Ukiwa muungwana sana watakutumia.
Ukiwa muelewa sana watakudanganya.
Ukiwa mkweli sana watakukwepa.
Ukiwa mnyenyekevu sana hawatakusemea.
Ukiwa imara sana watapambana kukudhoofisha.
Ukipatikana sana hawataona thamani yako.
Ukisamehe sana hawatabadilika.
Ukiwavumilia sana watakuzoea.
Kiasi ni muhimu.
Ukizidisha hata yalo’ mema unaumia.