Klabu ya Azam FC imetangaza kumsaini kiungo Faisal Salum โFeitotoโ nyongeza ya mkataba mpya wa mwaka mmoja.
Mkataba wa awali wa nyota huyo wa zamani wa Yanga ulikuwa ukamilike Juni, 2026 lakini sasa kiungo huyo aliyekuwa akihusishwa kwenda Simba SC ameongeza mwaka mmoja zaidi.
Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amesema awamu ya kwanza yanajengwa mabanda tisa huku Mhandisi Joseph Jonathan ambaye ni msimamizi wa ujenzi wa mabanda hayo anasema wanatarajia kukabidhi mradi huo kabla ya Septemba 10 mwaka huu kama ilivyopangwa.
Serikali mkoani Geita imeanza ujenzi wa mabanda ya kudumu katika viwanja vya maonesho ya Dkt. Samia Suluhu Hassan zamani EPZA vilivyopo kata ya Bombambili, halmashauri ya manispaa ya Geita lengo likiwa ni kuongeza thamani ya maonesho ya madini yanayofanyika kila mwaka.
Akizungumza mbele ya wananchi wakati wa makabidhiano Mhe. Muragila amesema mwenge wa uhuru ukiwa katika wilaya ya Bukombe utakimbizwa kilomita 148 ambapo utakagua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi kwenye jumla ya miradi 10 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 8.
Mkuu wa wilaya ya Bukombe Mhe. Pasikas Muragila ameupokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Mbogwe Mhe. Sakina Mohamed ambapo makabidhiano yamefanyika leo Septemba 05, 2025 katika viwanja vya shule ya msingi Bukombe.
DC Mbogwe Mhe. Sakina Mohamed ameupokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa DC Nyang'hwale Grace Kingalame leo Septemba 4 katika viwanja vya shule ya msingi Butimba.
Mwenge wa Uhuru ukiwa wilaya ya Mbogwe utakagua, utazindua na kuweka mawe ya msingi miradi 9 yenye thamani ya Tsh Bil 4.4.
Bei kwa mkoa wa Geita ni kama ifuatavyo:
-Geita DC Petroli ni 3,007 na Dizeli ni 2955.
-Bukombe DC Petroli ni 2996 na Dizeli ni 2944.
-Chato DC Petroli ni 3028 na Dizeli ni 2976.
-Mbogwe DC Petroli ni 3,045 na Dizeli ni 2993.
-Nyang'hwale DC Petroli ni 3,022 na Dizeli ni 2970.
DC Nyang'hwale Grace Kigalame ameupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa DC Geita Hashim Komba.
Makabidhiano yamefanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi Wavu na ukiwa wilaya ya Nyang'hwale utakimbizwa kwa KM 58 na kutembelea miradi 11 yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.5.
Mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na siku moja amekutwa amechomwa moto na kutelekezwa kando ya barabara mtaa wa Mwatulole Manispaa ya Geita.
Tukio limetokea Septemba mosi ambapo baadhi ya wakazi wa eneo hilo wameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa haraka kumbaini mhusika.