π ππππ ππππ ππππ ππ πππππππ πππ!!!
Simanjiro, Manyara | 03 Juni 2026
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Kenani Laban Kihongosi, leo anahitimisha ziara yake mkoani Manyara kwa kutembelea Wilaya ya Simanjiro.
Ziara hiyo imelenga kuimarisha chama, kusikiliza wananchi, kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na kupokea na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Wananchi na wanachama wote mnakaribishwa kushiriki katika shughuli za ziara hiyo.
Tembelea: https://t.co/XFsl2Qg9M9
________
#KazinaUtuTunasongaMbele
#CCMIpoKazini
#KaziInaendelea
#CCMImara
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN University) Moscow nchini Urusi.
#DiplomasiaYaUchumi#Dira2050#TabasamuLaUtu
#KaziNaUtuTunasongaMbele
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM chini ya Uongozi wa Mwenyekiti wake Ndg. Mohammed Ali KAWAIDA (MCC) unawatakia Watanzania wote Heri ya Miaka 6οΈβ£0οΈβ£ Ya Muungano.
Tumeshikamana na Tumeimarika kwa Maendeleo ya Taifa letu.
Leo nimeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa matanki 15 ya kupokea mafuta, Kigamboni mkoani Dar es Salaam. Mradi huu wa kimkakati ambao ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2025 utaimarisha usalama wa nchi yetu kwani, kwa mara ya kwanza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) itakuwa na matanki yake, hali itayotuhakikishia upatikanaji toshelevu wa mafuta kwa kipindi kirefu zaidi.
Aidha, utaimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha biashara na uwekezaji kwa kupunguza muda wa meli kushusha mafuta kutoka siku 22 hadi siku 7, muda wa meli kuhudumiwa gatini kutoka siku 7 hadi siku 1 na kupunguza gharama za uagizaji wa mafuta. Ufanisi huu utaifanya Bandari ya Dar es Salaam kuwa shindani na kuwa chaguo la wafanyabiashara wengi zaidi.
Katika kuhakikisha mradi unakuwa na tija, nimeelekeza Wizara ya Uchukuzi pamoja na TPA kuwa, kipaumbele cha ajira kiwe wananchi wanaozunguka mradi, pia zisimamie utekelezwe kwa wakati na kwa ubora unaozingatia viwango vya kimataifa na ulinzi wa mazingira.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha Tuzo ambayo Hifadhi ya Serengeti imeshinda kuwa Hifadhi bora Duniani (Worldβs Leading National Park, Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar tarehe 05 Januari, 2026.
Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) yenye Makao Makuu yake Jijini London, Uingereza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Andrew Lentz, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma, tarehe 08 Desemba, 2025.
#KaziNaUtuTunasongaMbele
"Niwaombe tena na tena Vijana na Watanzania wote, tusiendelee kujiumiza wenyewe kwa kushawishiwa na watu ambao hawapo Tanzania hatuna nchi nyingine, nchi yetu ni Tanzania lazima tuilinde na tuiheshimu,"
Ndugu Mohammed Ali Kawaida Mwenyekiti UVCCM na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Andrew Lentz, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma, tarehe 08 Desemba, 2025.
#KaziNaUtuTunasongaMbele
Mwenyekiti wa UVCCM, Ndugu Mohammed Ali Kawaida akisalimiana na Katibu mwenezi wa CCM, Ndugu Kenani Kihongosi walipowasili katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma kabla ya kuanza kwa Kikao Kazi na Viongozi wa UVCCM ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya na Seneti leo tarehe 07 Desemba 2025
KIKAO KAZI CHA MWENYEKITI
Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Mohamed Ali Kawaida alipowasili katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma kabla ya kuanza kwa Kikao Kazi na Viongozi wa UVCCM ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya na Seneti leo tarehe 07 Desemba 2025
#HatokiMtu#kazinaututunasongambele
Matukio mbalimbali ndani ya ukumbi Wa Jakaya Kikwete, ambapo Viongozi mbalimbali wa kitaifa, Mkoa, Wilaya na Vyuo wakiwa katika Kikao kazi na mwenyekiti Wa UVCCM, Ndugu Mohammed Ali Kawaida jijini Dodoma leo tarehe 07 Desemba 2025.
#HatokiMtu#Kazinaututunasongambele
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride rasmi la kumaliza Mafunzo la Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwenye sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli mkoani Arusha, tarehe 22 Novemba, 2025.