🚨EXCLUSIVE
Wale ambao hamkuweza kufika Mahakamani November 6, 2026 na mlitamani kumsikia Mhe. Lissu wakati anawashona Majaji kabla hawajasoma “Hukumu waliyopewa”.
Nimewaletea full clip ya Dakika 56 za Mhe. Lissu aisee ni noma na nusu.🙌
Repost 200
#FreeTunduLissu
‼️EXCLUSIVE‼️
Wale ambao hamkuweza kufika Mahakamani November 6, 2026 na mlitamani kumsikia Mhe. Lissu wakati anawashona Majaji kabla hawajasoma “Hukumu waliyopewa”.
Nimewaletea full clip ya Dakika 56 za Mhe. Lissu aisee ni noma na nusu.🙌
#FreeTunduLissu
“Sheria inapotaja adhabu ya faini au kifungo, ni lazima kwanza itoe adhabu ya faini. Huu ni msimamo wa kisheria.”
“Mkinipa maximum sentence itakuwa ni ushaidi kuwa mmeelekezwa.”
Soma kwa sauti ya LISSU ndio utapata vibe😄
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 501
Wakili wa Serikali kimsingi anasema kwamba matukio ya vurugu za Oktoba 2025 yalitokana na kauli zangu kama nimemuelewa sawa sawa.
Kwenye kesi hii sina hakika kama mmeletewa ushahidi wa hotuba ya Jaji Chande wala yeye hajaja kutoa ushahidi hapa kuthibitisha hizo vurugu zilisababishwa na vurugu za wanasiasa gani.
Mnaambiwa mnitolee adhabu kali kwa kosa ambalo kama lipo limefanyika kwazaidi ya miezi 6 limefanyika baadae mimi nikiwa gerezani, mkikubaliana na hoja hiyo huu utakuwa ni uthibitisho mwingine kwamba huu ni uamuzi wa maelekezo.
Watu kicheko😂😂😂😂😂
Wakili wa Serikali Mkuu anataka muamini projo za mitandaoni, mkikubali utakuwa ni uthibitisho kuwa ni maagizo.
Wakili wa Serikali Mkuu amewaambia vile vile kwasasa hawana taarifa zozote kama hili ni kosa langu la kwanza, maana yake anaashiria kwamba kuna previous conviction, sasa kwavile hana uhakika mimi nitawaambia ukweli, sijawahi kutiwa hatiani na kosa lolote la jinai, wamenishtaki kwa zaidi ya miaka 24 tangu 2002 hawajawahi kunipata, I have never ever been convicted for a criminal offence, kwahiyo mnapofikiria adhabu lazima mjue kwamba mnatoa adhabu kwa mtu ambaye hajawahi kupatikana na hatia.
Mhe. Lissu anaendelea
Waheshimiwa majaji nafaham mnajua kwamba nina msiba mkubwa sana wa mtu aliyenilea, amenifanya mimi kuwa mwanasheria, kwasabu sikupata nafasi ya kumuuguza, nilikuwa natumaini kuwa Mahakama itaniacha niende nikamzike Mzee Alutte, I was hoping that, inaelekea kuwa hiyo haipo kwenye mahesabu yenu, mnapokuwa mnafikiria adhabu mfikirie na hilo, family obligationdls is a factor kuamua adhabu, huyu mtu amefiwa, Dunia nzima inajua, magazeti everywhere, I was hoping that nitapata nafasi ya kwenda kumzika huyu aliyenilea.
Waheshimiwa majaji leo ni mwaka na miezi 7 niko gerezani, mnapofikiria adhabu kali muitoe msije mkasahau kwamba huyu mtu ameshakaa gerezani kwa kosa ambalo mmelisema wenyewe kuwa sio kosa, halijathibitishwa na wala msije mkasau walichokisema jopo la Majaji watatu wenzenu: Jaji Mruma, Dkt. Longopa na Jaji Rumisha kuhusiana na niliyotendewa gerezani.
Wamesema nimenyimwa fursa ya kuwasiliana na mawakili wangu, Viongozi wenzangu wa chama halali cha Chadema, nimenyimwa fursa hata ya kuomba Mungu. Majaji wenzenu wamesema hayo yaliyotendeka nilinyimwa fursa na haki ya kujitetea, msije mkasau hayo mnapofikiria adhabu kali.
Waheshimiwa Majaji mimi ni raia mwema wa nchi hii, mzalendo wa nchi hii, nimetumikia nchi hii kama Mbunge wa kuchaguliwa na Wananchi mara 2 nimekwenda Jeshini, nimekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria wa nchi hii, mimi sio mpiga kelele, I am a patriotic, ndio maana nimeona na mabalozi wako Mahakamani, wanajua mimi ni patriotic hivyo mnapofikiria adhabu msije mkasahau hoja hii.
Waheshimiwa Majaji gerezani sio mahali pazuri sana, nasema hivyo kwasababu nimeishi kwa siku 577, nakaa kwenye chumba cha sita kwa sita, sio sheraton hotel, unaweza ukasema tu funga kama hujui Gereza ni nini?
Nasema haya kwasababu mimi sio mzima sana, kwenye huu mwili wangu nina operesheni 25, visu vya madaktari, ninatembea na risasi mwilini.
Katika risasi 16 zilizoingia mwilini moja walishindwa kuitoa, ninatakiwa niwe naenda Hospital Ubeligiji, Hospital ya chuo kikuu cha Luven nilikotibiwa baada ya yaliyonikuta miaka 9 iliyopita, nimeshamiss appointment 4 kwasababu ya kesi hii, juu ya yote hayo Majaji nina kisukari huu mwaka wa 6 sasa, kwahiyo mtakapokuwa mnatafakari hiyo adhabu kali, mkumbuke hilo kwamba hali yangu ya kiafya sio nzuri sana.
Waheshimiwa majaji kosa la uchochezi mara ya mwisho nilipoangalia ni kosa lenye dhamana, kama itawapendeza Kwa vile hili kosa lina dhamana, mnipe dhamana ili nikatie uamuzi wenu huu rufaa nikiwa nje kwa dhamana lakini muhimu zaidi pia ili nikamzike huyu aliyelala (Mzee Alute), nilisema sina mpango wa kuomba ila dhamana naomba.
Part 502 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 496
Upande wa mashtaka walieleza kuwa kauli ya mshtakiwa inatakuwa itazamwe katika muktadha mzima kuwa aliitishia serikali na kuwa mshtakiwa alikuwa na lengo la kuitisha serikali regardless kama serikali ilitishika au la!
Ushahidi wa upande wa utetezi mshtakiwa alisema maneno hayo lazima yapimwe katika muktadha wa kisiasa na lengo kwa kauli hiyo ilikuwa ni kueleza msimamo wa kisiasa wa Chadema na lengo lake halikuwa kuitishia Serikali, mtazamo huu ulingwa mkono na shahidi wa 2,3,4 na 5 kuwa kauli ya No reforms, No election ililenga kueleza ushawishi wa kisiasa.
Upande wa utetezi ulisema neno uasi lazima nilitazamwe katika muktadha wa kisiasa na kauli hiyo haikuwa na lengo la kuitishia Serikali au kuchochea vurugu.
Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha nia hiyo kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia serikali na sio hisia tu. Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha
Kwa ushahidi uliotolewa kuna mambo ambayo hayabishaniwi, kwanza Chadema imekuwa inatetea mabadiliko ya kikatiba, na mfumo wa uchaguzi na msimamo wa No reforms, No election, kupitia mkutano huo wa 3/4/2025 mshtakiwa alitoa hayo maneno mbele ya viongozi wenzake, wanachama, watia nia na waandishi wa habari na mkutano huo ulirushwa live.
Upande wa utetezi wamemaintain kuwa kauli hiyo ni ya kisiasa ililenga umma to boycott uchaguzi na sio kuitishia serikali.
Tumeangalia kauli zilizotolewa na mshtakiwa na tumeona kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja hatujaona kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali, tumeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 tumeona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali.
Tumeona kwamba ushahidi uliotolewa na mashtaka una fall short kuthibitisha shitaka la uhaini hivyo katika kiini hiki cha pili tunaona ushahidi haujakidhi kuonyesha nia ya uhaini.
Kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kuna vitu vitatu ikiwemo factuai issues, mahakama lazima iangalie ushahidi kujiridhisha na tatu ni ushahidi uoi umetolewa.
Mahakama inaona kwamba tafsiri ya maneno ya Lissu bila tangible evidence tumeongozwa na kanuni kwamba nia (mens rea) ni internal state of mind lazima liambatane na ushahidi wa kimazingira na vitendo vya kufanya uhaini.
Nia ovu siku zote inakuwa inferred kutoka kwa maneno na matendo ya mshtakiwa.
Part 497 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
The Court has clearly said:"On the evidence available, the prosecution has failed to prove that Tundu Lissu intended to commit treason." Why are they now pulling a minor incitement crime. How far is this court willing to go just to kiss the zanzibari queen bee butcher's ass? Wtf!
Yani alieuwa watanzania kwa MAELFU #MO29 ni SAMIA ila adhabu wanataka apewe LISSU aliekuwa Jela siku hiyo ya mauwaji ya kikatili.
KATUGA huu upumbavu unaopambania utagharimu mpaka kizazi chako cha 7.
Mtu mmoja tu anaamua kuzima internet nchi nzima!!
Utawala wa aina hii ndio tunaukataa na kuupinga.
Nchi haiwezi kuendeshwa kwa mood na hisia za mtu mmoja.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 498
Jaji Ndunguru anasema katika kutafisiri hicho kifungu cha 319(1-2) cha CPA Mahakama ya Rufani ilielezea kwa marefu na mapana kwenye kesi ya DPP vs Zombe kuhusu kifungu hicho kuwa sio automatic.
Kwakuwa mshtakiwa hakushtakiwa na kosa dogo, Mahakama pia haiwezi kutumia kifungu hicho bila kumpa mshtakiwa haki ya kusikilizwa au kumpa notice.
Kwa mujibu wa ushahidi uliopo kuwa maneno hayo yalirushwa live ili kuuhabarisha umma na video hizo video hazikutolewa mahakamani na kwa vile hajakanusha kutamka maneno hayo na upande wa jamhuri umesema kuwa alilenga kuchochea umma na mashahidi wa upande wa utetezi nao hawajakataa kuhusu mshtakiwa kutamka maneno hayo.
Tumeridhika kwamba mshtakiwa kutamka maneno hayo hadharani mbele ya umma alilenga kuchochea umma ili kuvuruga uchaguzi wa 2025 kwa njia isiyo ya amani kutokana na maneno yake hivyo basi tukiongozwa na maamuzi mbalimbali na kwa muktadha wa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu kosa lililotengenezwa na kifungu cha 390 ni kosa dogo la uhaini, kifungu cha 390 kinalengo la kuzuia crime katika hatua ya mwanzo before public harm.
Kwa tafsiri yetu tunasema kifungu hiki kina prevent nia na present danger.
Upande wa mashtaka wanapaswa kuthibitisha kuwa maneno ambayo mshtakiwa aliyatamka kufanya instigation yalikuwa communicated, pia mshtakiwa alilenga kuwa mtu au watu watende kosa.
Tunaelewa kwamba kifungu cha 390 kinatumika kwenye kosa lolote hakijataja kosa lolote pale, tunaamini kwamba kufanya kosa la uchochezi kunaweza kupelekea present danger, tunaamini ni minor offence na ni cognate offence kwa mujibu wa 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu.
Ni kwa mtazamo wetu sasa kwamba ni common sense kwamba incitement ni component ya offence ya treason hivyo sio lazima mtu awe charged independently.
Kulingana na ushahidi uliotolewa mshtakiwa alichochea umma kuvuruga uchaguzi, kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi na kukinukisha vibaya sana.
Upande wa utetezi haujaonyesha ni kwa namna gani walipanga kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi, na mashahidi wa upande wa Jamhuri walieleza namna ambavyo walishawishika na maneno ya mshtakiwa mfano shahidi wa 4, 5,8 ,11, 13, 14 walishawishika na kujiunga na wale ambao walishawishika ili waweze kuvuruga uchaguzi.
Part 499 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 499
Jaji Ndunguru anasema kwamba Mahakama inaamini kwamba mshtakiwa alikuwa na notice ya kosa dogo hivyo alikuwa na nafasi ya kujitetea na ushahidi wote uliotolewa umejikita kwenye uchochezi na alichochea umma kuzuia uchaguzi wa 2025
Kwa mujibu wa kifungu cha 390 cha Kanuni ya Adhabu Mahakama imeridhika kwamba Lissu alitenda kosa la uchochezi kwa mujibu wa kifungu cha 390 cha Kanuni ya Adhabu.
Hivyo Mahakama hii inamtia hatiani kwa kosa hili la Uchochezi.
Jaji Ndunguru: Upande wa mashtaka
Anasimama Katuga anasema Kamba kwa mujibu wa kifungu cha 339 cha CPA mahakama hii inaweza kupokea mpaka ushahidi kwenye kutoa proper sentence.
Upande wa Jamhuri tunajua adhabu ina malengo mojawapo ni kutoa onyo kwa mtu aliyetenda kosa ili asirudie kosa hilo au makosa mengine na linakuwa onyo kwa watu wengine wenye nia ya kutenda kosa hilo ambalo mshtakiwa ametiwa hatiani.
Upande wa Jamhuri mbali na kutokuwa na previous records za mshtakiwa za makosa ya nyuma, kwa mujibu wa taarifa zilizopo polisi kumekuwa na ongezeko kubwa sana la watu wenye kutenda kosa la kuchochea umma wa watanzania kwa maslahi yao binafsi either ya kisiasa au ya kiuchumi.
Vitendo ambavyo mara zote vinaharibu amani ya nchi, vinaathiri uchumi wa nchi kwa maana ama vinapelekea uharibifu wa mali za umma zikiwemo na mali binafsi.
Hivi vitendo vya kichochezi vinaathiri uchumi wa nchi na vimepelekea umma wa watanzania kuwa na hofu kuwa kutakuwa na matukio ya uvunjifu wa amani hivyo wanashindwa kufanya shughuli za kiuchumi.
Waheshimiwa vitendo vya kiuchochezi vinaathiri uchumi wa wananchi na hili ni kosa kisheria, wakati mnatoa adhabu tunawaalika katika hotuba halali ya Jaji Chande na Tume yake baada ya kufanya uchunguzi bila kuchagua upande wowote walisema sababu za vurugu wakati na baada ya uchaguzi wa 2025 zilisababishwa na kauli za baadhi ya wanasiasa.
Kifungu cha 35 kinatoa general punishment ambayo adhabu yake ni miaka 5 hivyo tunaomba mahakama hii iangalie athari ambazo zimetokea kutokana na kauli ambazo mshtakiwa ametiwa hatiani pamoja na hotuba ya jaji chande.
Taarifa ya Chande inaonyesha hasara inayotokana na uchochezi uliotokana na kauli hizo.
Tunaomba adhabu kali Waheshimiwa majaji ili iweze kukidhi nia ya adhabu kisheria.
Waheshimiwa kifungu hiki kinasema adhabu kubwa ni miaka 5 au pamoja na faini.
Ni faini kiasi gani ni Mahakama kuangalia athari kutokana na athari zilizotokea. Ni hayo tu.
Jaji Ndunguru anamuuliza Mshtakiwa kama analolote la kusema?
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa majaji nina maneno ya kuzungumza ila naomba dakika 5 nifanye consultations na mawakili wangu ili niweze kuzungumza hayo ninayotaka kuzungumza.
Jaji Ndunguru:Sawa
Part 500 itaendea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 35 cha Penal Code, Cap. 16 R.E. 2023, endapo Tundu Lissu atapatikana na hatia ya uchochezi chini ya Kifungu cha 390, anaweza kuadhibiwa kwa kifungo kisichozidi miaka 5, kulipa faini au vyote viwili kwa pamoja.
Jamhuri imeshindwa kabisa kuthibitisha shtaka la uhaini dhidi ya Tundu Lissu. Kwa msingi huo, Mahakama imekubali kwamba ushahidi uliowasilishwa haujathibitisha kosa la uhaini.
Jaji Dunstan Nduguru anaeleza kwamba, pamoja na Jamhuri kushindwa kuthibitisha kosa kubwa la uhaini, Mahakama imepewa wajibu wa kisheria kuchunguza iwapo kuna kosa dogo linaloweza kuthibitika kutokana na ushahidi uliowasilishwa
Kwa mujibu wa maelezo ya Jaji Dunstan Nduguru wakati akisoma hukumu ya kesi hiyo anasema, mamlaka hayo yanatajwa chini ya Kifungu cha 339 cha Kanuni za Mwenendo wa Makosa ya Jinai,
Kifungu kinachoipa Mahakama uwezo wa kumtia mshtakiwa hatiani kwa kosa dogo linalotokana na kosa kubwa, pale ushahidi hautoshi kuthibitisha kosa kubwa lakini unathibitisha kosa dogo.
Jaji anasema Mahakama inatambua kwamba uchochezi unaweza kuwa cognate offence — yaani kosa dogo lenye uhusiano wa moja kwa moja na kosa kubwa lililokuwa katika shtaka la awali.
Jaji Nduguru anasema Mahakama imejielekeza katika (conviction for a minor and cognate offence) endapo mashtaka makuu hayajajitosheleza lakini ushahidi unaonyesha kosa lingine lililotendeka.
Mahakama imeridhika kwamba Tundu Antiphas Mughwai Lissu ametenda kosa dogo la uchochezi na hivyo Mahakama kumtia hatiani kwa mujibu wa Kifungu cha 380 cha Kanuni ya Adhabu.