“tutaanzisha tume ya maridhiano kwa ajili ya mchakato wa kuanza kuandika katiba mpya”.Ahadi ya Mgombea Urais CCM @SuluhuSamia wakati wa ufunguzi wa Kampeni za Uchaguzi Tanganyika Peakers Kawe Dar es salaam tarehe 28/08/2025.
Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema kuanzia Machi 2021 hadi Machi 2025, kiasi cha gesi asilia kilichozalishwa nchini kimefikia futi za ujazo bilioni 301.33, ambapo awali ilikuwa futi za ujazo bilioni 57.16 kwa mwaka.
Kiasi hicho ni kutoka Kitalu cha Mnazi Bay ambacho kimezalisha futi za ujazo bilioni 142.35 na futi za ujazo bilioni 158.98 kutoka Kitalu cha Songo Songo.
@TanzaniaLeaks@WilliamsRuto Tanzania ifanye hayo yote kwa manufaa gani? kama siyo tu kutaka kutuchonganisha na Wakenya. Tanzania haifungamani na upande wowote wa itikadi za kivyama za nchi yoyote mara zote huwa inaunga mkono maamuzi ya wananchi wa nchi husika.
Kesho tarehe 08 Juni, 2021 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre - Dodoma, Muda ni kuanzia saa 3 Asubuhi, Mhe Rais @SuluhuSamia atazungumza na wanawake wa Dodoma kwa uwakili wa wanawake wote nchini. Ndugu zangu wanawake tusikose kumsikiliza @CarolNdosi@fatma_karume
Maombi ya wawekezaji nchini yameongezeka kwa kipindi cha miezi miwili hadi mitatu iliyopita. Hii ni kutokana na wito wa Mheshimiwa Rais wa Tanzania, @SuluhuSamia kuwakaribisha wawekezaji wapya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. @SuluhuSamia ameondoka asubuhi hii kwenda nchini Uganda ambapo leo tarehe 12 Mei, 2021 atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika uwanja wa sherehe wa Kololo jijini Kampala.
Kwa kipekee pia Uongozi wa Wilaya ya Kisarawe na wananchi wote wanashukuru sana wadau wote walioshiriki na Watanzania kwa maana kupitia #KisaraweUshorobaFestival na #KisaraweUshorobaMarathon tumeweza kukarabati jengo letu la Baba/Mama na Mtoto na hivi karibuni tutalizundua rasmi.
Nawatakia kheir Wauguzi wote katika kuadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani. Serikali inatambua na kuthamini mchango wenu katika jamii. Nawaahidi kuwa tutaendelea kuboresha mazingira na maslahi yenu ya kazi ili mtimize majukumu yenu vizuri na kwa usalama. Chapeni kazi, tunawategemea.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameondoka asubuhi hii kwenda nchini Uganda ambapo leo tarehe 12 Mei, 2021 atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika uwanja wa sherehe wa Kololo Jijini Kampala