Ukijua UNATAKA nini maishani, utajua wapi ujiposition.
1. Ukijua njia yako ni teknolojia, utajisogeza karibu na teknolojia na watu wa teknolojia.
2. Ukiwa mjasiriamali, utatumia muda mwingi na waundaji, na sio watazamaji.
3. Ukiwa kwenye kilimo na ufugaji, utajizunguka na watu wenye maarifa na uzoefu kwenye sekta hiyo.
Mwelekeo wako huamua mazingira yako.
Ukishajua unachokitafuta, utajua pa kusimama, nani wa kusikiliza, na muda wako wa kuwekeza wapi.
Kumbuka;Kila jioni jiulize: “Leo nimefanya nini je ninachokifanya ndio kinachonileta karibu na maisha ninayotaka?
AMKA LADIES AND GENTLEMEN_
@stevenquotes360
Pesa hupenda watu wenye
1. Consistency
2. Patience
4. Nidhamu
3. Emotional control
Ukikosa control ya tamaa ndogo, huwezi kuaminiwa na opportunities kubwa.
#Elimikakifedha
Kuna hiki kitu kinaitwa 𝐍𝐞𝐞𝐦𝐚.
Pale inapokufikia, huwa haikagui vyeti vyako na wala haiangalii uwezo wako juu ya kitu chochote
Yenyewe huwa 𝐢𝐧𝐚𝐛𝐚𝐝𝐢𝐥𝐢𝐬𝐡𝐚 tu hadithi ya maisha yako.
𝐍𝐞𝐞𝐦𝐚 ya Bwana na imfikie kila mmoja wetu katika mwaka 2026 na kuendelea.
BRO TO BRO
Usikate tamaa haijalishi unapitia kipindi kigumu kiasi gani Usiogope kuanza upya kila unapoanguka. Jipe Moyo kwamba na kujiambia maneno haya "hapa ndipo nguvu yangu inapojengwa nitasimama tena"
Weka focus yako mbele, Badilisha mindset yako, Toka kwenye Comfort zone yako. Amini mchakato hata kama unaenda polepole.
Weka tumaini lako kwa MUNGU Hakika utainuka 💪
MAN TO MAN
Usimdhalilishe mwanaume anayepambana. Njaa tayari inabishana naye kila usiku akiwa amelala kwenye godoro lake. Maisha tayari yana kelele za kutosha. Pale mwanaume anapojaribu kuishi, kujijenga upya, na kulinda heshima yake huku mifuko yake ikiwa mitupu. Kama huwezi kumsaidia, basi usimdhalilishe au kumkatisha tamaa.
Baadhi ya wanaume sio wavivu bali wanapigana vita vyao kimya kimya ambavyo fahari yao haiwaruhusu kuvieleza sana kwa watu
Maisha yakikupiga vibaya sana
1. Usipoteze muda kulalamika. Hakuna anayekuja kukuokoa.
2. Badilisha tabia na maamuzi yaliyokufikisha hapo ulipoanguka
3. Acha kujionea huruma. Dunia haina muda wa kuwabembeleza waliovunjika moyo. Jikaze fanya kazi kwenye mwili na akili yako mpaka udhaifu wote uondoke
3. Tafuta pesa na nguvu ya kusimama mwenyewe, ili usiwe tena mtu wa kunyanyasika.
4. Jirekebishe na Kubali kwamba baadhi ya maumivu yaliletwa na makosa yako mwenyewe.
5. Punguza mawasiliano na Kata kabisa mahusiano na watu wasio na faida waliokuona ukianguka lakini hawakufanya chochote
6. Ondoka kwenye Eneo lako linalopokupa Faraja (Comfort zone)
Baada Ya Kufunzwa Na Ulimwengu Sishangai:-
1.Sishangai Mwanaume akiondoka Kwake Akaacha Kila Kitu akamuachia Mwanamke na Akaenda Kuanza Upya Kabisa
2. Sishangai Mtu mwenye Miaka 40 kumlilia baba Yake aliyefariki miaka 10 iliyopita
3. Sishangai Mwana Kukosa Usingizi siku zaidi Ya Mbili
4.Sishangai Mwana Akiwa anasali Machozi yanamtoka na analia Kwa Uchungu sana
5.Sishangai Kuona Mwana hafurahishwi/Halizwi na Chochote tena
6.Sishangai Kuona Mtu Hapewi Support na Yeyote
7.Sishangai Kuona mtu Haaminiwi Na Yeyote
8.Sishangai Kuona Mtu hayupo Sober Mda Wote
9.Sishangai Kuona Mwana Anaondoka Home Na Kupoteza Mawasiliano Kabisa na Kwao
10.Sishangai Kuona Mwana Hajihusishi na Siasa wala Mpira
Rafiki zangu wote ambao familia zao ni za kishua, wana michongo inayoeleweka sana.
Hawana shida hata na kazi za Gavo ,moja kwa moja wanasimamia biashara /michongo ya wazazi wao.
Wengine wamepewa mitaji ,saa hizi wanajitegemea na wana maisha mazuri.
Nadhari ya mtoto kuhangaika katika UMASIKINI haipo tena , kwani hakuna tuzo wala medali ya kuwa na maisha magumu.
Wewe ni Maisha bora ya mtu wako wa kesho , usichoke kupambana 🫵.
@gabyconscious I strongly agree 💯
This is so True. Wengi sana Wana shida na Pesa kuliko hata FUTURE zao. Ndio maana wengi wako tayari hata kuuza Utu wao, Rasilimali Zao, hata Kuhujumu Nchi kwa ajili ya tamaa za PESA! Ili mradi tu awe na pesa.
Na ukikata huo mrija anarudi kuwa Masikini.
Ukifanikiwa-Ku-Focus-Kwa-Miezi-6
Unaweza Rekebisha Makosa
Yako Yote Ya Miaka 5 Nyuma.
Nipe Sekunde 60 tu
Nikupe Madini...
Umeweza kuishi miaka 5
ya maisha ya KAWAIDA tu.
• Kazi ileile.
• Mwili uleule.
• Rafiki walewale.
• Shida zilezile.
Hakuna kinachobadilika
↳ unazunguka mzunguko uleule tu.
Lakini Nikwambie ..
Ukiamua..
Miezi 6 ya KU-FOCUS-SERIOUS
Inaweza Kubadilisha Kila Kitu.
Miezi 6 tu ya kuamua:
↳ Kuamka saa 10 alfajiri kila siku.
↳ Kwenda GYM bila kufeli.
↳ Kusoma, kujifunza, kuandika,
kuwekeza kwenye AKILI YAKO.
Miezi 6 ambayo hautoi kipaumbele
↳ kwa drama, kelele, na usumbufu…
bali kwa
• MWILI wako,
• AKILI yako,
• AKAUNTI yako ya benki,
na MCHEZO wako wote wa maisha Yako.
Francis: Haangalii miaka 10 mbele kwanza.
Anaangalia miezi 6 ijayo.
Anajiuliza:
“Nikiwa serious kwa miezi 6 mfululizo,
naweza kujibadilishia vipi game lote?”
Usiendelee kuuliza
“Kwa muda gani nimekwama hivi?”
Anza kujiuliza:
“Naweza kufanya nini ndani ya miezi 6
nikiamua KUKOMAA?”
Ukifanya kwa roho yote,
↳ bila kupoteza muda,
↳ bila kurudi kwenye mazoea yale yale—
UTASHANGAA.
Utakuwa MGUMU ZAIDI JIWE
( BE UNSTOPPABLE. )
...
Karibu Whatsapp Channell
https://t.co/WP9ikopivP
FRANCIS | ABRACADABRA
Kuna umri ukifika watu wanakuwa wanajua mengi yanayokuhusu lakini hawawezi kukuambia. Inaweza ikawa ni kukuheshimu, kukuogopa, kuamini unajua unachokifanya lakini saa nyingine ni ile tabia ya kusubiria waje waseme, ‘hili tulilijua mapema.’
Unazingua, kwa mfano, hawakuambii. Wanaambiana. Unawakera hawakuambii. Wanaambiana. Unaharibu hawakuambii. Wanaambiana. Unafanya vizuri wanaogopa kukuvimbisha kichwa. Hawakuambii. Wanaambiana. Ukiwa na uwezo wanasita kukusifia. Wanaambiana wenyewe kwa wenyewe.
Ukichunguza kile watu wanachoambiana, ukifuatilia ‘maneno maneno’ yanayokuhusu lakini usiyoambiwa moja kwa moja, utajua kwa nini mambo yanakuendelea hivyo yanavyokuendea. Kuna ukweli mwingi unaokuhusu na watu wanashindwa kukufikishia. Kuna hisia nyingi hazikufikii lakini zipo na watu wamezitunza wanasubiri ujichanganye kidogo waje waseme ‘tulijua.’
Usiwafanye watu wakawa na mengi wanayoyajua na hawawezi kukuambia ukiwepo. Kadhalika, ingawa tunapenda kuonekana wakamilifu, usikwepe sana kujua upande wako wa pili ambao ndio hasa wasifu wako unaotumiwa na watu kufanya maamuzi mengi yanayokuhusu. Unachokwepa kukijua huenda ndicho kinachoamua umbali utakaokwenda.
MAN TO MAN
Sehemu ya kazi sio mahali pa kupiga story kuhusu maisha yako binafsi wala kuongelea watu.
Nenda kazini kufanya kazi, lipwa ujira wako, kisha rudi nyumbani.
Ukikutana na watu wenye ujuzi zaidi yako, Jifunze maarifa kutoka kwao fanya nao kazi usishindane nao.
Kuwa mwaminifu, Heshimu muda wa kazi, Usiongee sana, acha kazi yako izungumze kwa niaba yako.
Jifunze kila siku, maana maarifa ndiyo mtaji mkubwa
Epuka drama za kazini utulivu hujenga taswira ya mtu makini.
Kuwa mkweli na mwajibikaji, maana uaminifu ndio unaofungua milango ya fursa na mafanikio
Nidhamu ya Musa kumuuliza Mungu mambo mbali mbali ilikuwa kubwa sana [the discipline/art of asking God about things]. Nilijifunza kwake miaka kadhaa iliyopita, lengo nipate comment/ushuhuda wa Roho Mtakatifu kwenye jambo fulani.
1. Mungu aki-comment anakupa ushauri/wazo/hekima ambayo hakuna mwenye nayo.
2. Lengo ni kukutofautisha na watu wengine
3. Lengo lingine ni ushuhuda, watu wakiona wajue ni Mungu, sifa na utukufu vimrudie yeye.
Haulipwi vizuri kutokana na jinsi unavyofanya kazi kwa bidii, unalipwa vizuri kutokana na jinsi gani ni vigumu zaidi kutafuta mtu mwingine wa kufanya kazi yako kwa kiwango chako au zaidi.
Kama watu wengi wanaoweza kufanya kazi yako kwa kiwango chako wanaweza kupatikana ndani ya siku 1, mshahara wako utaendela kuwa chini hata kama unafanya kazi kwa bidii.
Soko halilipii sana bidii. Linalipia sana uhaba na ugumu wa kureplace nafasi yako.