Ninajisikia heshima na furaha kubwa kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika @WHOAFRO .
Huu si ushindi wangu binafsi tu, bali ni ushindi wa Waafrika wote katika azma yetu ya pamoja ya kufikia lengo la afya kwa wote. Nawashukuru sana nchi wanachama kwa imani kubwa mliyonionesha. Tunapokabiliana na changamoto mpya na zinazoendelea katika mifumo ya afya barani Afrika, dhamira yangu ni kushirikiana na wadau wote kuimarisha mifumo hiyo, kuendeleza usawa, na kuhakikisha kuwa hakuna anayesahaulika. Safari hii ni yetu sote. Twende pamoja kwa mshikamano na maono ya pamoja. Asanteni sana.