Mhe. Rais @MagufuliJP tarehe 13.10.2020 ametembelea Msikiti Mkuu uliojengwa Kinondoni Jijini DSM. Ujenzi wa Msikiti huo ulianza mwaka 2019 baada ya Mh. Rais kumuomba Mfalme Mohammed VI ajenge Msikiti mkubwa kwa ajili ya Waislamu wa Tanzania. Hivi sasa umekamilika kwa 100%
Hivi karibuni Serikali itatangaza zabuni ya ujenzi wa uwanja wa michezo wa kimataifa jijini Dodoma. Baada ya kukamilika, uwanja huo utakuwa ni mkubwa zaidi Afrika Mashariki na utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji tkriban 100,000.
#TanzaniaKwanza#SerikaliKazini
Kwa upande wa migogoro ya ardhi baadhi ya hatua ambazo Serikali ilichukua ni kuanzisha Ofisi za Ardhi Mikoa yote, ambapo sasa huduma zote za upangaji, upimaji, umilikishaji, utathmini pamoja na usajili wa hati, nyaraka, ramani na michoro zinapatikana kwa urahisi.
#MitanoYaUshindi
Hivi sasa ATCL inatoa huduma ya usafiri wa anga katika vituo 10 ndani ya nchi (Bukoba, Dodoma, Dar es Salaam, Iringa, Kigoma, Kilimanjaro, Tabora, Mbeya, Mwanza na Zanzibar) na 7 vya nje ya nchi (Bujumbura, Entebbe, Hahaya, Harare, Johannesburg, Lusaka na Mumbai)
#Kazi_inaendelea
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) ikishirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inakusudia kupitia upya gharama/makato ya kutoa na kupokea pesa kutoka kwa mawakala wa simu, na makato/gharama za kutuma na kupokea pesa toka simu kwenda benki au benki kwenda simu.
Serikali ya awamu ya Tano imefanikiwa kuondosha suala la uvuvi haramu kupitia oparesheni za ufuatiliaji wa uvuvi katika bahari ya Hindi, ukanda wa Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, Bwawa la Nyumba ya Mungu na Mtera jambo lililopelekea hivi sasa kupatikana kwa samaki wenye viwango.
Rais MAGUFULI ambaye ni Mwenyekiti wa SADC alibeba ajenda ya KISWAHILI kuwa ni lugha iliyofanikisha ukombozi Kusini mwa Afrika na hivyo Mkutano wa 39 wa Viongozi Wakuu wa nchi za SADC kuamua kuingiza lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya nne rasmi katika nchi 16 za SADC.
#TanzaniaYetu
Rias MAGUFULI amechagiza kusambaa kwa lugha ya Kiswahili kwa kuitumia lugha hiyo katika shughuli zake za kitaifa na kimataifa, hivyo kulazimu mataifa mbalimbali duniani kutafuta wakalimani wa kutafsiri hotuba zake kutokana na kuvutiwa na aina ya uongozi na utendaji wake.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesaini mkataba na kampuni ya mawasiliano ya mkongo wa Taifa ya Burundi (BBS) kwa ajili ya kupeleka huduma ya intaneti nchini humo.
Mkataba huo wa Sh13.8 bilioni utatekelezwa katika nchi ya Burundi kwa kipindi cha miaka 10.
โMy generation led Africa to political freedom. The current generation of leaders and peoples of Africa must pick up the flickering torch of African freedom, refuel it with their enthusiasm and determination, and carry it forward.โ- Mwl.Nyerere @_AfricanUnion