Serikali yafuta usajili wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima ikidai limekiuka sheria kwa mahubiri ya kisiasa yanayoweza kuhatarisha amani. Hatua hiyo yachukuliwa siku moja baada ya Gwajima kukemea vikali vitendo vya utekaji na kupotea kwa watu.
Kwa niaba ya uongozi na familia nzima ya Radio 5, tunawatakia wasikilizaji na Watanzania wote heri Sikukuu ya Wafanyakazi. Endeleeni kuwa nguzo ya matumaini na maendeleo kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
#Radio5#TheOnlyChoice
Bodi ya Taifa ya Maji kwa kushirikiana na Bodi ya Bonde la Mto Pangani yakagua kazi ya ufukuaji Mto Nduruma wilayani Arumeru na Simanjiro. Mradi huo umeleta nafuu kwa wananchi 10,000 waliokuwa wakikumbwa na mafuriko. Awamu ya kwanza yagharimu zaidi ya milioni 250. #Maji#Arumeru
Mkazi wa Kasomela, Kahama, Modesta Shinganga (52) afariki dunia baada ya kushambuliwa na fisi usiku wa Aprili 22 akitoka kwenye sherehe za Pasaka. Polisi Shinyanga wathibitisha tukio hilo. #Radio5Fm#Shinyanga#Tanzania
CHADEMA yapokea majeruhi 21 wanaodaiwa kupigwa na polisi Aprili 24 wakiwa njiani kuelekea Mahakama ya Kisutu kufuatilia kesi ya Tundu Lissu. Polisi Dar es Salaam wathibitisha kuwakamata na kuwaachia kwa dhamana wafuasi 5 waliodaiwa kushiriki mkusanyiko usio rasmi. #Radio5Fm
Papa Francis afariki dunia leo Aprili 21, 2025, akiwa na miaka 88. Vatican yatangaza alifariki akiwa nyumbani Vatican. Amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya upumuaji na nimonia kwa wiki kadhaa. Taarifa zaidi kufuata. #RipPapaFrancis#Vatican
Wapenzi wasikilizaji wetu,
Katika msimu huu wa Pasaka, tunapenda kuwapongeza na kuwatakia heri, amani na baraka tele. Pasaka ni wakati wa kutafakari juu ya upendo, matumaini na mshikamano – na sisi kama tunajivunia kuwa sehemu ya maisha yenu kila siku.
#Pasaka2025
Radio 5 inawatakia Ijumaa Kuu yenye tafakari, amani na baraka.
Tukumbuke upendo, msamaha na sadaka ya Yesu Kristo kwa ajili ya wokovu wetu.
#IjumaaKuu#GoodFriday#Radio5
“Radio 5 FM inawatakia Waislamu wote Eid Ul-Fitr Mubarak! Mwenyezi Mungu akubali swaum na ibada zenu, na awajalie amani, upendo na mafanikio. Furahia sikukuu yako! #EidMubarak#Radio5FM”
Rais Museveni amemteua mwanawe Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi (CDF).
Muhoozi anachukuwa nafasi ya Jenerali Wilson Mbasu Mbadi aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Nchi wa Biashara katika mabadiliko mapya ya baraza la mawaziri yaliyotangazwa jioni ya leo
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Antony Blinken, ametangaza leo Jumanne kwamba Rais Joe Biden atatembelea Israel siku ya Jumatano kufuatia mashambulio ya Hamas, na ametangaza kwamba Israel imekubali kufanya kazi na Marekani na Umoja wa Mataifa kuwasilisha msaada Gaza.