Wengine background zetu ndo zinatufanya tusipige hatua haraka haraka kama mnavyodhania nyie, pengine kosa letu kubwa ni kutaka kupatengeneza kwanza tulipotoka kabla hatujajitengenezea sisi💔🥲
~Wazee wa Sumbawanga✍️
#BREAKINGNEWS
Wakili wa Serikali mkuu Nassoro Katuga anaiambia Mahakama kuwa upande wa Jamhuri umeoana ushahidi ambao umekwishatolewa unajitosheleza hivo basi hakuna sababu ya kuongeza ushahidi mwingine. Jamhuri wanaomba kufunga ushahidi wao kwa idadi ya mashahidi hao 17. @TunduALissu
Kutafuta haki si kiburi. Ujasiri wa kuitafuta haki si uadui.
Na kumwachia Mkt. Lissu si kushindwa. Kinyume chake, huenda ukawa ni ushindi mkubwa wa Taifa na hasa kwenu ninyi Serikali.
Wakati mwingine, busara si kushikilia mtu kwa nguvu. Busara ni kutambua wakati wa kumwachia. Nchi haiwezi kujengwa kwa visasi au kwa kutafuta nani ameshinda na nani ameshindwa.
Msilifanye suala hili kuwa personal. Kesi hii ni kubwa kuliko mtu mmoja, chama kimoja au Serikali ya wakati mmoja. Inahusu haki, utawala wa sheria, amani na mustakabali wa nchi yetu.
Kataeni ushauri wa wahafidhina wanaowaambia kuwa kumwachia Lissu ni udhaifu. Wakati mwingine, uamuzi wa busara unaohitaji ujasiri zaidi ni ule wa kuachilia kuliko kushikilia.
Muwe wakubwa kuliko hasira, wakubwa kuliko visasi, na wakubwa kuliko ushindani wa kisiasa. Mumwachie Mkt. Lissu. Msiogope, kwa sababu tu mtatafsiriwa kama mmelegea. Kuna nyakati ambazo kumwachia mmoja ni kuifungua nchi nzima.