Wafilipi : 2 : 3 - Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.
TUJIELIMISHE ILI KUJISAHIHISHA.
KESI YA LISSU: HAKUSHINDWA BALI MAHAKAMA ILIAMUA KUWA ANA KESI YA KUJIBU HIVYO UTETEZI UNAFUATA.
Pamoja na kuheshimu uamuzi wa Mahakama, mimi ninaendelea kuhimiza busara na hekima zitumike katika ngazi zote za maamuzi ili taifa letu liondokane na jambo hili la kusikitisha. Tuweze kuambizana ukweli, kusameheana na kuridhiana.
Sizungumzii hatia au kutokuwa na hatia kwa Lissu; hilo ni jukumu la Mahakama. Ninazungumzia mazingira ya kesi hii, historia yetu na umuhimu wa sheria kutumika kwa usawa. Tutambue:
1. Kesi ya Tundu Lissu ina tofauti kubwa na kesi nyingi za uhaini zilizowahi kutangulia hapa nchini. Katika kesi hizo za kihistoria kulidaiwa kuwepo njama, washirika, mipango ya pamoja ya kuipindua Serikali, na katika baadhi ya kesi washirika kutoka jeshini na madai ya kupanga kumuua Rais.
Katika kesi hii Lissu ameshtakiwa peke yake, na kiini cha shtaka kinahusu kauli zake za hadharani. Hii ni tofauti muhimu inayostahili kutafakariwa bila kuingilia kazi ya Mahakama.
2. Lissu anashitakiwa kwa uhaini chini ya kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, kutokana na kauli alizotoa katika mkutano wa CHADEMA tarehe 3 Aprili 2025. Kaulimbiu yake ilikuwa “No Reforms, No Election.” Upande wa mashtaka unadai kwamba kauli zake kuhusu “kukinukisha”, kuzuia au kuvuruga uchaguzi zilivuka mipaka ya siasa za kawaida.
Kauli hizo ni kali. Lakini katika historia ya siasa zetu tumewahi pia kusikia kauli kali zaidi. Mfano wimbo maarufu: “Wapinzani tuwashike, tuwachanechane, tuwatupe.”
Hata Bungeni wimbo huo uliwahi kulalamikiwa lakini ikachukuliwa ni utani wetu wa jadi. Pia mitandaoni leo tunasikia kauli za kutishia watu, kuwaua au kuwapoteza bila hatua zinazoonekana kuchukuliwa kwa kiwango sawa.
Ndiyo maana wapo wananchi wanaojiuliza: Je, sheria inatumika kwa usawa kwa kauli za wanasiasa wa pande zote? Bibi yangu aliwahi kunikanya kuwa :Ukitania uwe tayari kutaniwa".
3. Lissu alitoa matamko yake hadharani au katika mikutano ya kisiasa. Wananchi wengi waliyasikia na wanayajua. Kwa hiyo, pamoja na kuacha Mahakama ifanye kazi yake kwa uhuru, ni vigumu kuzuia mjadala wa wananchi kuhusu jambo ambalo liko hadharani na linagusa siasa, sheria na haki za kiraia.
Ili mradi staha izingatiwe na mjadala huo usibadilishwe kuwa hukumu ya hatia au kutokuwa na hatia kabla ya Mahakama kumaliza kazi yake.
4. Kama Mahakama ingelikuwa imeamua kuwa hakuna kesi ya kujibu, hatua ya utetezi isingefunguliwa. Sasa Lissu ameomba kuwaita baadhi ya viongozi wakuu, akiwemo Rais Samia na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, kutoa ushahidi.
Historia ya nchi nyingine inaonyesha kuwa jambo la Rais aliye madarakani kutoa ushahidi katika shauri la jinai lina utata lakini si geni kabisa.
Mwaka 1807, katika kesi ya uhaini ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Marekani Aaron Burr, Burr aliomba ushahidi kutoka kwa Rais Thomas Jefferson, bosi wake. Jaji Mkuu John Marshall ndiye alikuwa muamuzi na alikataa "dhana kwamba Rais ana kinga ya moja kwa moja dhidi ya mchakato wa Mahakama pale ushahidi wake unapohitajika katika kesi ya jinai".
Jefferson hakulazimishwa kusimama mwenyewe kizimbani, lakini alitoa ushahidi kwa nyaraka na kanuni muhimu ikawa: hadhi ya Urais haimaanishi kwamba ushahidi muhimu kwa mtuhumiwa hauwezi kupatikana.
Baadaye, Marais wengine wa Marekani wamelazimika kutoa ushahidi au taarifa katika mashauri ya jinai inapohitajika. Ni pamoja na:
James Monroe — 1818
Ulysses S. Grant — 1876
Gerald Ford — 1975
Jimmy Carter — 1978
Jimmy Carter tena — 1980
Bill Clinton — 1996
Richard Nixon mwaka 1974 aliamriwa kutoa kanda za Watergate.
Mara nyingi ushahidi huo ulitolewa kwa maandishi, nyaraka, viapo/deposition au video badala ya Rais kufika mwenyewe mahakamani.
5. Hakika Hatua inayofuata katika kesi ya Lissu ni nyeti. Itatuonyesha mwanga katika masuala haya muhimu kuhusu utawala wa sheria na haki ya mshitakiwa kupata utetezi stahiki.
6. Kiuhalisia Wengine tumejikita kwenye swala la HEKIMA, BUSARA na HURUMA YA MUNGU.
For 500 days, @TunduALissu has been imprisoned in #Tanzania. His fight for democracy, human rights & political freedom is our fight too. Full solidarity with Tundu Lissu, @ChademaTZ2 & all Tanzanians standing up for democracy.
The IDU is gravely concerned by today's High Court ruling in Dar es Salaam ordering our Vice Chairman @TunduALissu to stand trial for treason — a charge carrying the death penalty.
After 16 months in detention for a speech, this ruling prolongs a politically motivated prosecution designed to silence Tanzania's opposition. We call for his immediate and unconditional release, and urge democratic governments worldwide to do the same. #FreeTunduLissu 🇹🇿
“Waheshimiwa majaji, mimi sina shida na wao kufunga kesi upande wa mashtaka. Nilisema tangu awali, hawa wamekwisha kata pumzi. Mimi ninauo shida katika hoja yao ya pili, kuomba kufanya majumuisho kuhusu kesi ya kujibu. Wakili wa Serikali anasema hakuna kifungu. Mimi namueleza, kifungu kipo. Kifungu cha 312 (1) cha CPA. Tusipoteze muda hapa. Twende kwenye hatua inayofuata. Tupewe nafasi ya kuwasilisha maelezo yetu kama kuna kesi ya kujibu. Kwa ushahidi wao waliowasilisha hapa, hakuna kesi ya kujibu. Mimi nipo tayari kuanza, nianze mimi, nipewe nafasi ya kuwasilisha sasa…,” - Tundu A.M Lissu, Mahakama Kuu, 17 August 2026
Usikose usiku wa leo kwenye tovuti yetu ya #TheJeneraliUlimwenguPost — https://t.co/yMQ2kyCyQP
#MZENGWE: Jenerali Ulimwengu ahojiana na Jaji Joseph Warioba, wakigusia mada kuu na nzito, zikiwemo:
• Hali ya kisiasa nchini
• Uwajibikaji kwa yaliyotokea Oktoba 2025
• Jumuiya ya Madola
• Maridhiano
• Amjuavyo Emmanuel Nchimbi
• Kuachiwa kwa Tundu Lissu
• Chama Cha Mapinduzi (CCM)
• Na mengine mengi.
https://t.co/zP9NvmpNnR
https://t.co/6qYNVkS3qF
Kesi imeanza na Mwenyekiti Lissu akasema analo neno la kusema kabla ya kuanza kesi.
“ Lengo pekee la DPP (Mkurugenzi wa mashtaka)la kufungua mashauri haya ni ili kupoteza muda tu ili niendelee kukaa Mahabusu .
Leo ni siku ya 166 tangu tarehe 24 Februari tangu Mawakili wa serikali waende mahakama ya Rufaa na huko nikawashinda na sasa tumerudi Mahakama kuu lakini tumerudi baada ya siku 166,tuendelee lakini ipo siku tutazungumza kuhusu haya yote yalioendelea na kuhusu huyo anaewatuma na itambidi awajibike” anasema Mwenyekiti.
“Someone will have to pay for all of this someday” says Honerable @TunduALissu
Mtuhumiwa hawezi kujichunguza mwenyewe.
Tangu mwanzo tulisema tume ya Jaji Chande haiwezi kuleta ukweli, iliundwa kuficha ukweli na kusafisha watuhumiwa.
Ndio maana ile tume ilikuja na hoja za ajabu kwamba:
1. Watu wanatekwa kwasababu za kimapenzi
2. Kwasababu za ushirikina
3.kwasababu za kibishara.
Kuna familia zinasema na zina ushahidi wa ndugu zai kutekwa na kupotelea vituo vya polisi, lakini Chande hakusema hilo popote.
Kama ilivyokua tume ya Chande.
Hiki kinacholazimishwa kitaharibu na kuwagawa Watanzania zaidi.
Jaji wa Museveni ambapo wapinzani wanauwawa, wengine wako jela na wengine wamekimbia Nchi.. labda atawapa uzoefu zaidi wa namna ya kuumiza watu lakini sio kutafuta ukweli.
Asubuhi ya Leo nimepata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa kata sita jimbo Tarime vijijini.
Chama chetu kiko imara na tayari kutoa uongozi kwa Nchi yetu.
Mpaka sasa tumekusanya TSh. Milioni 269.5, na sasa tumebakiza TSh. Milioni 64.5 pekee kufikia lengo la TSh. Milioni 334 kwa ajili ya Baraza Kuu la Umma.
CHANGIA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba: 22606600140
Jina: Chama cha Demokrasia na Maendeleo