Dear Lord,
Today, let September give me my spark back, make waking up feel good again, put laughter back in places that got too serious, give me stories worth telling, pictures worth keeping and days I wish would slow down. Let me feel proud of myself, excited about my life and genuinely happy with where things are headed. in Jesus’ name. amen🙏🏽
"Maneno machungu huacha makovu katika moyo wa mtu. Ukilazimika kuyatumia dhidi ya mtu, basi yatumie kikamilifu mara moja kisha uachane nayo. Kuyarudia rudia ni kutonesha makovu na maumivu yake huishia kujenga chuki na ikiwezekana kisasi. Usiyarudie maneno machungu, buni mapya!"
Unaweza kuwa unatumia nguvu nyingi kulinda uhusiano usiokuwepo. Unawekeza kwenye ‘urafiki’ ambao ukijipa muda kidogo wa kutulia, ukapunguza kidogo mawasiliano si kwa lengo la kumwuumiza mtu bali kukagua uimara wa ‘mtandao wako,’ unagundua kumbe kile ulichofikiri ni urafiki ni kufahamiana na kukutana na watu mara kwa mara.
Unagundua kumbe, kwa muda mrefu umekuwa ukijiamulia mambo, ukiwapa watu mnaofahamiana nafasi ambazo hujajiridhisha pasi na shaka kuwa wanazihitaji, na kwamba jitihada zako za kudumisha uhusiano hazitambuliki kama unavyofikiri.
Halafu saa nyingine ukirudi nyuma kidogo, ukauvaa ujasiri kidogo wa kusema hapana, si kwa lengo la kuwa mchoyo bali kuusaili upya udhati wa ‘mtandao wako’, unagundua kumbe wanaokuita ‘rafiki’ ‘ndugu’ ni mtandao wa watu mnaofahamiana, mnaofanya nao kazi wanaonufaika na uwezo wako mdogo wa kujiwekea mipaka.
"Rizki ikiwa yako, ulimwengu wote utakula njama kuhakikisha inakufikia mikononi mwako. Rizki isiyo yako, binadamu mmoja tu anaweza akaikwamisha na usiipate. Na ikitokea umefanikiwa kuipata basi ulimwengu utakula njama utaiputa mkononi mwako au itakutemesha mdomoni mwako."
Maisha yana namna yake tofauti ya kutufundisha. Hakuna kinachokutokea kikawa hasara. Kazi isiyolipa ndiyo hiyo hiyo inakufundisha ujuzi. Kazi unayopoteza ndiyo inakupa ujasiri wa kujitafuta na kuanza upya. Ugomvi na mtu unayempenda unakufundisha umuhimu wa kuheshimu mipaka. Urafiki unaousitisha unakufundisha kile hasa unachokitaka. Biashara inayokutia hasara na hatimaye inakufa inakufundisha kufanya maamuzi sahihi.
Wakati wewe unasubiri ufurahie mema, saa nyingine utambe, ushuhudie na kuwanyong’onyeza watu, maisha yanakupiga tukio linalokukumbusha somo muhimu la unyenyekevu na kuheshimu watu. Wakati wewe unasubiri nyakati za neema, maisha yanakuletea maumivu yakuandae kushukuru hata kwa rasharasha za mema kadri zinavyojitokeza. Kuchelewa kupata kile unachokitaka kunakufundisha somo muhimu la subira na kupoteza ulichokipigania kunakufundisha kile hasa kinachobaki unapopoteza.
Ukweli tusioupenda ni kwamba hata mambo yanapokwenda kombo kinyume kabisa na matarajio, bado kuna somo muhimu katika maisha tunaweza kulipata. Ukichunguza vizuri utagundua yale maamuzi ya maana yaliyobadilisha kabisa mwelekeo wa maisha yako, aghalabu yalifanyika katika zile nyakati za machozi mengi—kukataliwa, kusalitiwa, kuishiwa, kufukuzwa, kuumizwa, kufilisika, kudharaulika, kushindwa na kadhalika. Ule ukurasa wa maisha usiopenda kuusoma kwa sauti ndio hasa uliokufundisha thamani ya kurasa nyingine unazozisoma kwa ujasiri mbele za watu.
"Maisha ni bundle unaishi kwa kulipunguza si kibubu kwamba unaishi kwa kuongeza. Ukishazaliwa,siku zako za kuishi haziongezeki tena bali zinapungua kutoka kwenye jumla ya siku zako za kuishi duniani.Kesho si nyongeza bali ni makato.Usihesabu zimebaki ngapi bali zimepungua ngapi."
"Ukiwa ujanani, uzeeni ni mbali kuliko utotoni ulikotoka, wakati ukiwa uzeeni, ujanani ni mbali kuliko unapokwenda. Ndio maana, ujana ni tajiri wa matumaini na uzee ni tajiri wa majuto. Chagua kutumia vizuri ujana wako ili uwe na majuto kidogo uzeeni." ~Togolani Mavura.
"Kila unayemuona, hata yule mwenye tabasamu pana kiasi gani na bashasha kama zote, ana yake moyoni na kichwani ambayo kwa kimo na kipimo chake yamemuelemea. Pambana na yako usitamani ya mwenzako." ~Togolani Mavura.
"Ni rahisi sana kushawishika kumuumiza au kumdhalilisha mtu kupitia aibu yake. Kabla ya kufanya hivyo usisahau kuna watu pia wamesitiri aibu zako. Kumbuka kila mtu ana aibu zake. Hakuna aliye mkamilifu, sote tumesitiriwa. Kila mtu ana 'mchomoa betri' wake." ~Togolani Mavura.
Dear Lord,
Today, I refuse to believe I’ve seen the best You can do with my life. There are places I haven’t been, people I haven’t met, money I haven’t made, and moments I haven’t lived yet. Don’t let disappointment make me expect less from my future. Surprise me with how much can change. Let the next season of my life make the last one look small. in Jesus’ name, amen 🙏🏽
Dear Lord,
Today, I step into destiny by force. No weapon formed will prosper. My feet won’t stumble, my hands won’t fail, my voice won’t be silenced. I decree favor, sudden breakthroughs, and divine surprises. What was locked is now open, what was denied is released, what was hidden is revealed. This week will showcase me and deliver miracles with my name on them. in Jesus’ name, amen 🙏🏽
"Yote tisa, katika maisha hatimaye tunatafuta amani ya moyo. Ama utamani kukuche ukimbilie kibaruani ukapate amani, au kuchwee jioni ukimbilie nyumbani ukapate amani ya moyo wako. Kupoteza amani ya moyo nyumbani na kazini ni kushindwa mechi 'home and away'. Chagua walau moja."
ربما السلام الحقيقي لا يأتي حين تنتهي المتاعب، وإنما حين نتوقف عن انتظار حياة بلا متاعب
Huenda amani ya kweli haiji pale matatizo yatapoisha, bali pale tutapoacha kutarajia maisha makamilifu yasiyo na matatizo.
الصدمة لا تأتي لتؤلمك فقط، بل لتكشف لك ما كنت ترفض رؤيته
Mshtuko hauji ili kukuumiza tu, bali unakuja kukufunulia yale ambayo ulikuwa unakataa kuyaona.
Dear Lord,
Today, i’m looking at everything i already survived. i went through hell behind closed doors and didn't even fold, so i know i can never doubt You. i declare that You are about to fix my life so beautifully that the struggle won't even make sense anymore. the payback for my pain is going to be legendary. In Jesus’ name. amen🙏🏽
#TajiriLaKihaya
Sheria Mpya imetoka rasmi 📢*
GN. NO. 158C - "Electronic Transactions (Mandatory Electronic Payments)"
Iliwekwa saini 30th June, 2026 na Waziri wa Fedha *KHAMIS MUSSA OMAR*
*MAANA YAKE KWA KISWAHILI RAHISI:*
Kuanzia sasa malipo haya 9 LAZIMA yafanywe kwa *malipo ya kielektroniki* tu. Pesa taslimu/Cash haitakubaliwa tena.
*MALIPO 9 YANAYOPASWA KUWA ELECTRONIC:*
1. *Usafiri* - Basi la haraka BRT, feri, madaraja, mabasi ya mikoani, taxi za online, ndege, treni, na maegesho
2. *Malls & Burudani* - Maduka makubwa, gym, sinema, ukumbi wa mikutano, viwanja vya michezo, vituo vya mafuta, maonyesho kama Saba Saba na Nane Nane
3. *Elimu* - Ada za shule za awali, msingi, sekondari, vyuo na vyuo vikuu
4. *Elimu ya Juu* - Michango ya vyuo na vyuo vikuu
5. *Hoteli & Migahawa* - Malazi, chakula na vinywaji
6. *Utalii* - Malipo yote ya huduma za utalii
7. *Mali* - Kupanga, kuuza au kununua nyumba, kiwanja au shamba
8. *Magari* - Kununua au kuuza gari
9. *Kilimo* - Kupitia vyama vya ushirika AMCOS kwa mazao ya kimkakati: pamba, korosho, kahawa, chai, mkonge, tumbaku + pembejeo na dawa
*VITU 3 MUHIMU KUVIJUA:
1. *Malipo ya Electronic ni yapi?* M-Pesa, TigoPesa, Airtel Money, HaloPesa, Bank Transfer, Card, NMB, CRDB nk.
2. *Kwa nini?* Kupunguza ufisadi, kuongeza mapato ya serikali, na kufuatilia mzunguko wa pesa
3. *Atakaeukiuka?* Biashara itapigwa faini na inaweza kufungwa
*ITAKUGUSA VIPI?*
- Ukinunua chakula hotelini > Lipa kwa simu
- Ukinunua tiketi ya basi la mikoani > Lipa kwa simu
- Ukipeleka mtoto shule > Ada kwa benki/sim
- Ukinunua mafuta > Lipa kwa card/sim
*Kwa kifupi:* Kuanzia sasa "beba pesa mfukoni" kwa malipo makubwa inakwisha pole pole
"Kujibu kunaweza kuamsha hasira zilizolala, kunaweza onyesha ujinga wako, kunaweza toa taarifa za ziada, kunaweza kukunasisha kwenye mtego, na kunaweza kuhitimisha dhana fulani watu walizonazo juu yako. Kutokujibu hakumaanishi huna majibu, bali kwaweza kuwa kipimo cha busara."
Dear Lord,
Today, i’m reclaiming my crown. no more wasting premium energy on low-value stress or checking for people who don't check for me. clear my circle of fake loyalty and cheap distractions. put that high-status peace on my life and elevate my vision. what’s meant for me can’t be blocked now. I’m too close to manifesting. in Jesus’ name, amen🙏🏽