Human Rights, Activist, for Loliondo Indigenous Rights &Land I Believe in Justice, democracy,rule of Law & people's progress, University of Iringa(UOI) Alumni
I wish you my brother, @PatricOleSosopi happy birthday. You are a champion and a fighter for Human Rights, a true advocate for Democracy, and a fighter for genuine freedom and the progress of people I wish you many more years, continuing to be the voice of the voiceless.
I wish you my brother, @PatricOleSosopi happy birthday. You are a champion and a fighter for Human Rights, a true advocate for Democracy, and a fighter for genuine freedom and the progress of people I wish you many more years, continuing to be the voice of the voiceless.
KIUMBE HUYU NI MZIGO.
Mtu ‘anayejiita mbunge’ anasema Serikali ya CCM imeongeza bei kidogo sana ya mafuta kulinganisha na Kenya. Huyu mtu hajajishughulisha vya kutosha.
Huwezi kulinganisha uchumi wa nchi na nchi kwa kutaja tarakimu tu. Kulinganisha uchumi wa Tanzania na Kenya anatakiwa kutumia vipimo viwili vikuu ambavyo ni;
GDP per Capita (Pato la Taifa kwa kila kichwa) na GDP per Capita PPP (Pato la Taifa kwa kuzingatia Uwezo wa Kununua - Purchasing Power Parity). Zingatia hivyo.
1.GDP Per Capita (Nominal); Hiki ni kipimo cha thamani ya fedha ya bidhaa na huduma zote zinazozalishwa nchini, ikigawanywa kwa idadi ya watu katika nchi.
GDP (pato la Taifa) inatumia viwango vya soko vya kubadilisha fedha (USD). Hii hutumia viwango vya soko vya kubadilisha fedha (market exchange rates).
Tofauti na Tanzania ambayo uchumi wake unategemea zaidi rasilimali za asili (kama madini), Kenya imejenga msingi wake katika sekta ya huduma na ubunifu.
Kenya ni kiongozi wa kidijitali barani Afrika, jambo lililoipa jina la utani la “Silicon Savannah.” Mapinduzi ya huduma za kifedha kwa njia ya simu yalianzia hapa.
Nairobi ni makao makuu ya makampuni makubwa ya teknolojia duniani (Google, Microsoft, na Amazon) yanayofanya shughuli zake katika bara la Afrika.
Benki za Kenya (kama Equity na KCB) zimepanuka na kutawala soko la kanda ya Afrika Mashariki na Kati, zikiwa na matawi nchini DRC, Rwanda, South Sudan
Uchumi wa Tanzania kwa sasa unapitia kipindi cha mpito ambapo matokeo yake katika thamani ya sarafu na soko la kimataifa yanachukua muda sana kuonekana.
Tanzania inasafirisha madini ghafi. Thamani kubwa ya soko inabaki nchi za nje ambako madini hayo yanasafishwa na kutengeneza bidhaa za mwisho.
Thamani halisi inayobaki ni asilimia ya mirahaba na kodi, wakati thamani kubwa ya soko la madini hupimwa masoko ya hisa ya kimataifa (London au Toronto).
Uchumi wa Tanzania una sehemu kubwa sana ya sekta isiyo rasmi inayozalisha fedha nyingi, lakini hazionekani kwenye takwimu rasmi za thamani ya soko la kidunia.
Kwa wastani, raia mmoja wa nchi ya Kenya anaonekana kuzalisha thamani ya fedha karibu mara mbili ya raia mmoja wa Tanzania katika soko la kimataifa.
2.Purchasing Power Parity (PPP); Hiki ni kipimo cha “uwezo wa kununua.” Kinarekebisha tofauti za gharama za maisha na bei za bidhaa kati ya nchi hizi mbili.
Kwa mfano, kama $1 inaweza kununua mikate miwili Tanzania lakini kwa bei hiyo, unaweza kununua mkate mmoja tu nchini Kenya, PPP inazingatia ukweli huo.
Kenya ina kipato kikubwa, gharama za maisha ni kubwa. Tanzania ina gharama ndogo za maisha baadhi ya sekta (vyakula vya asili na baadhi ya huduma za kijamii).
Kenya ina sekta ya huduma (Banking, Tech, Tourism) iliyoendelea zaidi, ambayo huzalisha thamani kubwa ya fedha. Tanzania inategemea zaidi Kilimo na Madini.
Kenya imekuwa kitovu cha kibiashara (Regional Hub) kwa muda mrefu, jambo linalovutia makampuni mengi ya kimataifa kufanya uwekezaji mkubwa Kenya.
Kwa sasa nchini Kenya, bei za mafuta zilizotangazwa na Mamlaka ya Kudhibiti Nishati na Petroli (EPRA) zinazotumika hadi Aprili 2026 kwa Mombasa;
Petroli (Super Petrol) KSh 189.60 kwa lita (Tsh3,771. Dizeli (Diesel) KSh 173.10 kwa lita (Tsh 3,452). Mafuta ya Taa (Kerosene) KSh 163.00 kwa lita (Tsh 3,253).
Hizo habari lita moja ya mafuta ya petroli Kenya inauzwa Tsh 5,450 ametoa wapi? Au amesogezewa kipeperushi na KIHONGOSI kutoka ma’group yao ya WOSAPU?
Mtu ambaye anayejiita ‘mbunge wa CCM’ alitakiwa apitishe ubongo wake maeneo hayo, halafu ajenge hoja zake. Vinginevyo ni MPUMBAVU mwenye ujasiri.
Hii ishu ya kupiga hela ya uwanja Arusha ambao unajulikana kama Samia ilikuwa ni mchongo wa muda mrefu tu. Wakati Makonda anateuliwa, aliambiwa kuna kazi anakwenda kufanya kule Arusha. Kuna mtu amewahi kuona ni kazi gani alikwenda kufanya Makonda maalumu? Makonda alipofika Arusha, akatajirika, akawa anaishi hotelini na kubadilisha magari ya kifahari. Mnafikiria ile ilikuwa ni pesa ya Halmashauri? Na hakuna CAG report yoyote imeona?
Kazi maalumu ilikuwa ni huo uwanja wa Arusha.
Wakati Samia anaingia madarakani, alikuta kuna ujenzi wa uwanja Dodoma, Magufuli Stadium (Morocco spends $100 million to construct a stadium in Tanzania https://t.co/gzgAWsCkDw). Kulikuwa na mikataba tayari na mkandarasi alingia site na kusafisha uwanja.
Hapo ndipo wajanja walipoingia kwa kusema unajenga vipi Magufuli Stadium usio na manufaa yoyote kisiasa kwako? Tukajenga uwanja mwingine, Samia Stadium huko Arusha. Huu, achana nao na usijengwe kabisa, hata Morocco tuwazingue. Pamoja na Morocco kuwa tayari kujenga, wakazinguliwa, maana kulikuwa na vita ndani ya kuua jina la Jiwe, lilikuwa too much kwa bibi Kizimkazi. Akaongea mwandishi mmoja kuandika kitabu cha "I am the State" kumchafua Jiwe. Hii project ilikuwa inasimamiwa sana na Msomali na Rostam, wakampiga sana Jiwe kwenye kitabu, na kufifisha maprojct yake yote aliyokuwa ameweka majina yake.
Ndio dili la Arusha lilipoibuka. Changamoto inakuja kuwa kubwa zaidi, Bi. Kizimkazi ana uwezo mdogo sana. Waliomzunguka wanajiongeza sana kupiga pesa maana wameona kwa mwanae. Na hata ukiiba mbele yake hana uwezo wa kuona namba zinamzumbua sana. Hawezi kaa chini akaelezewa na kuelewa namna milioni 1 ilivyoibwa kwenye milioni 10, akaelewa. Incompetent wa kiwango cha lami, hata hii kuua watu kwa incompetence yake anafikiri Tanganyika ni kama kijiji, kwamba ukiua watu 1,000 basi kijiji kitapoa. Kwa kweli hii ni nchi kubwa yenye watu wa aina tofauti. Akiambiwa na waganga kuwa ana uaua, akiambiwa na waganga huyu ndio mwaminifu imeisha. Ndio maana kina Msigwa wamefanikiwa sana kuiba kupitia wizara ya michezo. Hata ile goal sikui la mama, kuna mabilioni yamepigwa. Wafanyabiashara wamepigiwa sana simu kuhusu mambo hayo. Kuna mechi zilikusanywa milioni 250, wakisaka milioni 20, salio linabaki, ni upuuzi mtu. Hakuna namna uwanja wa shilingi bilioni 187 unaweza kuwa bilioni 347 bila kuongezeka ukubwa, hata kama kungekuwa na makosa kiasi gani. Maana bilioni 100 inaweza jenga uwanja wa site ya kati. Kama ni ongezeko, labda ingekuwa kati ya 20 hadi 50 billion max. Hii ya kusifiwa na kupewa majina, ndiko wizi umefanyika. Yeye alimtu Makonda, na Makonda amefanya kama Duli Balali. Wameongeza cha juu cha kufa mtu, na boss wao amekula, ndio maana anaona aibu, anasema watajeni majina waone aibu.
Waulizeni kwa nini wametelekeza uwanja wa Dodoma kama sio wizi ulikuwa unatengenezwa ni nini? kama Morocco wangejenga wa Dodoma hii deal ya Arusha ingekuwa ngumu sana kufanyika, wakaua uwanja wa msaada ili wachote mabilioni yetu watuibie
yaani mtu yuko tayari kitu cha bure akipoteze kabisa ila aingia kwenye gharama ambazo amepanga kuiba. maana hizo za morocco ingekuwa ngumu kuiba si wanasimamia mradi
wizi kwenye viwanja ni mchezo wa mabilioni ndio maana matajiri wako sana kwenye hii michezo na ukarabati wa mara kwa mara wa uwanja wa taifa
NINAZISIKIA KELELE ZA MARIDHIANO LAKINI SIZIELEWI (METANOIA)
Mwl. John Pambalu
Ukisikiliza kwa makini kauli za viongozi mbalimbali na na watu mashuhuri (Opinion Leaders) nchini, utabaini kuwa ajenda kuu inayopigiwa upatu ni "Maridhiano" na "Kuliponya Taifa." Ni maneno matamu masikioni, lakini je, yana uhalisia?
Ninalazimika kutoa mifano michache ya matukio yaliyokipata chama cha CHADEMA wiki iliyopita kama kielelezo tosha cha ghiliba ya watawala. Mifano hii inadhihirisha kuwa kile kinachoitwa maridhiano ni ganda tu, lakini ndani yake kuna ukandamizaji uleule.
Katika kilele cha maadhimisho ya miaka 33 tangu kuanzishwa kwa CHADEMA, yalitokea matukio matatu ya kusikitisha yanayofikirisha.
1. Dhuluma ya Alama na Itikadi ya Chadema (Mbeya).
Kule Mbeya, viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Masaga Karoli na Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mbeya Mhe. Elisha Chonya, walikuwa katika zoezi la kistaarabu la kushusha bendera nusu mlingoti kumuenzi Hayati Mzee Edwin Mtei. Badala ya heshima, Polisi waliwakamata wahudhuriaji wote na kuamua kushusha bendera ya chama kwa mikono yao wenyewe, kitendo cha chuki iliyopitiliza.
Kana kwamba hiyo haitoshi, usiku wa manane walivamia nyumbani kwa Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Mbeya Vijijini Getruda Lengesela na kumkamata kwa tuhuma hewa za "uchochezi."
2. Kuzuia Utu na Uungwana (Dodoma)
Katika kuadhimisha miaka 33, chama kiliamua kufanya tendo la huruma kwa kwenda hospitali ya serikali kuchangia damu ili kuokoa maisha ya Watanzania. Ajabu ni kwamba, walizuiliwa kufika hospitalini na kuzuiwa kutoa damu hiyo. Je, maridhiano yanakataa hata kutoa msaada wa kitabibu?
3. Ukandamizaji wa Kiuchumi na Teknolojia:
Wanachama na wananchi walipoamua kukichangia chama kupitia namba za simu za maafisa wawili JohnPambaluna Brenda Rupia, mifumo ilianza hujuma. Kampuni ya Airtel ilifunga namba ya Brenda Rupia, na baadaye Vodacom wakafunga huduma ya M-Pesa ya John Pambalu (0769823839). Hapa ndipo unapaswa kujiuliza. Inakuwaje matukio matatu katika mikoa mitatu tofauti (Mbeya, Dar es Salaam, na Dodoma), yanayohusisha sekta tofauti (Polisi, Wauguzi, na Makampuni ya Simu), yote yatokee kwa mpigo dhidi ya CHADEMA?
Jibu ni rahisi: Kuna nguvu inayofanya kazi gizani. Dola ya Rais Samia Suluhu Hassan inaonekana dhahiri kutotaka kuacha utamaduni wa kuifinyilia CHADEMA. Nini maana ya maridhiano katika mazingira ya namna hii?
METANOIA
Metanoia: Kiini cha Maridhiano ya Kweli
Neno "Metanoia" lina asili ya Kiyunani (μετάνοια), likimaanisha mabadiliko ya msingi ya akili, mtazamo, na mwelekeo.
Kifalsafa: Ni kubadili namna unavyofikiri na kuona mambo.
Kiroho (Toba): Si kuhuzunika tu, bali ni kugeuka kabisa na kuacha njia ya zamani, kubadili moyo na madhumuni ya maisha kwa ajili ya mwanzo mpya.
Hapa nchini, wanatamka "Maridhiano" majukwaani huku vitendo vyao vikiwa ni vilevile vya kale. Inasemekana Rais amemteua Mwigulu Nchemba kuwa kiongozi wa maridhiano, mtu ambaye kila kukicha anatumia lugha ya kashfa na matusi dhidi ya wale anaopaswa kuketi nao mezani. Nitakuwa wa mwisho kuamini "maridhiano" ya namna hii.
Wanataka maridhiano, lakini hawako tayari kwa Metanoia (kugeuka). Bado wanawashikilia kwa hila wakina Tundu Lissu, Yohana Kaunya, na mamia ya wafungwa wa kisiasa magerezani.
Bado wanakifungia CHADEMA kufanya shughuli za kisiasa kinyume na Katiba ya nchi, huku vyombo vya dola vikiendelea kuwa rungu la ukandamizaji.
Hata katika kile kinachoitwa "Tume ya Uchunguzi ya Oktoba 29, 2025," Mwenyekiti wake anapiga marufuku vyombo vya habari kuripoti mwenendo wa tume hiyo. Huku ni kuzika ukweli gizani.
Hitimisho: Huwezi kupata msamaha bila kukiri makosa, kuyajutia, na kuamua kugeuka. Hakuna maridhiano ya kweli bila Metanoia. Nitakuwa wa mwisho kuamini maridhiano yanayohubiri amani mchana, huku yakipanga hujuma na vifungo usiku.
Wasalaam,
John Pambalu
[email protected]
Mwalimu wa zamu.
Deutsche Welle (DW) wamefanya mahojiano na Veronica Lyimo anasema mume wake, Emmanuel Msoma aliuwawa kwa kupigwa risasi Oktoba 29, 2025 lakini cheti cha kifo hospitali ya Mwananyamala kimeandikwa alifariki kwa matatizo ya uti wa mgongo na walipewa mwili baada ya siku nane kupita ukiwa umeoza na kutoa harufu. Unatakiwa kusaini kilichopo vinginevyo hata huo mwili hupew. Kimsingi hili ni tukio ambalo haliwezi kusahaulika kirahisi. Halafu MADURO anasema Serikali yao katili ipo tayari kwa mazungumzo na maridhiano. Lakini akisimama jukwaani anaanza kuwasimanga waliouwawa anasema wamelipwa. SIYO mkweli. Hamtaki kukiri na kuwajibika kwa mauaji lakini mnataka kuridhiana. Kuridhiana na nani? Kuridhiana katika jambo gani? Kuridhiana ili kutafuta nini? Watanzania watawapa masikio yao siku wakiona kuna ukweli namna hii uwajibikaji tu.
EDWIN MTEI: MJENZI WA NCHI, KIONGOZI WA MFANO
Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe na wanafamilia wa marehemu Edwin Mtei,
Viongozi, wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Ndugu wananchi, waombolezaji, mabibi na mabwana;
Nimepokea taarifa za kifo cha Mwenyekiti Mwanzilishi na Mwasisi wa Chama chetu, marehemu Edwin Isaac Mbiliewi Mtei kwa masikitiko makubwa. Katika hili nafikiri sitakosea nikisema kwamba siko peke yangu. Hata hivyo, naombeni mniruhusu niwape pole nyingi watoto, wajukuu, ndugu na wanafamilia wa marehemu Mzee Mtei. Salamu hizi za rambirambi zinawahusu pia viongozi, wanachama na wafuasi wote wa CHADEMA popote walipo katika nchi yetu na nje ya nchi. Aidha, Mzee Mtei alisimama katika mstari wa mbele kabisa katika harakati za ujenzi wa nchi yetu; kwa sababu hiyo, salamu hizi ziwafikie pia wananchi wote wa Tanzania katika ujumla wao.
Maandiko Matakatifu yanatufundisha katika Zaburi 90:10, kwamba “miaka ya kuishi ni sabini, au tukiwa wenye afya, themanini…” Mwenyezi Mungu alimbariki marehemu Mzee Mtei kwa kumpa ziada ya miaka ishirini na nne (24) katika gawio lake la kawaida la miaka ya hapa duniani; na alimzidishia miaka kumi na minne katika nyongeza yake ya miaka kumi kwa wenye afya.
W.E.B Dubois, kiongozi wa harakati za ukombozi wa Waafrika duniani, aliandika katika kusherehekea miaka tisini ya kuzaliwa kwake kwamba “…kama kuishi hakukupi thamani, busara na maana ya maisha, basi hakuna sababu yoyote ile ya kuishi.”
Miaka tisini na nne (94) ya maisha ya marehemu Mzee Mtei yalitupa thamani kubwa, yalijaa busara tele na yalikuwa na maana kubwa. Naomba nikope maneno ya Amiri bin Sudi, au kwa jina lake maarufu ‘Andanenga’, mtenzi na mshairi maarufu wa Kiswahili, pale aliposema: Mzee Mtei …. “alisheheni sifa nyingi sana, njema zisizo idadi, za marefu na mapana, hazipimiki kwa yadi, ilobaki sisi kushindana, dua tumuombe wadudi, ampokee Baba yetu, kwa fukisho la ubani, udi na uvumba.”
Ndugu Waombolezaji,
Marehemu Mzee Mtei alikuwa mmojawapo wa wajenzi wakuu wa misingi mikuu ya kiuchumi ya nchi yetu, hasa katika miongo miwili ya mwanzo ya Uhuru. Alikuwa mmojawapo wa wasomi mahiri wa kwanza katika fani ya uchumi wa mara baada ya Uhuru. Kwa sababu ya umahiri wake, haikuwa ajabu kwamba pale wakuu wa nchi za Afrika Mashariki walipoamua kuvunja iliyokuwa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki, na kila nchi kuanzisha Benki Kuu yake, Edwin Mtei aliteuliwa kuwa Gavana Mteule, hata kabla Benki Kuu yenyewe haijaanzishwa rasmi. Kwa vyovyote vile itakavyokuwa, jina la Edwin Isaac Mbiliewi Mtei litahusishwa milele na Benki Kuu ya Tanzania; jina na saini yake yalikuwa kwenye noti za kwanza kabisa kutolewa na Benki Kuu ya Tanzania kati ya mwaka 1966 na 1974; na kati ya mwaka 1978 na 1981 alipokuwa Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa nafasi yake ya Gavana wa Benki Kuu na baadae Waziri wa Fedha, Mzee Mtei alikuwa mmoja wa washiriki wakuu katika kutunga na kutekeleza sera za kiuchumi za serikali ya Mwalimu Nyerere. Historia halisi ya nchi yetu haiwezi kumtenganisha Mzee Mtei na Azimio la Arusha lililopelekea utaifishaji wa mali za makampuni na mashirika binafsi na kuanzishwa kwa mfumo wa serikali kuhodhi njia zote muhimu za uchumi, yote yakifanywa kwa jina la Ujamaa na Kujitegemea. Na wala historia ya kweli ya nchi yetu haiwezi kumtenganisha Mzee Mtei na kushindwa kwa sera hizo kuanzia miaka ya mwisho ya sabini. Alikuwa ‘jikoni’ wakati sera hizo zinaandaliwa; na alikuwa mmoja wa ‘wapishi’!
Heshima yake kuu, na mchango wake kuhusu suala hili ambalo historia ya nchi yetu itauenzi milele ni huu; Mzee Mtei hakunyamaza mara alipogundua kwamba sera za kiuchumi za serikali yake, sera alizoshiriki kuzitunga na kuzisimamia hazitekelezeki tena. Mzee Mtei alimkabili Mwalimu na kumweleza ukweli wake; kwamba sera za kiuchumi za Azimio la Arusha zilikuwa zimeshindikana kutekelezwa; akamshauri Mwalimu kubadili msimamo wake ili kwenda sambamba na mahitaji ya nyakati na hali halisi ya uchumi wa kimataifa
UJUMBE WA RAMBIRAMBI WA @TunduALissu KUFUATIA KIFO CHA MZEE EDWIN ISAAC MBILIEWI MTEI.
EDWIN MTEI:
MJENZI WA NCHI, KIONGOZI WA MFANO
Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe na wanafamilia wa marehemu Edwin Mtei,
Viongozi, wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Ndugu wananchi, waombolezaji, mabibi na mabwana;
Nimepokea taarifa za kifo cha Mwenyekiti Mwanzilishi na Mwasisi wa Chama chetu, marehemu Edwin Isaac Mbiliewi Mtei kwa masikitiko makubwa. Katika hili nafikiri sitakosea nikisema kwamba siko peke yangu. Hata hivyo, naombeni mniruhusu niwape pole nyingi watoto, wajukuu, ndugu na wanafamilia wa marehemu Mzee Mtei. Salamu hizi za rambirambi zinawahusu pia viongozi, wanachama na wafuasi wote wa CHADEMA popote walipo katika nchi yetu na nje ya nchi. Aidha, Mzee Mtei alisimama katika mstari wa mbele kabisa katika harakati za ujenzi wa nchi yetu; kwa sababu hiyo, salamu hizi ziwafikie pia wananchi wote wa Tanzania katika ujumla wao.
Maandiko Matakatifu yanatufundisha katika Zaburi 90:10, kwamba “miaka ya kuishi ni sabini, au tukiwa wenye afya, themanini…” Mwenyezi Mungu alimbariki marehemu Mzee Mtei kwa kumpa ziada
ya miaka ishirini na nne (24) katika gawio lake la kawaida la miaka ya hapa duniani; na alimzidishia miaka kumi na minne katika nyongeza yake ya miaka kumi kwa wenye afya.
W.E.B Dubois, kiongozi wa harakati za ukombozi wa Waafrika duniani, aliandika katika kusherehekea miaka tisini ya kuzaliwa kwake kwamba “…kama kuishi hakukupi thamani, busara na maana ya maisha, basi hakuna sababu yoyote ile ya kuishi.”
Miaka tisini na nne (94) ya maisha ya marehemu Mzee Mtei yalitupa thamani kubwa, yalijaa busara tele na yalikuwa na maana kubwa. Naomba nikope maneno ya Amiri bin Sudi, au kwa jina lake maarufu ‘Andanenga’, mtenzi na mshairi maarufu wa Kiswahili, pale aliposema: Mzee Mtei …. “alisheheni sifa nyingi sana, njema zisizo idadi, za marefu na mapana, hazipimiki kwa yadi, ilobaki sisi kushindana, dua tumuombe wadudi, ampokee Baba yetu, kwa fukisho la ubani, udi na uvumba.”
Ndugu Waombolezaji,
Marehemu Mzee Mtei alikuwa mmojawapo wa wajenzi wakuu wa misingi mikuu ya kiuchumi ya nchi yetu, hasa katika miongo miwili ya mwanzo ya Uhuru. Alikuwa mmojawapo wa wasomi mahiri wa kwanza katika fani ya uchumi wa mara baada ya Uhuru. Kwa sababu ya umahiri wake, haikuwa ajabu kwamba pale wakuu wa nchi za Afrika Mashariki walipoamua kuvunja iliyokuwa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki, na kila nchi kuanzisha Benki Kuu yake, Edwin
Mtei aliteuliwa kuwa Gavana Mteule, hata kabla Benki Kuu yenyewe haijaanzishwa rasmi. Kwa vyovyote vile itakavyokuwa, jina la Edwin Isaac Mbiliewi Mtei litahusishwa milele na Benki Kuu ya Tanzania; jina na saini yake yalikuwa kwenye noti za kwanza kabisa kutolewa na Benki Kuu ya Tanzania kati ya mwaka 1966 na 1974; na kati ya mwaka 1978 na 1981 alipokuwa Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa nafasi yake ya Gavana wa Benki Kuu na baadae Waziri wa Fedha, Mzee Mtei alikuwa mmoja wa washiriki wakuu katika kutunga na kutekeleza sera za kiuchumi za serikali ya Mwalimu Nyerere. Historia halisi ya nchi yetu haiwezi kumtenganisha Mzee Mtei na Azimio la Arusha lililopelekea utaifishaji wa mali za makampuni na mashirika binafsi na kuanzishwa kwa mfumo wa serikali kuhodhi njia zote muhimu za uchumi, yote yakifanywa kwa jina la Ujamaa na Kujitegemea. Na wala historia ya kweli ya nchi yetu haiwezi kumtenganisha Mzee Mtei na kushindwa kwa sera hizo kuanzia miaka ya mwisho ya sabini. Alikuwa ‘jikoni’ wakati sera hizo zinaandaliwa; na alikuwa mmoja wa ‘wapishi’!
Heshima yake kuu, na mchango wake kuhusu suala hili ambalo historia ya nchi yetu itauenzi milele ni huu; Mzee Mtei hakunyamaza mara alipogundua kwamba sera za kiuchumi za serikali yake, sera alizoshiriki kuzitunga na kuzisimamia hazitekelezeki tena. Mzee Mtei alimkabili Mwalimu na kumweleza ukweli wake; kwamba sera za kiuchumi za Azimio la Arusha zilikuwa zimeshindikana kutekelezwa; akamshauri Mwalimu kubadili msimamo wake ili kwenda
sambamba na mahitaji ya nyakati na hali halisi ya uchumi wa kimataifa.
Hili halikuwa jambo jepesi. Mwaka ambao Mzee Mtei aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha, Mwalimu alisema katika mahojiano na BBC kwamba, alikuwa na madaraka, kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi yetu, ya kuwa Dikteta kama angetaka! Mfumo wa Kikatiba na kiutawala wa aina hii sio tu ulimgeuza Rais kuwa Mungu mtu, bali pia ulitengeneza mazingira mazuri ya ‘uchawa’ miongoni mwa viongozi na watendaji wa serikali na chama pekee cha siasa cha wajati huo, yaani TANU na baadaye CCM. Baadhi yenu mtakumbuka salamu rasmi za kisiasa za miaka hiyo; ‘Zidumu Fikra za Mwenyekiti wa CCM!’ Mzee Mtei alikuwa na ujasiri wa kumweleza Mwalimu, kwa heshima zote, kwamba fikra zake za kiuchumi zilikuwa zimefeli; hazikupaswa kuendelea kudumishwa!
Kwa ujasiri huo huo, marehemu Mzee Mtei aliwajibika kwa kujiuzulu nafasi pale Mwalimu alipomkatalia ushauri wake huo. Alikuwa na uadilifu wa kuona kwamba haikuwa sahihi kwake kuendelea kutumikia nchi yetu katika masuala ambayo msimamo wake ulikuwa tofauti na msimamo wa Kiongozi Mkuu wa Serikali yake. Leo hii, kwa jinsi ambavyo ‘uchawa’ kwa Rais umekuwa ni donda ndugu na umekithiri katika ngazi zote za utumishi wa umma na hata katika sekta binafsi, tunaweza kupima kiwango cha juu cha ujasiri wa Mzee Mtei na uzalendo wake kwa nchi yetu. Itoshe tu kusema, kama nyongeza, kwamba yale yote ambayo Mzee Mtei aliyapendekeza kwa Mwalimu na yakakataliwa, yalikubaliwa na kuanza kutekelezwa
Miaka miwili tu baada ya Mzee Mtei kulazimika kujiuzulu nafasi yake ya Waziri wa Fedha! Kwa maneno mengine, ukweli wa msimamo wake ulithibitishwa kwa vitendo, licha ya yeye mwenyewe kulazimika kuwa nje ya Serikali. Kwangu mimi, hii ndio thamani na maana kubwa ya maisha marefu ya Mzee Edwin Mtei.
Ndugu Waombolezaji,
Mzee Edwin Mtei alikuwa mjenzi wa demokrasia ya vyama vingi katika nchi yetu. Na kwenye hili, kama ilivyokuwa hulka yake, aliongoza kwa mfano na kwa vitendo. Alikuwa mmoja wa Waasisi na Mwenyekiti Mwanzilishi wa CHADEMA. Leo hii, CHADEMA ndio chama kikuu cha siasa katika nchi yetu; sio CCM, kwa sababu CCM ni chama-dola, sio chama cha siasa kinachoishi kwa ridhaa na mapenzi ya wananchi na wanachama wake. CHADEMA, chama cha Edwin Isaac Mbiliewi Mtei, kinaishi kwa ridhaa na mapenzi ya mamilioni ya Watanzania kwa sababu Mzee Mtei alitufundisha kuwa utumishi wa kisiasa sio biashara au mahali pa kujipatia fedha au vyeo, bali ni huduma na utumishi kwa wananchi.
Kama Mwenyektii Mwanzilishi, Mzee Mtei hakuwahi kupokea mshahara au posho yoyote kutoka kwa Chama. Hakuwahi kupatiwa gari au usafiri wa Chama; na wala hakuwahi kuwa diwani au mbunge wa CHADEMA. Hakuwahi kutumia uongozi wake wa Chama kujinufaisha yeye binafsi au watoto wake au ndugu na marafiki zake. Kwa Edwin Mtei uongozi ulikuwa ni dhamana, sio fursa. Alitumia
Muda wake, na mali zake na nguvu zake kukijenga Chama na kuwatumikia wanachama na wananchi wake. Na hii ndio thamani nyingine kubwa na maana muhimu ya maisha marefu ya Mzee Edwin Mtei. Thamani hii na maana hii ya maisha yake imejidhihirisha wazi katika miaka hii kumi ambapo Chama chetu, viongozi wake, wanachama na wafuasi wake tumepitishwa katika bonde la uvuli wa mauti mara kwa mara. Tumeumizwa sana, lakini tumeimarishwa sana pia, kwa sababu ya mfano wa utumishi na kujitolea aliotuwekea Mzee Edwin Mtei. Na kwa mfano huo tutashinda.
Ndugu Waombolezaji,
Mzee Edwin Mtei ametuachia urithi mwingine wenye thamani na maana kubwa kwa Chama chetu na nchi yetu. Alitumikia Chama chetu kama Mwenyekiti wake kwa kipindi kimoja tu cha miaka mitano. Ilipofika mwaka 1998, akiwa na umri wa miaka sitini na sita (66), Mzee Mtei aliamua kustaafu uongozi wa Chama ili, kwa maneno yake mwenyewe, “kupisha damu changa” kuchukua uongozi wa Chama. Kama angetaka angeweza kuendelea kuongoza Chama kwa kipindi kingine kimoja au hata viwili. Lakini, kwa Edwin Mtei, uongozi wa Chama ulikuwa ni dhamana, sio fursa ya kung’ang’ania madarakani. Na kwa sababu ya mfano wake huo, CHADEMA imekuwa na itaendelea kuwa Chama pekee chenye kubeba matumaini na ndoto za mamilioni ya wananchi wetu ya kujenga nchi yenye kujali haki, uhuru na utu na maendeleo ya kweli ya watu wetu.
Ndugu Waombolezaji,
Mambo ya kusema juu ya Mzee wetu huyu ni mengi na mazuri, hatutaweza kuyamaliza yote kwa muda mfupi tulionao leo. Naomba nimalizie salamu zangu hizi kwa jambo moja ninaloamini ni muhimu kwa nchi yetu. Jambo hili linatudhihirishia aina ya kiongozi ambaye Edwin Mtei alikuwa, na thamani na maana ya maisha yake marefu.
Kwa muda mrefu wa miaka ya uhuru, viongozi wetu wa kisiasa hawakujenga utamaduni wa kuandika na kuchapisha vitabu na maandiko yanayohusu historia za maisha na nyakati zao baada ya kuondoka madarakani. Mwalimu Nyerere na rika lake lote la kwanza la uhuru waliondoka bila kutuachia simulizi za maisha na nyakati zao na changamoto walizokabiliana nazo kutoka kwenye midomo na kalamu zao wenyewe. Hatuna ‘autobiography’ au ‘memoirs’ za Mwalimu au Rashid Mfaume Kawawa, au za kiongozi mwingine wa rika hilo. Kwa sababu ya ombwe hili katika kumbukumbu zetu za pamoja, ufahamu wetu kama viongozi na wananchi kuhusu historia yetu wenyewe na kuhusu matukio muhimu ya historia hiyo ni ndogo na wakati mwingine haupo kabisa. Mzee Edwin Isaac Mbiliewi Mtei alitupatia mfano wa namna ya kuondokana na upofu huu wa kujitakia. Mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka sabini na saba (77), Mzee Mtei alichapisha ‘From Goatherd to Governor’ (Kutoka Mchunga Mbuzi Hadi Gavana), historia ya maisha na nyakati zake. Kwa sababu ya ‘autobiography’ hii, tumeweza kufahamu mambo mengi kuhusu nchi yetu ambayo pengine tusingeyafahamu.
Tumeweza kufahamu, kwa mfano, jinsi sera za Ujamaa na Kujitegemea zilivyoipeleka nchi yetu kwenye lindi kubwa la matatizo ya kiuchumi. Tumeweza kufahamu angalau jinsi ambavyo kiongozi mmoja mwenye ujasiri na mwadilifu alivyosimama na kumwambia Mwalimu Nyerere ukweli wa hali yetu halisi na jinsi alivyowajibika kwa sababu ya kusimamia ukweli huo.
Kwa sababu ya mfano alioonyesha Mzee Mtei, viongozi wetu wengine nao walipata ujasiri wa kuandika na kuchapisha kumbukumbu za maisha yao na nyakati zao. Mwaka 2019, marehemu Rais Benjamin William Mkapa alichapisha ‘My Life, My Purpose’ (Maisha Yangu, Kusudio Langu), ambacho, kwa kiasi kikubwa, ni utetezi wake wa miaka kumi ya urais wake. Kwa kitabu hicho, marehemu Mzee Mkapa naye alituachia maelezo yake binafsi juu ya changamoto alizokumbana nazo katika maisha yake na alivyokabiliana nazo.
Pengine kiongozi aliyetupatia kumbukumbu bora zaidi za maisha ya utumishi wa umma na uongozi wa kisiasa ni ‘Mzee Rukhsa’, marehemu Rais Ali Hassan Mwinyi ambaye kitabu chake chenye kichwa hicho kilichapishwa mwaka 2022. Kitabi hicho kina hazina kubwa ya taarifa za matukio mbalimbali ya utawala wa Mwalimu Nyerere nay a utawala wa Rais Mwinyi yeye mwenyewe. Tumshukuru Mzee Mtei kwa kuwa mwasisi wa utamaduni huu mpya wa kisiasa katika nchi yetu.
Ndugu Waombolezaji,
Sasa naomba kumaliza salamu zangu hizi. Edwin Isaac Mbiliewi Mtei aliishi maisha marefu na yenye thamani, maana na mafundisho mengi kwetu. Hatupaswi kuomboleza kifo chake; tunapaswa kusherehekea maisha yake marefu. Hatumdai chochote; alikwisha lipa madeni yake yote kwetu na kwa nchi yake na riba juu. Alivipiga vita vilivyo vizuri; aliilinda Imani yake, na sasa mwendo wake ameumaliza.
Basi tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha mema na marefu, kwa malezi bora aliyotupatia, kwa utumishi uliotukuka na adilifu wa Edwin Isaac Mbiliewi Mtei. Na sisi sote ambao maisha yetu yaliguswa na kufadhiliwa na baba yetu huyu, tuungane katika dua hii:
“Ewe Mwenyezi Mungu, muumba wa mbingu na nchi, mapenzi yako yametimia, uyasamehe makosa ya baba yetu huyu, umwangazie nuru ya uso wako, uiweke roho yake mahali pema peponi. Amina.”
Nawashukuru kwa uvumilivu wenu na Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu.
Tundu Antiphas Lissu
Gereza Kuu la Ukonga - Dar es Salaam
January 2026
TUTASHINDA. MSIOGOPE.
Nelson Mandela alisimama mahakamani mara nne katika maisha yake ya mapambano. Siyo kwa sababu alikuwa mhalifu, bali kwa sababu alisimama imara kupinga mfumo dhalimu uliowanyima watu utu, haki, na sauti.
Kabla ya kesi maarufu ya Rivonia ya mwaka 1963/64, Mandela alikuwa amefungwa gerezani mara mbili. Kila kifungo kilikuwa ujumbe: dola ilitaka kumvunja moyo, kumchosha, kumkatisha tamaa. Lakini haikufanikiwa.
Hukumu ya miaka 27 gerezani haikuwa tu adhabu kwa mtu mmoja, Mandela; ilikuwa jaribio la kuzika ndoto ya ukombozi wa Waafrika Kusini. Mandela alitengwa, akanyimwa uhuru, familia, na maisha ya kawaida.
Miaka mimgi ilipita taratibu, siku zikafanana, mateso yakawa sehemu ya ratiba. Lakini hata ndani ya kuta za gereza, wazo la uhuru halikufungwa. Ndoto ya uhuru haikuzima. Mawazo hayawezi kufungwa kwa minyororo.
Mapambano hayakulipuka mara moja baada ya hukumu hiyo. Ilichukua takribani miaka kumi kabla ya wafuasi wa ANC na jamii ya kimataifa kuamka kwa nguvu mpya, kwa uelewa mpana zaidi, na kwa mshikamano wa kweli.
Mabadiliko ya kweli mara zote huchelewa, lakini hayapotei. Mbegu inapandwa leo, lakini huota kwa wakati wake. Ndiyo maana hatupaswi kukata tamaa. Ikiwa leo tunaona giza, haimaanishi alfajiri haitafika.
Ikiwa juhudi zetu zinaonekana kama hazina matokeo, haimaanishi kuwa ni bure. Historia inaonyesha kuwa wale wanaodumu, wanaostahimili, na wanaokataa kukata tamaa, hatimaye hubadilisha mkondo wa mambo.
Maumivu tunayopitishwa si laana; ni somo. Ndiyo yanayotujenga, yanayotufundisha uvumilivu, na yanayotupa mizizi ya uimara. Bila maumivu, dhamira hubaki dhaifu. Bila mateso, ushindi hukosa maana.
Kama Mandela alivyosimama tena, nasi pia tunapaswa kusimama—si mara moja, bali kila tunapoangushwa. Bado hatujachelewa. Wakati bado upo. Kile tunachopitia leo kinaweza kuwa msingi wa ushindi wa kesho.
Kinachotakiwa si kukimbia maumivu, bali kuyavumilia kwa hekima na kuyageuza kuwa nguvu. Historia inawaandika kwa heshima wale wanaodumu, si wanaokata tamaa njiani na kukimbia mapambano.
Tundu Antiphas Mughwai Lissu anatimiza siku 284 gerezani, amevunja rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza wa juu wa chama cha upinzani Tanzania kuwekwa kizuizini kwa muda mrefu zaidi tangu mwaka 1992
Dola katili la CCM haliwezi kuzuia na kuzima ndoto za kuitafuta Tanzania inayoheshimu haki za watu, misingi ya utu, usawa na uwajibikaji. Tundu A.M Lissu sio mhaini. Tundu Lissu arejeshewe uhuru wake. #FreeTunduLissu
Dear Mr. President @realDonaldTrump@POTUS, @SenateForeign@StateDept we,Tanzanians are asking you please ask Ms. McCormick and Mr. Zuckerberg to please look into the issue of meta disabling accounts of prominent Tanzanian activists after pressure from the Tanzanian government.
On December 3rd 2025, as one of Tanzanian’s most prominent activists, I was removed from all meta platforms, Instagram, facebook and WhatsApp.
My social-media platforms were essential tools for communicating , organizing peaceful civic action, and documenting human-rights abuses in real time. Their removal has severely hindered the ability of Tanzanians to access truthful information and to organize safely. Traditional media inside Tanzania has been effectively silenced; journalists who speak out risk being kidnapped, disappeared, or killed. This leaves social-media platforms run by diaspora activists like myself as one of the last remaining channels for Tanzanians to document and expose abuses.
I respectfully ask that you urge Meta to reinstate my accounts without delay. In today’s world, where civic freedoms and personal safety often depend on digital communication, it’s critical that meta does the right thing.
Wakati wa Magufuli IMF ilitoa takwimu kwamba GDP per capita yetu imepanda hadi $2,400 na tukaingia kwenye orodha ya nchi za uchumi wa kati (Lower middle Income). Leo IMF haohao wametoa takwimu kuwa GDP per capita imeporomoka hadi $1,300. Nini kimetokea?
Wakati ule tumeingia Uchumi wa Kati Machawa waliongea sana, kila kitu wakasema uchumi wa kati. Gari la uchumi wa kati, nyunba uchumi wa kati, simu uchumi wa kati. Hata mapenzi nayo yakawa ya uchumi wa kati. Lakini leo watazipita hizi takwimu za IMF kama wanaaga maiti.
Kutoka $2,400 hadi $1,300 something must be very wrong. Kwa kifupi purchasing power ya Mtanzania imepungua kwa karibu nusu. And this is not abt politics its abt economy. Nyie askari wa doria mnaopita mitandaoni kutafuta umbea, msilete mihemko. Hapa tunajadili uchumi. Najua hata nyie mmepigika, kwa hiyo kaeni kwa kutulia mpate shule ya uchumi.
Nini kimetokea mpaka tumetoka nchi ya uchumi wa kati hadi miongoni kwa nchi fukara duniani? Wastani wa pato la Mtanzania mmoja mmoja lilikua $2,400 (karibu TZS 6M) kwa mwaka, lakini ndani ya miaka michache limeporomoka hadi $1,300 (TZS 3M). Tumefikaje hapa na tunatokaje?? Wachumi tusaidieni.!
Credit @MalisaGJ_
Hali ambayo Tanzania imefikia, ikiwemo hatua za kidiplomasia kama kusitishwa au kuwekewa masharti magumu ya viza na baadhi ya mataifa, ni matokeo ya muda mrefu ya sera na maamuzi ya kisiasa yasiyoimarisha uwajibikaji na utawala bora. Hali hii inaashiria kupungua kwa uaminifu wa kimataifa kwa mifumo ya nchi.
Kiuchumi, athari zake ni kubwa. Vikwazo vya usafiri na uhusiano wa kimataifa hupunguza fursa za biashara, elimu, na ajira kwa Watanzania. Aidha, hali hii huathiri mtiririko wa uwekezaji wa kigeni, kwani wawekezaji hutegemea mazingira yenye uthabiti wa kisera, kisheria na kidiplomasia. Matokeo yake ni kudorora kwa ukuaji wa uchumi na kuongezeka kwa mzigo kwa mwananchi wa kawaida.
Kwa taswira ya kimataifa, Tanzania huanza kuonekana kama nchi yenye changamoto katika kuheshimu misingi ya demokrasia, haki, na diplomasia. Taswira hii hudhoofisha nafasi ya nchi kushiriki kikamilifu katika majukwaa ya kimataifa na kupunguza heshima yake miongoni mwa mataifa mengine.
Kwa ujumla, hali hii ni onyo muhimu. Bila marekebisho ya sera, uwazi wa uongozi, na kurejesha uaminifu wa kimataifa, gharama zake kwa maendeleo ya taifa zitazidi kuwa kubwa.
Anaandika Askofu Bagonza (PhD)
"POLISI NA “WAKATOLIKI”
1. Nalazimika kuwapongeza Polisi wetu kwa ukomavu wao na ustaarabu wa kutozuia maandamano ya “Wakatoliki” walioenda kueleza hisia zao kwa Balozi wa Papa hapa nchini.
2. Nachukulia uvumilivu wao kama ishara ya kuacha kupambana na maoni ya watu na hisia zao. Basi wafute hata kesi za Mzee Mwandambo aliyekamatwa kwa kueleza hisia zake za kidini.
3. Kumbe, msimamo huu wa Polisi ulianza mapema pale walipomvumilia kiongozi aliyesema atakata vichwa vya watakaoandamana. Shikilia hapo hapo Polisi, jizuie kuingilia uhuru wa watu na maoni yao.
4. “Wakatoliki” hawa wasiojua kusoma vizuri walichokiandaa; walioamua kumwimba “Mwamba ni Yesu” badala ya Bikira Maria Mlinzi wa Taifa letu, na waliosahau kuwa Baba Mtakatifu wa sasa anaitwa Papa Leo wa 14; wametimiza haki yao ya kikatiba.
5. Watakapokuja Wakatoliki halisi wanaojua kusoma na kuvaa kwa heshima mbele ya Balozi wa Papa, wakasoma tamko lao kuwataka Polisi wamkamate aliyempiga Fr. Kitima, na wamlete aliyeteka mapadre na kuwadhalilisha, akawavisha wake za watu mavazi ya kitawa ili waonekane ni watawa walioshika bendera za vyama nk - hawa Wakatoliki wakiandamana, polisi kuweni wavumilivu kama mlivyokuwa wavumilivu kwa “Wakatoliki” hawa.
Sisi Wajaluo tunaamini kuwa chuki dhidi ya Ukatoliki inayoendeshwa kwa mikakati mibovu, ina nia mbaya dhidi ya serikali kuliko ilivyo na nia mbaya dhidi ya Ukatoliki.
Kupigana na Ukatoliki ni lazima uwe na dini nyingine ndani yako inayokusukuma kupigana vita hiyo. Wajaluo “tusiotahiriwa” tunajiuliza hiyo dini ni ipi"?
Swali muhimu ninalojiuliza.
Kama kweli hao waliondamana ni wakatoliki kweli, kwanini hawakuandamana wakati Fr. Kitima alipojaribiwa kuuliwa na alipotekwa?
Acheni kuchezea imani.
Swali muhimu ninalojiuliza.
Kama kweli hao waliondamana ni wakatoliki kweli, kwanini hawakuandamana wakati Fr. Kitima alipojaribiwa kuuliwa na alipotekwa?
Acheni kuchezea imani.
Nimemaliza kutazama mini-documentary ya @CNN kuhusu mauaji ya raia katika na baada ya siku ya uchaguzi. Nchi yetu imepata dosari mbaya sana katika bendera yake. UKWELI na UWAJIBIKAJI ni LAZIMA.
Vyombo vya habari vya kimataifa vimekuwa msaada mkubwa sana katika kuonesha uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu ikiwepo mauaji ya kutisha ya raia tangu siku ya uchaguzi hadi sasa. Hakika, tunawapongeza.
Vyombo vya habari za ndani bado vinasubiri ‘gigs’ kutoka kwa serikali. Vimegeuka kuwa ‘REPORTERS’ wa propaganda na matukio ya serikali. Walisingizia internet, hata baada ya kurejea, hakuna kitu wamefanya.
Kilichofanyika na CNN ndiyo ‘investigative journalism’. Unaeleza jambo kwa kutumia ushahidi wa kisayansi pasipo kuacha mashaka kwa hadhira. Nafikiri, waandishi wetu wakitoka ‘honeymoon’ yao, watajifunza.
Wametumia ushahidi wa; Geolocated videos from the scenes, audio forensic analysis of the shots fired & first-hand accounts from witnesses & victim High-resolution satellite imagery from Planet Labs & Vantor.
CNN wameweka hadi picha za satelite kuonesha mauaji ya waandamanaji ambao walikuwa wanakimbia na wakapigwa risasi za mgongo. CNN wamethibitisha picha mjongeo za ‘mortuary’ katika maeneo tofauti.
CNN wameweka picha za satelite kuonesha ardhi ambayo inadhaniwa kuchimbwa na kufukia maiti. CNN wamelinganisha ardhi hiyo kwa kutumia picha za satellite za Oktoba 20, 2025 na November 15, 2025.
CNN wamesema walihoji madaktari ambao walieleza, majeruhi waliopigwa risasi na kupelekwa hospitali hawakuruhusiwa kupewa matibabu, maafisa wa usalama waliagiza wapelekwe mortuary wakafie huko.
Hizi ni habari mbaya za kutisha sana. Huwezi kuunda tume ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani ukapotezea matendo na matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu yaliyotajwa na uchunguzi wa CNN.
Pia, nafikiri kuna matukio mengi CNN hawajapata uhakika nayo, kwa weledi tu, hawakuweza kuyatumia katika mini-docs yao. Naamini, tunahitaji UKWELI na UWAJIBIKAJI. Nothing less, mothing more.
Anaandika Mtapa Ng'Wanandagula
TIMU YA UCHUNGUZI WA CNN – TANZANIA
Ripoti ya uchunguzi iliyotolewa na CNN iliandaliwa na wafuatao:
1. Larry Madowo
Mwandishi Mwandamizi, mwenye uzoefu wa kuripoti masuala ya kimataifa hususani uchumi na siasa. Ana Shahada ya Mawasiliano ya Umma kutoka Chuo Kikuu cha Daystar, Kenya, na MBA kutoka Chuo Kikuu cha Columbia, New York, USA.
2. Gianluca Mezzofiore
Mhariri Mwandamizi na mtaalamu wa uchunguzi wa taarifa za wazi. Amewahi kuthibitisha video ya wanajeshi wa Ethiopia wakiua raia na kutumia ubakaji kama silaha ya kivita huko Tigray. Ana Shahada ya Fasihi kutoka Chuo Kikuu cha Bologna, Italia, na Shahada ya Uzamili ya Uandishi wa Habari kutoka City University, London, UK.
3. Florence Davey-Attlee
Mwandishi Mwandamizi na mtayarishaji wa vipindi. Amewahi kuripoti matukio muhimu barani Ulaya, ikiwemo mashambulizi ya ISIS nchini Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji, Ujerumani na Uturuki. Ana Shahada ya Uzamili katika Uandishi kutoka Chuo Kikuu cha Westminster, UK, na Shahada ya kwanza ya Sayansi ya binadamu (BSc in Human Biology) kutoka Chuo Kikuu Oxford, UK.
4. Barbara Alvanitidis
Mwandishi Mwandamizi anayesimamia uzalishaji wa maudhui. Ni msaidizi wa Kitengo cha Habari za Uchunguzi cha CNN. Amesharipoti matukio mengi kwa kufichua na kubainisha wahusika. Ana Shahada ya Uzamili katika Uandishi wa Habari za Kimataifa kutoka City University, UK, na Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Kikuu cha Ottawa, Canada.
5. Benjamin Strick
Mwandishi wa Habari Mwandamizi na mtaalamu wa uchunguzi. Amejikita katika uchambuzi wa taarifa za ukiukaji wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita. Ana Shahada ya Sheria (LLB) kutoka Chuo Kikuu cha Bond, Australia, na Shahada ya Uzamili ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi. Ni mshindi wa tuzo ya OSINT Champion of the Year – 2021.
6. Julie Zink
Mhariri Mwandamizi wa Maudhui ya Video. Amewahi kuwa Mzalishaji na Mhariri wa maudhui kabla ya kuwa Mhariri mwandamizi. Ana Shahada ya Kwanza ya Lugha na Shahada ya Uzamili ya Uandishi wa habari kutoka Chuo Kikuu cha Virginia, Marekani.
Naomba CV za wale Waandishi went, Machawa wa Nduli Idd Amin Mama ili tufanye ulinganifu kuna kitu nataka kuona.
PART 9: kuna kiongozi mkubwa wa Kijeshi alilishwa Sumu, Mangula nae alilushwa sumu, magufuli nae akauawa. Kikwete anapaswa akamatwe haraka, na uchunguzi wa Amiri jeshi mkuu kuuawa ufanywe na Jeshi. 🔥🔥
Captain Tesha. ⭐️⭐️⭐️