Nasikitika kuona watu wengi wakiendelea kutapeliwa na wahalifu wa mitandaoni kupitia video fake za AI zinazotumia sura, sauti, na picha za watu bila ridhaa yao.
Tafadhali mjue kwamba sifanyi biashara yoyote ya mikopo kupitia Mo Dewji Foundation wala kupitia mitandao ya kijamii. Pia, sijihusishi na AI trading ya aina yoyote.
Taarifa yoyote rasmi kuhusu shughuli ninazofanya itatangazwa kupitia kurasa zangu rasmi pekee.
Naomba tuwe makini, tuhakiki taarifa kabla ya kuamini au kushiriki, na tusaidiane kuelimishana ili kulindana dhidi ya utapeli huu wa mtandaoni. Watu wengi wanaendelea kuumia. 🙏🏽
إذا قصرت يداك عن مكافأة صاحب معروفٍ، فليطل لسانك بالشكر والدعاء له
Kama mikono yako ni mifupi haiwezi kumlipa aliyekutendea wema, basi refusha ulimi wako kwa kumshukuru na kumwombea dua.
اعمل لدنياك كأنك تعيش أبدًا واعمل لآخرتك كأنك تموت غدًا
Fanya matendo kwa ajili ya dunia yako kama vile utaishi milele, na fanya matendo kwa ajili ya akhera yako kama vile utakufa kesho.