizi yatupiliwe mbali.
Anasimama Mh. Lissu kumjibu Kituga.
Nimesikiliza majibu yao naomba niseme yafuatayo.
1. Kifungu cha 308 cha CPA kinahusu shahidi mpya. Shahidi mpya kimesema ni yule ambaye maelezo yake au substance ya maelezo yake haikusomwa kwenye committal. Kwahiyo kifungu hicho kinahusu shahidi mpya na sio ushahidi mpya. Suala ni shahidi wa ziada na sio ushahidi wa ziada wa shahidi ambae tayari maelezo yake yapo tayari.
2. Kwenye notice hii suala la kuamua sio reasonable au laa. Ni suala la kinacholetwa ni shahid mpya au laa.
3. Hiyo kesi ya Remina Omary Abdul waliyoleta si mara ya kwanza inazungumzwa kwenye Mahakama hii. Ililetwa kipindi kile cha Committal. Inahusu kifungu cha 263 tu. Ukurasa wa 32 ni kuhusu section 246 ambacho ni 263 ya sasa. Kwahiyo hiyo kesi inahusiana na mambo ya Committal basi kifanyeni kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha CPA.
Mlango wa Amin Mahamba ulifungwa kwenye committal kama mnataka tafuteni shahidi mwingine sio Amin Mahamba.
Hoja ya kwamba hili ni pingamizi limeletwa pre mature nasema liko timely maana yanayohusika na kesi hii yalishakamilika na kuletwa Mahakamani.
Effect yake ni kunibadilishia shitaka maana shitaka langu ni la tar. 03/04/2025 haya ya October ni mambo mapya.
Mkiyaruhusu kwa kuruhusu notice hiyo na nimesema niko tayari, je wao watayaweza? Kwasababu ya October kuna genocide kuna mass killings, mass murder. Ya October ni magumu sana.
Pingamizi langu litalinda integrity ya shauri hili na mashauri haya. I'm only trying to help them wanafikiri kuna deal pale hakuna deal yoyote.
Angalieni kifungu cha 308 cha CPA.
Hii notice ifutiliwe mbali, naomba hivyo.
Majaji wanateta hapa.
Tunasubiri uamuzi wao kuhusu pingamizi hili.
Jaji Ndunguru amejadiliana na wenzake kwa muda mrefu sana hapa.
Anasema ili tuweze kuandika uamuzi na tutarudi kesho saa tatu asubuhi na tutaendelea na mashahidi wengine.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 221
Jaji Ndunguru ameteta sana na wenzake kama dakika 10 hivi.
Sasa anawasha kipaza sauti.
Anasema yafuatayo: tumesikiliza hoja zote hivyo vijembe vyenu msivilete.
Sasa mshitakiwa alisema anapingamizi na tukasema upande wa mashitaka walete open statement ili Mahakama iamue.
Mambo mengine ya kwamba imeambatana na nini na nini kipo wapi hayo sio mambo ya msingi.
Mshitakiwa endelea sasa, hawa upande wa mashitaka mmemaliza hapo, presentation ya notice na justification ya notice.
Watu wanacheka hapa 😂😂😂😂
Nafikiri mpaka sasa Katuga ameelewa nani ni Bingwa wa Sheria.
Mhe. Lissu amasimam, sasa Waheshimiwa Majaji kwa kuanzia niseme hivi waliyosema wenzetu.
1. Upande wa mashitaka unasema notice yao haileti shahidi mpya bali inaongezea ushahidi wa shahidi ambae ushahidi wake ulishatolewa kwenye committal.
2. Wamemtaja huyo shahidi kwa jina kabisa.
3. Wamesema wameleta viambatanisho vinavyotakiwa kwa mujibu wa kifungu cha 308(2) cha CPA.
Sasa baada ya kusema twende kifungu kinavyosema cha 308
A witness whose statement or evidence was not read during committal......
Kifungu kinasema shahidi mpya.
Kinachotakiwa kuletwa ni jina la shahidi wa ziada, huyu ndio anaweza kutolewa notice.
Wamesema wenyewe hawaleti shahidi mpya bali wanaongezea ushahidi wa shahidi aliyepo.
Sasa huyu shahidi ambae tayari yupo na wamemtaja huyo Shahidi ACP Amin Mahamba.
Sasa waheshimiwa Majaji naomba niwaalike kwenye ukurasa wa 90 na 91 na 99 na 100 wa record ya committal proceedings na ukurasa wa 134 wa record ya Mahakama hii ambapo upande wa mashitaka ulitaja majina ya mashahidi wao.
Huyo Amin Mahamba yupo na mimi maelezo yake ninayo hapa sasa Waheshimiwa majaji hiyo notice inaingiaje mahakamani.
Ushahidi wake tayari upo mahakamani na notice inatakiwa iwe ya shahidi ambae maelezo yake hayakusomwa mahakamani.
Hii sio notice ya additional witness ni notice ya additional evidence ambayo haipo kisheria nimetafuta CPA yote hicho wanachosema hakipo.
Jambo lingine ni kwamba wanaleta ushahidi wa mtu aliyefanya upelelezi wa matukio ya uchaguzi mkuu 2025 sasa Majaji matukio ya tukio ya tarehe 29/10 mimi tayari niko mahabusu
Anasimama Katuga anasema tunapinga anaanza kujadili ushahidi wetu kama mtakubali ni sawa tu.
Lissu: Si ndio kayaleta haya mwenyewe wanakatazaje nisiyazungumzie?
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa endelea.
Lissu: amesema mwenyewe kwa mdomo wake hapa Mahakamani. Nilimwambia asibwabwaje sana. Akang'ang'ania kuanza kusema mambo ya tarehe 29/10 ndio maana na mimi nasema hayo ya tarehe 29 mimi nilikuwa jela.
Wanafikiri hayo yatawasaidia maana wanataka kugeuza mashitaka kwa kuleta mambo ya tarehe 29/10/2026. They can not amend the information through the back door. Kama mnataka ku amend information nendeni kwenye kifungu cha 294 ch CPA.
Hiyo wanayoiita notice haipo kisheria. Haitambuliki. Hiyo notice muifutilie mbali. Yaani notice na yaliyomo.
Na mwisho, Wahe. Majaji hiyo notice ikiachwa ikawa sehemu ya record ya Mahakama itafungua sanduku la pandora ambalo lina kila aina ya mambo mabaya ambayo sidhani kama itaweza kushughulika mambo hayo.
Wanataka tuzungumze mambo ya October 29 mtakuwa mmefungulia balaa na isije ikawa shida. Mkifungua huo mlango tutaenda huko. Tutazungumzia mauaji ya kimbali na tutaulizana nani aliyeua watanzania. Hii kitu haina mashiko. Are they ready? Mimi niko tayari. Isiruhusiwe ikiruhusiwa niko tayari?
Jaji tafadhali naomba tusiende huko.
Katuga aliambiwa na Lissu kuwa huwezi kunifundisha Sheria akakataaa. Baada ya Lissu kumaliza hapa. Katuga amekuwa mdogo sana yani. Ni kama anataka kulia.
Katuga anasimama anasema napaswa kufanya nini reply au rejoinder
Mhe. Lissu anasema fanyeni reply halafu mimi ndio nitakuja kumaliza.
Wanakubaliana hivyo.
Part 222 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 23, 2026
Last time tuliishia Part 219 so leo tunaendelea na-;
Part 220
Mh. Tundu Lissu anaingia Mahakamani.
Mawakili wa Serikali wapo tayari na Majaji wana kila dalili ya kuingia muda wowote.
Kelele za Shujaa Shujaa Shujaa zinasikika.
Mh. Lissu ameingia anateta jambo pale na Wakili Kisabo na Mahinyila ni kama anawaagiza jambo.
Namuona Wakili Kisabo anachukua simu ni kama anafanya mawasiliano.
Majaji wameingia kuna mtu simu yake imeita, watu wanamshangaa.
Anasimama Kalani anasoma case number.
Anasimama Renatus Mkude, tupo Ajuaye, Katuga, Thawabu Issa na Cathbert Mbiringe. Shauri lilipangwa kwa ajili ya kusikiliza Notice ya kuongeza mashahidi na ushahidi na sisi tuko tayari.
Majaji wanaandika kidogo.
Wanamuuliza Mshitakiwa.
Mhe. Lissu anajibu na yeye kuwa yuko tayari.
Wanaitwa Upande wa Mshitaka anasimama Katuga kuanza.
Mhe. Lissu waheshimiwa Majaji nimepinga hiyo notice toka ijumaa kwahiyo ningesikilizwa.
Katuga Mheshimiwa Jaji utaratibu ni sisi kuiwasilisha ili yeye apinge kama ana hoja ya kupinga hii sio Application.
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji hicho wanachoita notice sio notice kabisa na hakitambuliki kisheria.
Jaji sisi tulitaka waeleze nini kinaendelea tu.
Mhe. Lissu: Kama ni hivyo sawa.
Katuga: Mnamo tar. 18/02/2026 kwa njia ya mtandao tulifile notice ya kuongeza ushahidi (notice to file additional statement of evidence) tuliifile kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha CPA.
Pamoja na notice hiyo tuliambatanisha substance ya ushahidi huo, ushahidi huu haumleti shahidi mpya bali ni nyongeza ya Ushahidi wa ACP, Amin Mahamba.
Kwamba ushahidi huu haujakuwa committed Mahakama ya hakimu mkazi kisutu.
Notice hii inakuja kukidhi matakwa ya kifungu cha 308 cha CPA ambacho kinasema hakuna shahidi au maelezo ya shahidi vitatolewa mahakamani unless viwe vimesomwa wakati wa mwenendo kabidhi (committal)
Kifungu hicho kinafafanua maana ya substance of evidence ikiwa ni pamoja na kitu chochote ikiwemo nyaraka na vitu vingine vinavyoshikika.
Kama ambavyo notice inajieleza, substance ya ushahidi kwamba Amin Mahamba alikuwa ni kiongozi wa timu ya upelelezi wakati wa uchaguzi wa 2025 na baada ya uchaguzi.
Na kile alichokipata kutokana na upelelezi ni kitu ambacho haukusomwa pale kwenye committal.
Ushahidi huo tumeupata na kuugundua wakati tumejiandaa kumuita ACP Amin Mahamba siku ya tarehe 16/02/2026 kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha CPA hakijaeleza ni kwa jinsi gani notice itakuwa. Hata kwenye zile prescribed form zilizopo kwenye Sheria hii haijawekwa.
Kifungu hicho kinasema notice ieleze jina la shahidi, substance ya ushahidi na details za shahidi kiujumla kwa mujibu wa kifungu cha 308 (2) cha CPA.
Hivyo vyote tumefanya kwenye notice yetu kucover matukio ya tarehe 29/10/2025.
Anasimama Mhe. Lissu, anasema waheshimiwa mbona kama anaendelea kufanya mambo ambayo hamjamuelekeza.
Katuga waheshimiwa kwani hiyo introduction iko chini ya Sheria gani? Sisi tunaintroduce kwa namna tunayoona ili mwenzetu.
Mhe, Lissu: Asinifundishe Sheria, asijaribu kabisa kunifundisha Sheria, anaanzaje kufanya submission ya hiyo notice kabla uhalali wake haujaamuliwa.
Katuga: Waheshimiwa hakuna bingwa wa Sheria, mabingwa ni nyie tu Majaji.
Majaji wanateta pale juu.
Tunasubiri muongozo wao.
Part 221 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 219
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Cross Examination Shahidi wa Jamhuri Coplo Amani.
Coplo Amani.: mimi sijalisema tu kama wewe umelisema basi ndio umesema.
Mhe. Lissu: Ni kweli kwamba P3 alikwambia kuwa ni mwanachama wa CHADEMA, kweli au si kweli
Coplo Amani : sio kweli
Mhe. Lissu: Wewe ndio uliandika maelezo yake kielelezo D12
Coplo Amani : kweli
Mhe. Lissu: Sasa ngoja nikusomee… “mimi pia ni mfuasi na mwanachama wa CHADEMA” kweli si kweli.
Coplo Amani : kweli
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama kwenye maelezo yako uliyasema hayo
Coplo Amani : sikuyasema
Mhe. Lissu: Alikuonyesha kadi yake cha chama
Coplo Amani : sikutaka anionyeshe
Mhe. Lissu: alikwambia wafuasi wa chadema wana alama gani?
Coplo Amani : sikumuuliza mm
Mhe. Lissu: ndo maana nasema huyu ni askari wa kitengo cha intelijensi halafu mnasema ni shahidi.
Mhe. Lissu: Turudi kwa Inspekta Jorum, ni kweli polisi inapopokea watu waliofanya uhalifu , Polisi wanafungua investigation register?
Coplo Amani : ni sahihi
Mhe. Lissu: waelezze majaji kama kwenye maelezo yako polisi walifungua investigation register
Shahidi: sijui
Mhe. Lissu: Waeleze majaji baada ya maafa yote hayo ya October 29 kama mmemchukulia hatua yoyote huyu baada ya kusema atapiga watu mawe?
Coplo Amani: Simfahamu chochote kuhusu swali lako
Mhe. Lissu: inaingia akilini hii
Coplo Amani : Mimi sifahamu chochote kwa kweli.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama unajua mashahidi wote wa kificho walisema waliona hiyo video yangu maarufu tarehe 4 april
Coplo Amani : Mimi sio mpelelezi wa mafile yote
Mhe. Lissu: Na unahabari wote waliokuja hapa ni boda boda na machinga hakuna afisa wa serikali au n.k
Coplo Amani : sina habari
Mhe. Lissu: Ulipomuachilia P3 kwa dhamana ulichukua hatua gani kuhakikisha aendelei na kupiga watu mawe na uasi?
Coplo Amani : sikupewa hilo jukumu
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji mimi sina maswali ya ziada.
Serikali: Kwa leo tulikua na shahidi huyu tu mmoja, tunaomba ahirisho kwasababu hali ya hewa ya Dar es salaam imebadilika na zimebaki dakika 20.
Kwasababu za kiusalama tunaomba ahirisho hadi siku ya Jumatatu ili tuje kuendelea kusikiliza juu ya notice tuliyoileta
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji kwa dakika 20 kwangu si haba, mimi ninaomba hizi dakika 20 kwasababu nilishasema nina mapingamizi, naomba niongee juu ya hayo leo ili tusiathiri muda wa mashahidi wengine Jumatatu.
Naomba nipate hizi dakika 20 kwasababu mimi niliyepo Gerezani ndiye ninayepata shida, kwahiyo naomba tutumie hizi dakika jambo lifanyike.
Wakili wa Serikali: Waheshimiwa sisi tunaomba ahirisho lakin vilevile kama mnavyojua dini zote mbili tupo kwenye mfungo kwahiyo tunaomba ahirisho.
Lakini vilevile PO yake haijasajiliwa bado kwahiyo kama ataweza kuisajili na kuisikiliza basi aisajili na sisi tupewe nafasi ya kuiona ili tu-submit
Mhe. Lissu: waheshimiwa majaji sikutarajia kwamba hili litakua na kubishana namna hii, nililetewa hii notice jana na nikatoa notice ya mdomo kwamba naipinga tena immediately nilipopatiwa tu notice hii.
Naijua sheria, sasa wanaposema tuahirishe ili niendelee kukaa gerezani ni sawa tukutane Jumatatu ili tuzungumzie PO yangu niliyoileta jana.
Na jana nilisema kabisa PO ni ya kisheria na itaenda na kifungu icho icho cha 308(1) cha CPA, mimi nakaa gerezani kwasababu ya michezo hii mnayoleta mawakili wa serikali kila siku.
Jaji Ndunguru anasema shauri litaendelea siku ya Jumatatu, tunatarajia serikali mlete mashahidi, tutaanza na hoja ya notice, tukimaliza tutaendelea na mashahidi wengine.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 218
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Cross examination Shahidi wa Jamhuri Coplo Amani.
Mhe. Lissu: Angalia D14 tuambie wapi alisema alimuona Tundu Lissu akihamasisha uasi, kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi wa 2025?
Coplo Amani : Hayo maneno kufanya vurugu hayapo kwenye kielelezo
Mhe. Lissu: April 17, 2025 kwenye ushahidi wako wa hii siku unasema ulikuwa kituo cha Polisi Ilomba na ukapewa maelekezo na inspekta Jorum kuandika maelezo ya mtuhumiwa kama shahidi kuhusiana na alichoeleza juu ya Mwenyekiti wake Tundu Lissu kuhusu kauli yake na akahamasika na akashawishi wenzake wafanye vurugu na kuharibu uchaguzi mkuu 2025, eleza kama maelezo hayo yapo
Coplo Amani : hayo maelezo hayapo
Mhe. Lissu: Coplo Amani shahidi haya yote ambayo nimekuuliza kama yapo au hayapo ma umesema hayapo katika maelezo yako, swali langu ni uliyasema hapa mahakamani kwasababu ni mambo muhimu kwa mahakama kuyasikia, kweli au si kweli.
Coplo Amani : Waheshimiwa majaji naomba nitoe ufafanuzi.
Mhe. Lissu: Hapana naomba ujibu swali langu
Coplo Amani: nawaomba majaji
Mhe. Lissu: hapana
Coplo Amani : ni kweli
Mhe. Lissu: Umewaeleza waheshimiwa majaji kwanini hayo mambo muhumu hayapo katika maelezo yako??
Coplo Amani : bado nina muda
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji naomba shahidi ajibu swali langu
Coplo Amani : sijayasema na sijayaeleza kwasababu ninazozijua Mimi.
Mhe. Lissu: Nataka uangalie icho kielelezo D14 ni nataka uangalie halafu uniambie kama nakosea umeandika baada ya kupata maelezo ya kazi ya Jorum nilianza ufuatiliaji Isyesye mtaa wa Mwantengule, kwa maneno hayo nitakuwa sahihi nikisema kwamba ulikwenda Mwantengule ukiwa tayari unamjua P3
Coplo Amani: nilikua simfahamu
Mhe. Lissu: Kama ulikua humfahamu uliendaje moja kwa moja ukamkamata
Coplo Amani : Nilishasema nilionyeshwa na askari wa intelijensi
Mhe. Lissu: hayapo kwenye maelezo yako and it is too bad.
Mhe, Lissu: P3 ni dereva wa boda boda sio
Coplo Amani : ndio
Mhe. Lissu: Na umesema askari wa intelijensi huwa wanajichanganya hata kwa boda boda
Coplo Amani : kweli
Mhe. Lissu: sasa waambie waheshimiwa majaji kama huyu P3 sio askari wa kweli wa intelijensia
Coplo Amani : si kweli
Mhe. Lissu: umesema P3 alipanga kupiga watu mawe, kuasi nchi halafu umesema Jorum alikwambia umuachie kwa dhamana, inaingia akilini??
Coplo Amani : inaingia akilini
Mhe. Lissu: mtu anayepanga uasi na kupiga watu mawe mnampa dhamana?! Kwanin tushangae yaliyotokea October 2025!
Coplo Amani : mimi sijui bwana muulize Jorum
Mhe. Lissu: Jorum hayupo kwenye kizimba
Mhe. Lissu: kwahiyo nyinyi Polisi ndo mlipanga mambo ya October 29
Coplo Amani : Mimi sina majibu ya hilo.
Mhe. Lissu: Eleza kama umeleta pikipiki uliyomkamata nayo
Coplo Amani : sijaonyesha
Mhe. Lissu: usajili wa Bodaboda
Coplo Amani : Hakuna
Mhe. Lissu:Kadi ya bodaboda
Coplo Amani : hakuna
Mhe. Lissu: Na huyu jamaa tunamtambua kama P3, hatujui jina lake, amejificha kwenye kibox hatujamuona tutajuaje kama ni boda boda?
Coplo Amani : hayo mambo yanahusika vipi kwenye kesi hii
Mhe. Lissu: yanahusika
Mhe. Lissu: Huyu P3 ulivyomfikisha Ilomba ulimuweka mahabusu, kweli au si kweli
Coplo Amani : Si kweli
Mhe. Lissu: Naomba nimsomee shahidi kielelezo D12 jinsi P3 alivyofikishwa kituoni……”tulivyofika kituoni aliniweka mahabusu”
Sasa swali langu kati ya ushahidi wako ww na ushahidi wa P3 Mahakama ichukue upi kuwa ni ushahidi wa kweli?
Coplo Amani : hilo ni jukumu la mahakama.
Mhe. Lissu: naomba ujibu swali langu
Coplo Amani : hilo ni jibu la mahakama
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji naomba shahidi ajibu swali langu
Katuga: Waheshimiwa shahidi ameshajibu sasa kama halimpendezi basi hilo ndio jibu
Mahakama: endelea na Cross
Mhe, Lissu: Kwenye ushahidi wako kizimbani umewaambia majaji kwamba P3 alikua anahamasisha watu kupiga mawe?
Coplo Amani : ni sahihi
Mhe. Lissu: Kwanini hujalisema wakati upo kizimbani
Part 219 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 217
Anaendelea Mhe. Lissu na Cross examination.
Mhe. Lissu: Sasa shahidi ili nikuhoji vizuri naomba uwaambie waheshimiwa majaji kama upo tayari maelezo yako yapokelewe kama kielelezo
Coplo Amani : nipo tayari
Serikali: hatuna pingamizi.
Mahakama; maelezo haya yanapokelewa kama exhibit D14
Mhe. Lissu: Waheshimiwa naomba exhibit D14.
Mhe. Lissu: Sasa shahidi maelezo yako sasa ni kielelezo D14 naomba uyaangilie vizuri
Swali langu la kwanza umesema unafanya kazi katika kitengo cha upelelezi chini ya Mkuu wa upepelezi wilaya
Coplo Amani : ni kweli
Mhe. Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kama hayo maneno yapo kwenye D14
Coplo Amani : yapo
Mhe. Lissu: wapi
Coplo Amani : angalia page ya pili
Mhe. Lissu: soma
Shahidi anasoma
Mhe. Lissu: Naomba niangalie hayo maelezo na waheshimiwa majaji naomba na nyie muangalie kwenye typed.
Mhe. Lissu: naomba na mimi nisome waheshimiwa majaji, yupo sahihi kama alivyosoma ya kwangu ndio yamekosewa.
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wako shahidi umesema wewe ni msaidizi katika shughuli zote za upelelezi wilaya ya Mbeya
Coplo Amani : sahihi kabisa
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama hayo maneno yapo kwenye kielelezo D14
Coplo Amani : hayo maelezo hayapo
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wako umesema ulikua unaelezea Kituo cha polisi Ilomba ulisema ni Kituo kidogo cha polisi kilicho chini kituo cha kati cha mbeya kama out post na ukisema ivi ina maana hakija-qualify kuwa Kituo cha Polisi?
Coplo Amani : sahihi
Mhe. Lissu: kama hayo maneno yapo kwenye maeleezo yako
Coplo Amani : hayapo
Mhe. Lissu: 4 april 2024 kwa majibu wa maelezo yako ulipewa maelekezo na Jorum kwenda mtaa wa Mtengule
Coplo Amani : Kweli
Mhe. Lissu: Lakini alikupa namba ya simu askari wa intelijensia ili akuongoze ukamkamate mhalifu
Coplo Amani : sahihi
Mhe. Lissu: waambie kama hayo maneno kwamba ulipewa namba ya simu yapo kwenye maelezo yako.
Coplo Amani : hayo maelezo hayapo katika kielelezo D14
Mhe. Lissu: uliwaeleze askari wa intelijensia kama askari wanaojichanganya na raia kama vile boda boda
Coplo Amani : ni kweli
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama huo ufafanuzi wako upo kwenye maelezo yako.
Coplo Amani : hakuna
Mhe. Lissu: : Baada ya kupewa namba ya mtu wa intelijensi uliwasiliana nae na badae ulikutana nae mtaa wa Mtengule
Coplo Amani : Kweli
Mhe. Lissu: waeleze kama hayo maneno yapo kwenye maelezo yako
Coplo Amani : hayapo
Mhe. Lissu: Umesema huyo Askari wa intelijensia alikuongoza na kukuonyesha huyo mtuhumiwa katika kijiwe cha boda boda na kulikua na watu wengi, waeleze kama hayo maneno yapo kwenye statement yako
Coplo Amani : hayapo
Mhe. Lissu: Umesema taarifa ulizopewa mtuhumiwa ndiye anayehamasisha wenzake kufanya vurugu na kuzuia uchaguzi wa 2025
Coplo Amani : kweli
Mhe. Lissu: waonyeshe hayo maneno kama yapo katika maelezo yako.
Coplo Amani : hayapo
Mhe. Lissu: Sasa ushahidi wako unasema ivi baada ya kuonyeshwa huyo mtuhumiwa ulimfata na kumtoa pembeni ya kijiwe, kisha ukajitambulisha kwake kwa jina na ukamwambia tuhuma zake za kuhamasisha vurugu na kuzuia uchaguzi wa 2025, sasa angalia D14 na ueleze kama hayo maeno yapo?
Coplo Amani: hayapo.
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wako umesema, ulimueleza kuwa anahitajika kituo cha polisi Ilomba na alikubali kwenda, ni kweli au si kweli
Coplo Amani : kweli
Mhe. Lissu: Waeleze kama hayo maneno yapo katika maelezo yako D14
Coplo Amani: Ndio yapo
Mhe. Lissu: yapo wapi, utusomee?
Coplo Amani : hayapo
Mhe. Lissu: Umesema kwamba, kwenye maelezo yako tuhuma iliyokuwa inamkabili ni kinyume na kifungu cha 390, waeleze waheshimiwa majaji kama kwenye maelezo yako yapo?
Coplo Amani : hayapo.
Mhe. Lissu: umesema baada ya kumhoji alikubali kuwa anashawishi wenzake juu ya vurugu na wakati akiangalia YouTube aliona Tundu Lissu akihamasisha uasi, kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi wa 2025
Coplo Amani :Kweli
Part 218 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 216
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa Maswali ya Dodoso.
Anasimama Mheshimiwa Lissu kwa ajili ya kumfanyia Cross Examination Shahidi ambae anaitwa Coplo Amani.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa kwa kuanzia naomba nipatiwe kielelezo D12, waheshimiwa majaji haya ni maelezo ya P3.
Mhe. Lissu : Sasa shahidi naomba uwaeleze majaji kama uliandika maelezo polisi
Coplo Amani : ni sahihi
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama unaweza kuyatambua ukionyeshwa
Coplo Amani : nikionyeshwa nitaweza kuyatambua
Mhe. Lissu: naomba shahidi aonyeshwe maelezo yake aliyoandika polisi.
Coplo Amani : haya ndio maelezo yangu
Mhe. Lissu: asante sana, sasa shahidi hayo maelezo yako naomba uwaeleze majaji kama uliyaandika mwenyewe au uliandikiwa na askari mwingine?
Coplo Amani : haya maelezo niliandikiwa na askari mwingine
Mhe. Lissu: mtaje jina tafadhali
Coplo Amani : Anaitwa H9207 detective coplo Robert
Mhe. Lissu: Kwenye maelezo yako hayo waeleze majaji kama ni utaratibu mtu anayeandika maelezo ya shahidi hawezi akawa ndio mtu huyohuyo kama shahidi?
Coplo Amani : ni sahihi
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji pamoja na majibu mazuri ya shahidi huyu nataka ku-impeach credibility yake, nitamsomea maelezo yake, nitamuonyesha maeneo nitakayotaka kumuuliza maswali halafu nitamtaka ayawasilishe kama kilelezo.
Mhe. Lissu anamsomea maelezo yake
Mhe. Lissu : Haya ndio maelezo yako kama nilivyoyasoma?
Coplo Amani : Waheshimiwa majaji mshtakiwa kuna maeneo amekosea naomba nimrekebishe, sio kata ya Isuesue ni Isyesye 😁
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji kwakua na nyie mnarekodi hii mimi nimeona imeandikwa isuesue waheshimiwa…
Kwenye maneno “ni dereva wa bodaboda isuesue Mwintengule”… kwenye original Isyesye… kwahiyo tutaenda na ya kwako.
Kuna eneo lingine ambalo lina shida?
Coplo Amani : hapana.
Mhe. Lissu : Sasa kuna maeneo nataka kukuhoji kwa ajili ya kukukanusha kama ifuatavyo;
1. Kwamba unafanya kazi chini ya OCCID Mbeya mjini
2. Kwamba wewe ni msaidizi wa upelelezi ndani ya Mbeya mjini
3. Umeelezea Kituo cha Polisi cha Ilomba kwamba ni kituo kidogo kilichopo chini ya kituo cha Kati Mbeya umesema ni kama out post.
4. Umeeleza kwamba kaimu OCCID Inspekta Jorum alipokupa maelekezo ya kwenda kumkamata P3 alikupa namba ya simu ya askari wa kitengo cha intelijensia kwa ajili ya kwenda kumkamata P3
5. Kwamba hawa askari huwa wanajichanganya na raia kama dereva boda boda n.k
6. Baada ya kupewa namba ya simu ukawasiliama nae na mkakutana Isyesye.
7. Kwamba kulikua na watu wengi na mlipita na akakuonyesha mtuhumiwa kwenye kituo cha boda boda.
8. Taarifa mlizopewa na Jorum ni mtuhumiwa ndiye anayehamasisha wenzake kufanya vurugu uchaguzi wa 2025
9. Baada ya kuonyeshwa huyo mtuhumiwa ulimfata na kumtoa pembeni ya kijiwe na kisha ulijitambulisha kwake kwa jina na kumueleza tuhuma zake.
10. Ulimwambia baada ya kumtoa pembeni kwamba anahitajika Kituo cha Polisi Ilomba na yeye alikubali kwenda.
11. Ni ushahidi wako maelezo aliyoandika mtuhumiwa ni uchochezi, kusababisha vurugu na kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025.
12. Shitaka uliloandika lilikua ni kukiuka masharti ya kifungu cha 390 cha Penal code
13. Wakati ukimhoji alikwambia kwamba aliona taarifa kwenye YouTube akamuona Lissu akiwa anahamisisha uasi, kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi 2025.
14. Baada ya kuandika maelezo yake ulimjulisha inspeka Jorum akakuelekea kumuachia kwa dhamana na we anaripoti kila baada ya siku tatu
15. Ni ushahidi unaohusu tareh 17 april 2025 kwamba siku hiyo wakati ukiwa Ilomba Kituo cha Polisi ulielekezwa na inspekta Horum kuandika maelezo ya mtuhumiwa kama shahidi kuhusiana maelezo ya Mwenyekiti wake Tundu Lissu na yeye kuwa mstari wa mbele kuhamasisha vijana wenzake kufanya vurugu.
16. Baada ya kurekodi malezo hayo na ulimjulisha Inspekta Jorum na ukamkabidhi malezo hayo.
Part 217 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 215
Katuga anaendelea kumuongoza Shahidi ambae ni Coplo Amani
Wakili wa Serikali: Kikafuata nini?
Coplo Amani: Baada ya kuonyeshwa mtu huyo, nilimfata na nikamuita nikamtoa eneo hilo la bodaboda tukakaa pembeni kidogo, nikajitambulisha kwake kwamba mimi ni G9304 natoka Kituo cha Polisi kati Mbeya, baada ya hapo nilimueleza tuhuma yake ya kuhamsisha vurugu na kuharibu uchaguzi wa 2025.
Wakili: Uchaguzi ulihusu nini?
Coplo Amani : Uchaguzi ulikua unahusu rais, wabunge pamoja na madiwani.
Wakili: Ukafanya nini?
Coplo Amani : Baada ya kumueleza tuhuma zake nikamueleza kwamba anahitajika Kituo cha Polisi Ilomba.
Wakili: kikafuata nini?
Coplo Amani : Baada ya hapo hakubisha na alikubali kwenda kituo cha polisi Ilomba.
Wakili: ukafanya nini?
Coplo Amani : niliondoka nae mpaka Kituo cha Polisi Ilomba
Wakili: ukafanya nini?
Coplo Amani : Baada ya kufika kituo cha Polisi nilimjulisha Inspekta Joram, akanipa maelekezo ya kumuandika mtuhumiwa maelezo.
Wakili: anaitwa nani huyo mtuhumiwa?
Coplo Amani: Mtuhumiwa huyo katika shauri hili anajulikana kama P3.
Wakili: Ikawaje?
Coplo Amani : Nilimuandika maelezo kwa tuhuma za uchochezi na kuhamasisha kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025.
Wakili: Nini kikafuata?
Coplo Amani : Baada ya hayo maelekezo nilimuandika maelezo kama nilivyoelekezwa na nilimuandika maelezo kama mtuhumiwa.
Wakili: kwa kosa gani?
Coplo Amani : makosa hayo ni kinyume cha kifungu cha 390 cha sheria ya kanuni ya adhabu
Wakili: Ikawaje?
Coplo Amani :. Baada ya kumhoji mtuhumiwa alinieleza kwamba ni kweli alihamasisha wenzake kufanya fujo na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025
Wakili: Nini Kingine?
Shahidi: Pia alinieleza siku hiyo ya tarehe 4 April 2025 alikua akipitia taarifa mbalimbali na wakati anaendelea kupitia taarifa kwenye mtandao wa youtube alisikia mtu ambaye alimtaja kama Mwenyekiti wa CHADEMA anayeitwa Tundu Antiphas Lissu akiomgea na kutoa kauli za kuhamasisha uasi, kufanya vurugu na kuharibu Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Wakili: kikafuata nini?
Coplo Amani : Baada ya kumaliza kumuandika maelezo nilimjulisha Inspekta Joram na akanipa maelezo kwamba mtuhumiwa adhamimiwe na aripoti kituo cha polisi Ilomba na aripoti kila baada ya siku tatu.
Wakili: nini kilifanyika Tarehe 17 April
Coplo Amani : Tarehe 17 april 2025 nikiwa kituo cha polisi Ilomba nilipewa maelekezo na Inspekta Joram ya kuandika maelezo kama shahidi.
Wakili: Kingine?
Coplo Amani : Nilipewa maelekezo ya kumwandika kama shahidi kuhusiana na kile alichoeleza kwenye maelezo yake kwamba aliona mwenyekiti wake wa CHADEMA akihamasisha vurugu na kuharinubuchaguzi mkuu wa 2025 na kwamba baada ya kuona kauli ile yeye kama mfuasi wa CHADEMA, alihamasika kutokana na kauli zile na alikua tayari kuwashawishi vijana wenzake kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025.
Wakili: Baada ya hapo?
Coplo Amani : Baada ya kumaliza kumuandika maelezo nilimjulisha Inspekta Joram.
Wakili: Ukafanya nini?
Coplo Amani : Hayo maelezo nilimkabidhi inspekta Joram.
Wakili wa Serikali : Waheshimiwa majaji ni hayo tu kwa shahidi huyu.
Part 216 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.