@MariaSTsehai Muungano kwa sasa sioni kama una tija, hata kama kutakuwa na serikali 3. Tulikofikia kila upande ubaki na serikali yake, Kisha tukutane EAC (Afrika Mashariki). Kero zote za zaidi miaka 60 zitaisha. Hivi inawezekanaje tembo kuungana na sungura, na wote kuwa na Haki sawa?
@godbless_lema Michango midogomidogo ndio ilimwezesha Mlm Nyerere na wenzake kufanya harakati za kudai uhuru wa Tanganyika, ikiwa ni pamoja na kuzunguka nchi nzima na hata kusafiri kwenda Umoja wa Mataifa. Kwa sasa fursa ni kubwa zaidi, Kila Mtu anaweza kuchangia!
@NamdiAzikiwe Ila Zanzibar wanataka uhuru zaidi, jambo linaloashiria kujitenga. Hii ni Haki Yao, wabaki na serikali Yao. Maana Muungano huu ni sawa na Tembo kuungana na Sungura; Kila mara Sungura anahisi kukandamizwa na Tembo; vivyo hivyo, Tembo naye hataki kutawaliwa na Sungura!
@joeselasini Kwa sasa, huu Muungano hauna tija Tena! Wala serikali 3 Si suluhisho! Kila upande ubaki na serikali yake, tubaki kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki! Vinginevyo tuwe na serikali Moja, yaani Zanzibar iwe Mkoa badala ya nchi, jambo ambalo Wanzanzibari hawawezi kukubali!!
@MariaSTsehai Ni Profesa ambaye, mbali na kufanya siasa hakuacha fani yake ya udaktari. Wizara ya Afya, aliendelea kutibu, Wizara ya Ulinzi aliendelea kutibu hospitali za jeshi, Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, alitibu! Alinyooka! RIP Prof!!
@MariaSTsehai Hapana!! Kama ni Muungano wa kweli, tuwe na serikali Moja, yaani Zanzibar iwe Mkoa. Vinginevyo, Zanzibar ibaki na serikali yake, na Tanganyika irudi; na wote kwa pamoja tuwe ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Suluhisho la UFISADI, UTEKAJI, UMASKINI NA UKANDAMIZAJI NI UGATUZI WA MADARAKA kikamilifu, mikoani, wilayani, na kuendelea!! Kwa sasa maamuzi na rasilimali khs maendeleo ya nchi zipo mikono mwa watu wachache!