#NenoLaLeo
Kila unaefahamiana nae au kujuana nae, ipo sababu ya msingi iliyowafanya mfahamiane au mjuane.
Jitahidi sana usiiharibu sababu hiyo, inaweza kuwa ndio njia ya mafanikio yako.
#NenoLaLeo
Usichukie mapito magumu unayokumbana nayo maishani mwako.
Nanasi ni tamu, limewekwa katikati ya miba.
Asali ni tamu imewekwa katikati ya kundi la nyuki.
Nyakati ngumu ni fursa, mapito tunayopita ni fursa…Tusikate tamaa ✍🏾✍🏾✍🏾
#NenoLaLeo
Tukisherehekea SIKU YA FURAHA ULIMWENGUNI Leo, tujitahidi sana kufanya vitu vinavyotupa furaha.
1. Kaa na watu wanaokupa furaha
2. Sikiliza vitu vizuri vya maana vinavyokupa furaha
3. Angalia vitu vizuri vya maana vinavyokupa furaha
4. Usipoteze muda kwa vitu vibaya
#NenoLaLeo#Tubadilike
“Vijana wanalalamika sio kwamba hawapendi kuwashirikisha matatizo yao, ila mnawatangaza, mnatumia shida zao kutoa mifano kama ya watu walioshindwa au kufeli maisha. Tukumbuke kuteleza sio kuanguka”.
Shida za watu sio matangazo, tubadilike.
#NenoLaLeo
Heri ya Siku ya Wanawake Duniani kwa wanawake wote 👏🏾
Tunawapenda ✅
Tunawathamini✅
Tunawajali✅
Tunawaheshimu✅
Tunatambua mchango wenu kwetu✅
Kwa Mwezi huu wa ibada, tunatumia muda wetu kuwaombea mafanikio mzidi kuilea, kuitunza na kuihifadhi Jamii🤲🏾
Safari ya Maisha ni Hatua, Muhimu kuzingatia Hatua zinatofautiana. Kamwe usilinganishe Hatua zako na za mwingine. Ukijifananisha utajiongoza vibaya, utajidanganya, utatengeneza husda na chuki. Heshimu na Ridhika na Hatua Zako, huyu ndio wewe🙏🏾
#AsanteKwa2025#HeriYaMwakaMpya2026
#NenoLaLeo#Uwekezaji
“Mafanikio ya Uwekezaji mzuri hudhihirika na kutamalaki iwapo utafanyika kwa watu.
Wekeza kwa kuibua, kuinua, kuchochea ukuaji wa Ustawi wa Maisha ya Watu.
Wekeza kwa kujenga mahusiano mazuri na watu.
Uwekezaji wa namna hii hulipa maradufu”
Wema Hauozi
#Neno_La_Leo#Heshima_Ni_Mali
Ikitokea upo katika mazingira ya kuchagua kati ya Heshima na Pesa, basi chagua Heshima.
Pesa ikiondoka inaweza kurudi. Heshima ikiondoka haiwezi kurudi.
Tunza Heshima yako ufurahie Maisha yako.
#Pesa_Ni_Kitu#Heshima_Ni_Utu
#Neno_La_Leo#Jali_Hisia_Za_Mtu
Muhimu sana kujua hisia au hali ya mtu kabla hujamshirikisha jambo lako. Tafakari kwanza kabla hujamshirikisha jambo lako mtu Mwenye Njaa, mwenye hasira, au anaepitia changamoto fulani. Jali kwanza hisia au hali yake kisha mshirikishe la kwako.
#NenoLaLeo#Jali_Muda_Wa_Mtu
Ukipata nafasi ya kuchat kwa sms na kiongozi, usitumie muda mwingi kumueleza mambo tofauti na lile mahsusi unalotaka kumshirikisha, viongozi wengi hawana muda mwingi wa kuongea kila kitu
#Muda_Ni_Mali
#NenoLaLeo
Huduma ya Kitaalamu inaenda sanjari na Malipo ya Huduma hiyo
Huduma ya Kitaalamu (mf: kutoka kwa Mawakili) inahusisha
1. Muda
2. Ushauri wa Kitaalamu
3. Utekelezaji/Ufanikishaji wa huduma
Kila mojawapo ina thamani yake.
Ukihudumiwa kimoja au vyote TAFADHALI LIPIA.
#TodaysThoughts
Professional work, attracts professional invoice. Experts’service include;
1. Time
2. Professional Inputs/Opinion/Guidance
3. Execution/Performance/Delivery
Each of the above categorically bear its value.
If any or all is furnished, please PAY accordingly.
#MojaYaLeo_NaSSH
Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia iliyobebwa na Dkt. @SuluhuSamia ili kuokoa afya ya kila mmoja wetu na kutunza Mazingira yetu imepelekea kufanyika kwa Mkutano Mkubwa Wa Wakuu wa Nchi 25 barani Afrika hapa Dar ea Salaam kuieneza Afrika nzima. Pongezi sana #SSH
#NenoLaLeo
“Mtu akitambulishwa kwako na “A” ili mshirikiane katika kazi fulani, halafu baadae mtu huyo akaongeza kazi nyingine na akakwambia usimwambie “A”, achana na huyo mtu, kama hawezi kuwa MWAMINIFU (Loyal) kwa “A”, hawezi kuwa MWAMINIFU kwako
#UAMINIFU NI UTU
#Tafakari
#NenoLaLeo
“A” akikuunganisha na LINE au NETWORK yake anataka mfanikiwe kwa pamoja.
Sio uungwana kwenda kufanya biashara na LINE au NETWORK hiyo bila “A” kufahamu tena unadiriki kumfahamisha usimwambie “A”.
Jiulize “A” akijua atakufikiriaje?
UAMINIFU NI UTU
#Tafakari✍🏾✍🏾✍🏾
#NenoLaLeo
“Ukishakua mvuvi usiogope bahari, yakija mawimbi, upepo mkali au ghasia za baharini uwe tayari kukabiliana nazo”
Kuwa tayari kukabiliana na changamoto unazokumbana nazo katika harakati za maisha.
Usiwe mnyonge, pambana, usikate tamaa.
#Tafakuri✍🏾✍🏾✍🏾
#NenoLaLeo
Kwa kawaida wanaume huwa hawaelezi shida zao, huwa wanateseka kimya kimya.
Ukiona mwanaume mwenzako anakueleza shida zake ujue wewe ni tumaini lake la mwisho, ukiwa na nafasi MSAIDIE, USIMWANGUSHE ~Dr. D. Marandu
#Tafakuri✍🏾