In God I Trust๐| Damian poppa๐.| Double Thinker๐ถ๐ถ๐ถ| Manchester United ๐ฅ, Young African Fc๐๐,Chicago Bulls ๐And Golden State Warriors ๐|Love&Peace.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanasimamia kwa umakini suala la usafi, hususan katika miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam.
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumatano, Septemba 2, 2026, wakati akiwaapisha Wakuu wa Mikoa wateule pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani (RAS), katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar.
Amesema bado kuna baadhi ya maeneo ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam ambayo hayaridhishi kwa kiwango cha usafi, akisisitiza kuwa hali hiyo inahitaji kuchukuliwa hatua na viongozi wanaohusika.
Kwa mujibu wa Rais Samia, Dar es Salaam ni jiji linalotazamwa na wageni na wananchi kuanzia wanapowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa hadi maeneo ya Posta, hivyo usafi unapaswa kupewa kipaumbele katika maeneo yote na si sehemu chache zinazotazamika pekee.
Amewataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi na yanavutia, huku wakisimamia utekelezaji wa majukumu hayo kwa vitendo.
#KitengeUpdates
Klabu ya Yanga imetambulisha jezi mpya za michuano ya Klabu Bingwa Afrika msimu huu 2026/27.
Jezi hizo zimezinduliwa na mwandishi wa habari za michezo Fabrizio Romano.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 341
Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Tanganyika Amani Golugwa.
Mhe. Lissu: kuna ushahidi umeletwa mahakamani eti nilichapisha hayo maneno Jambo TV nikiwa na nia ya kuitishia serikali ya JMT, je kwenye maneno ya hati ya mashtaka, kuna neno Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Golugwa: Mimi nilikuwepo siku unatoa hotuba, hukutaja kabisa neno Serikali na kwenye hayo maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtaka hakuna neno Serikali ya Jamhuri ya Muungano
Mhe. Lissu: waeleze majaji uwepo wa neno Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Golugwa: hilo neno halipo kabisa
Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Makamu wa Rais wa JMT
Golugwa: Waheshimiwa majaji hilo neno halipo
Mhe. Lissu: waeleze majaji uwepo wa maneno Waziri Mkuu wa JMT
Golugwa: Hilo neno nalo halipo
Mhe. Lissu: waeleze majaji uwepo wa neno Baraza la Mawaziri
Golugwa: Hilo neno halipo
Mhe. Lissu: waeleze majaji uwepo wa maneno Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya JMT au Mkurugenzi wa Mashtaka nchini
Golugwa: hayo maneno hayapo
Mhe. Lissu: sasa shahidi kuna ushahidi umeletwa hapa eti nilitishia vyombo vya dola, sasa waeleze majaji uwepo wa maneno Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Jeshi la Mgambo, Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi, Jeshi la Magereza au jeshi lolote la nchi hii
Golugwa: Maneno yote hayo hayapo kabisa waheshimiwa majaji.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa neno Serikali katika hati ya mashtaka ambayo nimekusomea
Golugwa: Neno Serikali haipo
Mhe. Lissu: Hii tuhuma wewe unaionaje?
Golugwa: ni tuhuma ya uongo, ya kutunga sio ya kweli, imetengenezwa kwa nia ya kisiasa ili kurudisha nyuma jitihada za Tundu Lissu kwenye kudai mabadiliko kwenye mifumo ya kiuchaguzii
Mhe. Lissu: Mtu akisema akisema msimamo huu unaashiria uasi anakuwa ametenda kosa gani?
Golugwa: kwa ufahamu wangu hakuna kosa lolote anakuwa ametenda katika nchi hii Bara na Visiwani.
Mhe. Lissu: Kwa ufahamu wako, mtu akisema tutauvuruga uchaguzi anakuwa ametenda kosa gani nchi hii?
Golugwa: kwa ufaham wangu hakuna kosa lolote atakuwa ametenda katika nchi hii
Mhe. Lissu: mtu akisema tutauzuia uchaguzi huu anakuwa ametenda kosa gani katika nchi hii?
Golugwa: Mtu akisema tutauzuia uchaguzi anakuwa hajatenda kosa lolote katika nchi hii
Mhe. Lissu: waeleze majaji, kwa ufahamu wako wa masuala ya uchaguzi uwepo wa sheria inayosema kuwa ni kosa mtu kusema atazuia au kuvuruga uchaguzi
Golugwa: kwa ufahamu wangu hakuna sheria inayosema kuwa ni kosa kuzuia au kuvuruga uchaguzi
Mhe. Lissu: kuna ushahidi uliletwa hapa wa kamusi kutafisiri neno uasi kuwa ni kitendo cha kuvunja sheria, waeleze majaji, kitendo cha kuvunja sheria kama ni kosa la uhaini
Golugwa: kwa ufahamu wangu kitendo cha kuvunja sheria sio kosa la uhaini
Mhe. Lissu: Tumeletewa kamusi inatafsiri uasi kuwa ni kupinga mamlaka, taasisi, serikali au Taasisi je waelezo majaji kupinga serikali au taasisi kama ni kitendo cha uhaini
Kitendo cha kupinga serikali au taasisi ni kosa kisheria?
Golugwa: kwa ufahamu wangu kupinga serikali au taasisi sio kosa kisheria
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwa ufahamu wako maana ya neno kukinukisha
Golugwa: waheshimiwa majaji kwa tafisiri ya kawaida tu kukinukisha ni kukifanya kitu kitoe harufu, harufu ya marashi yaani unyunyu, kusababisha harufu itoke
Watu wanacheka sana hapo kwenye unyunyu๐๐๐๐๐
Mhe. Lissu: mtu akisema tunaenda kufanya kitu kitoe unyunyu, yanatishiaje serikali ya JMT?
Golugwa: maneno hayo hayawezi kuitishia kabisa maneno ya kutoa harufu nzuuuri au uvundo, kwakweli sioni kabisa mahali serikali inapoweza kutishika
Mhe. Lissu: Serikali ya JMT inatishikaje na maneno tutauzuia uchaguzi, tutauvuruga uchaguzi? ambayo kwa ushahidi wako sio makosa kwa mujibu wa sheria
Golugwa: Sioni kwa namna gani Serikali inaweza kutishika kabisa
Part 342 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
"Bado tunaomboleza. Ila ukiangalia serikali inaona hakuna kikubwa. Hata yale ya kuwa tuwe na siku ya kuomboleza husikii, wanaona ni kawaida tu. Majeraha tuliyopata kama taifa ni makubwa. Inaonekana wanataka kusema twende hivi itasahaulika. Mimi nasema HAPANA." - Joseph Warioba
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi ametoa wito maalum kwa baadhi ya Wasanii maarufu mitandaoni kuhudhuria kikao maalum, huku ajenda za kikao hicho zikitarajiwa kuwekwa wazi kesho, Septemba 1, 2026.
Miongoni mwa Wasanii waliotajwa kuitwa katika kikao hicho ni Dudu Baya, Pipi Tida, Chidi Benz, Lokole na Noel pamoja na wengine, huku orodha ya walioitwa ikisomwa na Gigy Money na Dotto Magari.
Hadi sasa, ajenda rasmi za kikao hicho hazijawekwa wazi, ingawa majina ya baadhi ya walioitwa yameibua hisia kuwa huenda kikao hicho kikagusa masuala yanayohusu maadili na matumizi ya mitandao ya Kijamii.
#MillardAyoUPDATES
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 329
Job Mrema: Ni sahihi ubaguzi ni kinyume na Katiba yetu ya Tanzania?
Mnyika: Ni sahihi.
Job Mrema: Yale makusanyo ya Tonetone kuna uamuzi ulifanyika kuwa kuna wachache wanufaike na wachache wasinufaike angali wengine wapo?
Mnyika: Sio Ubaguzi. Na ungetaka walipwe wote ukirudi ofisini mshauri Boss wako mwanasheria Mkuu wa Serikali alipe pesa zetu zaidi ya Milioni 400 ili tuwalipe wafanyakazi wetu wote. Hizo posho ni ndogo tu.
Job Mrema: Zaidi ya milioni 39 za Tonetone zimetolewa kati ya Tarehe 18 na 19 August 2026?
Mnyika: Hizo Habari nazisikia kutoka kwako.
Job Mrema: Ikitokea wanachama wa Chadema wamepata ushahidi wakasema kuna pesa zimetoka huoni kiti chako kitakuwa rehani?
Mnyika: Tutasubiri kuona kama kuna aliyeidhinisha pesa kutoka ni nani na kwa sababu gani?
Job Mrema: Kutoa pesa za Tonetone kwa mujibu wa ibara ya 4.1.2 ni kuwaonea?
Mnyika: Anaisoma hiyo ibara. Inasema kukandamiza watu kwa rangi, dini
Job Mrema: Ndio maana wengine hamkuwalipa?
Mnyika: Mimi Katibu Mkuu ndio ninayejua kwamba kwa hali tuliyonayo. Alipwe Mlinzi pekee. Kwasababu yeye yuko ofisini kila siku na sio mfanyakazi mwingine. Wewe unajua nini kuhusu haya mambo kuliko mimi?
Job Mrema: Ibara ya 3.2.4 inasema kama inavyosema hapo?
Mnyika: anaisoma na kusema inasema hivyo.
Job Mrema: Sasa kama hizo fedha chache zimelipwa kwa ubaguzi unasemaje kuhusu hilo?
Mnyika: Sisi hatuna Ubaguzi wenye ubaguzi ni nyie Serikali ambao mmezuia fedha za Chadema. Ndio maana Chadema tunapambana fedha za umma zibaki salama.
Job Mrema: Utakubaliana na mimi kuwa ukiaminika kwa dogo utaaminika kwa kubwa?
Mnyika: Chadema inaaminika kwa dogo na kwa kubwa pia. Ndio maana watanzania wameendelea kuiunga mkono.