#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Agosti 14, 2026
Jana tuliishia part 242 so leo tunaendelea na -;
Part 243
Imepigwa high Court ila tofauti na siku nyingine leo kaipiga Mwakasala
Majaji wameingia,
Karani wa Mahakama anasimama kusoma namba ya shauri.
Mawakili wa Serikali wamekaa kama hawana shahidi leo maana hawaeleweki.
Crimina 19605/2025 Jamhuri dhidi ya Lissu. kisha karani anakaa chini.
Iwapendeze naitwa Ajuaye, Ignas mwinuka, Thawabu Issa, Cattbert Mbilinyi na Winniwa Kasawa na Mshitakiwa yupo kizimbani.
Na shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa.
Waheshimiwa Majaji shahidi tuliyemuandaa leo amepata dharula kwahiyo ameenda muhimbili kwahiyo tunaomba ahirisho hadi jumatatu tutaleta mashahidi wetu wote.
Mheshimiwa Tundu Lissu anacheka tu. Kile kicheko cha kusema hivi haya majitu yana akili kweli? Unakijua kile kicheko cha hasira na cha kusema wewe ni mpumbavu nini?
Watu wanasonya sana.
Majaji wanaandika kidogo hapa.
Ngoja tusubiri Mheshimiwa Lissu anasemaje.
Amesimama anasema mimi niko tayari kuendelea na kesi le, ninapinga ombi la kuahirisha kesi hii kutokana na sababu zilizotolewa na wakili wa serikali.
Kulikuwa na amri ambayo mlitoa mwaka jana kwamba upande wa Mashitaka ulete mashahidi wasiopungua wawili kila siku kesi hii inaposikilizwa. Na hii amri mmeirudia juzi ukiachia jana, siku ya Jumatano na mmeirudia jana.
Upande wa mashitaka walete mashahidi wengi sasa hautekelezi amri za Mahakama kwasababu wanaamini nyie Majaji mmeshindwa kuwachukulia hatua na wanajua Mahakama itawakubalia.
Mimi kusema maneno haya sio kitu chepesi sana lakini naamini hamjachukua hatua kabisa. Kila siku mnawapa maelekezo wao wanapuuza. Wanatuaminisha hapa na Dunia kuwa wanaweza kufanya lolote.
Sasa kwa vile jana mlirudia tena kwamba walete mashahidi na hawajaleta.
Msikubali Mahakama kuu ya Tanzania ikageuzwa kama ile Mahakama iliyomuhukumu Jomo Kenyatta. Mahakama ya Jaji Thucker ilisemwa kule London kuwa iliwakubalia kila kitu kilichoombwa na Mawakili wa serikali.
Msije mkafanywa hivyo, msiwakubalie mambo yasiyokuwa na msingi kwanini hawako tayari kuheshimu maamuzi ya Mahakama.???
Mimi naamini wamekata pumzi na huyu mbaya wao aendelee kusota gerezani na wao waendelee kuvuta posho za Serikali, Msikubali kugeuzwa kama hiyo mahakama niliyoisema.
Again for the record hii ndio kesi kubwa kuliko zote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo hii mahakama inapaswa kuonekana ikisimamia amri zake ili kulinda hadhi ya Mahakama.
Hatutembelei kwenye njia ambayo haijafagilia. 1970, Grey Likungu Mataka kesi ya ugaidi ya kwanza.
Kesi ilichukua miezi sita kuanzia Mahakama kuu hadi ile ya rufani, njia hii ikasafishwa vizuri zaidi Mwaka 1982 Khatibu Gandi na wenzake katika Mahakama Kuu chumba hiki hiki kesi ilichukua mwaka 1 na siku 17.
Na haya ninayosema yapo kwenye record ya hizo kesi mbili kwahiyo mnayo mifano. Leo ni siku ya 493 yani mwaka 1 na miezi 4 hatujamaliza.
Nikija kusema aitwe Samia Suluhu Hassan si itachukua miaka 5 mtastaafu bila kesi hii kuitwa.
Maana nataka Philip Mpango, Kassim Majali na IGP nikisema waje kesi si haitaitwa milele? Jitahidini hii Mahakama isiwe Kangaroo Court.
Nimemaliza.
Anasimama Ajuaye, Wakili wa Serikali tumemsikia mwenzetu alichoongea lakini mashahidi ni wanadamu na kwakuwa wanadamu changamoto inaweza kutokea muda wowote na kwa binadamu yeyote.
Sisi upande wa mashitaka tunakili kuwa ni kweli bado tuna mashahidi wengi lakini sio lazima tulete wote, pengine ni shahidi wa mwisho na ndio huyo tunayemtegemea sasa hakuna namna kifungu cha 265 CPA.
Tunaomba Mahakama yenu iahirishe shauri hili mpaka Jumatatu na tutaleta mashahidi wote waliobakia, wote kabisa waliobakia na itakuwa ndani ya session hii na kikao hiki kilichopangwa.
Part 244 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Agosti 12, 2026
Kesi ya uhaini dhidi ya Mhe. Lissu inaendelea katika Mahakama Kuu ya Dar es salaam ambapo Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Cross Examination Shahidi wa Jamhuri ACP Amin Mahamba.
Jana tuliishia part 231 so leo tunaendelea na
Part 232.
Imepigwa high court.
Majaji wameingia wapo watatu kama kawaida yao.
Mtuhumiwa nae ameingia japo leo Askari Magereza wamemzonga sana ili asisalimiane na watu.
Mtuhumiwa yani Mhe. Lissu amechukua nafasi yake, na shahidi Amini Mahamba amekaa katika kizimba tayari.
Karani anaita kesi kwa namba yake : JAMUHURI dhidi ya TUNDU LISSU
Mawakili wa serikali wanaongozwa na AJUAYE, Katuga, Job Mrema , Cuthbert Mbilingi na Winniwa Kasalla.
Majaji wanamuuliza mtuhumiwa kama yupo tayari…
Mhe. Lissu anaomba kufanya consultation toka kwa Mawakili wake/researchers
Majaji wanamruhusu
Mawakili wake Nashon Nkungu Na Sisty Aloyce wanainuka na kusogea kizimbani kumconsult Mhe. Tundu Lissu wanateka Kama dakika tano hivi kisha wanarudi kukaa kwenye viti vyao.
Jaji anamkumbusha Shahidi kuwa bado yupo chin ya kiapo.
Mhe. Lissu anaruhusiwa aanze kumuhoji Shahidi.
Anamwambia leo hana maswali mengi sana
Anamuuliza kama alidhamiria kuwa maelezo yake aliyotoa alidhamiria yaaminiwe kama ushahidi wa kweli.
ACP Amin Mahamba anajibu kwamba ndio alidhamiria
Mhe. Lissu : Ulidhamiria kuwa maelezo yako uliyotoa kule Polisi yawe ushahidi Mahakamani?
Lissu anasema “IM TYING UP THE LOOSE ENDS”
Anamuuliza kuhusu wale mashahidi waliofichwa waliotolewa mikoani.
Mhe. Lissu : Swala la kwanza eneno hilo; unakumbuka ulisema kwamba hawa mashahidi waliofichwa ni watu waliokamatwa na Polisi ni KWELI walikutwa wakipanga njama?
ACP Amin Mahamba : sio tu kupanga niama, na kuhamasisha
Mhe. Lissu: Walipokamatwa walikiri Polisi kupanga kufanya njama na vurugu Uchaguzi na kadhalika ni kweli??
ACP Amin Mahamba : Hayo yalikuwa ni makosa ya jinai.
Mhe. Lissu: Wakakiri kwa maandshi?
ACP Amin Mahamba : Sahihi.
Mhe. Lissu: Waleleze Majaji hizo tuhuma za kijinai mlizowakamatia ziliishia wapi?
ACP Amin Mahamba : Waheshimiwa rejea maelezo yangu ya siku ya kwanza, kuwa baaada ya watu hao kukamatwa tuliitisha jalada, tukasoma tukapitia.
Mhe. Lissu: Umeelewa swali langu shahidi?
Nimesema sitaki unipotezee muda, nataka kutumia nusu saa.
Katuga anainuka
Kabla hajasema chochote Mhe. Lissu anamwambia kaa,
Katuga anasema si jukumu la Mhe. Lissu kumwambia akae chini.
Mhe. Lissu anakubali na kumueleza Shahidi kuwa akiuliza swal anataka jibu sio hotuba
Mhe. Lissu anauliza kuwa hizo tuhuma za kupanga njama ziliishia wapi?
ACP Amin Mahamba : Baada ya kupitia majalada…
Mhe. Lissu: kweli kuwa mliwafutia kesi wote?
ACP Amin Mahamba : sahihi
Mhe. Lissu : Tuanze na DSM… 29/10.. kulitokea vurugu zilizoua watu 182
ACP Amin Mahamba: Mimi sio msemaji wa Jeshi la Polisi, hizo ni taarifa nyeti.
Kwa mujibu wa Tume ya Jaji Chande watu 182 waliuwawa DSM.
ACP Amin Mahamba : si kweli
Mhe. Lissu: Katika wale watu waliokamatwa wapo wa kutoka Arusha
ACP Amin Mahamba : Kweli
Mhe. Lissu: Walikiri kupanga uhalifu, kupiga watu nk na Mkawaachia,?
ACP Amin Mahamba : Kimya
Mhe.Lissu : Siku ya uchaguzi 29, kwa mujibu wa Tume ya Jaji Chande, waliuwawa watu 53 Arusha, watu ambao mlikuwa mnajua walichopanga mkawaachia, wakaenda kutekeleza hayo.?
ACP Amin Mahamba : Aaah, eeh
Mhe. Lissu : Twende Mbeya, kuna watu mlikwakamata Mbeya, walisema wanapanga kufanya vurugu kwenye Uchaguzi, watapiga watu mawe wakakiri halafu mkawafutia mashtaka kweli si kweli.
ACP Amin Mahamba : KWELI
Mhe. Lissu : Arusha, Dar es Salaam, Mbeya jumla ya watu waliouawa ni 315.
Eleze kama kuna Mkuu wa Polisi, au DC, alichukuliwa hatua kwa uzembe wa maafa haya?
ACP Amin Mahamba : Sina hakika kama kuna aliechukuliwa hatua
Part 233 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 233
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa Jamhuri ACP Amin Mahamba.
Mhe. Lissu : Eleza kama hao waliosema watafanya vurugu, mkawaachia na wakaenda kweli kufanya vurugu kama kuna hata mmoja mliemchukulia hatua?
ACP Amin Mahamba : Kimya
Mhe. Lissu : Kimya maana yake hamkuchukua hatua
ACP Amin Mahamba ; Hapana, nimeona unakumywa maji
Mhe. Lissu : Ninakunywa kahawa
Mhe. Lissu : Mkoa wa Mwanza 29/10 kwa mujibu wa ripori ya jaji chande waliuawa watu 90, eleza kama Mwanza ina RPC?
ACP Amin Mahamba : Yupo
Mhe. Lissu : Yule ambaye yupo kwenye vyombo vya habari kila siku hata gerezani namsikia? Anaitwa Mutafungwa
ACP Amin Mahamba : ndio
Mhe. Lissu : Kwa Mikoa minne watu 405 kwa mujibu wa taarifa ya Chande, kuna aliyechukuliwa hatua?
ACP Amin Mahamba: Sina taarifa
Mhe. Lissu : Kwa Mikoa 7, ni Songea tu mlipopewa taarifa kuwa watafanya vurugu?
ACP Amin Mahamba : Ndio lakini waliachiwa kwa mujibu wa taratibu ya sheria
Mhe. Lissu : Waeleze Majaji kama Wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao hawakuripoti wamechukuliwa hatua kwa maafa yalitokea???
ACP Amin Mahamba : Sina uhakika
Mhe. Lissu : Mara ya mwisho watu waliuawa na vyombo kiasi kikubwa hivyo ni mwaka 1905 kwenye Vita ya Majimaji.
Mhe. Lissu anaendelea kueleza awamu zote watu hawakuuawa kiasi iko kama ndani ya wiki 1 ya Samia wameuawa watu wengi
Mhe. Lissu anaelekea kwenye Ushahidi wa video, kwenye ushahidi wako kuhusiana na video, ulisema wewe na timu yako baada ya wewe kupanga timu zako 3, Je video mliyoangalia ilikuwa mtandaoni au ilikuwa kwenye memory card? Au ile iliyokuwa kwenye flash.??
ACP Amin Mahamba; Tuliangalia ile ya kwenye mtandao, Youtube
Mhe. Lissu; Nitakuwa sahihi kusema hamkuangalia ile video ya kwenye flash wala ya kwenye mamory card??
ACP Amin Mahamba ; Hizo hatukuangalia
Mhe. Lissu: Nitakuwa sahihi kusema pengine flash na memory card huenda hazina hata hizo video?
ACP Amin Mahamba ; sio kweli
Mhe. Lissu: umejuaje wakati hujaangalia?
Waeleze Majaji unajuaje kilichokuwa kwenye flash disk wakati hukua.???
ACP Amin Mahamba anakwepa
Mhe. Lissu anarudia
Shahidi umejuaje?
ACP Amin Mahamba: Wenzangu KAAYA na mwenzie walipakua hizo video na kuziweka kwenye flash.
Mhe. Lissu anarudia, swali langu wewe unajuaje kama zipo wakati hujaziona?
ACP Amin Mahamba: najibu kitaalamu sasa,
Mhe. Lissu anamkatiza jibu swal langu
ACP Amin Mahamba : Ngoja nijibu basi, nimefahamu kupitia taarifa ya mchunguzi
Mhe: Lissu: Hiyo taarifa ipo Mahakamani kama kielelezo???
ACP Amin Mahamba : Kimya
Mhe. Lissu anasema mimi nachojua taarifa ilikataliwa hapa mahakamani sababu haikuandaliwa na mtaalamu
Mhe. Lissu: Mpaka sasa wewe ni Shahidi wa 16, na nyie wote hakuna hata mmoja aliyewasilisha ushahidi wa video, taarifa ya uchunguzi wala nyaraka yoyote hakuna.
Mhe. Lissu: Nyaraka zote zilizoingia Mahakamani ni ushahidi wangu,
Mpaka sasa hakuna kilelezeo chochote zaidi ya story kwenye kesi hii.
ACP Amin Mahamba : sina kumbukumbu
Mhe. Lissu: Mkutano wangu ulizungumzia Katiba Mpya?
ACP Amin Mahamba anakataa
Mhe.Lissu : Waeleze Majaji kama unafahamu madai ya Katiba Mpya na mfumo huru wa uchaguzi ni madai yaliyopo kwa miaka 35 hapa Tanzania.
ACP Amin Mahamba : sifahamu
Mhe. Lissu; Eleza kama unafahamu au hufahamu kuwa Tume ya Jaji Nyalali, ilipendekeza itungwe Katiba mpya itakapofikia 1993?
ACP Amin Mahamba : Sijawah kuipitia
Mhe. Lissu: Eleza kama mapendekezo hayo yalikataliwa na Mwinyi?
ACP Amin Mahamba : Sifahamu
Mhe’s Lissu: Mkapa aliunda tume iliyoongozwa na Jaji Kisanga na ikapendekeza kuwe na Katiba mpya halafu Mkapa akasema hadharan mimi sikuwatuma waangalie maswala ya Katiba mpya, unafahamu au hufahamu???
ACP Amin Mahamba : Sifahamu
Part 234 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 234
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa Jamhuri ACP Amin Mahamba
Mhe. Lissu: Kama unafahamu au hufahamu Tume iliundwa pia ya Mark Boman.. kuangalia utaratubu wa Katiba nayo ikapendekeza kuwe na Katiba mpya na Serikali ya Mkapa na ccm yake ikakataa????
ACP Amin Mahamba : Sifahamu
Mhe. Lissu: Kama hufahamu au unafahamu Kikwete aliunda Tume ya Mabadilio ya Katiba (ya Warioba) ambayo sio tu ilipendekeza Katiba mpya bali pia iliandaa Rasimu halafu Serikali ikakataa???
ACP Amin Mahamba; Sijawah kupitia
Mhe. Lissu: Eleza kama unafahamu au hufahamu tunafanya Uchaguzi Mkuu kila baada ya mikaa 5???
ACP Amin Mahamba : sahihi
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama unafahamu au hufahamu katika kila Uchaguzi mkuu wa vyamana vingi Watazamaji wa Kimataifa na Kikanda, Jumuiya ya Ulaya, COMMON WEALTH, Marekani., Canada, Japan, AU, SADC, Jumuiya ya Afrika kila Uchaguzi Mkuu wamependekeza kuwa Serikali itungwe Katiba mpya na mfumo mpya wa Uchaguzi ili kuondoa matatizo mengi ya kiuchaguzi???
ACP Amin Mahamba : Sifahamu
Mhe. Lissu Tumeambiwa kila baada ya miaka 5 na ccm imekataa, Eleza kama unafahamu ilani ya ccm ilikuwa na ahadi ya Katiba mara baada ya uchaguzi 2015 na 2020.
ACP Amin Mahamba anajibu haraka SIFAHAMU hata kabla swali halijaisha.
Watu Wanacheka 😀😀😀😀
Mhe. Lissu : Samia alisema Katiba haiweki ugali mezani, unafahamu?
ACP Amin Mahamba ; Sifahamu
Mhe. Lissu: Kwasababu ya kukataa huku kila Uchaguzi mkuu lazima uendane ma maujaji ya Watanzania???
ACP Amin Mahamba -Sina uhakika na hilo
Mhe. Lissu: Eleza Kama baada ya maujaji ya Oktoba 29 mlichukua hatua ya kuniuliza haya maneno yana maana gani, unaposema mtakinukisha una maana gani au haya maneno ya uasi yana maana gani?
ACP Amin Mahamba : Hapana
Mhe. Lissu; Hamkutafuta ufafanuzi wa hayo maneno yangu?
ACP Amin Mahamba : Hukuwa tayari
Mhe. Lissu: Ningekuwa mjinga kiasi gani kujibu nikiwa kwenye pingu?
Mhe. Lissu: Nitakuwa sahihi kusema kuwa No reforms, No election ilikuwa sahihi kwa mazingira yale???
ACP Amin Mahamba : sio sahihi
Mhe. Lissu: Kwa mujibu wa tume ya jaji Chande Ghasia za oktoba 2025 zimetokana na changamoto mbalimbali ambazo hazikutatuliwa, anazisoma kama madai ya katiba mpya.
Waeleze majaji kwamba huo ni msimamo sahihi?
ACP Amin Mahamba ;Unakosea
Mhe. Lissu: kwahiyo hata Jaji Chande alikosea?
Lissu anamsomea sababu kama zilivyo kwenye hotuba ya Jaji Chande.
ACP Amin Mahamba: Sikupata nafasi ya kupitia
Mhe. Lissu: Hayo mnayodai ni makosa yangu, waeleza Majaji kama unafahamu au hufahamu kuwa 13/2/2026, Kikosi kazi cha Kamati ya Umoja wa Mataifa, Kikosi kazi cha Haki za Binadamu, kinachoshughulikia watu wanaokamatwa bure arbitrary detention) kimetoa taarifa na taarifa hiyo inasema kukamatwa kwangu na kushtakiwa huku ni kukuka haki za binadamu na wakapendekeza nilipwe fidia???
ACP Amin Mahamba : sijawah kufahamu
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama unafahamu au hufahamu mwezi ulipoita 10 july, kamati ya Mawaziri wanaowakilisha nchi za Jumuiya ya Madola imetoa taarifa inayoitaka Serikali ya Tanzania kuniachilia huru bila mashart yoyote ndan ya siku 30 kuanzia 10 july na wakaeleza watatake appropriate action isipofanyika hilo…???
ACP Amin Mahamba : Sifahamu
Mhe. Lissu: Kama Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola, Mawaziri kabisa sio wale WANAHARAKATI msiowapenda wanasema aachiliwe ndani ya siku 30 vinginevyo tutawashughulikia, huyu mtu anayepiganiwa na Taasisi hizi ni mtu mbaya anayetakiwa kunyongwa hadi afe?
ACP Amin Mahamba ;Sina uhakika
Mhe. Lissu anamaliza maswali na kukaa chini
Kimya kinaendelea mahakamani kwa muda kidogo
Part 235 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 235
Bado kimya kimetawala mpaka muda huu.
Wakisubiriwa upande wa Serikali waanze kumhoji Shahidi wao (Re-examination) kwa ajili ya kufukia mashimo yaliyotengenezwa na utetezi na kurepair.
Majaji wanatoa maelekez, tuendelee kwa Re- examination.
Wakili wa Serikali Anasimama anasema tunayo maswal machache
Atauliza Katuga.
Katuga Anasimama anamwambia Shahidi pole kwa maswali mengiiii yaliyojaa hotuba, Relax
Katuga : Usitegemee kukuta maswali ya sijui Tume, Sijui nini sawa? Anarudia sawa mara kadhaa..
Katuga : Kama unakumbuka uliulizwa maneno kwamba tutazuia uchaguzi, tutakinukisha hayo maneno yana neno Serikali, ulijibu lipo, Ulimaanisha nini?
ACP Amin Mahamba : Nilipotamka neno Serikali lipo nilikuwa naamanisha kwamba Serikali ndo yenye mamlaka au wajibu wa kutekeleza au kusimamia Sheria za nchi, kwahiyo kutamka maneno kama hayo.. kwamba utavuruga uchaguzi, utazuia maana yake ni kuitishia Serikali ambayo ndo ina jumumu la kulinda na kutunza usalama wa nchi nlikuwa namaanisha hivyo.
Katuga: -Tuendelee kijikita hapa hapa kwenye maswala yaliyopo mbele ya Mahakama.
Uliulizwa ni nani aliyechapisha maneno hayo, ukajibu ni wewe, tena ukamkomali, ukapelekwa kwenye ushahidi wa P ukieleza kwamba wao ndo waliosambaza P na P1, ukasomeshwa kwamba bwana Bagyemu aliona hayo maneno kwenye YouTube
lakini ukazidi kusema ni wewe(Lissu) ndo uliyechapisha.?
ACP Amin Mahamba : Nilikuwa naamanisha kwamba mshtakiwa ndo alikuwa kaiongea mbele yao wale wote waandhsi wa habari.. yeye ndiye aliongea mbele ya wale waandshi wa habar ambao walikuwa wakirusha yale live so yeye ndiye aliyesababisha warushe ye live. Na kwamba naamini kama ile ilikuwa nia yake sababu kama alikuwa hataki yale matangazo yarushwe mubashara asingeruhusu yarushwe sababu aliruhusu yarushwe.
Katuga: kwahiyo ndo maana ukakomaa ni wewe ni wewe ???
ACP Amin Mahamba : Ndio
Katuga: Ulisomeshwa kifungu cha 39 japo wewe si Mwanasheria, ukaulizwa haya maneno kuzuia uchaguzi, kukinukisha.. yamo kwenye hicho kifungu?
Na majibu yako uliendelea kusisitiza yamooo
ACP Amin Mahamba ;Nilikuwa namanisha kuwa katika kile kifungu cha 39(2)b kuna neno limeandikwa kwa nia ya kutishia serikali, Kwahiyo yale maneno alimaanisha ile nia.
Katuga: Shahidi kingine umeulizwa sana… sijui mwaka fulan, madai ya Katiba, ccm sijui nn, mimi sio mwanasiasa
Ifafanulie haya madai ya Katiba na madai haya ya uhaini nini majibu yako kwenye hii Katiba na kesi ya uhaini???
ACP Amin Mahamba : Napenda kusema kwamba, kama una madai ya msingi….
Shahidi anakatishwa na wakili wa serikali Katuga hivyo vitakiwa vitu vipya
ACP Amin Mahamba; hayahusiani na haya
Katuga: Sasa shahidi kuna maswali mengi lakini swal moja wapo linahusiana na vurugu za 29/2025.
Uliulizwa kwamba wewe na timu yako ya polisi mlifanya vurugu siku hiyo, ulijibu ukazuiwa na ulikuwa unaamanisha nini???
ACP Amin Mahamba : Sio kweli kuwa mimi na timu yangu au na Jeshi la Polisi tulihusika na zile vurugu kwan upelelezi tuliofanya tulibaini kuwa zilitokana na uhammishishaji au uchochezi uliofanywa awali na kubaini kwamba kulikuwepo na maandalizi ya vurugu hizo kabla ya 29/10/2025.
Mhezz Lissu anainuka anasema Waheshimiwa majaji mimi sikuuliza hilo swali, Shaidi anajibu kitu kipya… akiruhusiwa nitaomba nami ni mcross examine
Jaji: tuendelee
Mhe. Lissu anasimama na kusisitiza kuwa akiruhusiwa nitaomba niruhusiwe
Jaji: tuendelee
Mhe. Lissu: kama mmesema hivyo tuendelee
Katuga; Uliulizwa je unataka maelezo uliyotoa polisi uaminiwe, ukajibu ndiyo ya hapa Mahakamani, ukajibu pia ndio.
Hebu tupe ufafanuzi kuhusiana na utofauti, uliotoa polisi na uliotoa mahakaman?
Mhezz Lissu anainuka tena na kusema hicho kitu sicho nilichouliza.
Lissu anasema niliuliza kama ameeleza kuwepo kwa tofauti, Akieleza sababu nitataka ku pewa nafasi ku cross
Katuga anaelezea hapa
Na Mhe. Lissu anaeleza pia…
Part 236 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 236
Mabishano yanaendelea hapa kidogo kati ya Mhe. Lissu na Wakili wa Serikali.
Mhe. Lissu anawambia Majaji kwamba yeye aliuliza kama Shahidi alielezea sababu ya huo utofaut so hawezi akatoa sababu sasa hivi itakuwa kitu kipya hivyo na yeye ataomba aruhusiwe kufanya cross examination kwa Mara nyingine.
Jaji Ndunguru anamwambia Katuga rephrase swali lako.
Katuga: Hebu shahidi sijui kama tunaelewana tuambie kama umeeleza sababu ya utofauti kati ya maelezo uliyotoa polisi na haya uliyotoa hapa Mahakama.
Ulikuwa unamaanisha nini..???
ACP Amin Mahamba :Kwa kweli sijaeleza sababu ya utofauti lakini nachofahamu yale niliyoandika nikiwa ofisin na haya ya hapa mahakamani, majibu niliyotoa yalitokana na jinsi nilivyoongozwa na waendesha mashtaka basi.
Kimya kinapita kama sekunde kadhaa, Wakili wa Serikali Katuga anarud kukaa na kujaribu kuzungumza na Mawakili wenzie wa serikali
Jaji: tuendelee
Katuga: Samahani Waheshimiwa dakika mbili nizungumze na wenzangu.
Katuga anajadili na wakili Mkuu Serikali Ajuaye na wakili Job Mrema, baadaye anaongea na Wakili mwingine wa Serikali Ignas Mwinuka..
Huenda wanatafuta maswali😀😀😀
Anamaliza kuconsult Wakili Katuga na kusimama tena
Katuga : Baada ya ku consult na wenzangu, tumeona tuishie hapa kwa faida ya Mahakama
Ni hayo kwa shahidi huyu
Ukimya unaendelea tena kwa sekunde kadhaa…
Jaji anasema: shahidi umemaliza kutoa ushahiid wako, Mahakama inakuruhusu.
Shahidi anatoka mahakamani nduki kama mwizi aliyekwapua simu.😂
Ikumbukwe kwamba shahidi huyu ambaye ndo mpelelezi Mkuu wa kesi hii, dhidi yake kumekuwa na minong’ono mingi kuhusu identity yake.
Ukiacha madai yalizonguka mitandaoni ya mtu anayedai kuwa ni mjane wa MAHAMBA lakini pia karibuni zimejitokeza taarifa kuwa shahidi huyu sio MAHAMBA halisi.
Haya yanasemwa na watu waliofanya kazi na shahidi huyu kwa miaka mingi wakidai kwamba jina halisi la shahidi huyu anaitwa PETER JUMAMOSI
Anasimama wakili wa Serikali Ajuaye kwa leo tulikuwa na shahidi huyu tu hivyo tunaomba Mahakama iridhie mpaka kesho
Mhe. Lissu: Kama mtakumbuka sawasawa kulikuwa na amri upande wa mashtaka walete mashahidi wawili ama watatu, je amri hii imekuwa vacated?
Tumeshachelewa sana na hatukuchelewa kwa sababu zenu wala zangu ila sababu ni zao upande wa Jamhuri, tukiendelea kuchelewa hivi mimi naendelea kukaa Gerezani wakat narudia tena SINA HATIA.. kwa hiyo kuanzia kesho waje na mashahidi wa kutosha
Jaji Ndunguru anasema kesi imehairishwa hadi kesho asubuhi.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 17
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Na mazungumzo ya Kisabo pia ulisema yasimamiwe kwenye ofisi ya kaimu mkuu wa gereza.
Ntamamiro (Bwana Jela) : ndio
Mhe. Lissu: Na tunakubaliana wale watu wote akina Mumbii, legal officer Stima, Kopro Dani, na akina mama watatu. Je hawa watu wanakuwemo humo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Si kweli. Huwa wanatoka. Wanaacha mazungumzo yafanyike.
Jaji: Lissu umeridhika na majibu ya shahidi.
Mhe. Lissu: Ngoja nataka kukamata watu waongo.
Mhe. Lissu: Kumbe maafisa wote mle chumbani wanatoka nje, sasa soma kiapo chenu ndugu yangu. Nakusomea kwenye kiapo chako
Kiapo kinasomeka kuwa walikuwepo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kuna ambao walikuwepo na kuna ambao walitoka.
Mhe. Lissu: Waliokuwepo ni akina nani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Waliosindikiza
Mhe. Lissu: Akina nani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sikumbuki
Mhe. Lissu: Waleta maombi wote wamewataja majina akina Mumbii, Koplo. Dani, Akina mama watatu mle ndani, legal officer na mtu wa usalama. Wamewataja majina. Wewe unasemaje?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sikubaliani nao mimi.
Mhe. Lissu: Twende kwenye ofisi ya Recha ACP. Soma SUPP 4 Tar. 24/12 ulisema alipokuja Kisabo. Asimamiwe kwa kaimu mkuu wa gereza na kusema wayafanyie ofisini ukawataja majina ambao wanapaswa wasimamie. Waeleze majaji kuwa wakati wote Recha anakuwepo, asipokuwepo atakuwepo Mumbii, Mohamed lazima awepo au Hamisi na anakuwepo Stima na maaskari wanaonifuata muda wote.
Ntamamiro (Bwana Jela) : sio kweli
Mhe.Lissu: Umewahi kuhudhuria mazungumzo hayo kwa Recha?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijawahi.
Watu wanacheka. 😂😂😂😂
Mhe. Lissu: Tumewahi kufanya mazungumzo ofisi kwako mimi na mawakili wangu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Tar. 12/12 imeandikwa SUPP 6 Umeiona?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sioni
Mhe. Lissu: Mawakili msaidieni mmeleta wenyewe.
Ukiiona siku hiyo niliyosema tar. 12/12 ulielekeza hivi kaimu mkuu wa gereza, Mtu wa usalama na mwanasheria wa gereza ulisema mazungumzo yawe ya kisheria zaidi. Kweli au sio kweli?
Ntamamiro (Bwana Jela): Kweli
Mhe. Lissu: Je hawa uliowaelekeza wote zaidi ya watu watatu walikuwepo au hawakuwepo kwenye haya mazungumzo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hawakuwepo.
Mhe. Lissu: Walisikiliza au hawakusikiliza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hawakusikiliza.
Mhe. Lissu: Waliwezaje kusimamia mazungumzo wakati hawakuwepo na hawakusikiliza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kuna facial impression.
Majaji wanacheka.😂😂😂😂
Ntamamiro (Bwana Jela): Naomba nifafanue.
Mhe. Lissu: Sitaki unifafanulie. Sasa kama hawakuwepo facial expression walizionaje wakati hawapo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hili suala ni la kisheria tunamkagua wakili kitambulisho.
Mhe. Lissu: Nani kakuuliza hayo.
Jaji: Usitupotezee muda. Hebu soma maelekezo yako kuwa wasimamie mazungumzo na watu hawakuwepo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ukiona wanakumbatiana hayaruhusiwi.
Jaji: Uliwaelekeza wafanye nini kwenye mazungumzo hayo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Walisimama mbali wakawa wanaangalia.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kama kitendo cha kukumbatiana ni maneno au kitendo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : ni kitendo.
Mhe. Lissu: Ulisema wakasimamie vitendo au maneno?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Mazungumzo yaani maneno.
Watu wasonya tu. Majaji pia wamekasirika sana kwa majibu haya. Watu wengine wanacheka kimya kimya.
Mhe. Lissu: Sasa twende SUPP 6 ukurasa unaofuata. Wapo mawakili watatu ambao ni Catherine Chanjarita, Shamumoyo na Constatine kwenye comment zako umesema Adm. Officer simamia mazungumzo yao kwa karibu. Sasa swali langu simamia kwa karibu yanawezekana kutekelezwa bila maaskari hao kuwepo kwenye mazungumzo hayo?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sijasema wasikilize nimesema wasimamie kwa karibu.
Part 18 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 18
Anaendelea Mhe. Lissu na maswali ya Dodoso.
Mhe. Lissu: Karibu ipi ambayo hawasikii?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Unaweza kuwa karibu na usisikie.
Mhe. Lissu: Kuna mawakili jumla 37 ambao umeleta nyaraka zao hapa pamoja na mawakili wangu. Sasa kwenye comment zako umekuwa ukisema simamia kwa karibi, simamia mazungumzo yao. Ni kweli kwa mawakili wote?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli lakini ni kweli naomba niseme ni kweli nimesema comment hizo kwa wote.
Mhe: Lissu: Katika Mawakili wote hao kuna mahali hata pamoja ulipoandika simamieni lakini msisikilize mazungumzo yao?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hakuna
Mhe. Lissu: Je katika mawakili wote 37 umeandika wakiingia ofisini tokeni nje wazungumze ipo sehemu umeandika?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hakuna nilipoandika.
Mhe. Lissu: Kuna mahali kokote umeelekeza kuwa angalieni lakini msisikilize?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hakuna mahali hapo.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama ni kweli au sio kweli kati ya Tar. 18/04/2025 nilikuwa nazungumza kwenye kioo na mawakili wangu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kilikuwepo hicho kipindi.
Mhe. Lissu: Tulikuwa tunawasiliana kupitia simu zilizopo pale?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kweli
Mhe. Lissu: Je upande anaokuwepo mgeni ndio uko karibu na reception na kuna kachumba ambacho ni control room ya hizo simu zote? na kwenye hiyo control room anakuwepo afisa magereza anayeuwasha na kuuzima. Ili watu wazungumze yeye ndio anaamua hapo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : ni kweli.
Mhe. Lissu: Huyo Wakili anapozungumza kuna askari wanakuwepo kumsikiliza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli a
Mhe.Lissu: Je huu upande wangu nakuwa pia na askari wananisikiliza niliotoka nao lockup na wengine wananisikiliza?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sio kweli.
Lissu: Kwenye hicho chumba kuna CCTV Camera inayorekodi kinachoendelea humo?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sio kweli
Mhe. Lissu: CCTV camera hiyo iko controlled ofisini kwako?
Ntamamiro (Bwana Jela): sio kweli.
Mhe. Lissu: Je ni kweli kwamba baada ya matukio ya Oktoba 29 uliniita ofisini kwako?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli
Mhe. Lissu : Ulivyoniita ukaniambia kuanzia sasa ni marufuku viongozi wa Chadema na wanachama wa Chadema kuja kukutembelea.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli
Mhe. Lissu: Na pia ulisema ni ndugu zako wa karibu tu ndio watakutembelea?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli
Mhe.Lissu: Na ukasema mazungumzo yako na mawakili yatakuwa kwa mambo ya kisheria tu?
Ntamamiro (Bwana Jela): sio kweli.
Mhe. Lissu: Wakili Gaston Garubindi alikuwa anakuja kunitembelea Gerezani kabla ya Tar. 14/11/2025
Ntamamiro (Bwana Jela) : kweli
Mhe. Lissu: kuanzia hiyo tarehe hajawahi kuruhusiwa?
Ntamamiro (Bwana Jela): Simpangii.
Mhe. Lissu: Kuanzia niingie Gerezani Wakili Dickson Matata na Deogratias Mahinyila hujawahi kuwaruhusu waingie gerezani. Huyu Matata ni Mwenyekiti Kanda ya Magharibi na Mahinyila ni Mwneyekiti wa Vijana Taifa hawajawahi kuruhusiwa?
Ntamamiro (Bwana Jela): Siwalazimishi waje au wasije.
Mhe. Lissu: Kumbe ndio hivyo. Haya Mahinyila na Matata kesho njooni Ukonga.
Ntamamiro (Bwana Jela): Kesi iko Mahakamani sitawaruhusu
Mhe. Lissu: John Heche, Amani Gorugwa, Katibu Mkuu Mnyika wakiwa kama mashahidi wangu kwenye kesi ya uhaini wamezuiwa kuingia?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hawawezi kuingia.
Jaji: Hilo la kwamba huwezi kuruhusu umelitoa wapi? Kuna amri yoyote ya Mahakama?
Ntamamiro (Bwana Jela): Siwezi kuwaruhusu.
Jaji Mruma: Tumefikia huko. Unaiambia Mahakama kuwa huwezi kuruhusu na hauna amri yoyote ya Mahakama? Uko serious kweli au hujaelewa ili tufanye maamuzi na sisi sasa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Waheshimiwa majaji naomba radhi.
Jaji anamkata jicho
Mhe. Lissu: Soma hati yangu kinzani kuhusu Nashon Nkungu.
Anasimama Wakili wa serikali tunaomba Break.
Majaji wanashauriana.
Wakili John Seka anasema ni sawa tu.
Mhe. Lissu: Ni sawa.
Jaji basi tukutane mara baada ya lisaa limoja.
KITUKO KILICHOTOKEA MAHAKAMANI.
Wakati Mkuu wa Gereza yaani BWANA JELA ambae ni Andrew Shabani Ntamamilo alipohojiwa na Mhe. Tundu Lissu kuhusu Kuwazuia kabisa Mawakili kama Vile Deogratias Mahinyila, Dickson Matata lakini pia viongozi wakuu wa Chama akiwemo John Heche, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu wa Chama, John Mnyika na Amani Golugwa ambao ni mashahidi katika kesi ya Uhaini wamekataliwa kuingia Gerezani Ukonga.
Majibu ya Mkuu wa Gereza amesema yeye hajawazuia. Mhe. Lissu akasema basi watakuja kuanzia kesho. Akasema SITAWARUHUSU waingie kwasababu kesi bado iko mahakamani.
Jaji Amir Mruma ndio akaanza kumuhoji kuna amri yoyote ya Mahakama kuwa watu hawa hawapaswi kuja kumtembelea Tundu Lissu? Akasema kwa kiburi tena kuwa SITAWARUHUSU.
Jaji akavua miwani na kumuuliza unataka tufike huko. Uko serious kweli? Akiwa amekasirika sana. Maaskari Magereza walioko nyuma niliokaa nao karibu wamekimbilia nje kucheka.
Baada ya Jaji kukasirika Bwana Jela akaanza kuomba radhi kwa Jaji. Majaji wote watatu wametikisa vichwa vyao na kuonesha wanashangaa mambo haya yanawezekanaje kwenye Taifa lenye sheria na taratibu.
Kesi hii imeendelea tena kutuonesha watawala wa nchi hii wakoje. Ukisikia majibu ya Mkuu wa Gereza unajiuliza kiburi anakitoa wapi?
Ngoja tusubiri maamuzi ya Majaji mwisho wa kesi hii utakuwaje lakini naamini kila mtu anashuhudia uhalisia wa mambo ulivyo katika Taifa letu.
Tuendelee kusubiri lisaa likamilike turudi kuendelea.
Wanachama leo ni wengi mno. Mahakama imetapika. Yupo Makamu Mwenyekiti John Heche, Yupo Katibu Mkuu, Mnyika. Mama Suzan Lyimo, Mwenyekiti BAZECHA, Yupo Boniface Jacob Mwenyekiti Kanda ya Pwani, Dua Lyamzito, Katibu Mkuu BAVICHA, Pamela Massey, Katibu Mkuu Bawacha. Mzee Azaveli Lwaitama, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama na wanachama wengine mbalimbali.
Tutaendelea kuwaleteeni live moja kwa moja mwenendo wa kesi hii kutokea Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es salaam.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 19
Mahakama Imerejea.
Majaji wameingia.
Wakili wa Serikali amesimama kujitambulisha anaitwa Narindwa Sekimanga.
Shaidi Mkuu wa Gereza nae yuko pale kizimbani yeye muda wote amekaa tu pale kizimbani.
Hajajihangaisha kusimama labda kwa vile ni mrefu na hicho kitambi anachoka kusimama pengine.😂
Jaji Mruma: Shaidi nakukumbusha bado uko chini ya kiapo.
Mhe Lissu: Sasa turudi kwa viongozi wangu wa Chama uliowakatalia wasije kuniona kule Gerezani. Angalia majibu yangu na uangalie kiapo kinzani kuhusiana na kiapo kinzani nilichomjibu Kisabo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ametoa macho. Hafanyi lolote.
Mhe. Lissu: Mawakili wa Serikali mnafanya nini si mumsaidie shahidi wenu azione hizo nyaraka naona ananiangalia tu.
Wakili wa Serikali anaenda.
Mhe. Lissu: Hizo aya kwenye kwenye kiapo changu kinzani zinaonesha namna ulivyowazuia viongozi na wanachama ikiwemo mashahidi na mawakili watatu ambao ni Dickson Matata, Deogratias Mahinyila na Gaston Garubindi. Swali langu waeleze majaji kama umewahi kupinga haya maelezo yangu yaliyopo kwenye kiapo changu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Waheshimiwa Majaji nimeshalijibu hilo.
Jaji: Umeelewa swali lake kweli.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sina jibu.
Mhe. Lissu: Nalo ni jibu pia. Haya kwenye aya ya nne wewe umefanya kampeni ya muda mrefu ya wewe na mlalamikiwa wa pili kamishna mkuu mmehakikisha nashindwa kujitetea wala kuandaa utetezi wangu na matukio nimeyasema kwenye para H na Y. kwamba umewazuia mawakili wangu watatu ambao Ni Mahinyila, Matata na Garubindi kama umewahi kujibu hili.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli nimewazuia.
Mhe. Lissu: Je umeleta supplimentary affidavit? Au majibu yoyote kwenye jambo hilo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : anatoa macho. Anashika makaratasi na kuyaacha.
Jaji: Umeelewa swali?
Mhe. Lissu: Ulileta counter affidavit mara ya kwanza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio
Mhe. Lissu: Baadae ukaleta suplimentary affidavit?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
Mhe. Lissu: Sasa kwenye hizo nyaraka zako mbili kuna mahali kokote ulijibu tuhuma za kuwa umewazuia mawakili wangu na viongozi wa Chama?
Ntamamiro (Bwana Jela) : sijajibu.
Mhe. Lissu: Tuhuma dhidi yako na maafisa wako kusearch mawakili na nyaraka zao kisheria. Jibu swali kwamba waleta maombi wote watatu wamesema wanasearchiwa, wanakaguliwa na kusomwa hizo nyaraka.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Reg. 17(2) ya kanuni za Magereza inasemaje?
Anatafuta hiyo kanuni.
Mhe. Lissu: Ni kweli mgeni anayekuja Gerezani kutembelea mfungwa atasachiwa endapo atakuwa na wasiwasi na huyo mgeni?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Haya isome sasa
Ntamamiro (Bwana Jela) : A prison officer when has any ground suspiciously may direct to search that visitor. Anasoma kingereza kibaya sana.
Mhe. Lissu: Any ground for suspicion may search or cause to search. Kumbe ataamuru asachiwe kama atakuwa na sababu za kumshuku?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Mgeni ataambiwa aondoke akikataa kusachiwa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kwa mujibu wa kanuni hii ni kweli.
Mhe. Lissu: Anayemfukuza atatakiwa kuandika sababu za kumfukuza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : yuko kimya tena. Hebu rudia swali.
Mhe. Lissu anarudia swali. Si ni lazima uandike sababu za kumfukuza.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Siku mjibu maombi wa Kwanza alipokataliwa kuingia gerezani tar. 28/11 alipokataliwa kuingia gerezani iliandikwa sababu kuwa amekataa kusachiwa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kwa kanuni hii.
Mhe. Lissu: Tutajie kanuni hizo zingine tuzione? Kwenye kanuni kuna sababu yoyote nyingine kwa mujibu wa kanuni?
Bwana Jela: Sijaipitia kanuni yote.
Mhe. Lissu: Sasa mimi niliyepitia kanuni zote na hakuna sababu nyingine unasemaje?
Bwana Jela: Sina jibu.
Part 20 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
If you’re a Muslim and this appears on your timeline, please retweet. It might be the reminder someone needs to complete their solat. May Allah accept it from us.
Sometimes life forces you to grow faster than you planned.
Unajikuta unawajibika mapema kuliko wenzako.
Unabeba majukumu ambayo hukuwahi kufikiria utayabeba.
Na wakati mwingine unajisikia kama umeibiwa ujana wako,