Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemwakilishaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliyofanyika kwa njia yaMtandao, leo tarehe 29 Juni 2026, Makamu wa Rais akiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo umeongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa.
Tamaduni tofauti, historia tofauti na mitazamo tofauti - lakini ndani ya Muungano tunakuwa taifa moja. Utofauti wetu ndio unaotajirisha utamaduni wetu na kuimarisha mshikamano wa Watanzania.
Kwa pamoja tunajenga taifa lenye umoja, amani na maendeleo.
#Muunganotanzania
Leo tumeandika historia nyingine kubwa kwa Taifa letu kwa kuzindua Makao Makuu ya kwanza ya Ulinzi wa Taifa mkoani Dodoma. Hatua hii imekamilisha maono ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ya mwaka 1964 wakati Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilipoundwa.
Majengo haya ambayo tumeyajenga kwa fedha na wataalamu wa ndani ni uthibitisho wa ukomavu wa Taifa letu katika kupanga, kuamua na kutekeleza kwa ufanisi miradi mikubwa. Kuziweka pamoja ofisi za JWTZ na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kutaongeza tija na ufanisi wa kazi, na ni kielelezo cha dhamira yetu ya kujenga taasisi imara za kulinda uhuru, mipaka, rasilimali na watu wetu.
Mafanikio ya mipango tuliyojiwekea yanategemea sana uwepo wa amani na utulivu. Hivyo, wito wangu kwetu sote ni kuendelea kuimarisha ulinzi, usalama, umoja na mshikamano wa nchi yetu.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. @zainabkatimba, Februari 24,2026 jijini Dar es Salaam amefungua Kongamano la Nchi za Afrika Mashariki kuhusu mchango wa teknolojia katika utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na upatikanaji wa haki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na Mabondia wa ngumi za kulipwa na ngumi za wazi. Rais Mhe. Dkt. Samia aliwaandalia hafla ya chakula cha mchana na kuwapongeza Wanamichezo waliofanya vizuri Kimataifa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Januari, 2026.
___
#TanzaniaYetuSote
#NchiYetuKwanza
#MaendeleoEndelevu
Vijana wa Tanzania wameonyesha busara ya hali ya juu. Walikataa kushawishiwa na lugha ya chuki na vurugu. Kama ilivyokuwa Dec 9, waliupuuza wito wa maandamano Dec 25, wakilinda amani na mustakabali wao kwa vitendo.#ActivistsHaveFailed
Vijana Wakataa Kutumika
Ninawatakia kheri ya Sikukuu ya Krismasi Wakristo na Watanzania wote. Mnaposafiri na kujumuika na ndugu, jamaa na marafiki katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, tusherehekee kwa furaha na upendo.
Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kutukumbushe upendo kwa Mwenyezi Mungu, upendo kwa kila mmoja wetu, wajibu wa kujitoa kuwasaidia wenye uhitaji, uvumilivu na unyenyekevu. Tuendelee kukumbuka wajibu wetu wa kutunza Taifa letu ili lidumu katika amani, utulivu, haki, ukweli na ustawi wa kila mmoja wetu sasa na vizazi vijavyo.
Mwenyezi Mungu awabariki nyote.