Kama serikali itampa masikio huyu binti ata dk 1.
Kuna viongozi mpaka muda huu hawapaswi kuwepo tena kazini.
Binti anaongea ukweli mtupu juu ya taifa.
Then
Na ukute hana ata acc ya X ila haya mashangingi ya humu.
Kazi yao ni kuniblock tu mimi pumbavu zenu.
Freeman Mbowe hajawahi kupata dakika moja amtembelee Tundu Lissu gerezani au mahakamani. Lakini ana muda wote wa kuzurura na Samia, na leo yuko Rufiji kupiga picha ktk bwawa la umeme. I’m proud of y’all for ending his politicalpreneur career!
Nyie watu wabaya na wakatili. Msijaribu kumuua Humprey Pole Pole , chukueni hili ONYO very serious. Najua mnapima upepo. Msijaribu, Msijaribu.
Tunalia kama taifa kuona mmoja wetu akitoweka bila maelezo. Humprey ana haki ya kuwa salama na kuishi bila mateso. Msijaribu.
Ukurasa Wa @mangekimambi ni Moja kati ya Ukurasa unao-ongoza kupost habari za Uhakika kwa 100%, Mange Hapost Umbea Ukiona Taarifa yoyote Kaipost Kuhusu Serikali jua kwa 100% ni kweli..
Ukurasa wake kwa Sasa unafati liwa na Kila Mtanzania, Taarifa zoote Watu wanazitoa Pale. 1/2
Jana nilikuwa nimewasiliana na rafiki yangu mwanaharakati wa nchi nyingine na aliniuliza mambo vipi nikamjibu mengi ila nikasema wanachosha hawa mafedhuli, akaniambia “ that’s how they win… just...persisting”
Na mi nikasema, “We need to be more resilient than they are”
✊🏽
Nawashukuru WOTE mnaonitumia ujumbe wa kunipa moyo na kuniombea! Nimegundua kuwa TUTASHINDA maana hata tukielekea kuchoka tunapeana moyo
Nawapenda sana nyote ❤️
Na #TutaelewanaTu
Impunity!
Vyombo vya dola vipo, wanaona watu wanabebwa kwenye malori, sheria zetu haziruhusu.
IGP yupo, mkuu wa usalama barabarani yupo.
Watu wanatumia kwasababu ccm wako juu ya sheria.
Aibu kubwa kwa ccm na vyombo vya dola, Nchi yetu inahitaji ukombozi wa haraka.
Watu wetu wanateseka kwasababu ya umasikini, umasikini wa kipato na uelewa kwa pamoja.
#NoReformsNoElection
Nimepata taarifa na siwezi kuzipuuza.
Kwamba hawa jamaa wanaandaa mbinu ikiwemo kushambulia viongozi wetu kwa mbinu za kijambazi.
Kwahiyo kuna genge litavamia watu kwenye makazi yao, au hata barabarani.
Alafu itasemekana ni majambazi..
Mambo haya ya kihuni hayakubaliki na hayatawezekana Tanzania.
@ReganTesla_ Au kama mmeuziana shamba basi mnalishika kwa pamoja na kuliotesha huku mkinena yeyote atakaeleta tamaa kwenye haya makubaliano basi limkute la kumkuta
@_belindaPINDA01 @izzysimon30@azamtvtz Hizo jamii kwa sasa hapa Tanzania wana nguvu kuliko wewe asili ya hii ardhi,hatari sana lakin kila jambo lina mwisho wake
Shikamoo Mama @SuluhuSamia ,
Wengi wanasema tusikuite mama, lakini mimi pia ni mama, na ninakuita hivyo kwa heshima. Baba yangu, ambaye alifariki mwezi uliopita (apumzike kwa amani), alinilea katika maadili ya nidhamu na heshima na kunishauri kukuheshimu katika maandishi. Maadili niliyoyaendeleza hata nikiwa mwanafunzi pale Jangwani nilipopata cheti cha heshima. Leo hii, ninapokuandikia, naendelea kubeba urithi huo.
Mama, mengi yametokea, na Watanzania wengi wanalia. Tumekuzwa katika misingi ya nidhamu na amani, lakini sasa tunaona taifa limegawanyika: wakristo/ waislam, Chadema/CCM (na vyama vingine etc ila isiwe kwa kiwango cha chuki🙏🏽 Mimi mwenyewe nimekulia katika familia ambayo baba alikuwa Muislamu na mama Mkristo, lakini mwisho wa siku tulipendana. Huo ndio uzuri wa Tanzania niliyoijua. Tanzania yenye tofauti za mawazo na imani, lakini bado yenye mshikamano.
Nafahamu kila uchaguzi una changamoto, lakini huu unaonekana kuwa utakuwa mgumu zaidi. Ndiyo maana nakuandikia. Hii si mara yangu ya kwanza kujaribu kufikisha sauti yangu kwako. Nakumbuka ulipochaguliwa, niliongea na mawasiliano yako na nikaambiwa ningeweza kukuona ulipokuja Washington, DC. Ingawa siishi DC, nilipanda ndege kuja kukuona, nikiwa na matumaini makubwa ya Tanzania bora….hii haikuwezekana kwa sababu ya maandamano. Nimehimasisha sana kuhusu Tanzania nilipoishi Marekani au nilipokuwa Ujeruman au popote ila leo, ninakuomba tuzingatie uchaguzi huu unaokuja.
Mama, upo kwenye nafasi kubwa sana kuhakikisha Tanzania inabaki salama na yenye amani. Kama walivyosema mh. Polepole na mh. Gwajima, wewe ndiye Commander-in-Chief mwenye uwezo wa kutuliza wananchi kabla mambo hayajaharibika zaidi. Mimi naongea na Watanzania wachache wa diaspora. Wanasema wazi kuwa wataandamana kama mambo hayatazingatiwa.🇹🇿 pia wananchi wanapanga kuonyesha kutoridhishwa kwao kwa maandamano. Lakini bado, mama, wewe unaweza kusuluhisha tofauti hizi. Najua wengine walinilaumu nilipozungumza na wanasiasa wa Marekani kuhusu Tanzania, na pia wengine watanilaumu hata kwa kuandika barua hii. Wengine wasioelewa historia yangu watasema, “Who does she think she is?” Simply, Mimi ni mama wa kawaida, ambaye kwa upendo wa Mungu ameniweka kwenye nafasi ya kuzungumza pale ambapo wengine hawawezi. Nitaendelea kutoa sauti yangu, si kwa sababu sipendi nchi, bali kwa sababu naipenda Tanzania na wananchi wake. Mama, tafadhali sikiliza Watanzania. Maamuzi yako leo yataamua historia ya kesho.
Ombi:
1. Muachie Tundu Lissu kwa hizi kesi za kisiasa. Itakuwa vigumu kueleweka 🇹🇿 na kimataifa kufanya uchaguzi bila kiongozi mkuu wa upinzani au chama chake kuwepo kwenye uchaguzi. Kuna maisha baada ya uchaguzi, na wengi watagoma kushiriki au kukubali matokeo kama hili halitafanyika.
2. Chaguzi huru na za haki ni muhimu. Watu wachague viongozi wao bila hila. Hata Marekani nilipo bado wanaheshimu kura ya wananchi. Baada ya maneno ya Mh. Polepole kuhusu tinted elections, ni vigumu wananchi kukubali matokeo bila kuwepo mfumo wa uwazi, ufuatiliaji wa karibu, na uwajibikaji wa kimataifa.
3. Jeshi? Historia ya mataifa yaliyowageukia wananchi wake kwa kutumia nguvu za kijeshi haijawahi kuwa nzuri. Watu wanaweza kuogopa kwa muda tu, lakini siku moja hawataelewa-na inaweza kuwa hivi karibuni kwa Tanzania. Hekima vyombo vya usalama vilinde wananchi na siyo tu serikali🙏🏽
4. Mengi ningeweza kuongelea kama ya uraia pacha, free press etc, lakini kwa sasa tuanze na haya muhimu👆🏼
5. Uhuru wa kuabudu. Mama, tafadhali fungua makanisa. Ukiondoa uhuru wa kuabudu, wengi hawaelewi na bado wataendelea kutafuta njia nyingine za kumuabudu Mungu wao na wengine kutoka imani yao pia wataingilia. Hata kama ni kwa masharti, ruhusu makanisa yaliyofungwa, yafunguliwe.
UNGA (United Nations General Assembly 80) mwezi huu Marekani. Dunia itakuwa inaitazama Tanzania na kujadili. Huu ni wakati wa kuonyesha kwamba tunaweza kufanya vizuri zaidi …vinginevyo, kufikia Oktoba inaweza kuwa kuchelewa. Mimi ni muandishi.naishia leo hapa @ikulumawasliano