Kuna viwanja vya mpira, Salasala, ambavyo watoto na vijana walishiriki kuondoa visiki vya miti na kusafisha kwa ajili ya michezo. Hata hivyo, viwanja hivyo vimekuwa vipara, bila mmea.....hivyo inawezekana kabisa kuwasukuma vijana hawa kupanda nyasi na kuzitunza. #Mazingira
Tunawezaje kuvitunza viwanja vya michezo vya watoto visivyo na nyasi hata kidogo kwa kuzingatia gharama za nyasi, utunzaji wake na ufuatiliaji? #Mazingira
Utunzaji wa mazingira, si kupanda miti tu au kutunza vyanzo vya maji. Ni pamoja na kuyaweka nadhifu mazingira yetu, kwa kuwa na njia mbadala wa kugeuza taka kuwa bidhaa.
Kuna baadhi ya shule zinatumia chupa za plastiki kutengeza wigo wa vimbweta, kupanda maua n.k. #Mazingira
How can you be the parent that your child needs?
Getting to know who he/she is, can be a good place to start.
What can you do today to get to know your child a bit better?
#Malezi
Hello #Parenting family.
There are times as a parent when you realize that your job is not to be the parent you always imagined you'd be or the parent you always wished you had.
Utunzaji wa mazingira, si kupanda miti tu au kutunza vyanzo vya maji. Ni pamoja na kuyaweka nadhifu mazingira yetu, kwa kuwa na njia mbadala wa kugeuza taka kuwa bidhaa. Kuna baadhi ya shule zimetua chupa za plastiki kutengeza wigo wa vimbweta, kupanda maua n.k.
#Mazingira
Shule nyingi za msingi na sekondari zimekuwa na kampeni ya mazingira, ambazo zimewajengea uwezo wanafunzi si kwa darasani tu hata katika kutunza mazingira, uwajibikaji na kuwa na shughuli zenye kuwafanya kuwaza zaidi na kuja na suluhu ya changamoto zinazowazunguka.
#Mazingira
Miti ni mizuri kwa nafsi ~ TreeClicks.
Mh. Kassim Majaliwa alisema, "Suala la kupanda miti na kuitunza ni la muhimu kwa ustawi wa Mazingira ya Taifa letu hatua inayokwenda sambamba na uhimili wa mabadiliko ya tabia ya nchi." Aliyasema haya mwezi Juni, 2022 - Dodoma. #Mazingira
Uongozi na wafanyakazi wa TCE unawatakia heri na fanaka katika msimu huu wa sikukuu.
Furaha ikatawale kwako na kwa familia yako.
#TumpendeTumlindeTumthamini
Huduma ya Afya kwa Wote (UHC) Inawaondoa Watu katika Umasikini, Inaendeleza Ustawi wa Familia na Jamii, Inatoa Ulinzi dhidi ya Majanga ya Afya, na Inaisukuma Jamii kuelekea kwenye Utekelezaji wa Mpango wa Huduma za Afya kwa Wote
Soma https://t.co/GFpME6z1A1
#UHCDay2022#JFAfya
Haki za binadamu haziwezi kuwa kamili kama haki za wanawake na wasichana hazitaheshimiwa. Kila mmoja ana haki ya kufurahia maisha bila kujali jinsi yake. Heshimu utu wa mtu. #16DOA#MaleziChanya#HumanRightsDay2022
Watoto wafundishwe wajibu wao, kuheshimu watu wote kwa usawa bila kujali jinsi zao. Hivi ndivyo tunaweza kuwa na kizazi kinachojali utu wa mtu. Malezi chanya ndiyo njia bora zaidi ya kubadilisha fikra, ufahamu wa watu ili kukomesha vitendo vya ukatili. #16DOA#MaleziChanya
Tuliyopitia, tuliyoona tukiwa watoto yanatengeneza vile tunavyoamini tukiwa watu wazima. Kuna baadhi ya watoto waliona wazazi wakirushiana maneno yasiyo na staha, kupigana, na sasa katika utu uzima wao, wanafanya vivyo hivyo. Mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo! #16DOA#MaleziChanya
Ni vyema wazazi wakajenga mazoea ya kujibu maswali magumu na yenye kufikirisha kutoka kwa watoto wao. wana maswali mengi, je, mtoto wako akiuliza, "Kwa nini nimemuona jirani yetu akimpiga ngumi mke wake na hujawahi kwenda kumsaidia?"...Je, utajibu vipi? #16DOA#MaleziChanya
Wazazi wawazoeze watoto kufikiri wenyewe, kwa kuwauliza maswali ya kufikirisha kulingana na umri wao, hii itawasaidia kujitegemea kifikira, kuchanganua masuala mbalimbali hata pale atakapokuwa mtu mzima, suala moja wapo linaweza kuwa ukatili wa kijinsia. #16DOA#MaleziChanya https://t.co/JgM67ua39p