Ee Baba yetu Mungu Mkuu,
Umenilinda usiku huu.
Nakushukuru kwa moyo,
Ee Baba Mwana na Roho.
Nilinde tena siku hii,
Niache dhambi nikutii.
Naomba sana Baba wee,
Baraka zako nipokee.
Bikira safi, Ee Maria
Nisipotee nisimamie.
Mlinzi Mkuu Malaika wee,
Kwa Mungu wetu niombee,Amina.
Baba Yetu uliye mbinguni. Jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo Mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu. Kama nasi tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi. Lakini utuopoe maovuni, Amina🙏
"Twaeni mnywe nyote; Hiki ndicho kikombe cha Damu yangu, Damu ya Agano jipya na la milele, itakayomwagika kwaajili yenu na kwaajili ya wengi kwa maondoleo ya dhambi. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu!"
Baba Yetu uliye mbinguni. Jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo Mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu. Kama nasi tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi. Lakini utuopoe maovuni, Amina🙏
Tunaukimbilia, ulinzi wako mzazi Mtakatifu wa Mungu, usitunyime tukiomba katika shida zetu, utuokoe kila siku tuingiapo hatarini, Ee Bikira Mtukufu mwenye baraka, Amina.🙏
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, Kama mwanzo na sasa na siku zote na milele amina!
Padre anaposema “Inueni mioyo” nasi tukaitika “Tumeiinua kwa Bwana”, sio mwitikio wa kawaida. Ni tendo la kuingia uweponi mwa Mungu. Mioyo yetu inainuka kutoka hofu, dhambi na kelele za dunia na kuelekea kwa Mungu. Moyo ulioinuliwa kwa Mungu unashinda na zaidi ya kushinda!
Neema ya Mungu hushinda yote. Hakuna kinachopita neema. Neema ni nguvu na msaada wa Mungu tunaoupokea bila kuustahili. Mungu hatoi tu msamaha, bali pia hutupa uwezo wa kustahimili majaribu, kufanya mema, na kuvuka nyakati ngumu. Ukipata neema za Mungu maishani, umepata yote.✍️