@George_Ambangil Wakati naanza kushabikia mpira back 2003 mchambuz wangu bora alikuwa Dr. Leaky na Ezekiel Malongo. Nakumbuka enzi za Uefa Channel 10 na kwenye kipindi cha michezo pale rtd. Imepita miaka mingi kuja kupata mchambuzi bora kwangu ambaye ni wewe. Sikio langu litamiss madini yako bro
Watu walikuwa wakifurahia Iran kufunga mlango wa Hormuz wakasema Iran anampelekea moto Us sasa hivi moto tunapelekewa sisi Us kasema tukachukue mafuta wenyewe 😂😂😂😂 Iran tuonee huruma
In the last decades, #Africa has had great men like the late Nkrumah, Samora Machel, Julius Nyerere, & Nelson Mandela. All of them were involved in struggle against oppression. We're deeply fond of #Africa because this region has always stood up against oppression.
Dec. 9, 1997
UTARATIBU WA MKRISTU MKATOLIKI KANISANI
•Unapoingia Kanisani, chovya maji ya baraka na kusema:
"Unitakase Ee Bwana uovu wangu wote, ili nipate kushiriki ibada takatifu: Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu Amina!
•Kama Kanisani kuna Ekaristi Takatifu iliyohifadhiwa katika Tabernakulo, piga goti huku ukisali: "Bwana wangu na Mungu wangu". Haya ni maneno aliyotamka Tomaso baada ya kumwona Yesu Mfufuka (Yoh 20:28).
•Ukiinuka sali: "Nitakusifu na kukuabudu katika Ekaristi takatifu"
•Nenda mpaka kwenye kiti, piga magoti huku ukitoa nia yako ya kusali Misa siku hiyo, mfano:
"Ee Mungu, ninaungana na jeshi la mbinguni, pamoja na Bikira Maria, nikiwa na nia ya kumwombea mama yangu ambaye ni mgonjwa, jirani yangu ambaye hatuelewani na pia familia yetu ambayo haina amani. Kwa Sadaka hii ya Misa Takatifu, mponye mama yangu, leta uelewano na jirani yangu, na pia rejesha amani ya familia yetu pamoja na familia zote ambazo hazina amani"
NB: KILA MISA UNAYOSHIRIKI HAKIKISHA UNA NIA YAKO NA UINGANISHE NA SADAKA HIYO YA MSALABA. USISHIRIKI MISA KAMA MTAZAMAJI BILA KUWA NA NIA YAKO MOYONI.
•Endelea na ibada ya Misa na Kushiriki Litrujia kikamilifu.
NB: Hakikisha unashiriki kikamilifu kwa kuimba, kuitika kwa sauti, kusimama, kupiga magoti nk kwa uchangamfu.
Misa huwa tunashiriki wote kwa pamoja lakini MATUNDA YA MISA kila mmoja anapokea tofauti kulingana na jinsi alivyoshiriki.
Kama ni kwa asilimia, basi sio wote huwa tunapata asilimia zinazolingana za neema kwenye Misa. Kuna wanaopata neema nyingi zaidi, wanaopata kidogo nk kulingana na maandalizi ya moyo na ushiriki hai katika kupokea matunda ya adhimisho lenyewe.
Kama ni bomba linalotiririsha maji, basi kila mmoja wetu ni mtekaji akiwa na chombo chake. Wingi wa maji (Neema) utakaoingia ndani ya chombo (Roho/moyo) utategemea:
1. Chombo chako kipoje wakati unateka hayo maji
2. Nafasi (kama ndani ya chombo nafasi ni ndogo, ndivyo na maji yatakavyoingia machache. Kama nafasi ni kubwa, ndivyo na maji yatakavyoingia mengi. Kama moyo umejaa hauna nafasi, ndivyo na Neema hazitaingia kabisa kwasababu hazina sehemu ya kuingia)
3. Umekiwekaje bombani ili maji yaingie ndani (hapa sasa ndio USHIRIKI HAI katika adhimisho.
Hivyo, tuliza akili na moyo wakati wa Misa, na shiriki kikamilifu Liturujia hatua kwa hatua.
Ndiposa kila mmoja anapokea neema za Misa kwa kadiri ya maandalizi aliyofanya na ushiriki anaoonyesha wakati wa adhimisho.
NB: Utofauti wa kupokea matunda ya adhimisho la Misa haupo kwa mtoaji (Yesu) bali kwa mpokeaji (Anayeshiriki). Utofauti wa maji tunapoenda bombani kuteka, haupo kwa bomba linalotoa maji, bali kwa aina ya chombo na utayari wa mhusika kuteka maji hayo.
Tuendelee
•Wakati wa Kupokea Ekaristi (Komunyo) ukikumbuka kuwa una dhambi kubwa (ya mauti), komunika kwa sala ya tamaa. Usithubutu KAMWE kupokea Ekaristi ukiwa na dhambi ya mauti.
"Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo. Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana. Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe. Maana alaye na kunywa, HULA NA KUNYWA HUKUMU YA NAFSI YAKE, KWA KUTOKUUPAMBANUA ULE MWILI. Kwa sababu hiyo wako WENGI KWENU WALIO HAWAWEZI NA DHAIFU, NA WATU KADHA WA KADHA WAMEKUFA." (1 Kor 11:26-30)
Hivyo, usipokee Ekaristi ukiwa na dhambi. Baki upokee kwa tamaa ya moyo. Jisikie wivu Mtakatifu wakati huo, na jitahidi ujitakase kwa kuungama ili adhimisho lingine usikae tena bila kupokea.
•Mwisho, wakati wa kuondoka chovya maji ya baraka na ujibariki. Kwa kuwa baada ya adhimisho huwa tunapaswa kwenda kuishi kile tulichoadhimisha, waweza kusali sala ya binafsi "Unilinde Ee Mwenyezi Mungu, nikapate kuwa mfano katika jamii yangu, na nikushuhudie katika matendo yangu"
Hapo unachovya maji ya baraka na kufanya ishara ya Msalaba "Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina"
Tumsifu Yesu Kristu. Mungu akubariki