#TajiriLaKihaya
Wewe Kijana ulieajiriwa;
Achana na kufanya fadhila kwa kampuni yako, fanya kile unacholipwa na uende nyumbani.
Unapofanya kazi kwa kampuni kwa masaa 8, usiende nyumbani uangalie TV au Kucheza Game au kushinda mtandaoni…
fikiria kuanzisha biashara ili familia yako iweze kurithi,
Hawawezi Rithi kazi yako.
Kujifunza hakuishi…
Usafirishaji wa Parcel bongo unahitaji upate jamaa mmoja mwenye mtaji mzito aliye serious awekeze mikoa karibu yote!!
kuna mabilioni kwenye hiyo biashara
Nimetafakari nimekuja kugundua kwamba vita kubwa kuliko zote katika maisha ya mwanadamu ni ya kiuchumi.
Hii vita kila mmoja anapambana nayo.
Si serikali, si ndugu, si majirani, si marafiki, si majamaa, si wanafamilia hata wasiokufahamu wote hawa hawataki ukue kiuchumi.
#TajiriLaKihaya
Asanteni sana ndugu, jamaa, marafiki na wote waliotufikia kwa simu, ujumbe, dua na maneno ya faraja kufuatia msiba wa mdogo wangu. Mchango wenu wa kiroho na kihisia umetupa nguvu katika kipindi hiki kigumu. Mwenyezi Mungu awalipe kheri na awabariki kwa wema wenu.
Kwa wale ambao hawakupata taarifa mapema, napenda kuwajulisha kwamba mdogo wangu alifariki jana, na kwa kufuata maelekezo ya dini ya Kiislamu alizikwa jana mchana.
Mwenyezi Mungu amesema katika Qur’an:
“Kila nafsi itaonja mauti.”
(Surat Aal-Imran 3:185)
Na pia amesema:
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika kwake Yeye tutarejea.”
(Surat Al-Baqarah 2:156)
Mtume ﷺ pia ametuusia kuwahisha mazishi, akisema:
“Fanyeni haraka katika mazishi; kwani akiwa mwema mnamsogeza kwenye kheri, na akiwa si hivyo basi ni shari mnayoiondoa mabegani mwenu.”
Sahih al-Bukhari na Sahih Muslim.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu amsamehe marehemu, ampanulie kaburi lake, amjaalie Pepo ya Firdaus, na atujalie sisi sote subira na uimara katika kipindi hiki cha majonzi.
Asanteni sana kwa dua, faraja na upendo mlioonyesha kwetu. Mwenyezi Mungu awajaalie malipo mema. Aamiin. 🤲🏽🕊️
Nina miaka takribani sita kwenye Ndoa sasa Baba yangu alibariki Uamuzi wangu nikiwa na miaka 22 tu, lakini katika miaka sita (6) hii ya ndoa nimegundua mambo kadhaa.
1- Ndoa yangu huyumba sana kipindi ambacho Mimi huwa nayumba yaani siketi katika mstari sahihi.
2- Ndoa yangu hustawi sana kipindi ambacho Mimi huwa nasimama imara kwenye mstari sahihi.
3- Mimi kama Baba wa Familia napaswa kuwa na mambo mengi lakini hayapaswi kuathiri familia yangu.
4- Naishi kwa kuamini Mimi sio Mkamilifu nina makosa na nakosea, ni sahihi kumwomba radhi Mke wangu napomkosea kwakuwa ni Ubinadamu, ni sahihi kuwaomba radhi Watoto wangu napowakosea kwakuwa ni Uungwana.
5- Hakuna Mwanamke Mkamilifu ila kila mmoja anapambana kufit kwenye Ndoa yake, tumetoka mazingira tofauti na Malezi tofauti hivyo kuelekezana na kustiriana huku tukisonga.
6- Talaka ni hatua ya mwisho sana ambayo sio baraka kwenye dini, sio sifa kwa Mtaliki wala Mtalikiwa na sio hatua njema kwa Wazazi wa pande zote mbili, hakuna kisichorekebishika kikitangulizwa na IBADA.
7- Kwenye sababu za KUOA haipaswi kuwa Makalio, Urembo ama sifa, hatuoi ili kuficha madhaifu bali tunaoa kwasababu tupo tayari kuingia kwenye darasa la furaha na huzuni lakini tutafika salama.
8- Ndoa ikileta baraka ya Watoto mtagundua tunaoana kwasababu ya Familia, kwasababu ya Watoto na hatupaswi kuwarithisha shida zetu sote tuishi na tusonge kwa ajili yao.
9- Ingali nimeoa Kijana najitahidi kutoleta Ujana kwenye Ndoa, Usela wa Masela kuja Maskani kila Wakati HAPANA, mapema kurudi home na kuchelewa kutoa taarifa ni MISINGI.
10- Mwalimu wa ndoa? Hayupo na hatotokea kwasababu kila mmoja ana Mtihani wake wenye maswali tofauti, jitahidi kujibu mtihani wako kwa mazingira yako naamini hivyo.
MWISHO, hakuna Mwalimu wa Mapenzi wala Ndoa, ni kudra za Mwenyezi Mungu katika kila kitu ukiweza hata kuvuka mwaka kwenye Ndoa basi shukuru Mungu, hii ni Ibada ina vita yake.
Mwenyezi Mungu awajalie kheri Wana Ndoa wote🙏 Taasisi yetu ya Migogoro hii unalala Kitanda kimoja na Adui yako na anakupikia unakula😀
1. All needs: Rabbi inni lima anzalta ilayya min khairin faqir.
2. Difficulties: Lailaha illa anta subhanaka inni kuntu minazalimeen.
3. Any problem: Allahumma arhamni birahmatika ya arhamar rahimeen.
4. To fulfill wishes: HasbiyAllahu la ilaha illa huwa alayhi tawakkaltu wa huwa Rabbul 'Arshil 'Adhim.
5. Asking for highest rank in Jannah: Allahumma adkhilni Jannatal firdaws.