African agriculture without African farmers
Mass dispossession of smallholder farmers is not a side effect of the ‘African Green Revolution’. It is the whole point.
https://t.co/ApaoFwiCET
The rapid adoption of AI has led to 'unusually high levels' of unemployment among college graduates in Texas, the US state with the most data centre capacity under construction. https://t.co/KStIwpmthS
“Siioni Tanzania ikipata Katiba mpya kufikia 2029. Tukiingia kwenye uchaguzi mkuu ujao bila Katiba, Tume ya Uchaguzi na mfumo huru wa uchaguzi , tutapata madhara makubwa.
Pia taifa lina majeraha na hizi tume zinaundwa ili kutusahaulisha yaliyotokea October 29 2025”. ~Joseph Sinde Warioba katika Jukwaa la Demokrasia Tanzania
#TanzaniaDemocracyForum #Democracy #KatibaMpya
Yaani ukisikia hata viongozi wanaona ni idadi ndogo kwamba watu 518 ni idadi ndogo, ndiyo maana hata kuomboleza kitaifa hakupewi kipaumbele ~ Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Warioba.
VIDEO:
Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka, amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa katika mapambano ya kuleta mabadiliko nchini kwa muda mrefu, akilinganisha juhudi hizo na mapambano ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza leo katika Jukwaa la Demokrasia, Profesa Tibaijuka amesema mapambano ya Mwalimu Nyerere ya kudai uhuru wa Tanganyika yalidumu kwa takribani miaka 7, kuanzia mwaka 1954 hadi 1961, wakati CHADEMA imekuwa ikiendelea na mapambano yake kwa muda mrefu zaidi.
“Hawa wenzetu juhudi inaendelea, tuwape nguvu, lakini kazi ni ngumu kwa sababu kubadili 'establishment' ya ndani, mjue ni ngumu kuliko kuwabadilisha 'external establishment',” amesema Profesa Tibaijuka.
Aidha, Profesa Tibaijuka amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inaweza kufanyiwa mabadiliko ili kutoa nafasi zaidi kwa demokrasia, ikiwemo suala la usajili wa vyama vya siasa akitoa mfano kupitia vijana wanaojaribu kusajili chama cha siasa lakini wamekumbana na vikwazo, huku akieleza kuwa suala hilo sasa liko mahakamani.
“Sasa ngoja niwaambie nyie Wanasheria, wameshindwa hawa vijana, wanataka kuandikisha chama cha Siasa, wamewekewa mizingwi, sasa hivi wako Mahakamani wanapambana,” amesema.
Miongoni mwa mabadiliko aliyopendekeza Prof. Tibajuka kwenye katiba ya 1977 ni pamoja na mabadiliko ya uandikishaji wa Vyama vya siasa pamoja na suala la uraia pacha.
@HildaNewton21 Aliwahi kusema ni kuhusu mauwaji tofauti na kukubali madaraka ya damu? He needs to come out clean hizi sifa hastahili na hana heshima yoyote—heshima haikai na damu!
TUJIELIMISHE ILI KUJISAHIHISHA.
KESI YA LISSU: HAKUSHINDWA BALI MAHAKAMA ILIAMUA KUWA ANA KESI YA KUJIBU HIVYO UTETEZI UNAFUATA.
Pamoja na kuheshimu uamuzi wa Mahakama, mimi ninaendelea kuhimiza busara na hekima zitumike katika ngazi zote za maamuzi ili taifa letu liondokane na jambo hili la kusikitisha. Tuweze kuambizana ukweli, kusameheana na kuridhiana.
Sizungumzii hatia au kutokuwa na hatia kwa Lissu; hilo ni jukumu la Mahakama. Ninazungumzia mazingira ya kesi hii, historia yetu na umuhimu wa sheria kutumika kwa usawa. Tutambue:
1. Kesi ya Tundu Lissu ina tofauti kubwa na kesi nyingi za uhaini zilizowahi kutangulia hapa nchini. Katika kesi hizo za kihistoria kulidaiwa kuwepo njama, washirika, mipango ya pamoja ya kuipindua Serikali, na katika baadhi ya kesi washirika kutoka jeshini na madai ya kupanga kumuua Rais.
Katika kesi hii Lissu ameshtakiwa peke yake, na kiini cha shtaka kinahusu kauli zake za hadharani. Hii ni tofauti muhimu inayostahili kutafakariwa bila kuingilia kazi ya Mahakama.
2. Lissu anashitakiwa kwa uhaini chini ya kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, kutokana na kauli alizotoa katika mkutano wa CHADEMA tarehe 3 Aprili 2025. Kaulimbiu yake ilikuwa “No Reforms, No Election.” Upande wa mashtaka unadai kwamba kauli zake kuhusu “kukinukisha”, kuzuia au kuvuruga uchaguzi zilivuka mipaka ya siasa za kawaida.
Kauli hizo ni kali. Lakini katika historia ya siasa zetu tumewahi pia kusikia kauli kali zaidi. Mfano wimbo maarufu: “Wapinzani tuwashike, tuwachanechane, tuwatupe.”
Hata Bungeni wimbo huo uliwahi kulalamikiwa lakini ikachukuliwa ni utani wetu wa jadi. Pia mitandaoni leo tunasikia kauli za kutishia watu, kuwaua au kuwapoteza bila hatua zinazoonekana kuchukuliwa kwa kiwango sawa.
Ndiyo maana wapo wananchi wanaojiuliza: Je, sheria inatumika kwa usawa kwa kauli za wanasiasa wa pande zote? Bibi yangu aliwahi kunikanya kuwa :Ukitania uwe tayari kutaniwa".
3. Lissu alitoa matamko yake hadharani au katika mikutano ya kisiasa. Wananchi wengi waliyasikia na wanayajua. Kwa hiyo, pamoja na kuacha Mahakama ifanye kazi yake kwa uhuru, ni vigumu kuzuia mjadala wa wananchi kuhusu jambo ambalo liko hadharani na linagusa siasa, sheria na haki za kiraia.
Ili mradi staha izingatiwe na mjadala huo usibadilishwe kuwa hukumu ya hatia au kutokuwa na hatia kabla ya Mahakama kumaliza kazi yake.
4. Kama Mahakama ingelikuwa imeamua kuwa hakuna kesi ya kujibu, hatua ya utetezi isingefunguliwa. Sasa Lissu ameomba kuwaita baadhi ya viongozi wakuu, akiwemo Rais Samia na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, kutoa ushahidi.
Historia ya nchi nyingine inaonyesha kuwa jambo la Rais aliye madarakani kutoa ushahidi katika shauri la jinai lina utata lakini si geni kabisa.
Mwaka 1807, katika kesi ya uhaini ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Marekani Aaron Burr, Burr aliomba ushahidi kutoka kwa Rais Thomas Jefferson, bosi wake. Jaji Mkuu John Marshall ndiye alikuwa muamuzi na alikataa "dhana kwamba Rais ana kinga ya moja kwa moja dhidi ya mchakato wa Mahakama pale ushahidi wake unapohitajika katika kesi ya jinai".
Jefferson hakulazimishwa kusimama mwenyewe kizimbani, lakini alitoa ushahidi kwa nyaraka na kanuni muhimu ikawa: hadhi ya Urais haimaanishi kwamba ushahidi muhimu kwa mtuhumiwa hauwezi kupatikana.
Baadaye, Marais wengine wa Marekani wamelazimika kutoa ushahidi au taarifa katika mashauri ya jinai inapohitajika. Ni pamoja na:
James Monroe — 1818
Ulysses S. Grant — 1876
Gerald Ford — 1975
Jimmy Carter — 1978
Jimmy Carter tena — 1980
Bill Clinton — 1996
Richard Nixon mwaka 1974 aliamriwa kutoa kanda za Watergate.
Mara nyingi ushahidi huo ulitolewa kwa maandishi, nyaraka, viapo/deposition au video badala ya Rais kufika mwenyewe mahakamani.
5. Hakika Hatua inayofuata katika kesi ya Lissu ni nyeti. Itatuonyesha mwanga katika masuala haya muhimu kuhusu utawala wa sheria na haki ya mshitakiwa kupata utetezi stahiki.
6. Kiuhalisia Wengine tumejikita kwenye swala la HEKIMA, BUSARA na HURUMA YA MUNGU.
@HecheJohn Kabla TAL kupigwa risasi 16 alialamika kufuatiliwa kila alipoenda, wakasema haya haya kuwa apeleke ushahidi. History repeats itself - the script remains underdeveloped.
2027 imebaki miezi 6 tu.
2016 ilikuwa miaka 10 iliyopita.
COVID ilianza zaidi ya miaka 6 iliyopita.
Waliozaliwa 1990 wamebakiza miaka 14 tu kutimiza miaka 50.
Na leo, 2007 iko mbali zaidi kuliko 2040.
Muda unakimbia.
Acha kusubiri. Anza sasa.
Vitol yuko na nani?
Nani wamempa tenda ambayo Watanzania wanauziwa mafuta kwa usd 200-260 wakati Uganda anauziwa usd 83 na Msumbiji anauziwa usd 90.
Hawa Namaro waliosajiliwa Dubai mwaka 2023 ni kina nani? Wana uhusiano gani na wizi huu mkubwa unaoumiza Watanzania.
Vyombo vya habari Tanzania kwanini hamfuatilii na kuandika huu ujambazi unaongamiza Nchi kwenye wizi wa mafuta..
TPDC kwanini hawakutoa tenda shindanishi katika suala kubwa kama hili la mafuta.
BAJETI 2026/2027. Hapa jambo kubwa ni je mikopo yetu ni HIMILIVU? Hapana imezidi. Kwani kwa takwimu hizi
Mapato ya serikali ni Shs T36.99 kodi+T9.24 mengineyo =T36.23.
Madeni ni T7.84 yaliyoiva+T6.86 riba=T14.70.
Madeni kama asilimia ya mapato halisi ya serikali : T14.70/T36.23 = 40.57%.
Deni himilivu halitakiwi kuwa zaidi ya asilimia 18% ya mapato ya serikali. Kwa hiyo tumevuka mpaka (kima cha juu) hata kama WAKOPESHAJI watatwambia vinginevyo. Bila misaada zaidi TWAFA🏃🏻♂️🏃🏻♂️🏃🏻♂️Kodi zikizidi uwezo wa wananchi kulipa zinakwepwa au kufirisi walipaji. Inakuwa vicious circle.
Ukienda Dodoma ukamwuuliza mtu kama yupo Dodoma na akakujibu ametoka kidogo, lakini ukaenda mahali ukamwona amekaa akiendelea na shughuli zake, basi meza mate somo lieleweke kimya kimya na utulie kama mtu anayechemsha maziwa anategea lile povu. Kuwepo mahali haimaanishi mtu anapatikana ukimhitaji.
Kadhalika, ukiwa Dodoma ukaenda mahali ukamwona mtu mnayefahamiana na hamna miadi naye lakini ukataka umsalimie bila kuonekana umemvamia. Ikitokea umejitahidi sana nyuso zenu zikutane msalimiane ‘kwa bahati mbaya’ na ukaona macho hayakutani milele, huenda mtu huyo alitangulia kukuona lakini asingependa msalimiane. Utamsaidia sana ukiheshimu haki yake ya kuwa na faragha halafu endelea na shughuli zako kama vile hujamwona.
Mwanangu Magesa alikuwa na shida ya tumbo. Awali aliambiwa ana vidonda vya tumbo.
Kuna nyakati tumbo likimshika alikuwa hawezi hata kutembea.
Siku moja alizidiwa. Tukakimbia hosp.
Niliitwa pembeni Daktari akaniuliza: "Magesa ni nani yako?" Nikamjenga!
🧵🧵