Wakati Serikali inapitia sheria za uchaguzi na vyama vya siasa, ipitie pia Sheria kandamizi ya mifuko ya hifadhi ya jamii hasa sekta binafsi @nssftz. Mtu akiacha kazi kwa lazima/hiari apewe mafao yake yote ili apate mtaji wa kujiajiri.
#KujiajiriKunalipa#TupeniPesaZetuTujiajiri
#BreakingNews
Kesi ya Mgawanyo wa mali za CHADEMA imefutwa leo naona Said Issa na waliomtuma wameweka mpira kwapani.
Na bado hata kesi ya Mhe. Lissu watafuta tu
Kumbe VISA mnataka.๐
REPOST 200
Wewe ni malaya mzoefu wa kisiasa, arenโt you?
Umerudi kwakuwa ccm wameuwa, au kwakuwa hukuamini watauwa?
Walianza kuuwa Oktoba 29?
For some of us it, it will take a village to trust clowns like you!
Pole sana!
@godbless_lema Msenge motivational speaker kama mpuuzi Nanauka.. mtu yeyote wa maana hawezi kuwa sehemu ya serikali ya muuwaji Samia. Soft tongue haisaidii. Usi endorse hawa wapumbavu Mangi.
Tarehe 15 Septemba ni maadhimisho ya siku ya demokrasia duniani, Chadema tutaadhimisha siku hii kidigitali ka kuwakutanisha watoa mada #Barazani na kujadili hali ya kidemokrasia nchini.
Kauli mbiu ya mwaka huu "Demokrasia na Uchaguzi Bandia Tanzania." Watu mbalimbali wa ndani na nje ya Chama watashiriki.
#NoReformsNoElection
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 14
Anaendelea Mhe. Lissu
Swali je mfanyaje?
Mahakama ifanye nini?
Turudi Kisutu?
Ndio Swali lililoulizwa tangu juzi. Turudi Kisutu?
Mnakumbuka wakati namalizia hoja yangu nilisema futeni haya mashauri nirudi nyumbani kwangu nikalale niliwaambia.
On the bases of the law of this country you have no option than setting me free.
Kama mahakama ya kisutu haikuwa na mamlaka basi maana yake tunaendaje kisutu?
Kuna kesi gani sasa kama mmefuta committal?
Mkiamuru turudi Kisutu ndio Kisutu itakuwa na jurisdiction kwa kuwa mmesema kwasababu Kisutu haina mamlaka Kisheria.
Pia hoja ya Mrema kunirudisha nikaanze mwanzo pale Kisutu.
Kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Mahakama ikifuta kesi imefuta proceedings anaendeleaje kukaa gerezani mshitakiwa?
My submission is that decision was made per incurium na maana yake ni kwamba mahakama imefanya uamuzi kwa kusahau sheria kwa ambao hamjui kilatini. Maana yake ni hiyo.
Watu wanacheka hapa ๐คฃ๐คฃ
Decision made per incurium hatusemi majaji hawajui sheria tunasema wamesahau.
Wahesimiwa majaji hii sio kesi rahisi na kufanya maamuzi ninayotaka mfanye sio maamuzi rahisi pia.
Mnapaswa kufanya maamuzi bila kuogopa chochote.
Msimame kwa miguu yenu.
Mjiamini na mquash this proceedings, yaondoeni haya mashtika.
Swali linabaki kuwa what about Mbinga?
Mpaka hapa tulipo mkinipeleka Mbinga naenda kufanya nini? Labda niende kumsalimia Dada angu Songea na sio mimi kwenda Mbinga.
Mkifuta kesi siendi ukonga Prison tena. Naenda nyumbani kwahiyo majibu ya hilo swala la Mbinga ndio hilo.
Nawaombeni individually and collectively. Each one of you will have to write ruling.
Ameanza kuzungumzia kanuni za kuteua majaji watatu mamlaka hayo anayo CJ ZIMETUNGWA juzi hapa tarehe 05/09.
Nimemaliza Waheshimiwa majaji, nimemaliza mimi.
Nawashukuru sana.
Sasa uamuzi wa watu waliosahau sheria hauwezi kunirudisha gerezani nikifutiwa mashitaka yangu narudi nyumbani. I walk home free.
Mhe Lissu kamaliza kuwasilisha hoja zake hapa.
Sema nini hapa mwisho Mhe. Lissu kaongea kwa hisia mpaka tumachozi tumenitoka, si unajua sisi Wanawake tukogo emotional sana.๐ฅน
Tuendelee
Baada ya Mhe. Lissu kumaliza
Watu wanateta na sauti zinazosikika nyingi sana ni watu wanasema KIMEUMANA๐
Majaji wanaandika jambo hapa na kuteta pamoja.
Mhe Lissu anakusanya vitabu vyake vingi vya sheria na makaratasi yake kibao aliyonayo.
Sijui kwanini ameanza mapema kuyakusanya si angesubiri mahakama iahirishwe ndio aanze kuyakusanya na hawa magereza tumsalimie hata kidogo juu kwa juu.๐๐๐๐
Watu waliokuja mahakamani badala wasilitike kwa hii kesi lakini sura zao zinaonekana zina amani na bashasha sana. Watu wamefurahia show za Mh. Lissu.
Tulikuwa tunafuatilia kesi ambayo mwisho wake mtu anaweza hukumiwa kunyongwa lakini wafuatiliaji tunaenjoy utadhani tunaangalia movie tuipendayo.
Au kama mtu aliyeshinda bingo
Nimewasikia waliokaa huko gorofani wanasema taratibu Utatoa hutoi?
Sijui wanamwambia nani maana hawakawii kuwa wanataka kumwambia Job Mrema hayo mambo.๐๐๐๐
Sasa Jaji anahangaika kuwasha kipaza sauti hapa tusikie ataahirisha kesi au watasema wanasoma ruling Leo leo.
Maana hapa ni either watupe tarehe au watuambie watasoma ruling mchana wa leo.
Sidhani kama kwa ubishani hili suala litaisha leo leo lazima wapate muda wakuandika na kutafakari kama sio maelekezo kutoka juu kama yatakuwepo ingawa juzi hapa Jaji Mkuu alisema maelezo kutoka juu yasiwepo.๐๐๐
Sasa Jaji Ndunguru anaongea.
Nawashukuru sana pande zote.
Mmewasilisha mambo mengi sana toka jumatatu. Mmetoa authorities nyingi kurejea hoja zenu na kufanya uchambuzi wa vifungu nbalimbali vya sheria.
Na sisi tunahitajika kwenda kuandaa uamuzi wetu.
Tukasome na kuvipitia kwahiyo tukutane hapa siku ya Jumatatu tarehe 15/09/2025 saa tatu asubuhi kwa ajili ya ruling (uamuzi mdogo). Ahsanteni sana.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
SUMMARY KUHUSU KESI YA UHAINI ALIYOBAMBIKWA MHE. LISSU
Kwa faida ya wafuatiliaji.
Kilichofanyika kwa hizi siku tatu ni kusikilizwa pingamizi moja kati ya mapingamizi mawili aliyoyaibua Mh. Tundu Lissu.
Hili la kwanza ambalo tulikuwa tunalisikiliza ni kuhusu mamlaka ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam kusikiliza shauri hili wakati kuna mapungufu mengi kwenye mahakama ya ukabidhi yani Kisutu.
Tayari limesha sikilizwa na sasa tunasubiri uamuzi wake ambao Jaji Nduguru amesama atatoa siku ya jumatatu.
Pingamizi la pili lenyewe litasikilizwa mara baada ya mahakama kutoa uamuzi juu ya pingamiza la kwanza.
Endapo kama Mahakama itasema kuwa kesi hii iendelee basi mshitakiwa atasomewa mashitaka yake, atayajibu na baada ya kuyajibu sasa kabla ya kesi kuanza kusikilizwa Makamana italazimika kusikiliza hayo mapingamizi ya awali kwamba
Hati ya mashitaka iliyoletwa ni defective yaani ni hati mbovu, haiko kisheria ina matege na inaumwa sana haiwezi kuwa na afya ya kusimama na kuchukuliwa kama ni nyaraka ya kufungua mashauri kwa mujibu wa sheria.
Inatakiwa hati ya mashitaka kisheria ukiiangalia uone inayaelezea hayo mashitaka haswa ni yapi na yawe yameandikwa kisheria na kuelezea hilo kosa ni lipi?
Sasa hilo pingamizi litasikilizwa hapo baadae so kwasasa acha tuhangaike na yaliyopo.
Nawashukuruni sana kwa kufuatilia kesi hii kupitia ukurasa huu.
Mengine nitawauliza wanasheria wetu ili tupate uchambuzi wa kina ili tueleweshana kipi ni kipi.
Hadi hii kesi itakapoisha wengi wetu tutakuwa tumejifunza mengi kuhusu sheria
Unaweza unakuta baada ya hapa wengine wakaananza hata kupiga deal za kisheria akitokea mteja kajichanga maana maisha yenyewe yashakuwa magumu.
Tunaishia hapo kwa leo.
Nawatakia mchana mwema!
Mhabarishaji wenu Hilda Newton.
Wahuni walipochukua nchi offficially
Walianza na EPA 2005/2008
wakafuatia Richmond 2006/2008
Wakaja na Escrow 2013/2014
Haya yalifanyika kwenye awamu ya Kikwete na Rostam.
Wote wataenda jela.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 13
Anaendelea Mhe. Lissu
Upande wa mashitaka unalazimisha kuipa mamlaka Kisutu ambayo haikuwa na hayo mamlaka, wao wanasema inayo mamlaka mimi nasema haina.
George Abdon Kilinga mahakama inasema walikubaliana.Totally wrong. It is distinguishable.
Joseph Mkenda vs Ladislaus...... tulipewa kesi hiyo nyingine....kesi inahusiana na mauziano ya ardhi na mnunuzi aliuziwa ardhi na mtu ambae sio mmiliki kwahiyo mahakama ilishughulika na jambo kama kesi ya mkataba na sio kesi ya ardhi.
Jaji alitoa Obiter dictum kwamba Jurisdiction of the court is the creature of the law.
Obiter dictum maana yake ni maneno yaziada kwenye hukumu sio yanayoamua kesi husika.
Sasa hata ingekuwa sio ibiter dictum mimi sina pingamizi mambo yaliyosemwa hapo na mimi nasema hii kesi inaunga mkono ninachosema nashukuru sana kwa wao kuniletea hii kesi.๐
Kesi ya tatu Commisioner General TRA na wenzake.
What was the issue before the Court of appeal? Whether the High Court has the jurisdiction to assume its revisionary jurisdiction. Ilifanya review ya mambo ya kodi kwenye mgogoro mwingine.
Nani atakayebisha msimamo huo baada ya kusoma aliyosoma? Mimi sibishi.
Hoja ya msingi the question of jurisdiction ambayo kisutu iliendelea na shauri ambalo haina mamlaka kulisikiliza.
Je mnatakiwa kuendelea na hilo kwa mtindo huo. You should not condon such illegality.
Na hii kesi ya Job Mrema nayo pia inaunga mkono hoja yangu ndio maana niliwashukuru kwakweli.
Kuhusu kesi ya Elias John.
Kesi hii ii ilikuwa ndio Climax ya hoja za wakili wa serikali mwandamizi alileta kwa mbwembwe sana.
Kwamba huyu mshitakiwa angejua wala asingeleta haya mambo alisema hivyo.
Hii kesi ilikuwa ni kesi ya mauaji na wakata rufaa Elias , Daniel, Dotto walikuwa convicted of murder and sentenced to hell the committal proceedings were conducted to Chato District Court where they have arrested.
In the High Court ilisema kulikuwa na makosa mengi mahakama ya Committal kule chini.
Mahakama kuu iliona hii committal haikuwa halali ikaifutilia mbali na kuamua committal ifanyike de novo. Ifanyike upya. Hiyo committal denovo haikufanyika.
Mahakama kuu ikaendelea na kesi bila committal kufanyika na mahakama kuu ikaendekea na kesi na kuwahukumu kifo washitakiwa wote wawili.
Kesi ikaenda mahakama ya rufaa mtaona majaji kuanzia ukurasa wa 6 mpaka wa 9 mahakama ya rufani inazungumzia jinsi mahakama kuu ilikosea kuendesha kesi bila committal order.
Mahakama ya rufani kwa kutumia revisionary power ikafutilia mbali proceedings za mahakama kuu na mahakama ya Chato.
Halafu mwisho kabisa mahakama kuu baada ya kuwa imefuta proceedings zote watu wamehukumiwa kifo, ikasema sasa hawa waliohukumiwa kifo waendelee kukaa gerezani meanwhile the Appellant shall remain in custody for afresh new committal.
Ndio maana wakili Job Mrema alikuwa anasema tutarudi Kisutu, tena alikuwa anasema kwa mbwembwe kabisa.
Sasa naomba niseme yafuatayo.
1. On its facts Elias Dotto case is completely distinguishable with the case at hand in other words is completely irrelevant here. Kwenye facts zake. Kesi ilisikilizwa na sentenced to death.
Mimi I'm a mere accused. Charge yangu inahusiana na mambo ya kisiasa tu je inafananaje na convicted murderers.
2. Committal ilifanyika vibaya na mahakama kuu ikaifuta na wakaendelea na kesi.
Hapa kwangu bado hamjasema kuwa committal ilikuwa ni mbovu, hoja yangu hapa ni kwamba toka jumatatu nawaambia msiendeleee na kesi hii kutokana na makosa yaliyofayika kisutu.
Sasa hizi kesi zinalinganaje?
Mfanano wake ni upi?
I'm asking the court not to follow in that trap. Msifanye kesi iliyotoka committal Court unlawful inalingajaje na hii?
Hata hii kesi is totally irrerelevant to this case.
Part 14 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 12
Anaendelea Mhe. Lissu
Tatu. Mahakama ya Rufaa kwenye kesi ya Dodoli Kapufi ilisema nini kuhusu kifungu cha 183?
Jaji Chande alisema in essence that section is deal with trial not deal with Committal. Section inayodeal na committal ni S. 261.
Nimemaliza na hiyo niendeleee na kesi yao nyingine.
Hii nayo imeletwa bure kabisa.๐
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba nishughulike na JOB MREMA.
Huyu Katuga nimemaliza nae.
Anasimama Katuga anasema kifungu cha 187 hajakisemea.
Mhe. Lissu anasema nawashukuru sana Katuga. Ngoja nije hapo.
Hicho cha 187 trial at a place where act done.
Hii section is about trial na section about committal is 262, 263 hadi 265.
Hivyo basi kama ambavyo sect. 183 ilivyo irrelevant basi hata section 187 nayo ni hivyo hivyo haihusiki hapa tunazungumzia committal. Tofautisha Committal na trial.
Sasa nirejee kwenye suala la Mashahidi. Nalo lilizunguzwa na Mrema na nimesema naanza kushughulika nae.
Suala la Mashahidi wangu kutokuandikwa. Walilizungumza.
Katuga anasema hawakuitwa na kuandikwa wanaweza kuandikwa baadae hakuna tatizo. There is no prejudice.
Wakili Mrema pia alisema Mshitakiwa alishauriwa kuwa majina ya mashahidi atakuja kuwasema mahakama kuu. That one was premature kwahiyo hamna shida.
Waheshimiwa majaji naomba niwaonyeshe jinsi ambayo hii nayo ni shida kubwa.
Mashahidi kutokuandikwa kwenye commitall proceedings.
Ipo hivi Waheshimiwa majaji, Mshitakiwa ana haki ya kutamka majina na anuani ya mashahidi wake wakati wa committal maana asipoitumia inabaki fadhila ya mahakama.
Kwenye committal nilikuwa na haki ya kusema mashahidi wangu na anuani zao. Kwenye mahakama hii ni descretion yenu sio haki yangu tena.
Mnaweza kuamua au msiamue sasa niwapeleke kwenye sheria.
Kifungu cha 264 cha CPA ndo kinatoa haki kwa mshitakiwa kutaja majina ya mashahidi wake wote.
Nikisema nina mashahidi wewe Hakimu KISWAGA huwezi sema nitawasemea mahakama kuu, unapaswa kuandika.
Hilo halikufanyika.
Mawakili wa serikali wanasema ni premature, unaweza kuita baadae, sasa hiyo baadae iko kifungu cha 281 na 314 ya CPA. (Kumbukeni CPA ni Criminal Procedure Act - Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai)
S. 281 inasema hivi msajili wa mahakama kuu ataandaa wito kwa mashahidi wote ambao orodha yao ipo. Registrar/ msajili anatoa summons/wito kwa hao uliowataja. Kinasema hivyo.
Sasa kama hujataja nini kinapaswa kufanyika ndio S. 314 inaingia hapo. Kinasema hivyo mtuhumiwa hawezi kuwa na haki ya kuita mashahidi wake ambao hawakuwa kwenye orodha yake labda mahakama ijiridhishe kuwa kuna umuhimu wa mashahidi hao kuitwa.
Sasa hii ni fadhira ya majaji haki yangu nimesema ilikuwa Kisutu.
The accused person shall not be entitled to call witness without approval au consent ya majaji sasa kuna prejudice kubwa kuliko hiyo kunyang'anywa mashahidi wangu.
Haya maneno ya kwamba naweza kuwaita baadae ni maneno ya watu wenye nia mbaya sana na mimi.
Wanasema mambo ambayo sheria haiyatambui na kuyakubali, naomba waheshimiwa majaji msikubali jambo hili.
Sasa Job Mrema alisema majaji mnapaswa mjiulize hili pingamizi kama liko sawasawa mbele ya mahakama hii.
Na alilisema jambo hili kwa mbewembwe kabisa.
George Abdon Kilinga na wenzake vs Anna na wenzake ni mashauri ambayo aliyaleta hapa.
Kwanza hii ni kesi ya mirathi ilianzia mahakama ya mwanzo, ikaenda mahakama ya wilaya ya Babati ambayo iliamua kwamba wadaaawa wataamua watumie sheria gani? Mahakama kuu rufaa ya pili sasa Madam Justice alisema parties can not by agreement confer jurisdiction to a Court.
Wadaawa hawawezi jiamulia kuipa mamlaka mahakama hii kwasababu suala la jurisdiction (mamlaka) ni suala la Jaji.
Kwenye kesi yangu sasa Mshitakiwa anasema alikuwa committed na mahakama ambayo haikuwa na mamlaka.
Part 13 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 11
Anaendelea Mhe. Lissu
Walinipa uamuzi wa kesi ya Ishengoma na wenzake sita.
Kesi ya Mahakama ya Rufani hiyo Kesi ya Donatus Ishengoma ukurasa wa 15 umecite kesi ya Mbogo niliyoitaja hapo awali.
Anasoma hiyo kesi hapa ilichosema. Maelezo marefu hapa.....
Waheshimiwa majaji nani anauwezo kuwa na ubishi na hili, Mimi sina.
Sina ubishi na superior Court can do on interference to surbodinate court.
Kifungu cha 265 hakina descretion kihivyo wanavyodhani. Its only partially decretion. Naomba nikisome hicho kifungu.
Anakisoma sasa hicho kifungu hapa.
Descretion nimeambiwa hapa kwamba ni kumpeleka mtuhumiwa gerezani. Hiyo ni 265(1).
Ukianza kusoma vifungu vingine ikitaka kuahirisha iandike sababu za hayo maahirisho.
Mamlaka haina option ya kutokuandika sababu na haina option ya kutokutoa reason hizo.
Naomba niendleee hiyo kesi ya ishengoma imeenda kwa kiwango hicho.
Naendelea na kesi zao zingine.
Waheshimiwa majaji wakili Kasuga aahhh samahani Katuga aliuliza a very rhetorical question kwamba sasa turudi kisutu?
Hili nitalijibia lamwisho.
Twende kwenye improper dating kubadilisha proceedings na kubadilisha tarehe za matukio mahakamani.
Tuliambia hiyo ni amere sleeping of the pen na tukapewa Kesi ya Baraka Mashaka Kesi ya Mahakama kuu PC Civil appeal/2023.
Hoja yangu ni kwamba kukiwa na kosa moja au mawili kwenye kurasa 101 unaweza kusema ni sleep of a pen.
Sasa ukiwa na makosa mia kwenye nyaraka hiyo hilo la kukosea tarehe haliwi kosa dogo kabisa lazima yaangaliwe kwa uzito.
They are part of the designing kwangu mimi na naomba hayo makosa ya kuteleza kwa mkono naomba yachukuliwe kuwa sio kuteleza kwa mkono yachukuliwe kama sehemu ya uchafu mwingi uliopo humu na niliousema toka siku ya kwanza.
Kwenye hiyo kesi hiyo mshitakiwa alihukumiwa maisha kwa kumfanya kinyume na maumbile mtoto lakini mahakama ikamfunga kwa kosa la armed robbery.
Mahakama ya rufaa ilisema kwa vile adhabu ni ileile kwa makosa hayo basi ni sleep if a pen.
Sasa huwezi kuleta kesi ya namna hii itumike kwenye hoja za kesi tuliyonayo leo hapa.
Kuna kitu amekisema sana Katuga kwamba malalamiko yangu ni kutaka huruma amekisema toka kisutu.
Sympathy..!! Ilianzia Kisutu imekuja hadi mahakama hii.
Pamoja na kwamba sidhani kama itaamua one way to other naomba niweke for the record kupata huruma unapoonewa sio jambo baya.
Kuomba huruma unapokuwa kwenye matatizo sio jambo baya.
Kama anadhani ukipata matatizo unahitaji huruma.
Sasa la msingi ni nini? Siwaombi Majaji chochote mtakachoamua msiamue kwa huruma. Muamue yote kwa haki na kwa mujibu wa viapo vyenu. Msinihurumie na sihitaji huruma yenu nahitaji muamue kwa haki.
Nayasema haya for the record nimeona Katuga anayarudia rudia sana.
Kuna hoja ilitolewa na Katuga na imerudiwa na Mrema kuhusu kifungu cha 183 cha CPA.
Job Mrema anasema inapaswa kusomwa na 187 pia za CPA izo zote zinazungumzia mamlaka ya mahakama.
Mahakama ya Kisutu. CPA ni sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
S. 183 inazungumzia general authority of Court in Tanzania. Kwamba mahakama yoyote ina mamlaka ya kuamrisha mtu kwenda mahakamani ndani eneo la mahakama hiyo kama mtu huyo amefanya kosa ndani ya eneo la utawala wa mahakama hiyo.
Sasa wameleta hii ili waseme kwamba uliletwa kisutu kwasababu ulifanyia kosa Dar es salaam hicho kifungu walichotaja cha 183 kinazungumzia tayari ameshashtakiwa kinaipa mamlaka amri aletwe kwenye mahakama husika.
Mimi nilikamatwa Mbinga na wakati nakamatwa sikuwa mshitakiwa.
Mimi nimekuwa mshitakiwa baada ya kupelekwa Kisutu na kusomewa mashtaka.
Sababu ya pili ni kwamba kwani nilipelekwa Kisutu kwasababu mahakama iliamua nipelekwe kisutu? Hakukuwa na order hiyo.
Kwahiyo S. 183 haiwezi ku apply kabisa.
Part 12 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 11, 2025
Jana tuliishia Part 9 so leo tunaendelea na
Part 10
Hali ya hewa ya mahakama ni nzuri na imetulia.
Askari magereza wameingia hawa wawili watatu ambao wamekuwa wakivaa haya madude usoni ingawa wengi wao siku hizi hawajifichi sura zao kama walivokuwa wanajificha wakati tupo Kisutu.
Imesikika sauti ndogo ya askari High Courtttttttttt.
Kinyonge sana ni kama jamaa hajapata breakfast.๐
Majaji wanaingia na watu wote wamesimama.
Mheshimiwa Lissu ameingia na style yake mpya anakunja ngumi na kuizungusha kwa vibe sana kama kwenye ile video mliyoiona juzi.
Majaji wanaandika andika muda huu.
Wameingia kwa tabasamu kubwa sana leo Majaji wote watatu.
Wamevaa haya magauni yao mekundu na hivi vitai vyeupe shingoni kwao.
Jaji Nduguru kiongozi wa jopo anateta jambo na Kalani wa mahakama.
Sasa Jaji anataka kuongea hapa huku anamuangalia Mh. Tundu Lissu.
Karani anaita kesi Criminal Case No. 19605/2025.
Jaji: Jamhuri Karibuni.
Katuga: Nipo na Misieh Kahima, Thawabu Issa, Harrison Lukosi, Cathbert Mbirnge hawa wote ni Mawakili wa Serikali ambao ni 6 tunaiwakilisha Jamhuri katika shauri hili na mshitakiwa yupo Mheshimiwa Jaji.
Katuga: Tunaendeela na usikilizaji wa mapingamizi na mwenzetu mshitakiwa kama yupo tayari aendeleee. Sisi hatuna shida.
Jaji: anaandika. Anamuuliza Mh. Lissu vipi uko tayari.
Mhe. Lissu: Niko tayari na imara kabisa.
Jaji: anaandika na kuteta kidogo na wenzake.
Sasa unaweza kuendelea ndugu Lissu.
Mhe. Lissu Waheshimiwa Majaji nimefurahi kuwaona na niwapongeze kwa kazi kubwa mliyofanya toka jumatatu.
Lissu anaendelea sasa.
Jana niliomba ahirisho ili nikasome kesi walizonipa hawa jamhuri naomba niseme hiyo kazi nimeifanya vizuri sana.
Niwashukuru mawakili wa serikali kuleta hizo kesi kwasababu zitanisaidia sana kuja kusema nitakachosema siku ya leo.
Ni kesi wamezileta wenyewe sio mimi.
Wakili wa serikali Katuga na Mrema walitoa hizo kesi wenyewe kwahiyo nitaonesha namna hizo kesi kama ni relevant au sio relevant kwa kesi tuliyonayo.
Kwa kuanzia naomba nizungumzie kauli ambayo ilitolewa juzi na wakili wa serikali Mkuu Katuga kwamba committal proceedings lengo lake ni kuhakikisha fair trial.
Hiyo position ipo kwenye maamuzi mengi ambayo yametajwa toka jumatatu mimi nakubaliana na msimamo huo ni kuhakikisha kuna fair trial katika kesi zinazosikilizwa mahakama kuu. Na kesi hizo ni kesi kubwa.
Kama lengo ni kuhakikisha fair trial/hearing hivyo basi committal Court is responsible to make sure the accused person is given full opportunity
Huwezi kumpa nyaraka nusunusu mtuhumiwa kwenye kesi yake, huwezi kuacha makosa mengi yote kama yaliyopo.
Ni lazima mshitakiwa apewe nafasi ya kusema maelezo yake yote. Apewe hiyo fursa na ipo hoja ya whether nilipewa fursa ya kutoa maelezo yangu kwenye committal Court (mahakama ya ukabidhi)
Mahakama ya ukabidhi ilipaswa pia kunipa nyaraka zote zilizopatikana kwenye committal processes.
Hayo yote yakitimizwa kutakuwa na fair trial na yasipotimizwa hayo hakutakuwa na fair trial kabisa.
Waheshimiwa Majaji Wakili wa Serikali Kiswaga watu wanacheka.๐๐๐
Anasema Waheshimiwa huyu Kiswaga amenikaa sana kichwani. Samahani ni Katuga.
Sasa anasema lengo la niliyosema ni kuupotosha umma na nyie majaji kwa hayo ambayo nimeyasema tangu jumatatu mimi binafsi siamini kama kuna chochote nimesema cha kuipotosha mahakama.
Nafikiri nimewezesha mahakama hii na umma kuwaleeza mambo mengi ambayo yalikuwa yamefichwa.
Katuga anasema kuhusu S. 265(1) of CPA anasema hayo mamlaka ya kuahirisha kesi na kutoa sababu za msingi za kuahirisha na kuandika sababu hizo alisema all that is descretion..
A superior court like this should not interfere that power.
Nikapewa kesi ya MBOGO and ANOTHER 1993 kwamba inaunga mkono msimamo wao huo.
Waheshimiwa majaji hiyo kesi ya Mbogo vs Shah sina library yangu ningeipata hiyo kesi yote.
Part 11 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako kwenye tweet hii.