Kila anayepambana kwa Nguvu zake mwenyewe bila Support ya wazazi au Ndugu Kiuchumi Mwenyezi Mungu ampe Haja ya moyo wake na amzidishie Nguvu ya kupambana na kutokata Tamaa amuondolee vikwazi vya kila namna Amen!
#SisindowaletunaosaidiwanaMungu@Joy_Mbura
Hii ni TUNDUMA wanangu.
Na hii ni nyomi ni baada ya MKURUGENZI kuleta UHUNI wake wa kuhamisha eneo la mkutano kutoka Tunduma MJINI na kuuhamishia 15KM nje ya mji.
Lakini UMBALI SIO ishu ya kuzuia watu kufuata IBADA YA HAKI. Asante sana CHADEMA kwa kuleta injiri kwenye mkoa wetu ambao tulipoteza ndugu zetu wengi sana kwenye maandamano ya MO29.
Asante wapenda haki wote mlioshiriki IBADA HII YA HAKI na poleni kwa USUMBUFU wa wakoloni weusi.
REPOST 200
#KatibampyaFreeTunduLissu
#FreeTunduLissu
Mmeona #ToneTone la Mbeya?🙌
Imagine watu wamekuja kwenye mkutano wetu kwa nauli zao, hawajasombwa kwenye mafuso kama akina mwafulani.😂😂😂
Halafu baada ya kusikiliza Nondo za Viongozi wa Chama, wametuchangia na pesa kutuzesha ili tuendelee kuhubiri Injili ya Ukombozi wa Taifa letu
Huu ni upendo wa kiwango cha juu sana, watu wa Mbeya peponi moja kwa moja🙏❤️dhambi zenu apewe Nduli Idd Amin Mama na familia yake.
Omba msamaha kama ulisema Cristiano Robaldo ameisha. Record breaker, history maker, CR7 amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga kwenye michuano ya World Cup Sita tofauti. Respect kwa huyu GOAT, tena ndo kwanza ameanza mashindano rasmi. Hawa Ureno wakitulia ni timu hatari sana.
Asubuhi hii Mlowo imetupokea kwa furaha namna raha.
Nimefurahi kuongea na wananchi wa Mlowo na jimbo la Mbozi.
Watanzania wako tayari kwa mabadiliko makubwa ya uongozi.
Tofauti na mitazamo ya baadhi ya wanachama wa CCM na wachambuzi wa siasa waliokuwa wakidai kuwa CHADEMA imepoteza mvuto na inaelekea ukingoni mwa siasa za Tanzania, ziara ya viongozi wake wakuu katika mikoa ya Mbeya na Njombe imeonesha picha tofauti baada ya maelfu ya wananchi kujitokeza katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo.
Ziara hiyo inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara @HecheJohn pamoja na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, imevutia umati mkubwa wa wananchi waliofurika katika viwanja vya mikutano tangu saa kadhaa kabla ya viongozi hao kuwasili.
Katika baadhi ya maeneo, wananchi walionekana wakisongamana kandokando ya barabara na viwanja vya mikutano ili kupata nafasi ya kusikiliza ujumbe wa viongozi hao.
Mbali na mahudhurio makubwa, jambo lililoibua mjadala ni mwitikio wa wananchi katika uchangishaji wa fedha za chama kupitia kampeni ya “Tone Tone”, mamia ya wananchi wakionekana kujitokeza kwa hiari kutoa michango yao, huku wengine wakisukumana kuelekea jukwaani ili kukabidhi michango yao mbele ya viongozi wa chama hicho.
Baadhi ya wananchi waliozungumza baada ya mikutano hiyo walisema wamehamasishwa na ujumbe wa viongozi wa CHADEMA kuhusu demokrasia, uwajibikaji na mustakabali wa taifa, hali iliyowafanya waone umuhimu wa kuchangia shughuli za chama. Walisema michango yao, licha ya kuwa midogo kwa baadhi yao, ni ishara ya kuunga mkono harakati wanazoamini kuwa zina manufaa kwa jamii.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema mwitikio huo katika mikutano ya Mbeya na Njombe unaonesha kuwa ushindani wa kisiasa nchini unaendelea kuwa hai, huku vyama vya upinzani vikionesha uwezo wa kuhamasisha wananchi na kukusanya rasilimali kupitia michango ya wanachama na wafuasi wao.
The time has come to release Tundu Lissu and pack your bags and go! Contrary to what Kombo, Nyalandu and Kabudi are telling you, this is it! Your illegitimate presidency is now obvious to the world and there is not path to legitimacy!
#SamiaMustGo
Huku Brussels “BUNGE LA ULAYA” leo linapiga kura wanangu.🔥🙌🏿
Huyu DIKTETA JIKE dunia imemkataa kama MAITI YA FARAO.
TUTAKUWEPO KUSHEREKEA HAPA HAPA.
REPOST 200
Kamati ya Mahusiano ya Nje ya Seneti ya Marekani imepitisha muswada unaotaka kufanyika kwa tathmini ya kina ya uhusiano kati ya Marekani na Tanzania kufuatia kile kilichoelezwa kuwa ni ongezeko la matukio ya vurugu za kisiasa na kudorora kwa misingi ya demokrasia nchini Tanzania.
Muswada huo wa pande mbili za kisiasa, ulioandaliwa na Seneta Jeanne Shaheen kwa kushirikiana na Seneta Ted Cruz, unaielekeza Serikali ya Marekani kufanya mapitio ya kina ya ushirikiano wake na Tanzania pamoja na kutathmini athari za mwenendo wa kisiasa wa nchi hiyo kwa maslahi ya Marekani katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
"Muswada huo utahitaji kufanyika kwa mapitio ya kina ya uhusiano wa Marekani na Tanzania kufuatia ongezeko kubwa la vurugu za kisiasa na kurudi nyuma kwa demokrasia nchini Tanzania. Pia utaelekeza tathmini ya uhusiano unaokua wa Tanzania na China na Urusi, pamoja na athari zake kwa maslahi ya kimkakati na kiuchumi ya Marekani katika Afrika Mashariki." Imesema sehemu ya muswada huo.
Kwa mujibu wa maelezo ya muswada huo, tathmini hiyo pia itachunguza kwa kina uhusiano unaokua kati ya Tanzania na mataifa ya China na Urusi, huku ikipima athari zake kwa maslahi ya kimkakati na kiuchumi ya Marekani katika eneo hilo.
Akizungumza baada ya kamati hiyo kupitisha miswada mbalimbali ya sera za nje, Seneta Shaheen alisema hatua hiyo inaonesha dhamira ya Kamati ya Mahusiano ya Nje ya Seneti katika kuimarisha uongozi wa Marekani duniani, kulinda usalama wa taifa na kuhakikisha sera za nje zinawanufaisha wananchi wa Marekani.
Iwapo muswada huo utapitishwa na Bunge la Marekani na kutiwa saini kuwa sheria, utailazimu Serikali ya Marekani kuwasilisha tathmini rasmi kuhusu hali ya uhusiano wake na Tanzania pamoja na mwelekeo wa kisiasa na kidiplomasia wa nchi hiyo katika mazingira ya ushindani wa kimataifa unaohusisha mataifa makubwa kama China na Urusi.
Maamuzi haya yamefikiwa Juni 17, 2026 wakati Kamati ya Mahusiano ya Nje ya Seneti ya Marekani (Senate Foreign Relations Committee) ilipokutana na kupitisha miswada kadhaa ya sera za nje, ikiwemo huu wa Reassessing the United States–Tanzania Bilateral Relationship Act inayohusu Tanzania.
Muswada wenyewe uliwasilishwa kwa mara ya kwanza Mei 19, 2026 na Maseneta Jeanne Shaheen na Ted Cruz na Juni 17, 2026 Kamati ya Mahusiano ya Nje ya Seneti iliupitisha (advance) muswada huo kutoka ngazi ya kamati kwenda hatua inayofuata ya mchakato wa kutungwa sheria.
Mwakilishi wa ACT-Wazalendo wa Jimbo la Gando Pemba, Said Ali Mbarouk ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia nafasi za uwakilishi, ameitaka Serikali ya Muungano kufanyia marekebisho utaratibu wa Zanzibar kukopa fedha kwa ajili ya maendeleo.
Akichangia mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inayoendelea kujadiliwa leo Juni 18, 2026 Mbarouk amesema Zanzibar imekuwa ikikumbana na changamoto ya kuhitaji idhini kutoka Tanzania Bara kila inapokusudia kukopa, hali anayodai wakati mwingine husababisha kucheleweshwa au kukwamishwa kwa mipango ya maendeleo.
Amesema utaratibu huo umekuwa ukileta “chenga za kifedha” na kuathiri kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kisiwani humo, hivyo akataka kuwepo kwa mjadala wa kina kuhusu namna Zanzibar inavyoweza kuwa na uhuru zaidi wa kifedha ndani ya mfumo wa Muungano.
Aidha, amegusia suala la ongezeko la deni la Taifa la Zanzibar, akieleza kuwa baadhi ya Taasisi zimekuwa zikibanwa kifedha, hali inayoweza kuathiri utekelezaji wa shughuli nyingine za Serikali.
#MillardAyoUPDATES
Now that the bill has passed committee and moves to the next stage, we will continue to keep you updated on its progress. Kazi itaendelea. 🙏🏾
The Reassessing the United States–Tanzania Bilateral Relationship Act has passed the Senate Foreign Relations Committee. 💪🏽🇺🇸🇹🇿
Calling all diaspora to continue reaching to your senates to make sure they all know the truth of what happened in Tanzania and what continue to happen. Keep speaking truth, don’t relax because the bill passed one stage- keep pushing for justice.
Interestingly, the partisan bill passed while Kombo is in Washington, D.C., advancing his government’s narrative, Go figure. Wananchi, Please always confirm actual facts na siyo picha za propaganda au story za magazeti yanayoambiwa cha kuandika.
As Congress noted, Tanzania’s growing ties with China and Russia, coupled with concerns over democratic governance, human rights, and regional stability, continue to draw international attention. Safari na picha za urusi yaani zililetwa tukiwa conference room za senates-Ahem.
Ulaya nao-On June 3, committees of the European Parliament voted 81–1, with four abstentions, to oppose a proposed €156 million funding package for Tanzania, citing concerns arising from the aftermath of the October 2025 elections and broader human rights issues.
They are using taxpayers’ money. We used truth, testimony, evidence, and prayers.
Bottom line will be justice and accountability. Till justice, till accountability.
The journey is not over, but today, truth moved one step closer to justice and accountability. FACTS✅
Mwakilishi wa ACT-Wazalendo wa Jimbo la Gando Pemba, Said Ali Mbarouk ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia nafasi za uwakilishi, ameitaka Serikali ya Muungano kufanyia marekebisho utaratibu wa Zanzibar kukopa fedha kwa ajili ya maendeleo.
Akichangia mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inayoendelea kujadiliwa leo Juni 18, 2026, Mbarouk amesema Zanzibar imekuwa ikikumbana na changamoto ya kuhitaji idhini kutoka Tanzania Bara kila inapokusudia kukopa, hali anayodai wakati mwingine husababisha kucheleweshwa au kukwamishwa kwa mipango ya maendeleo.
Amesema utaratibu huo umekuwa ukileta “chenga za kifedha” na kuathiri kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kisiwani humo, hivyo akataka kuwepo kwa mjadala wa kina kuhusu namna Zanzibar inavyoweza kuwa na uhuru zaidi wa kifedha ndani ya mfumo wa Muungano.
Aidha, amegusia suala la ongezeko la deni la Taifa la Zanzibar, akieleza kuwa baadhi ya Taasisi zimekuwa zikibanwa kifedha, hali inayoweza kuathiri utekelezaji wa shughuli nyingine za Serikali.
Waridhiane na nani? Hivi hawana hata chamber ya aibu hawa?
Kuna tetesi akiwa RC Mbeya anajua Redrack Chaula na Dioniz Kipanya walivyopotea maridhiano si yaanze kwa kuwaweka huru?
Bila Lissu na wote waliotekwa na walio mahabusu kuachiwa hakuna maridhiano.
🇪🇺 Bunge la Ulaya lapinga mpango wa kutoa msaada wa Euro milioni 156 (takribani TZS bilioni 484) kwa Tanzania mwaka 2026.
“Who are you” wanaendelea kujitambulisha wao ni wakina nani.
Mwaga moto mwingi wanangu kama madragon.🔥🔥🔥
REPOST 200
UNAPOSHINDWA KUJISIMAMIA, KUTII SHERIA NA KUWALINDA RAIA WAKO, JUMUIYA YA KIMATAIFA NA MAJIRANI WANA WAJIBU WA KIUTU WA KUKUKUMBUSHA NA KUKUTAKA UFANYE HIVYO.
Matukio ya Oktoba 29, 2025 yalikuwa mauaji ya kinyama, ya kifashisti na shambulio kubwa dhidi ya raia wengi wasio na hatia. Huu ni ukweli ambao historia itaendelea kuubeba, na hakuna propaganda wala upotoshaji unaoweza kuufuta.
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba badala ya kutafakari kwa kina, kukubali makosa yaliyotokea na kutafuta njia ya haki ya kuponya taifa, baadhi yetu tunaendelea kuzunguka kwenye propaganda za kijinga na simulizi za kujidanganya.
Kama alivyotuasa Bob Marley:
“You can fool some people sometimes, but you can't fool all the people all the time.”
Ukweli unaweza kucheleweshwa, lakini hauwezi kuzimwa milele.
Tusipojirekebisha, tusipojiwajibisha, na tusipojenga misingi ya haki, ukweli na uwajibikaji, tutadhibitiwa na mazingira tuliyoyatengeneza wenyewe.
Tuwaunge Mkono Shaheen na Wenzake wote wenye mapenzi mema na Taifa hili na wanaotaka uwajibikaji.
Njia pekee ya kulikwamua Taifa kutoka katika mkwamo huu si propaganda, si vitisho, wala si kuficha ukweli. Njia pekee ni HAKI, UKWELI na UWAJIBIKAJI.
Bila hayo, hakutakuwa na maridhiano ya kweli.
Bila hayo, hakutakuwa na amani ya kudumu.
Bila hayo, hakutakuwa na Taifa lenye umoja na heshima.
Tusipojidhibiti, tutadhibitiwa. Historia imethibitisha hilo mara nyingi.
BAK MWABUKUSI.
Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Jackson Kiswaga, ameishauri Serikali kubana matumizi yasiyo ya lazima, hususan matumizi ya misafara mikubwa ya magari katika ziara za viongozi wa ngazi ya Mawaziri, akisema yanachangia kuongeza gharama zisizo na tija kwa taifa.
Akichangia mjadala wa Hotuba ya Mapitio ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Kiswaga alisema ipo haja ya Serikali kuangalia upya matumizi ya rasilimali ili kuelekeza zaidi fedha kwenye maendeleo.
Kiswaga alieleza kuwa ni vigumu kuelewa sababu ya msafara mkubwa wa magari unaofikia hadi 30 kwa ziara za Mawaziri mikoani, akisema hali hiyo ni mzigo kwa walipa kodi na haiakisi uhalisia wa ufanisi unaohitajika serikalini.
“Hakuna sababu ya kwenda kukagua miradi na magari 30, au Waziri kwenda kufanya ziara mkoani akiwa na msafara wa magari 30. Hii yote ni ufujaji wa fedha. Hatuna sababu ya kufanya hivyo,” alisema Kiswaga Bungeni.
Ameongeza kuwa Serikali inapaswa kuweka mkazo katika matumizi yenye tija na kuhakikisha kila shilingi inatumika kwa uangalifu, hasa katika kipindi ambacho wananchi wanahitaji huduma na miradi ya maendeleo kuharakishwa.
Mbunge huyo pia alisisitiza kuwa nidhamu ya matumizi ya fedha za umma ni muhimu ili kuhakikisha rasilimali za taifa zinaelekezwa katika maeneo ya kipaumbele kama afya, elimu na miundombinu badala ya matumizi ya kifahari au yasiyo ya lazima.
They tried to bury you, they didn’t know you were a seed!
Stay strong Tundu Lissu
Hii vita imekaribia mwisho na umeshaweka historia ya kipekee! Kupitia mateso yako, tumepata njia na haki itapatikana! Mungu yu pamoja nasi
#FreeTunduLissu