Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema kuwa โTanzania imekuwa ni rejea muhimu ya amani na mshikamano wa kijamii barani Afrika na duniani kote,โ.
Kauli ya Guterres imetolewa leo tarehe 14 Desemba 2025 wakati akipokee Ujumbe Maalum kutoka Tanzania uliobeba salamu na ujumbe kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, uliowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Kombo, pamoja na ujumbe wake.
Ameeleza kuwa taswira ya Tanzania kama kielelezo cha amani ilijaribiwa katika uchaguzi wa hivi karibuni uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025, lakini taifa liliweza kuvuka mtihani huo kwa mafanikio, ikiwa ni mara ya kwanza kukabiliwa na changamoto hiyo.
โUmoja wa Mataifa ungependa kuona Tanzania inaendelea kubaki katika umoja wake na kuwa mfano bora kwa mataifa mengine,โ amesema Katibu Mkuu Guterres.
Aidha amesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mazungumzo ya kitaifa yenye maana, jumuishi na shirikishi ili kushughulikia chanzo cha matukio ya vurugu yaliyotokea tarehe 29 Oktoba, pamoja na kutafuta njia za kudumu za kuyazuia yasijirudie tena.
Ameahidi msaada kamili wa Umoja wa Mataifa wakati wote na hata baada ya Tume ya Uchunguzi iliyoanzishwa nchini Tanzania kukamilisha majukumu yake.
Khaaa sasa hii ndiyo hotuba ya RAIS yaaani!.. ๐ค๐ค๐ค
Muda wote tumejipanga yaani! Njooni mtakuta tumejipanga yaani!...
Mmesikia nyie wanaharakati!?
#BREAKING: BUNGE LA ULAYA LAPINGA UCHAGUZI WA TANZANIA OKTOBA 2025 KAMA USIO WA HURU WALA WA HAKI
Bunge la Ulaya limekosoa vikali uchaguzi mkuu wa Tanzania uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025, likisema haukuwa huru wala wa haki.
Katika tamko la pamoja, Wabunge wa Ulaya wamesema uchaguzi huo ulifanyika katika mazingira ya ukandamizaji, vitisho na hofu, hali iliyodhoofisha misingi ya kidemokrasia.
Wametaja kukamatwa kwa viongozi wa upinzani, kufungiwa kwa vyombo vya habari huru, na kuwekewa vikwazo waangalizi wa uchaguzi kama ushahidi wa kuvurugika kwa mchakato mzima.
Kesi ya uhaini dhidi ya Tundu Lissu, ambaye alidai uchaguzi wa haki, imetajwa kama ishara ya kuporomoka kwa uhuru wa mahakama na haki za kisiasa.
Bunge hilo limeitaka jamii ya kimataifa kuchukua msimamo thabiti kutetea demokrasia na haki za binadamu nchini Tanzania, likionya kuwa kimya siyo kutokuwa na upandeโni kushiriki kwa njia isiyo ya moja kwa moja.
โHakuna uchaguzi unaoweza kuwa wa kuaminika wakati upinzani mkuu unanyamazishwa, uhuru wa kukusanyika na kujieleza unazuiwa, na vyombo vya habari huru vinatishwa na kufungwa,โ taarifa hiyo ilisomeka.
Duru zinasema kwamba muda wowote kuanzia sasa Mstaafu ataenda kuungana na Vijana wake aliowatanguliza mbele kama watoto wa bata.
Mliokaribu nae mwambieni akithubutu kwenda kuungana na hao vijana wake Watanzania watakuwa wanamuona kama Profesa Lipumba.
Nafikiri bado ana heshima anayopaswa kuilinda kwa manufaa ya kizazi kijacho.