An independent initiative of Africa's civil society & the International Federation for Human Rights observing & Analyzing current affairs as the Sources Reveals
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) kwenye hafla iliyofanyika chuoni hapo Moscow nchini Urusi, tarehe 04 Juni, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi wa Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN University), Wanafunzi wa Chuo hicho, wageni mbalimbali baada ya kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa).
Ninalishukuru Baraza la Taaluma la Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi (RUDN University) kwa kunitunuku Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa). Nimepokea heshima hii kwa unyenyekevu mkubwa kwa niaba ya Watanzania wote ambao ndiyo msingi wa mafanikio tunayojivunia na yanayoitangaza nchi yetu.
Chuo hiki ni sehemu muhimu ya maendeleo tuliyonayo kwani maarifa, ujuzi, nidhamu na weledi ambao zaidi ya Watanzania 1,100 wamepata kwa kusoma hapa, vimechangia ustawi wa wananchi, kuijenga nchi yetu na kuimarisha uhusiano wetu. Mchango huu bado unahitajika, sawa na ilivyokuwa wakati kinaanzishwa.
Ahsanteni sana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Juni 3, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Urusi, Vladimir Putin.
Rais Samia yupo Nchini Urusi kwa ziara ya Kitaifa hadi Juni 5, 2026 kufuatia mwaliko wa Rais Putin ambapo wamekutana katika Ikulu ya Kremlin Jijini Moscow, Urusi.
#MillardAyoUPDATES
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Mheshimiwa Vladimir Putin, Ikulu ya Kremlin jijini Moscow, tarehe 3 Juni, 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Matukio tofauti ya Picha alipowasili Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Vnukovo jijini Moscow tayari kwa Ziara ya Kitaifa Nchini Urusi Leo Juni 02,2026.
MANYARA - WILAYA YA HANANG
01.06.2026
Katibu wa NEC Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa CCM Ndugu Kenani Laban Kihongosi ameanza Ziara mkoa wa Manyara kwa kutembelea Mabalozi na kufanya vikao vya shina,Kukagua miradi ya Maendeleo na Kufanya mkutano wa hadhara kusikiliza na kutatua kero
Mizani ya ndondi za kisiasa inazidi kumpa ushindi mzito ndugu Kenani Labani Kihongosi ambaye ni msemaji wa Chama Cha Mapinduzi kulingana na mbinu anazozitumia kutekeleza majukumu yake ya kikazi huku zikileta matokeo mazuri kwenye medani za siasa.
Sasa tunaingia KILIMANJARO 🔥