Wapendwa,
Nafikiri tumebakiwa na hatua moja tu kufikia lengo letu. Hebu fikirieni, kama kila mmoja ambaye tayari ameshachangia ataamua kutoa tena mchango wa kiwango kilekile alichotoa mwanzo, basi kufikia kesho tutakuwa tumekamilisha asilimia 100 ya mahitaji ya fedha za Baraza Kuu.
Hii ndiyo roho ya Tone Tone haswa Weekend hii, hatuhitaji mzigo mkubwa kutoka kwa mtu mmoja, bali moyo wa pamoja kutoka kwa wengi.
Tukiamua, tunaweza. Tukisimama pamoja, tunafika.
Asanteni sana kwa kujitoa, mshikamano wenu, na kuendelea kuamini katika wajibu huu mwema.
TONE TONE WEEKEND MISSION
“Kila tone lina thamani; pamoja tunatimiza kusudi.”
@SuluhuSamia Mhe Rais naendelea kushauri kwa dhati Tundu Lissu aachiwe huru kwani kesi haikamiliki. Hekima na busara iliyokufanya kutangaza sera ya 4Rs mara ulipoingia madarakani ikuongoze tena katika jambo hili. Simulizi hizi za kutisha za vyombo vya habari vya kimataifa, zinaibua hisia kali hasa kwa vijana, hata wazee tumekumbushwa kadhia ya operation Sogeza iliyounda vijiji vya ujamaa 1974 -1976. Taarifa hizi zinaathiri kikubwa taswira ya taifa letu na maslahi yake. Athari ni kubwa. Tutafute muafaka kupitia uwajibikaji na maridhiano. Tuwe na hofu ya Mungu na kutambua miujiza yake mfano wa risasi 16 kushindwa kukomesha uhai ingawa maumivu ni makubwa. Tutubu na kusali kuliombea taifa letu kila mtu kwa imani yake.
Ninyi ambao mnataka hiyo tume iliyoundwa kuchunguza kitu kinachoitwa ‘matukio ya uvunjifu wa amani’, mnataka taarifa yake kwa matumizi gani? Kama awali tulisema uundwaji wake hauna uhalali, ni batili, kwanini tusumbuke wao wakihangaika kuhairisha na kuchakata uongo, uzushi na ulaghai wao katika tume yao? Hata kama wakijiongezea siku 100 za kupika taarifa zao, sisi hiyo tume isiyotuhusu, tunateseka kwanini? Hata kama itatolewa au wataacha kuitoa, sisi ambao haituhusu, tunashughulika nayo kwanini? Nafikiri, hatujui kitu ambacho tunatakiwa kusimamia. Wanachama wa CHADEMA, kujadili jambo ambalo tayari mamlaka za chama chetu zimesema ni batili ni kupoteza mwelekeo. Mezani kuna mambo mengi sana ya kujadili. Tuachane na maigizo yao. Kila mtu ashinde mechi zake; tusiingilie yasiyotuhusu. Kamwe, tusisahau Oktoba 29, 2025.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, pamoja na wananchi wote kufuatia kifo cha mwanasiasa mkongwe, Selemani Bungara maarufu kama Bwege, kilichotokea leo tarehe 30 Machi, 2026 jijini Dar es Salaam.
MAWAKILI WA CHADEMA WAKIWASILI DODOMA KUTETEA CHAMA CHAO: Ni haki kwa mlalamikaji yeyote kutafuta haki yake mahakamani ila historia inaonesha matumizi ya mifumo ya mahakama kutatua migogoro ya vyama vya siasa hayajaonesha mafanikio ya kudumu barani Afrika. Mfano mashuhuri ni ANC iliyopigwa marufuku mwaka 1960 na Makaburu, ikalazimika kufanya shughuli zake kwa siri, takriban miaka 32 viongozi wake wakifungwa au kukaa uhamishoni.
Matokeo ANC ikajijengea uhalali mkubwa ndani na nje ya nchi na hatimaye, Mfumo wa ubaguzi ulipoanguka, ANC iliibuka ikiwa na nguvu zaidi na kushinda uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia mwaka 1994 chini ya uongozi wa Nelson Mandela. Jaribio la kukiondoa chama hicho kupitia sheria liliishia kukiimarisha.
Pili ni Senegal, chama cha PASTEF kilipigwa marufuku mwaka 2023. Hatua hiyo ilichochea hisia za wananchi dhidi ya kile kilichoonekana kama ukandamizaji wa kisiasa, na mwaka mmoja tu baadaye, 2024, viongozi wanaohusishwa na chama hicho walishinda urais. Tukio hili linaonyesha jinsi hatua za kisheria zinavyoweza kubadili chama cha upinzani kuwa alama ya mapambano ya kisiasa.
Tatu, Gambia, wakati wa utawala wa Yahya Jammeh, vyama vya upinzani vilikumbana na vizuizi vikali, ikiwa ni pamoja na kupigwa marufuku. Hata hivyo, vyama hivyo vilijipanga upya, vikaungana, na hatimaye kushinda uchaguzi wa mwaka 2016. Hivyo basi, ukandamizaji haukuondoa nguvu zao bali uliwafanya wawe na mshikamano zaidi.
Tanzania tunatambuliwa kuvisaidia vyama vya ukombozi wa Afrika hadi uhuru wao, huku vikiwa vimepigwa marufuku na tawala za kikoloni ikiwemo: ZANU-PF ya Zimbabwe, MPLA ya Angola, na FRELIMO ya Msumbiji.
Matumizi ya mahakama katika ushindani wa kisiasa hakulipi. USHAURI WANGU TUJISAHIHISHE NDANI NA NJE YA VYAMA VYETU kushindania uongozi bora hasa wakati huu tunapohitaji MARIDHIANO na MSHIKAMANO ili kulileta taifa letu Pamoja.
Tangu Mwenyekiti wetu akamatwe mwezi wa nne,
Leo ni miezi 11.
Watanzania wanajua na Dunia inajua kwamba Lissu hajafanya kosa, kesi hii ni ya uongo kwaajili ya kulinda Utawala usio na ridhaa, kutishia watu na kutaka tusitimize wajibu wetu kama chama kikuu cha siasa Tanzania.
Tangu mwezi wa 10 mwaka 2025, Mwenyekiti alikaa Magereza kwa zaidi ya miezi minne bila kesi kuendelea huku akiteseka bila sababu yoyote.
Tunajua hii kesi imefunguliwa kumtesa kiongozi wetu ili abadili msimamo wake kuhusu mambo ya Nchi yetu… kuhusu ufisadi wa serikali ya Samia , mauaji, utekaji, wizi wa mali za umma, maisha mabovu na uchumi wa hovyo kwa watu wetu… Tunajua anateswa kwasababu yetu Watanzania.
Rufaa ya juzi kwa mambo yasikatiwa rufaa ni ushahidi mwingine kwamba hakuna kesi bali kumpotezea Mwenyekiti muda wake na kumtesa..
Huu ni mwezi sasa Mahakama iko kimya, tunajiuliza kesi yenye uzito kama huu kwa mtu ambae amekaa ndani mda wote huu.. inakuaje mahakama isione urgency kwenye jambo hili..
Mahakama iliyotegemewa kutoa haki na kumaliza jambo hili kwa haraka, inapokaa kimya kunakua na mashaka makubwa..
Sisi hatuwezi kuendelea kunyamazia suala hili.
Tunataka huu uhuni ukome haraka , Mwenyekiti wetu aachiwe arudi kufanya wajibu wake.
Wanachama wetu na Watanzania hawataendelea kukalia kimya uonevu wa wazi kwa mtu asiye na hatia.
MAHAKAMA YA RUFAA KUSIKILIZA MAOMBI YA MAREJEO YA KESI YA CHADEMA TAREHE 24-03-2026
Leo Machi 13, 2026 CHADEMA tumepokea wito kutoka Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, unaosema Mahakama ya Rufaa itasikiliza marejeo (Revision) ya kesi ya Said Issa Mohamed na wenzake dhidi ya Bodi ya wadhamini wa Chama na Katibu Mkuu wa Chama tarehe 24/03/2026 mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa ambao ni Mhe Jaji Mwarija, Maige na Mwampashi.
CHADEMA mnamo tarehe 23/02/2026 kupitia Wanasheria wa Chama chini ya Dr Rugemeleza Nshala iliandika barua kwa Mhe Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, tukiomba kuitwa kwa dharura kwa mwenendo wa kesi ya madai ya Saidi Issa Mohamed na wenzake dhidi ya Bodi ya wadhamini wa Chama pamoja na Katibu Mkuu wa Chama, pamoja na maombi mengine yaliyotokana na kesi hiyo, yakiwemo maombi yaliyopelekea amri ya zuio kwa chama, maombi ya kupewa nyaraka pamoja na maamuzi yote yaliyofanyika kuhusiana na kesi husika.
Sababu ya Chama kuomba Mahakama ya Rufaa kufanya Revision ni kutokana na mwenendo wa shauri huo ambao chama kinaona uko kinyume na matakwa ya sheria mbalimbali, maamuzi ambayo yanakinzana na maamuzi ambayo Mahakama ya Rufaa iliyatoa na hivyo, Chama kikaomba mahakama ya Rufaa kutumia mamlaka yake kufanya Revision.
Mhe Jaji Mkuu baada ya kupata barua ya malalamiko ya Chama, mnamo tarehe 06/03/2026 alitoa maelekezo kwamba Mahakama ya Rufaa ifungue jalada na kufanya Revision ya shauri namba 8323/2025 na maombi yote madogo yaliyotokana na shauri hilo, ambapo mahakama ya Rufaa imefungua Civil Revision No. 1/2026, Said Issa Mohamed na wenzake dhidi ya Bodi ya wadhamini na Katibu Mkuu ambayo ni Revision inayotokana na mwenendo na uamuzi wa mahakama kuu ya Tanzania, Masijala ndogo DSM mbele ya Jaji Mwanga, kwenye shauri namba 8323/2025.
Pili, Mahakama ya Rufaa imefungua pia Civil Revision No. 2/2026 Kati ya Said Issa Mohamed & wenzake dhidi ya Bodi ya wadhamini wa Chama namba Katibu Mkuu, Revision inayotokana na mwenendo,Uamuzi na Amri ya Mahakama kuu, Masijala ya DSM ya tarehe 18/08/2025 mbele ya Mhe Jaji Mwanga, yaliyotokana ma civil cause no. 8960/2025 maombi pia ambayo yalitokana na kesi ya msingi namba 8323/2025.
Tatu, Mahakama ya Rufaa pia imefungua Civil Revision No. 3/2026 baina ya wadawa hao hao, ambapo mahakama itafanya revision kwenye mwenendo, uamuzi na amri za mahakama kuu, Masijala ya DSM mbele ya Mhe Jaji Mwanga ya tarehe 29/09/2025 kwenye maombi madogo namba 20585/2025 nayo yakitokana na kesi ya msingi namba 8323/2025.
Nne, Mahakama ya Rufaa pia imefungua Civil Revision No. 4/2026 Kati ya wadawa hao hao , revision inayotokana na mwenendo, uamuzi na amri za mahakama kuu, Masijala ya DSM mbele ya Jaji Mwanga, ya tarehe 10/06/2025, maombi ambayo yalitokana na kesi ya msingi No. 8323/2025. ( Mwenendo na uamuzi huu ndiyo vilitoa amri ya zuio kwa Chama)
Revision hizo zimeitishwa na mahakama yenyewe, kwa lugha ya kisheria inaitwa “suo motto Revision” na kupangiwa majaji niliowataja hapo awali.
Revision hizi ni fursa kwa Chama, kama ambavyo tumepokea wito kufika mbele ya Mahakama ya Rufaa kuieleza mambo yote yaliyofanywa na mahakama kuu kwa maana ya Mhe Jaji Mwanga ambayo yalikuwa kinyume na katiba, sheria za nchi hii na au kinyume na maamuzi ya Mahakama ya Rufaa.
Mawakili wa Chama wanaendelea na Maandalizi, watafika Dodoma kama wito unavyosema na kutetea na kulinda Chama Mahakamani.
Director for Legal and Human Rights - CHADEMA
Tarehe 13-03-2026 kesi ya Jinai namba 21/2026 inayomkabili Yohana Kaunya (Katibu Mkuu Mstaafu wa Baraza la Vijana Chadema Taifa) itaendelea kusikilizwa, Mahakama ya wilaya Bunda kuanzia saa tatu kamili Asubuhi.
Shauri hilo litaendelea kwa upande wa Jamhuri kuendelea na mashahidi wao, ambapo hadi sasa jumla ya mashahidi 6 wameshatoa ushahidi wao.
Awali, Jamhuri walidai wataleta jumla ya mashahidi 41 kuthibitisha mashitaka yao.
Wananchi mliokaribu na Mahakama ya wilaya ya Bunda na viunga vyake, tukutane Mahakamani kesho, kama ilivyo desturi yetu!!!
Katibu Mkuu Mhe. John Mnyika pamoja na Mwanasheria Mkuu wa chama, Dr. Rugemeleza Nshala wakiwa kwenye picha pamoja na mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa United Nations, Mhe. Parfait Onanga-Anyanga, baada ya kufanya mazungumzo jana katika ofisi za Umoja wa Mataifa Dar es Salaam.
#BreakingNews Leo tarehe 06, Machi 2026 Mahakama ya Wilaya ya Magu imetoa hukumu katika kesi ya jinai namba 2037/2026 inayowakabili Peter Jackson Masulya na wenzake sita, kwa kuwaachia huru washitakiwa wote baada ya Mahakama kubaini kuwa hawana hatia.
Washitakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na tuhuma za kuchoma moto majengo ya Serikali kufuatia vurugu zilizotokea tarehe 29 Oktoba 2025. Awali, walikuwa wameshtakiwa kwa kosa la uhaini, ambapo upande wa Jamhuri ulieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa bado unaendelea.
Baadaye katika mwaka huu, Jamhuri iliwasilisha hati nyingine ya mashitaka ikidai kuwa washitakiwa hao walihusika pia na kuchoma moto Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kisesa, Mahakama ya Mwanzo Kisesa, pamoja na Ofisi ya Katibu Tarafa.
Hata hivyo, katika uamuzi wake uliotolewa leo, Mahakama imeeleza kuwa upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa hao pasipo kuacha shaka yoyote. Kutokana na hali hiyo, Mahakama ikaamua kuwaachia huru washitakiwa wote.
IT GOES WITHOUT SAYING " MTANI " AND BROTHER HON. EMMANUEL NCHIMBI.
We all aim to serve this same Nation.
Even the Circus against an innocent person like Adv.Tundu Antipas Lissu is manifestation of hatred in our community
The Office of the Registrar of Political Parties and the Tanzanian Police Force are the champion in attacking and propagating hatred.against the true and credible opposition parties
The silence on the massacre of women, youth and children in October was caused by hatred against the Opposition and people with alternative views.
TRUTH, JUSTICE AND ACCOUNTABILITY will heal the Nation
BAK MWABUKUSI.
Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) linatarajia kuadhimisha Siku ya Mwanamke Duniani Machi 08, 2026 ambapo kitaifa itaadhimishwa Mkoani Mara katika wilaya Musoma.
MREJESHO WA KESI ZA WANACHAMA MAGU, BUKOBA NA ILEMELA:
Leo Mahakama ya Wilaya MAGU imeahirisha kusoma hukumu dhidi ya wanachama 7 wanaotuhumiwa kuchoma moto majengo ya umma hadi tarehe 6 Machi 2026.
KUTOKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI BUKOBA.
Leo pia mahakama imemwachia aliyekuwa maya wa Manispa ya Bukoba, Mhe Chief Kalumuna na wenzake 14 waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya jinai.
KUTOKA MAHAKAMA YA WILAYA ILEMELA:
Jana mahakama ya wilaya ikifika kesi ya Uhaini dhidi ya viongozi 5 wa kata ya Buswelu baada ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai kudai Hana nia ya kuendelea na shitaka hilo. Viongozi hao bado wanakabiliwa na kosa lingine la wizi.
Tarehe 2, Machi kesi hiyo ya tuhuma za wizi itaendelea mahakama ya wilaya ya ilemela ambapo pia tunatarajiwa watuhumiwa watapata dhamana baada ya kosa la Uhaini lisilo na dhamana kufutwa.
Wakati mwingine huwa namwona Anthony Mtaka kama mbegu nzuri iliyoanguka kwenye udongo mbaya.
Jamaa ni leadership material fulani hivi ambayo haiendani kabisa na system anayoiwakilisha.
Baada ya ile massacre ya Oct 29, nadhani ni Mtaka pekee aliyekiri magnitude ya ushenzi wa dola na kutoa chozi hadharani.
Sijui ilikuwaje akawa sehemu ya utawala wa kishetani kama huu!