#Today in Tanzania 🇹🇿
Check out the programme details for Aga Khan University’s first-ever global convocation. Watch the live stream today, 22 May 2021 at 3:30pm Tanzania time at https://t.co/sSNErGSyoT or https://t.co/ESAwEtJoT2. #AKU20#AKUConvocation#AKDN
Melinda French Gates, co-chair of the Bill & Melinda Gates Foundation, will be the chief guest at AKU's first global convocation on May 22, 2021.
Learn more https://t.co/6oylYmn83t #AKUConvocation#AKU20
#Today
Check out the programme details for Aga Khan University’s first-ever global convocation. Watch the live stream today, 22 May 2021 at 3:30pm Tanzania time.
#AKU20#AKDN#AKUConvocation#Tanzania#URT
Mwenyezi Mungu ndiye aliyetupatia uongozi hivyo tuutii na kuuombea tena kwa Umoja wetu.Lakini pia, tuwaombee viongozi wote wa ngazi zote hata huko Wilaya zetu, Tarafa zetu na Kata zetu. Niwaakikishien; Huwezi kumchukia mtu unayemuombea- Askofu Dkt.Cheyo #RaisSamiaNaViongoziWaDini
Miaka takriban 6 imepita tangu niondoke kwenye Jengo hili.. Leo ninayo furaha kurudi tena na kupata fursa hii ya kulihutubia Bunge hili ambalo limenilea, limenijenga, kuninoa na kufanya uwezo wangu uonekane na wote mpaka kuweza kushika nafasi hii niliyonayo - #RaisSamiaBungeni
Nimefarijika kuona baadhi ya wenzangu niliokuwa nao bado wapo ndani ya Bunge hili. Lakini, nimepata faraja zaidi baada ya kuziona sura mpya zenye ari na matumaini ya kuwatumikia Watanzania. - #RaisSamiaBungeni@bunge_tz@MsigwaGerson
Mhe.Spika; Nashukuru sana kwa ukarimu wako pamoja na Waheshimiwa Wabunge kunikaribisha leo hii ndani ya Bunge hili. Nimekuja kulihutubia Bunge hili baada ya nchi yetu kupita kwenye kipindi kigumu cha historia ya uongozi. - #RaisSamiaBungeni
Kwa sababu hiyo, kabla sijaendelea mbele na hotuba yangu, naomba sote tusimame kwa dakika moja tumuombee Hayati Rais Magufuli...
Mwenyezi Mungu aipumzishe Roho yake mahali pema peponi. Amina. - #RaisSamiaBungeni
Hivyo basi, napenda nitumie fursa hii kurudia tena kutoa pole nyingi sana kwa familia, hususan Mama Suzan Magufuli, Mama wa Marehemu; Mjane wa Hayati Dkt. Magufuli, Mama Janet Magufuli; watoto, ndugu pamoja na jamaa. - #RaisSamiaBungeni@tanzaniagov@IkuluTanzania@ikuluzanzibar
Napenda pia kutoa pole kwa Bunge hili Tukufu ambalo kabla awe Rais alikuwa mwenzenu kwa miaka 20. Aidha, kama ivyofahamika, kwa mujibu wa Katiba yetu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni sehemu ya Bunge hili. Hivyo basi, sina budi kulipa pole Bunge hili.- #RaisSamiaBungeni
Nitumie fursa hii pia kurudia kuwapa pole nyingi Watanzania wote kwa kumpoteza Kiongozi wetu mpendwa. Kwa hakika, Taifa letu limeondokewa na mmoja wa viongozi mahiri, mzalendo, mwana mwema wa Tanzania ambaye tulimpenda na tunathamini mchango wake kwa taifa. - #RaisSamiaBungeni
Mapenzi haya ya Watanzania yalidhihirika wazi kipindi cha maombolezo na mazishi ambapo sote tulishuhudia idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza kumuaga. - #RaisSamiaBungeni
Mimi binafsi, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kushusha kudra yake kwangu mimi mja wake, kwani dhamana hii ni kubwa na yenye mitihani mingi. Hivyo, namwomba Mwenyezi Mungu anisaidie. - RaisSamiaBungeni @bunge_tz@IkuluTanzania@Sheria_Katiba@tanzaniagov
Na hapa naomba niwashukuru kwa moyo wa dhati kabisa, Waheshimiwa Marais Wastaafu wote pamoja na Viongozi wote Wakuu wa Kitaifa kwa kuwa nami bega kwa bega katika nyadhifa zangu mbalimbali za utumishi nilizopitia na kushika. - #RaisSamiaBungeni
Niseme wazi kuwa uwezo wangu wa uongozi uliibuliwa na Mhe. Amani Karume aliyenipa nafasi ya Uwaziri katika kipindi changu cha mwanzo na cha pili nikiwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. - #RaisSamiaBungeni