Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania Oktoba 29, 2025 Jaji Mohamed Chande Othman amesema vifo vilivyotokana na ghasia zilizotokea katika kipindi cha uchaguzi mkuu ni watu 518, ambapo wanaume ni 490 wanawake 28.
Mwenyekiti wa Tume iliyoundwa na Rais Dkt. Samia kuchunguza matukio yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu October 29,2025, Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman amesema Tume imejiridhisha kuwa matukio yaliyojiri October 29, hayakuwa maandamano ya amani bali ghasia zilizochangia uvunjifu wa amani kwakuwa maandamano hayo hayakuzingatia sheria za Nchi na Waandamanaji walibeba silaha.
Jaji Mstaafu Chande amesema hayo wakati akiwasilisha Ripoti ya Tume hiyo mbele ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Aprili 23,2026 Ikulu Jijini Dar es salaam.
MADHARA YA GHASIA
Idadi ya Vifo
“Tathmini ya Tume ni kuwa jumla ya vifo vilivyotokana na ghasia za Uchaguzi Mkuu ni 518, ambapo, wanaume ni 490, sawa na asilimia 94.6 na wanawake ni 28, sawa na asilimia 5.4. Vingi kati vya vifo hivyo vilikuwa sio vya kawaida (unnatural). Mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na vifo vingi zaidi, ukiwa na vifo 182, ikifuatiwa na Mkoa wa Mwanza vifo 90; Mbeya vifo 80; na Mkoa wa Arusha vifo 53.”
Kati ya vifo hivyo 518, ishirini na moja (21) vilikua vya watoto. Katika kundi hilo, 15 walikuwa watoto wenye umri kati ya miaka 15 – 17, wanne (4) walikuwa na umri kati ya miaka 7 - 10, na wawili (2) umri chini ya miaka mitano.
“Vifo 502 sawa na asilimia 96.9 vilikuwa vya raia (civilians), na 16 sawa na asilimia 3.1 vilikuwa vya maafisa na askari wa vyombo vya ulinzi na usalama.”
“Kati ya watu 518 waliofariki, 373 walifikishwa hospitali wakiwa wamefariki, majeruhi 121 walifariki wakati wakiwa wanapatiwa matibabu, na maiti 24 hakuna taarifa kutoka vituo vya kutolea huduma za afya. Kati ya Maiti 518, maiti 480 sawa na asilimia 92.7 zilitambuliwa na kuchukuliwa na ndugu na familia.”
HISTORIA MPYA UZINDUZI WA SOKO LA KIMATAIFA LA KARIAKOO
Leo Februari 8, 2026 historia imeandikwa jijini Dar es Salaam ambapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekata utepe na kuzindua rasmi Soko Kuu jipya la Kariakoo baada ya ukarabati mkubwa na ujenzi wa soko la kisasa kufuatia moto mkubwa ulioteketeza soko la awali Julai 2021.
Serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 28 katika mradi huu ili kutoa miundombinu ya kisasa ikiwemo mifumo ya kuzuia moto, mifumo ya kisasa ya kidijitali na ulinzi kwaajili ya soko kufanya kazi saa 24, vizimba zaidi ya 1,500 kwa wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa, na kuifanya Kariakoo iwe kivutio cha biashara ya kimataifa kwa wafanyabiashara kutoka nchi jirani kama Comoro, DRC, Rwanda na zaidi.
NINI BBC WANAKITAFUTA DHIDI YA TANZANIA?
Golf Microphone Uniform.
Upo ushahidi wa wazi kabisa kuhusu Ushiriki wa moja kwa moja wa baadhi ya Waandishi wa Habari wa mashirika ya Habari ya kimataifa kama vile CNN- BBC na Aljazeera waliyopo jijini Nairobi Nchini Kenya katika kukuza na kuchochea propaganda dhidi ya Tanzania kupitia vurugu zilizotokea October 29,2025. Mwanaharakati wa Kitanzania kwa jina la Maria Sarungi, ambaye pia amekuwa kama mshauri Mkuu wa harakati za Chadema,alitumia fedha nyingi kuendesha Kampeni kubwa kwenye Mitandao ya kijamii kwa kushirikiana na Waandishi wa CNN Nairobi Bereau, na sasa ameibukia katika shirika la utangazaji BBC kwa kuwatumia baadhi ya wanachama wa Chadema na wanaharakati anaowafadhili kwa makazi na malazi jijini Nairobi akiwemo SATIVA ambao walikuwa wakihamasisha Maandamano ya October 29 Nchini Tanzania.
Vyombo vya Habari vya Kimataifa kama BBC na CNN mara kwa mara vimeshutumiwa sana dhidi ya Nchi fulani fulani na dhidi ya hata watu maarufu duniani kwa(I)kupika habari(II) kuandika habari zenye kuchafua wasifu wa watu fulani fulani na hapa nanukuu kwa Kingereza👇🏾👇🏾
Aplogies & Editorial Failure.
"Once BBC leadership aknowledge tag"mistakes were made" failed its own standards of accuracy" for Instance,BBC apologize for running a demonization story about former Ukrainian President Petro Poroshenko.
Mwandishi wa Habari wa CNN- Nairobi na Mkuu wa Kituo cha CNN Nairobi Bereau ,Ndugu Larry Madowo alilipwa fedha nyingi ili kuweza kuratibu Kampeni nyingi kupitia Social Media ikiwemo ile Kampeni ya No Reforms No Election ya Chadema na baadae tena akalipwa fedha ili kuweza kutengeneza Makala ya kile kilichoitwa Mauaji ya watu 10,000 wakati wa vurugu za October 29,2025 Nchini,Tanzania.Mpaka leo Makala ile ya CNN haijawahi kuthibitisha Makaburi ya Halaiki ambayo walisema yapo eneo la UNUNIO,Dar es salaam. Chaajabu zaidi kabla ya kuanza kwa vurugu za Oktobar 29 katika eneo la kimara, Mwandishi wa BBC kwa jina moja la frank alikuwa mwandishi wa kwanza kufika katika eneo hilo, je alifika kwa bahati mbaya au kuna jambo alikuwa analijua? Vyombo hivi ni vya kuvitafakari!!!
Kwa muda mrefu CHADEMA kwa kushirikiana na Mshauri wao mkuu MARIA SARUNGI na wafadhili wao wa kimataifa ikiwemo AMNESTY INTERNATIONAL na KONRAD ADENAUER STIFFTUNG wamekuwa wakipambana kutaka kuonesha ubaya wa Tanzania na serikali iliyopo katika jamii za kimataifa bila mafanikio, ambapo baada ya Wanaharakati wa Ndani na Nje ya Nchi kuona Amani na Usalama wa Nchi ya Tanzania umeanza/Umeendelea kuimarika ndani ya muda mfupi tokea kutokea matukio ya vurugu ya October 29,2025, kupita Jarida la BBC-African Eye , watu hao wa Chadema waliokimbilia Nchini Kenya wameamua kuja tena na Mradi wao mpya unaoitwa "STATE OF FEAR" kwa malengo yale yale ya kuhakikisha Serikali ya awamu ya Sita haipati "Usingizi".
Baada ya kushindikana kwa Mapinduzi ya October 29,2025,Chadema sasa kwa ushirika na Waandaaji wa Jarida la BBC Africa Eye wameamua kuja na kitu kinaitwa "SECOND ATTEMPT TO TANZANIA'S DISTABILIZATION AGENDA".
Hii sio mara ya kwanza,mwaka 2024 Makada hawa hawa wa Chadema wakiongozwa na MARIA SARUNGI na SATIVA MWAKABELA kupitia The Chanzo Online TV walitengeneza Makala kama hii ya "State Of Fear" wakiishutumu serikali kwa Utekaji na Upotevu wa watu bila kuipa Serikali nafasi ya kujibu ndani ya Makala hiyo(Story Balancing).
Mradi huu wa kupangwa, wa Mahojiano ya Makada wa Chadema waliokimbilia Nchini Kenya(Hilda Newton,Twaha Mwaipaya,Sativa na Rose Mayemba) na Waandishi wa BBC ni sehemu ya kutaka kuifanya Nchi irudi kwenye vurugu na kufifisha juhudi za Serikali za kuleta maridhiano Nchini.
Usishangae kwenye Makala ya Kesho ya BBC African Eye "State of Fear" wahusika wakuu kwenye mahojiano hayo ni wale wale yaani Hilda Newtown Rose Mayembe,Twaha Mwaipaya na Sativa na usitegemee kuona taarifa yoyote(balance),kutoka Jeshi la Polisi wala Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali.
WAJASIRIAMALI SOKO LA FERI WAMSHUKURU RAIS SAMIA NA KUMPONGEZA KWA "BIRTHDAY" YAKE
Wajasiriamali wa soko la Kimataifa la Feri, Magogoni Jijini Dar Es Salaam wamesema tangu kuingia madarakani kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, biashara zao zinakwenda vizuri na kutoa faida zaidi, huku wakinufaika na uwezeshaji wa serikali kiuchumi ikiwemo mikopo isiyokuwa na riba pamoja na majiko ya gesi na mazingira rafiki ya ufanyaji wa biashara.
Hayo yamebainishwa na Wajasiriamali hao leo Januari 27, 2026 wakati wa maadhimisho ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais Samia, wakimuombea kheri, afya njema na maisha marefu ili aweze kuwatumikia zaidi, wakimshukuru pia kwa kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii na kiuchumi tangu kuingia kwake madarakani kama Rais.
Baadhi ya akinamama hao akiwemo Bi. Amina Johnson Kihondo, Mama muuza uji wa eneo la Feri, ameeleza kufurahishwa na Uongozi wa Rais Samia, akisema malezi na upendo wake umewezesha watoto wao kupata elimu bora bila ubaguzi pamoja na huduma nyinginezo muhimu.
"Mama Samia tunakupongeza kwa upambanaji wako dhidi ya changamoto zilizopo nchini, leo tuna amani na maendeleo na tunaendelea kutafuta riziki zetu kwa amani. Kingine tumpongeze pia kwa bidii yake katika kutuhudumia mahitaji yetu muhimu." Amesema Mjasiriamali Lucy Abunuai.
Aidha Katibu Mkuu wa Wa waendesha Bajaji wenye ulemavu Mkoa wa Dar Es Salaam, Bw. Juma Kiswanya, amemuombea kheri, afya njema na umri mrefu Rais Samia, akishukuru pia kuwa miongoni mwa Watanzania walioshiriki kusherehekea siku hii muhimu ya kuzaliwa kwa Rais Samia.
"Upandaji miti si tu kama tukio la mara moja bali ni sehemu ya mabadiliko ya kiutamaduni na sera ya taifa ya kuhifadhi mazingira, kulinda vyanzo vya maji, na kukuza maendeleo endelevu" Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
SERIKALI YAWAASA VIJANA KUTUMIA FURSA ZINAZOPATIKANA KUTOKANA NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO
Serikali imewataka vijana wanaohitimu masomo katika vyuo mbalimbali nchini kutumia fursa zinazopatikana kutokana na mabadiliko ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuweza kuendeleza maisha watakapokuwa wakifanya shughuli mbali mbali za kiuchumi kwenye sekta binafsi na sekta ya umma.
Hayo yalibainishwa jijini Dar es salaam, na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) katika Mahafali ya 11 ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika yaliyofanyika katika Kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Mhe. Luswetula alisema kuwa mabadiliko makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano yaani TEHAMA yanayojiri sehemu mbalimbali duniani na hata barani Afrika ambayo kwa sasa yamepewa jina la mapinduzi ya viwanda ya kizazi cha nne (Fouth Industrial Revolution) yamebadili kwa kiasi kikubwa uzalishaji mali katika uchumi na utoaji wa huduma za Umma kupitia mifumo ya kidijitali.
Aidha, Mhe. Luswetula aliwataka wahitimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na vijana kwa ujumla kuongeza nguvu katika kukabiliana na changamoto zinazotokana na mazingira ya mabadiliko ya kidijitali na kuzigeuza changamoto hizo kuwa fursa za kuongeza ufanisi wa utoaji huduma, kukuza masoko pamoja na kuhimili ushindani kwenye soko.
Mhe. Luswetula pia alitoa rai kwa wadau wa sekta binafsi hususani rika la vijana, walio masomoni, wahitimu na walioko makazini, kuwekeza zaidi katika sekta ya ubunifu wa mifumo ya biashara kidijitali katika sekta wanazofanyia kazi.
‘’Tukumbuke pia mwelekeo wa sera ya elimu ni kukuza ubunifu, na hatimaye uzalishaji katika sekta mbali mbali pamoja na uwezo wa vijana kujiajiri na kutengeneza ajira. Yapo pia maboresho ya sera na sheria mbali mbali kama vile sheria za haki miliki, sera za uwezeshaji mitaji kwa makundi mbali mbali ya jamii yote yakilenga kuleta nafuu katika sekta hizo’’ aliongeza Mhe. Luswetula.
Awali akizungumza katika Mahafali hayo kwa niaba ya Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Dkt. Tumaini Katunzi, Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu, Dkt. Indiale Kaaya alisema Katika mwaka wa masomo 2024/2025, Chuo kimetekeleza majukumu yake ya ufundishaji, utafiti na kutoa huduma za kiushauri ambapo Chuo kimekamilisha na kufanya udahili na ufundishaji wa programu mpya ngazi ya shahada ya kwanza ya Acturial Science. Chuo pia kimeandaa utaratibu wa ufundishaji kozi zake kupitia elimu masafa kwa njia ya mtandao.
Dkt. Kaaya aliongeza kuwa sambamba na elimu Masafa, Chuo kimeendelea kuwekeza katika ujuzi na utaalamu katika masuala ya sayansi ya Data na TEHAMA ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya kasi ya uelimishaji vyuoni na ongezeko la mifumo ya kidijitali na akili mnemba kutumika kwenye mafunzo.
Dkt. Kaaya aliishukuru Serikali kupitia Wizara ya Fedha kwa kufanikisha Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kutoka huduma za elimu kwa muda wa miaka sitini toka kuanzishwa kwake ambapo kwa sasa chuo kinahudumia nchi takribani 19 barani Afrika.
‘’Nipende kuchukua nafasi hii kudokeza kuwa tarehe 30 mwezi Agosti mwaka huu, 2025, Chuo kilitimiza miaka sitini tangu kuanzishwa kwake hapa Dar es salaam Tanzania na hadi mwaka huu chuo kinahudumia nchi wanachama kumi na tisa (19). Nichukue nafasi hii kushukuru Serikali kupitia Wizara ya Fedha ambayo imeendelea kukilea na kugharamikia Chuo hiki kwa niaba ya nchi wanachama.’’ Alisema, Dkt. Kaaya
Katika mahafali ya 11 ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika jumla ya wahitimu 312 walitunikiwa shahada ya Umahili, Stashahada ya Uzamili, Shahada ya awali, Diploma ya Juu na stashahada katika Takwimu rasmi, Takwimu za Kilimo, Takwimu za Biashara na Uchumi, Takwimu za Kilimo na Uchumi na Shahada ya Sayansi ya Data.
WASTAAFU ELFU 50 KUPATIWA VITAMBULISHO VYA KIELEKTRONIKI
Wastaafu wanaolipwa na Serikali wapatao 609 katika Wilaya ya Dodoma Mjini, wamepatiwa vitambulisho vya kielektroniki katika zoezi la kugawa vitambulisho hivyo linalotekelezwa na Wizara ya Fedha ambapo inalenga kuwafikia wastaafu wapatao elfu 50 nchini.
Hayo yalibainishwa na Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi- Huduma za Mfuko Mkuu, Wizara ya Fedha Bw. Perfectus Killenza, alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya zoezi la kutoa vitambulisho vya kielektoniki kwa wastaafu kutoka Wilaya ya Dodoma Mjini, linaloendelea katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma.
Bw. Killenza alisema kuwa vitambulisho vya kielektroniki ni salama, imara na vinaondoa changamoto zilizokuwepo awali za vitambulisho vya karatasi ambavyo vilikuwa vikiharibika kwa urahisi na kufanya taarifa zisomeke kwa shida.
“Vitambulisho hivi vipya vitarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wastaafu wetu kwa kuwa taarifa zao zitasomeka kwa urahisi kwa njia ya kielektroniki, sambamba na kuongeza ulinzi na uhakika wa kumbukumbu zao,” alisema Bw. Killenza.
Bw. Killenza alieleza kuwa zoezi hilo limekuwa muhimu pia katika kuboresha taarifa za wastaafu waliofanikiwa kufika Ofisi za Hazina kuchukua vitambulisho vipya jambo linaloondoa changamoto ya taarifa za baadhi ya wastaafu kutokusomana vizuri.
Pia Bw. Killenza alisisitiza wastaafu wote wa Wilaya ya Dodoma Mjini wanaohudumiwa na Hazina kufika katika Ofisi za Wizara ya Fedha wakiwa na nyaraka zao muhimu ili kurahisisha zoezi la kuhakikiwa na kupatiwa vitambulisho vipya vya kielektroniki kwa muda uliotajwa.
Bw. Killenza aliongeza kuwa zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya kielektroniki kwa wastaafu wote wanaolipwa na Hazina litafanyika nchi nzima kuanzia mwezi January mwaka 2026 kwa ratiba itakayotolewa.
Aidha, Bw. Killenza aliwakumbusha wastaafu wote wanaohudumiwa na Hazina kuwa huduma zote hususan zinazohusiana na pensheni ni bure hakuna gharama yoyote na hivyo kuwataka kuwa waangalifu ili kuepukana na matapeli.
‘’Wastaafu wote wanaolipwa na Hazina ni muhimu kuepuka watu au makundi yanayodai kuwawezesha kupata huduma kwa malipo, kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuwaweka kwenye mtego wa udanganyifu na kupoteza fedha zao,’’alisisitiza Bw. Kilenza.
Kwa upande wao Wastaafu wanaolipwa na Hazina Bw. Selemani Ramadhani na Bi. Severina Kivangala ambao wamefanikiwa kupata vitambulisho vipya vya kielektroniki, wameishukuru Serikali kwa kufanikisha zoezi hilo na kuomba elimu iendelee kutolewa ili kuwawezesha wastaafu au warithi wao kupata mafao yao.
Wizara ya Fedha, inaendelea na zoezi la kugawa vitambulisho kwa wastaafu wanaolipwa na Hazina, katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma, kwa muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe 15 Desemba 2025 hadi tarehe 30 Desemba 2025.
KAMATI YA MAMBO YA NJE YA BUNGE LA MAREKANI KUTEMBELEA TANZANIA,,,TANZANIA YAENDELEA NA JITIHADI KUIMARISHA MAHUSIANO NA MAREKANI
Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anafanya ziara Rasmi ya kikazi jijini Washington, D.C., nchini Marekani.
Katika ziara yake hiyo, Mhe. Waziri Waziri atakukutana na wadau Mbali mbali muhimu katika kuimarisha uhusiano wa baina ya Tanzania na Marekani.
Wakati akiwa nchini Marekani, Mhe. Waziri pamoja na masuala mengine, atakutana pia na kufanya mazungumzo ya kina na Serikali na Wabunge mbalimbali wa Bunge la Marekani.
Miongoni mwa viongozi ambao tayari amekutana nao ni Mbunge machachari wa Chama cha Republican Mhe. Brian J. Mast wa Jimbo la Florida, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Wawakilishi la Marekani na kukubaliana mambo kadhaa juu ya Uimarishaji mahusiano hayo na Tanzania pamoja na kupokea Mwaliko wa Kamati yake hiyo ya Bunge la Marekani kufanya ziara Rasmi nchini Tanzania mapema iwezekanavyo.
Imetolewa kutoka Ubalozi wa Tanzania Washington DC.
TANZANIA NI SALAMA KWA WATALII
Serikali ya Tanzania inawakaribisha watalii kutoka kote duniani kuendelea kutembelea nchi yetu. Tanzania ni salama na ina vivutisho vingi vya asili na kitamaduni vinavyovutia wageni.
Miundombinu imara ya utalii, Amani na huduma bora, zinaifanya Tanzania kuwa mahali pazuri kwa ajili ya mapumziko na burudani.
Serikali inaendelea kufanya kazi kuhakikisha usalama na faraja ya wageni wote. Karibuni Tanzania!
Videoni ni baadhi ya watalii waliongia Tanzania mwezi Desemba, 2025
TANZANIA NI SALAMA KWA WATALII
Serikali ya Tanzania inawakaribisha watalii kutoka kote duniani kuendelea kutembelea nchi yetu. Tanzania ni salama na ina vivutisho vingi vya asili na kitamaduni vinavyovutia wageni.
Miundombinu imara ya utalii, Amani na huduma bora, zinaifanya Tanzania kuwa mahali pazuri kwa ajili ya mapumziko na burudani.
Serikali inaendelea kufanya kazi kuhakikisha usalama na faraja ya wageni wote. Karibuni Tanzania!
Videoni ni baadhi ya watalii waliongia Tanzania mwezi Desemba, 2025
TANZANIA NI SALAMA KWA WATALII
Serikali ya Tanzania inawakaribisha watalii kutoka kote duniani kuendelea kutembelea nchi yetu. Tanzania ni salama na ina vivutisho vingi vya asili na kitamaduni vinavyovutia wageni.
Miundombinu imara ya utalii, Amani na huduma bora, zinaifanya Tanzania kuwa mahali pazuri kwa ajili ya mapumziko na burudani.
Serikali inaendelea kufanya kazi kuhakikisha usalama na faraja ya wageni wote. Karibuni Tanzania!
Videoni ni baadhi ya watalii waliongia Tanzania mwezi Desemba, 2025
TANZANIA NI SALAMA KWA WATALII
Serikali ya Tanzania inawakaribisha watalii kutoka kote duniani kuendelea kutembelea nchi yetu. Tanzania ni salama na ina vivutisho vingi vya asili na kitamaduni vinavyovutia wageni.
Miundombinu imara ya utalii, Amani na huduma bora, zinaifanya Tanzania kuwa mahali pazuri kwa ajili ya mapumziko na burudani.
Serikali inaendelea kufanya kazi kuhakikisha usalama na faraja ya wageni wote. Karibuni Tanzania!
Videoni ni baadhi ya watalii waliongia Tanzania mwezi Desemba, 2025
TANZANIA NI SALAMA KWA WATALII
Serikali ya Tanzania inawakaribisha watalii kutoka kote duniani kuendelea kutembelea nchi yetu. Tanzania ni salama na ina vivutisho vingi vya asili na kitamaduni vinavyovutia wageni.
Miundombinu imara ya utalii, Amani na huduma bora, zinaifanya Tanzania kuwa mahali pazuri kwa ajili ya mapumziko na burudani.
Serikali inaendelea kufanya kazi kuhakikisha usalama na faraja ya wageni wote. Karibuni Tanzania!
Videoni ni baadhi ya watalii waliongia Tanzania mwezi Desemba, 2025
TANZANIA NI SALAMA KWA WATALII
Serikali ya Tanzania inawakaribisha watalii kutoka kote duniani kuendelea kutembelea nchi yetu. Tanzania ni salama na ina vivutisho vingi vya asili na kitamaduni vinavyovutia wageni.
Miundombinu imara ya utalii, Amani na huduma bora, zinaifanya Tanzania kuwa mahali pazuri kwa ajili ya mapumziko na burudani.
Serikali inaendelea kufanya kazi kuhakikisha usalama na faraja ya wageni wote. Karibuni Tanzania!
Videoni ni baadhi ya watalii waliongia Tanzania mwezi Desemba, 2025
TANZANIA NI SALAMA KWA WATALII
Serikali ya Tanzania inawakaribisha watalii kutoka kote duniani kuendelea kutembelea nchi yetu. Tanzania ni salama na ina vivutisho vingi vya asili na kitamaduni vinavyovutia wageni.
Miundombinu imara ya utalii, Amani na huduma bora, zinaifanya Tanzania kuwa mahali pazuri kwa ajili ya mapumziko na burudani.
Serikali inaendelea kufanya kazi kuhakikisha usalama na faraja ya wageni wote. Karibuni Tanzania!
Videoni ni baadhi ya watalii waliongia Tanzania mwezi Desemba, 2025