Day 3: SALA YA KUIOMBEA TANZANIA: Ee Mungu Mwenyezi wa milele, Baba wa mataifa yote na wa watu wote, utuangalie kwa macho ya huruma sisi watu wako wa Tanzania, ambao nasi sasa twahesabika kati ya mataifa ya dunia. Kwa baraka
yako uhuru wetu huu usipokonywe, na utuwezeshe kuishi maisha mema zaidi kadiri iwastahilivyo waana wa Mungu.
Tunakuomba nchi yetu iwe ya amani, waliopotea wapatikane na waliotekwa wapate uhuru wao, walioumizwa wapone, na waliouawa wapate uzima wa milele na uovu ukome katika nchi yetu. Tunakuomba ubadilishe nyoyo za watenda maovu na washirika wao katika uovu ili zikuelekee wewe, kwani sisi
tulio wanyonge hatuna uwezo wa kuzibadilisha nyoyo ovu.
Uendelee kututawala na kutuongoza. Daima nchi hii iongozwe na viongozi ambao ni chaguo lako. Waangazie watawala hao, sheria wanazotunga kwa kutufaidia kwa mambo mema ya hapa duniani zipatane na Wewe uliyetuumba kwa ajili yako. Wajalie watu wetu wote paji lako la Imani. Tukiwa Mahujaji wa Matumaini, tuthibitishe tusishindwe kupambana na maovu yawezayo kutufikia
kutoka nje au ndani, tupe hekima ya kutafuta ukweli katika mambo yote, na kuishi kwa uaminifu katika amri zako. Ee
Mwenyezi Mungu, uongozi wa kweli unatoka kwako, tunakuomba ujalie wale watakaosimamia na kuiishi Demokrasia ya kweli, Haki na Amani katika nchi yetu ili haki ituletee Amani ya kudumu. Washa nyoyo zetu na mapendo yako ya kimungu yatakayotuwezesha kushinda utengano, ushindani, na chuki ya ukabila au utaifa, na tuunganishe wote katika muungano wa kidugu utakaotuwezesha, kwa msaada wa neema yako, kutufanya tuwe umoja katika Wewe Baba wa wote. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.
Bikira Maria Mtakatifu Mkingiwa dhambi ya asili. Utuombee.
Atukuzwe Baba.... Amina.
#UPDATES_SHAURI_LA_UHAINI
Part 1
Mahakama imeamuru kuwa committal itasomwa yote bila kurushwa live.
Wakili wa Serikali Katuga anaendelea kusoma kwa sasa.
Maajabu yaliyotokea ni kwamba mawakili wa serikali waliomba maelezo ya mashahidi wa siri yasirushwe live.
Lakini cha ajbu mahakama imesema maelezo ya mashahidi wote yafichwe na yasiwe live.
Kifupi mahakama imetoa uamuzi ambao hata serikali haijaomba. Imefunga kila kitu na kesi kuzimwa.
Katuga anaendelea, amemkumbusha Mtuhumiwa Shitaka lake na kumkabidhi taarifa ya mashitaka.
Anasema Jamhuri itakuwa na mashaidi 30 na vielelezo vya myaraka 9.
Maelezo yataanza kusomwa na Thawabu Isa wakili wa serikali.
Anasimama na kuanza kusema SSP Kangio, atakuwa shahidi wa kwanza. Ameapa kusema ukweli na maelezo yake ni kama ifuayavyo.
Nimeajiriwa 2003 polisi na mikoa mbalimbali ninefanya. Nimekuwa na vyeo tofauti na sasa ni mrakibu wa polisi kanda ya Dar es salaam. Nafanya majukumu ya kusimamia askari katika majukumu ya kiupelelezi.
04/04/2025 nikiwa ofisi afande Kaaya anayefanya Doria mtandaoni nilimtaka anipe picha mjongeo kuhusu maudhui yakiyokuwa yanatoa taarifa yenye uchochexi.
Maudhui hayo ni mapolisi wanakuja na mabegi ya kura feki kwenye vituo. Jambo ambalo ni uongo. Majukumu yetu ni ulinzi na sio kuiba kura.
Pia maelezo yaliyokuwepo ni kuhusu majaji ni MACCM hivyo wanafanya kazi kwa mujibu wa CCM. Na sio kweli kwamba majaji wanafanya kazi kuwaonea wapinzani. Na hivyo taarifa hii ni uongo na yalilenga kuleta chuki.
Pia alisema kuenguliwa kwa wapinzani ni mkakati wa serikali hivyo zilikuwa ni uongo na kutengeneza chuki dhidi ya Rais.
Na msimamo wetu ni wa uasi. Ni kweli ni msimamo wa uasi kwani tunaenda kukinukisha na huu uchaguzi tunaenda kuuvuruga kwelikweli.
Katika picha mjongeo hiyo mzungumzaji alikuwa ni LISSU. Na aliyokuwa anafanya yalikuwa na nia ya kuitishia serikali ili ayapate yeye na wafuasi wake.
Niliamuru Insp. Kaaya aanze kufanya uchunguzi wa jalada hilo na taarifa hiyo ndio akafungua kesi na kuanza uchunguzi. Na akaanza kujaza PF500
Baada ya kutoa maelekezo kutafuta mjengeo iliyoerekodiwa eneo husika nilitoa taarifa kwa mabosss wangu na kuhusu kile alichosema TUNDU LISSU mtandaoni. Niliripoti kwa afande DCI akasema tuendeleee
Nilimtafuta kiongozi wa JAMBO TV anipe video ile na baadae akasema video anayo P ambae kasafrir. Hivyo nikatoa taarifa kwa maboss kuwa video tutaipata kwa P ambayo yuko Dodoma.
DCP NG'ANZI nilimpa taarifa kuwa tutaipata kwa kijana wa Jambo TV ambae yuko Dodoma.
Haya ni maelezo ya George ambae ni kaimu mkuu wa upepelezi kanda ya Dar es salaam. Yansomwa maelezo yake hapa mahakamani.
Nikaeleza lifunguliwe kosa la uhaini kwasababu aliesema TUNDU lisuu hayo maneno yake, yeye ni Askari ambae ana cheti cha Kujenga taifa kutoka jeshi la JKT hivyo alikuwa na wajibu wa kulinda amani ndani ya Taifa letu. Kusema maneno kama hayo ni kosa kisheria.
Hayo ndio maelezo yangu yote. Yameisha maelezo ya George na anasemaa anayo maelezo ya nyongeza Ya huyo SSP George akasema pia nilikabidhiwa TUNDU LISSU akitokea RUVUMA.
Nilimpokea Lissu na wakati nafanya mahojiano walikuja mawakili wake pia Tulienda kwenye ofisi yenye utulivu na nikamuonya kuwa anatuhumiwa kosa la uhaini. Na kumpa haki zake za msingi.
Huyu George ni msaidizi wa Mafwele. Anasemaa Lissu aligoma kutoa maelezo yoyote.
ASP. John. Ni shaidi wa pili ambae ni mkazi wa Temeke. Amekula kiapo na ushaidi wake ukaanza kuandikwa.
Nimeajiriwa 2005 na nina elimu ya computer na mfanyakazi wa polisi. Nimesoma vyuo ikiwemo Chuo Cha Polisi kurasini.
Nafanya kazi kwa DPP dawati la Doria mtandaoni. Na huwa napeleleza makosa yanayofanywa mitandaoni.
Huyu sasa ni shaidi wa pili baada ya yule wa kwanza ambae ni George.
Part 2 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
Kesho, Jumatatu 18.08.2025 Jaji Hamidu Mwanga atatoa maamuzi kuhusu uhalali wa kusitisha shughuli za kisiasa za CHADEMA. Kesi hii itakuwa Mahakama Kuu ya Tanzania โ Masjala ndogo ya Dar es Salaam
Kesho, Jumatatu 18.08.2025 kesi ya uhaini aliyopewa Tundu Lissu itaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam - Kisutu na sasa kesi hiyo ya uhaini imefikia hatua ya kusoma committal
Tundu Lissu atafanya submission ya taarifa yake ambayo itakuwa na kurasa 130. Hii ni submission kubwa mara tatu (3) ya submission ya Nelson Mandela katika Rivonia Trial โ I Am Prepared To Die.
I Am Prepared To Die โ hii ilikuwa hotuba ya dakika 180 za kujitetea ambayo Nelson Mandela aliitoa akiwa kizimbani, Mahakama Kuu ya South Africa, Pretoria katika kesi maarufu ya RIVONIA (Rivonia Trial)
Ni katika kesi hiyo ya uhaini โ upande wa Jamhuri kupitia Mawakili wa Serikali wameomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu matangazo mubashara (LIVE) ya mwenendo wa shauri la uhaini, YASITISHWE.
Kwamba, katika 'committal bundle' kuna taarifa za mashahidi wa upande wa Jamhuri ambazo zinatakiwa kufichwa zikiwepo โ taarifa za majina yao, taarifa za makazi yao, taarifa za shughuli zao na nyinginezo.
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam โ Kisutu, Franco Kiswaga alisema atatoa amri (order) siku ya 18.08.2025 kuhusu ombi la pingamizi la kurusha mwenendo wa shauri hilo.
Maagizo ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu ulinzi wa mashahidi hayawahusu mashahidi wote wa Jamhuri bali ni mashahidi wale ambao ni raia wa kawaida โ Jamhuri inataka taarifa zao zote ZIFICHWE..
Kesho waumini wote wa haki tunayo kazi kubwa ya kuhudhuria katika kesi hizo mbili zinazohusu CHADEMA โ kesi moja dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu na kesi nyingine dhidi ya CHADEMA.
Wakati Nelson Rolihlahla Mandela anatoa utetezi wake โI AM PREPARED TO DIEโ 20 April 1964 alikuwa ni mwanasheria aliyesoma University of Fort Hare (Eastern Cape) na University of Witwatersrand.
Wakati Fidel Alejandro Castro Ruz anatoa utetezi wake wa HISTORY WILL ABSOLVE ME 16 October 1953 alikuwa ni mwanasheria aliyesoma katika Chuo Kikuu cha Havana, Cuba (Universidad de la Habana).
Tundu Lissu mwanasheria aliyesoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (University of Dar es Salaam) kesho 18.08.2025, Kisutu, anakwenda kutoa submission yake ambayo tunakwenda kuita โDEATH ROW DIARIESโ
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila