#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 100
Mhe. Lissu: Sasa hayo maneno yalisemwa mbele ya watu wote hao watia nia na viongozi wengine.
Kaaya: Sijui kama walisikia wote
Mhe. Lissu: unafahamu kuna kosa linaitwa mispresion of treason yaani kupata taarifa za kigaidi na usizitoe polisi ni kosa la uhaini adhabu yake ni kifo?
Kaaya: Sijui kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa hao wote niliowataja wameshitakiwa kwa mispresion of treason? Au shida yenu ilikuwa ni Mwenyekiti tu awepo jela ili asimsumbue Mama. Nani aliyeshitakiwa mwingine sema?
Kaaya: Hakuna aliyeshitakiwa.
Mhe. Lissu: Nataka tuzungumzie maelezo yako uliyotoa Polisi. Waeleze majaji nani aliyeandika maelezo haya? Exhibit D1.
Kaaya: Ni mimi binafsi.
Mhe. Lissu: Nani alikuapisha au kukukanya kwamba ukisema uongo ni kosa?
Kaaya: Hakuna aliyenikanya.
Mhe. Lissu: Nani aliyethibitisha kwamba hayo maneno ni kweli.
Kaaya: Ni mimi mwenyewe.
Mhe. Lissu: Nani alikuwa shahidi yako? Aliyekushuhudia ukifanya hayo.
Kaaya: Hakuna.
Mhe. Lissu: ni kweli au sio kweli kifungu cha 11(4) cha CPA kinasema maelezo hayo ya shahidi yanatakiwa yaandikwe na Polisi mwingine?
Kaaya: Naomba unisomee kwanza kifungu. Anasomewa hapa.
Amemaliza kusoma anamuuliza unasemaje?
Kaaya: Hakuna kifungu kinachomkataza police officer kujikanya na kujiandikia.
Mhe. Lissu: Mimi niliambiwa Mahakama sio Mama yangu sasa na mimi nawauliza nyie Mapolisi hizi Sheria ni MAMA YENU? Nyie mnadhani sisi raia ndio tunapaswa kutii sheria bila shurti?
Kaaya: Sio Mama yetu ndio.
Mhe. Lissu: PGO No. 236 inasema any police officer is authorised to record statement from any person who he believe has knowledge on the matter. Kumbe mnapaswa kuandika maelezo ya mtu yeyote. Tuko pamoja hapo?
Kaaya: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: ukiendelea kusoma hapo inasema kwamba Jambo hilo limeelezwa kwenye sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai na inaeleza signature of the recording officer must be there, the recording officer will comment on the witness reliability, kama ni mkweli au vipi? Sasa unasemaje kuhusu yote haya.
Kaaya: hapo haijazungumza
Mhe. Lissu: Utajijazia nini kwenye sehemu ya comment ya kusema police atoe comment kuhusu alichosema shahidi ni uongo au sio uongo.
Kaaya: Mimi sidhani kama polisi anaweza kusema uongo.
Mhe. Lissu: Nyie mapolisi wa Tanzania ndio msiseme uongo?π
Mhe. Lissu: wewe ni aina ya afisa wa polisi wa aina gani usiyefahamu mambo yote niliyokuuliza kuhusu yapo kwenye PGO? Ndio maanaa hupandi vyeo we Polisi kwa miaka 15?
Jaji: Mshitakiwa taratibu tusifike huko.
Mhe. Lissu: Naendelea sasa nataka tusome kwenye introduction ya PGO pale mwanzo kabisa. PGO inasema mnatakiwa kuwa na weledi katika kazi ili kufanya majukumu yenu.
Sasa wewe kila saa unasema SIJUI, SIFAHAMU,SIO KWELI utapanda vyeo kama majibu yako ndio haya hujui hujui kila saaa?
Kaaya: Sio kweli.
Mhe. Lissu: katika maelezo yako ulisema miongoni mwa matamshi hayo mi pamoja na HAO AMBAO HUWEZI KUWAJUA POLISI WANAKUJA NA VIBEGI VYA KURA FEKI. Je hayo maneno anakuwa amefanya kosa la Uhaini?
Kaaya: Inategemea
Mhe. Lissu: Inategemea nini?
Kaaya : grhdwht
Mhe. Lissu: huna jibu haya tuendeleee.
Mhe. Lissu: Matamshi mengine ulisema ameandika kuwa Majaji nao ni watu wa Rais wanataka kuteuliwa vyeo kwahiyo mahakamani hakuendeki. Je mtu akisema maneno hayo ni uhaini.
Kaaya: Inategemea
Mhe. Lissu: Inategemea na Mapolisi mtakaobambikia watu kesi.?
Kaaya: kimya
Mhe. Lissu: Tuendelee Maneno mengine ulisema nimesema mimi eti " Rais alisema hakikisheni wapinzani hawaendi kokote" je yana shida gani?
Kaaya: Sidhani maelezo hayo kama yapo kwenye shitaka. Maelezo yangu hakuna niliposema hapa na hapa ni uhaini.
Mhe. Lissu: Ni sawa wewe hujasema kabisa mimi ni muhaini. Shahidi Na. 2 nakuelewa vizuri. Sasa tuendelee unasema pia nilisema NA MIMI NATAKA NICHAGULIWE KWENYE KACHEO FULANI. Je kusema hivyo ni kosa la uhaini?
Part 101 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Hiyo elfu 10, Elfu 20 wanayokupa huko kwenye kampeni ili ukajaze viwanja na uwachagueβ¦β¦..Utairudisha na chenchi juu!
Ni kama wanakuazima tu, na utawarudishia na faida!!
Utanunua umeme wa elfu 10, utapewa umeme wa elfu 7 utakatwa buku tatu!!
Hizo buku tatu unazokatwa katwa ndio hilo liten unalolichekelea sasahivi!!
SASA KAMA SIO UCHIZI NI NINI!!?
Na hawatakupa maisha bora kamwe.
Kwasababu wanajua ukiwa na maisha bora hutakubali kwenda kuchomwa na jua kupanda malori ili upewe elfu 10 kujaza viwanja.
Wanaendelea kukufanya uwe masikini ili waendelee kukutumia kwa maslahi yao na familia zao!!
Hivi tutumie lugha gani kuwaambia mtuelewe nyie raia π‘ π‘ π‘ π‘
Usikubali kutumia kumsindikiza mtu kwenye utajiri, Huku anakudanganya na kukutisha kuwa kudai haki zako ni kuvunja amani.
Wakati yeye na familia yake wanafaidika na kuishi maisha bora kupitia wewe!!
TUONDOKE 29th Oct.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 80
Job Mrema: ukawa unafanya nini?
Inspector Kaaya: nikawa naperuzi na niliingia YouTube. Nilivyoingia YouTube nilibaini machapisho mbalimbali ya video. Mojawapo ya Chapisho ni katika ukurasa uliosajiliwa kwa majina ya JAMBO TV na niliona picha iliyokuwa imeambatana na maneno TUNDU LISSU USO KWA USO NA WATIA NIA MAJIMBONI. NO REFORMS NO ELECTION NJIA PANDA.
Baada ya kuona picha mjongeo hiyo niliweza kuchezesha picha mjongeo hiyo ili niweze kuona maudhui yaliyochapishwa.
Lengo la kuchezesha lilikuwa ni nini?
Kaaya; Ili nione maudhui yaliyopo humo ni nini?
Sasa ili iweje ukishaona hayo maudhui?
Kaaya: Lengo ni kubaini kilichozungumzwa.
Kwanini uliingia sasa?
Kaaya: Nilishangaa kuona video ile ina watizamaji wengi elfu na 39 nikaona ngoja na mimi niingie kuona kuna nini na watizamaji 300 niliona wamecomment.
Sasa shahidi unaweza kueleza mahakama majukumu yako ni yapi?
Kaaya: Majukumu yangu ni kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii kubaini makosa yanayofanywa.
Sasa ieleze mahakama hiyo sjju ya tarehe 04/04 uliingia kule kufanya nini?
Anasimama Lissu kuwa hilo swali lilishajibiwa alishasema aliingia kuwa video ile ilikuwa imetizamwa na watu wengi na waliocomment nikashawishika ni maudhui gani yamechapishwa humo.
Baada ya kuingia ulibaini nini humo ndani shahidi?
Kaaya anajibu nilivyotizama niliweza kubaini baadhi ya matamshi yenye viashiria vya jinai.
Viashiria hivyo ni vipi?
Shahidi anasema viashiria ni aliposema kuwa kwa kuwa hatuna access na hizo server za tume na Mapolisi ndo hao mnawaona na vibegi vya kura feki.
Mhe. Lissu anasema haya mambo ya vibegi feki yalishakataliwa na Mahakama siku ya juzi hauwezi kuletwa leo tena unahusiana na kesi iliyopo kisutu.
Naona Majaji wanajadili kidogo.
Job Mrema anajibu kwamba kwa upande wa Jamhuri tunapinga hilo pingamizi kwasababu kesi ya Mukisa Biscuits imeeleza pingamizi lazima liwe na sheria iliyotajwa.
Kuibuka ubishani wa kisheria hapa kati ya Mawakili wa Serikali na Mhe. Lissu
Sasa anasimama Mh. Lissu kuwajibu mawakili wa Serikali kuhusu hilo pingamizi dogo la namna ya kutoa ushahidi.
Waheshimiwa majaji nimesikiliza majibu marefu ya hawa wenzangu: nilidhani wasingebisha.
Cha ajabu wamemuachia anijibu huyu Job Mrema wakati yeye hakuwepo sasa mkimkubalia huyu na mlikataa kwa yule PW1 ambae ni George.
With all due respect nafikiri Mrema alikuwa anaongea jambo ambalo halifahamu.
Unaleta kesi ya Mukisa ambayo yenyewe inahusu mapingamizi ya mamlaka ya Mahakama.
Sasa hiyo kesi unatutajia leo ya nini kwenye hatua hii ambayo tupo sasa?
Waheshimiwa Majaji naomba mlikubalie ombi langu.
Majaji wanajadiliana hapa
Kwenye chuma cha Mahakama kuna ukimya fulani hivi nakumbuka tukiwa watoto mkiwa darasani mnapiga kelele ghafla mnajikuta wote mpo kimyaaaaa, tulikuwa tunasema shetani kapita ndo kama huo sasa.π
Tunasubiri Majaji wamalize kujadiliana then watoe uamuzi kuhusu ombi la Mhe. Lissu.
Part 81 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 75
Mhe. Lissu : Je unafahamu siku chache kabla sijachaguliwa kuwa Rais wa TLS nilikamatwa Dodoma na kusafirishwa kuja Dar es salaam siku nne na nilipotoka nikaenda Arusha kuchaguliwa kuwa Rais wa TLS?
George: Sifahamu hilo
Mhe. Lissu : Unajua nilipotangaza ndege ya Bombadier ilipokamatwa na walinikamata walisema wanaenda kunipima mkojo ili wanisingizie madawa?
George:Hilo sifahamu.
Mhe. Lissu: Katika kipindi cha MAGUFULI nilikamatwa mara nane na kushitakiwa mara 6 hapo Kisutu?
George: Sifahamu ila nashangaa kwanini ni wewe tu?
Mhe. Lissu: hujui Mbowe alishtakiwa na nini? Hawa akina Heche hujui kesi walizowahi kuwa nazo?
George: Aah! Nimekumbuka, nafahamu basi.
Mhe. Lissu : Tar. 11/08/2024 unafahamu kuwa nilikamatwa jijini Mbeya nikiwa nimeenda Mbeya kusheherekea siku ya Vijana?
George: Nakumbuka mliletwa hadi Central na tukawapeleka majumbani.
Mhe. Lissu: acha kiherehere sijakuuliza hayo ya nyumbani wewe George.
Mhe. Lissu: Unafahamu nilikamatwa na kupelekwa Vwawa na kesho yake nililetwa kwenye kituo cha Polisi Central Dar?
George: Mimi niliona umekuja Central Dar es salaam.
Mhe. Lissu : Na unafahamu nilivyofika Central hamkunishitaki kwa lolote mliniambia nirudi nyumbani tu?
George: Hiyo sahihi.
Mhe. Lissu : Mwaka jana umesema nilikamatwa Magomeni?
George:Ndio nimesema hivyo.
Mhe. Lissu : Wewe ulikuwa Depeuty ZCO wakati nakamatwa hapo Magomeni?
George: Ndio nilikuwa na cheo hicho.
Mhe. Lissu : Nikisema mimi sikuwahi kukamatwa na Polisi magomeni?
George: Sijui ulikamatiwa magomeni.
Mhe. Lissu: Nikikwambia sijawahi kupelekwa Oysterbay toka nizaliwe utasema nasema uongo?
George: Ndio utakuwa unasema uongo.
Mhe. Lissu : Sasa mimi nakwambia nilikamatwa nyumbani Tegeta na kupelekwa Mbweni kituo cha polisi ukiwa chini ya kiapo unadhani unafaa kuwa Askari wa Jeshi la Polisi?
George: Ndio ninafaa hivyo hivyo.
Mhe. Lissu: Shahidi nikikwambia nimekwambia tar. 09/04/2025 nimekamatwa ili tu niwe Gerezani mpaka uchaguzi upite na ili huyu UTU NA KAZI asiwe na Mpinzani wa maana?
George: Sio kweli
Mhe. Lissu : Je baada ya mimi kukamatwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhani Kailima walitangaza Chadema hairuhusiwi kuweka mgombea?
George: Hilo sikumbuki.
Mhe. Lissu : Na ni kweli au si kweli ndani ya mwezi huo huo mmoja niliposhitakiwa kwa uhaini msajili wa Vyama vya siasa Francis Mutungi amesimamisha Ruzuku kwa Chama cha Chadema ni kweli au sio kweli?
George: Sikumbuki
Mhe. Lissu : Msajili wa Vyama vya siasa, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, IGP na DCI, DPP hawa wote ni wateule wa Rais?
George: Hawa wote ni kweli.
Mhe. Lissu : Ndani ya mwezi huo huo mmoja Jaji wa Mahakama hii akaamuru shughuli za siasa zote za Chadema zisimame?
George: Ni Kweli.
Mhe. Lissu : Na huyo Jaji alikuwa mjumbe wa tume Zanzibar na ni mteule wa Rais?
George: Ni kweli.
Mhe. Lissu : Sasa tuambie huyu Mwenyekiti wa Chadema amefunguliwa mashitaka ya uhaini na wateule wa Rais?
George: Sio kweli.
Mhe. Jaji: Waheshimiwa majaji nimemaliza na shahidi huyu.
Jaji anasema kwasababu ya muda nahairisha kesi hadi kesho saa tatu asubuhi ambapo tutaendelea na Re Examination halafu baada ya hapo
hakikisheni Jamhuri mnakuja na shahidi mwingine ili tutakapomaliza Re Examination tuendelee na usikilizwaji wa shauri hili.
So Wapendwa tukutane kesho saa tatu asubuhi.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 68
Anaendelea Mhe. Lissu na maswali kwa Shahidi wa Jamhuri
Mhe. Lissu : Je mtu akisema kukinukisha vibaya sana ni kosa la uhaini?
George: Ndio amefanya kosa la uhaini.
Mhe. Lissu : Sasa kifungu cha 39(2)d ya Penal Code inasema kuhusu kosa la uhaini anamsomea. Je hapo kwenye hicho kifungu wapi kuna KUKINUKISHA SANA SANA?
George: Hayo maneno hayajatajwa kwenye hicho kifungu.
Mhe. Lissu : ulisema nimeitisha serikali?
George: Ni sahihi nilisema hivyo.
Mhe. Lissu : Ulisema uchaguzi mkuu uko Kikatiba?
George: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu : Sasa waeleze katika kifungu cha 39(2)d kama neno uchaguzi limetajwa?
George: Halijatajwa.
Mhe. Lissu : Uchaguzi Mkuu je?
George: Halijatajwa.
Mhe. Lissu : Kuzuia uchaguzi mkuu halijatajwa?
George: Halijatajwa.
Mhe. Lissu : Wewe hivyo vyeti vyako umenunua sio bure.
Watu : ππππππ
Mhe. Lissu : Ulisema Tundu Lissu alitaka kulazimisha serikali kufanya anayoyataka yeye?
George: Ni sawa sawa nilisema.
Mhe. Lissu : Uliandika hivi maelezo yako maneno haya niliona yana nia ya kuitisha serikali.
Sasa nakusomea kifungu cha 55(2) cha Penal Code Pia nitakusomea Media Services Act p. Sec. 52 pia nitamsomea sheria ya TISS (Idara ya Usalama wa Taifa) kifungu cha 3 kinasema tishio kwa usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Lissu : Ni ushahidi wako kuwa mtu anayepinga sheria ni kosa la jinai?
Georg : Inategemea.
Mhe. Lissu : Sasa nianze na Penal Code S. 55(2) kuhusu nia ya Uchochezi inasema kitendo kauli au chapisho hakitakuwa cha uchochezi kama kitakuwa na lengo kuwa serikali imekosea haitakuwa ni uchochezi. Kama unaonyesha makosa au mapungufu katika serikali au katika sheria au utendaji wa haki mahakamani kwa lengo la kubadilisha mambo hayo na anayehamasisha wakazi wa jamhuri ya muungano kubadilisha kwa njia halali sio kosa la jinai.
George: Kwa njia ya halali sio kosa.
Mhe. Lissu: Sasa hujaonyesha sheria toka nianze.
Mhe. Lissu : Sheria ya habari inasema kuionesha serikali imekosea halitakuwa kosa la uchochezi sasa mimi kusema uchaguzi wa hovyo unasimamiwa na serikali ya hovyo ni kosa la jinai?
George : Ndio ni kosa la jinai.
Mhe. Lissu : Twende kwenye Sheria ya usalama wa taifa. Imetaja mengi ikiwemo ujasusi, uhujumu uchumi na matishio ya kutumia serious violence je sheria hii ya usalama wa taifa ni kosa la jinai?
George: Kweli ni Kosa la Jinai.
Mhe. Lissu : Je kusema kutaka mabadiliko ni kosa la uhaini kwa mujibu wa sheria hii?
George: Ukifuata utaratibu sio kosa.
Mhe. Lissu : Huo utaratibu ukoje?
George: Kwenda kuyapeleka Mahakamani.
Mhe. Lissu : Je kuitisha maandamano ya amani ni utaratibu?
George: Ndio utaratibu.
Mhe. Lissu : Ni wapi sisi tulisema hatufuati utaratibu?
George: Sasa kuzuia uchaguzi ni kosa.
Mhe. Lissu : Nani alisema hatafuata sheria?
George: Ni wewe mwenyewe.
Nyie huyu George kuna nati haiko sawa kuna vitu anaongea mpaka unaweza kudhan kakatwa kichwa.π eniwei tuendelee
Mhe. Lissu : Jana ulisema kwamba baada ya kuonyeshwa ile video clip uliunda team ya Wapelelezi?
George: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu : Nimesoma maelezo ya Amin Mahamba. Je ulisoma maelezo ya Amin Mahamba?
George: Mimi sikusoma maelezo ya Mahamba halafuβ¦..
Mhe. Lissu : Acha kiherehere ulisoma maelezo au hukusoma?
George:Sikusoma.
Mhe. Lissu : Mahamba anasema aliunda timu tatu za upelelezi?
George: Ni kweli aliunda.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze Majaji kuwa kama ulionesha Amin Mahamba aliunda timu ya wapelelezi?
George: Sikuandika maana nilishaandika maelezo tar. 08.
Mhe. Lissu : Sasa uliandika maelezo tarehe 10 ya nyongeza pia ulisema kuhusu mahamba kuunda timu ya upelelezi?
George: Sikuandika hilo hata tar. 10.
Mhe. Lissu : Ulisema uliripoti kwa Kamishna Ng'anzi kuhusu kuteua timu ya wapelelezi kama lipo kwenye maelezo yako?
George: Linawezekana kuwa sijaliandika kabisa.
Part 69 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 56
Wamemaliza amesimama Lissu kujibu hilo pingamizi.
Kwa vile ni sheria.
Shahidi amesema yeye hana shida maelezo ni yake na yapokelewe.
Mawakili wake hawataki kabisa yapokelewe wanasema kama lengo ni kufanya impeachment sasa kama hana lengo hilo wamejuaje mapema hivi kwamba yasipokelewe kabisa.π Ngoja tuone lakini.
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji nimewasikiliza mawakili wa serikali na jibu langu ni fupi, nakubaliana nao, nakubali kuwa nilikosea kuanzia hatua ya tatu ili nisipoteze muda niko tayari nianze upya kwa utaratibu ambao mahakama ya rufani imemuelekeza.
Anasema siwezi kufanya ilivyo sahihi kwasababu ya Estoppel. Kwasababu I'm estooped.
Kifungu cha 131 cha Evidence Act kinasema ukifanya jambo na upande mwingine ukachukua hatua, Mawakili wa serikali wamepinga wakati nyaraka bado haijapokelewa na mimi nimewakubalia.
Estopel haihusiki hapa hili jambo wao linawaathiri nini kama shahidi ni wakwao na maelezo ni ya kwao.
Hakuna wanachoathirika.
Majaji wanaandika hapa
Anaitwa Katuga kwa ajili ya rejoinder anasema kifungu cha 131 cha Evidence Act kinatuzuia kurudi nyuma anapokuwa amekosea.
Intentionally kinatuzuia, tunamalizia kuwa pingamizi letu liko kishseria na limeletwa kwa ajili ya kulinda integrity.
Lissu anasema hii ya integrity nayo kaitoa wapi? Katuga anasimama anasema basi naomba niitoe.
Watu wanacheka ππππ
Wanaandika majaji kwa muda sasa kama dakika 15 hivi
Wamemaliza na kuanza kujadili kidogo.
Majaji wanasema ni endapo una concede PO mahakama inapaswa kufanya nini?
Mahakama ya rufani imeshatoa maelekezo kwahiyo PO kama itakuwa sustained basi itakuwa sustained na kuidismiss kwasababu upande wa Pili na inareject hiyo nyaraka. Nyaraka haijapokelewa.
Maswali yanaendelea sasa.
Mhe : Elimu yako ulisema jana. Ulisoma kozi ya kwanza Moshi mieizi 6?
George : Ni kweli.
Mhe.Lissu : na baada ya hiyo course ukafuzu na kupata cheti? Jibu: Ni sahihi kabisa.
George : ukaajiliwa kama Polisi Constable?
George : ni sahihi kabisa.
Mhe.Lissu : Baada ya hapo ulienda kusomea Course ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi hapa Dar es Salaam.
George : Ni kweli.
Mhe.Lissu : hayo mafunzo ya mkaguzi msaidizi wa polisi yalichukua miezi mingapi?
George : Miezi 9.
Mhe. Lissu : na baada ya hiyo miezi 9 ulipata cheti?
George: Kweli nilipata cheti.
Mhe. Lissu : Ukapandishwa cheo pia?
George : Kweli nilipandishwa cheo kuwa Assistant Insp. of Police.
Mhe. Lissu : Sasa shahidi baada ya mafunzo hayo ulienda kusoma course ya tatu, Gazette officers course
George : ni sahihi kabisa, nilienda chuo cha Polisi Dar ni kweli.
Mhe. Lissu : na ulisoma kwa miezi 9.
George : kweli kabisa,
Anasema kweli kwa nguvu sana huyu shahidi.π
Mhe. Lissu : Baada ya hapo hujawahi kusoma tena na kupata cheti hadi leo? Kwa mujibu wa ushahidi wako?
George : nimesoma course nyingine ndogondogo.
Mhe. Lissu : Sijakuuliza ndogo ndogo.
George: Nimesoma refresher course kwa mwezi mmoja.
Mhe. Lissu Chuo gani?
George: Mwezi mmoja pale Kidatu. Nikapata cheti.
Mhe. Lissu : na Chuo gani kingine?
George: Mubarak Police Academy kule Egypt miezi miwil kipo Cairo.
Mhe. Lissu : Ukapata shahada gani?
George: Nikapata vyeti viwili pale.
Mhe Lissu: Sasa naomba uwaeleze majaji kama kuna mafunzo mengine uliyohudhuria yaliyokupa kitu kingine zaidi ya Cheti? Nataka kujua mafunzo mengine uliyowahi kupata.
George : nina advance diploma ya uhasibu nilimaliza 2001, Post Graduate Diploma in finance Chuo cha Sauti.
Part 57 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 58
Naona George kapewa PGO
Anaisoma hapa kuhusu duties of regional and division crime officers.
Inasema investigators watakuwa responsible kwa maboss wao.
Mhe Lissu : Ni kweli wewe kama kaimu ZCO ulikuwa unawajibika kwa Murilo kama Boss wako?
George: aaah! eeeh unajua
Mhe Lissu : ni kweli au si kweli kama acting ZCO ulikuwa unawajibika maelekezo kutoka kwa ZPC.
George: Ni sahihi nina channel mbili.
Mhe. Lissu : Kwa mujibu wa PGO hii ulikuwa unawajibika kumpa taarifa ZPC ni sahihi?
George: Ni sahihi na alikuwa anapata taarifa na kila hatua alikuwa anapata.
Mhe. Lissu : turudi kwenye maelezo yako ya shahidi yote kuna mahali kokote umemtaja ZPC
George: Kwa maelezo haya hakuna nilipomwandika.
Mhe. Lissu : Je kuna mahali ulisema ulikuwa unampa taarifa, kuna mahali umesema?
George : Kwenye maelezo hakuna hilo jambo, sijasema kwenye hayo maelezo.
Mhe. Lissu :Je kuna mahali ulisema Muliro amekupa maelekezo yoyote hapo?
George: Hakuna mahali nimesema hilo kwenye maelezo yangu.
Mhe. Lissu : wambie majaji Mafwele alirudi kazini lini?
George : kama sikosei kati ya tar. 01 au 02 mwezi wa 5 kwahiyo nisingeweza kumtaja. Unajua upelelezi uliendelea
Mhe. lissu anamdakia kwa juu Kaka unajibu maswali yangu acha rongorongo.
Mhe. Lissu : ni kwelI Dcp Ng'anzi alikuletea Boss mpya anayeitwa Amin Mahamba?
George: ni kweli alifanya hivyo.
Amin kama ile ya Idd Amin lissu anasema hivyo π
George : Tar. 08/04 ndio alimleta ACP Amin Mahamba.
Mhe Lissu : Ni sahihi nikisema kuanzia tar. 04 hadi 08 ni sahihi wewe ndio uliongoza hiyo timu? na alipokuja Amin akaanza.
George ni sahihi Mahamba ndio akawa kiongozi.
Mhe. Lissu : Je Amin alilichukua jalada likiwa la uhaini au la uchunguzi?
George ; lilishakuwa la uhaini tayari.
Mhe. Lissu : wewe ndie uliyefanya maamuzi ya kulifanya liwe jalada la uhaini na sio Mahamba Amin.
George : Ni mimi ndie niliyeamua.
Mhe. Lissu nimefurahi sana. Mimi napenda kukamata waongo. Ngoja tumsubiri Amin Mahamba.
Mhe. Lissu : wambie majaji kwamba aliyekwambia kwamba ufungue uhaini ni Kingai?
George: si kweli, nilivyoona element zimekamilika nikaelekeza mimi mwenyewe.
Mhe. Lissu : hizo siku nne ulizochunguza kama ulitoa taarifa ya ofisi ya DPP au hukutoa? Nina maelezo yako kumbuka.
George : Kwamba?
Mimi kama mimi sikutoa hiyo taarifa na sikumwambia ofisi ya DPP.
Mhe. Lissu : Miaka yako 22 ya Upolisi umewahi kufanya uchunguzi wa appendix C makosa ambayo yanashughulikiwa na watu wa ngazi yako.
George: hizo za appendix C.
Mhe. Lissu: usiwe na kimbelembele
Mhe. Lissu : sasa waeleze kama umewahi kufanya uchunguzi wa kesi ya aina hii.
George : publication ya false information ya Dr. Slaa.
Mhe. Lissu : Iliishia wapi?
George Hiyo sikumbuki iliishia wapi,Kesi nyingine ya Lembeli, alikuwa Mbunge
Mhe. Lissu: iliishia wapi?
George : kimya
Mhe. Lissu : waeleze majaji katika miaka yako 22 umewahi kufanya kesi ngapi mtu muhimu kisiasa ni mshitakiwa. Mfano Kama Tundu Lissu? Nataka kujua kama una uzoefu.
George : Kesi ya nne nae iliondolewa ya John Heche Tarime iliondolewa kule Tarime akimuita Rais wa Nchi ana akili ya Tope.
Swali: Je iliishia wapi?
George: Nayo baadae iliondolewa.
Mhe. Lissu : kwahiyo miaka 22 yako ya Upolisi hujachunguza kesi yoyote ya makosa ya aina hii hajapatikana na hatia?
George : ni kweli hakuna ambae aliwahi kukutwa na hatia.
Mhe. Lissu : Kuna yeyote ukiachana na hii ambayo mahakama ilifikia mwisho mahakama ikatoa hukumu?
George: zote hazikufika hatua ya judgement.
Part 59 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
Video ya Mwisho ya kaka Yake Polepole Alisema Jamaa yuko na Chip za kutosha Mwilini,hivyo anaweza kuwa Tracked sehemu alipo., Wenye Taarifa kaka mtu anasema nini kwani saiv ? maendeleo yakoje ? Maana hata kujua sehemu alipo tu ni mafanikio
Repost 300.