Ukichukua 8 ukatoa 2 unapata 6, lakini 8 hiyo hiyo ukitoa 9 lazima ukope kwa 2 ili upate jibu. Maisha nayo yako hivyo, kuna muda huwezi kufika bila ya wale unaodhani wako chini yako. Heshimu kila mtu, mafanikio hayaji kwa nguvu zako tu bali pia kwa msaada wa uliowahi kuwadharau.
Jifunze kuheshimu kila mtu. Watu ni wale wale; usipokutana naye leo hapa, utakutana naye kesho kule. Heshima haigharimu chochote, lakini inaweza kukufungulia milango mingi kwenye maisha..✍️
Maji yanapochemka, yai huwa gumu lakini hufanya viazi huwa laini. Tatizo lilelile linaweza kumfanya mmoja awe imara na mwingine avunjike. Kinachofanya tofauti si tatizo, bali jinsi unavyolikabili. Jitahidi kuwa na mtazamo chanya.
Ukishika mchanga kwa nguvu sana, huanza kumponyoka kati ya vidole. Kwenye maisha si kila kitu kinahitaji kukilazimisha ili kibaki, vingine viache viende.
Ukifuta digit moja kwenye namba 1,000,000 unaweza kubadilisha milioni kuwa laki. Ukilitafakari hili vizur utagundua kwamba kosa moja linaweza kufuta miaka mingi ya kujenga jina lako. Kabla ya kufanya uamuzi wa dakika moja, fikiria thamani ya miaka uliyoitumia kujenga heshima yako
Namba 100 ina sifuri mbili, lakini bila ile namba 1 mbele yake zote zingekuwa hazina thamani. Maisha nayo yako hivyo, pesa, umaarufu na mali ni sifuri tu kama huna maadili yanayovipa thamani....✍️
Kwenye hesabu 2+8=10, 9+1=10, hata 0+10 bado ni 10. Njia ni tofauti lakini jibu ni lile lile. Vivyo hivyo katika maisha, watu wanaweza kufika sehemu moja, lakini safari zao huwa tofauti kabisa. Usijilinganishe na mtu, kila mmoja ana njia yake kuelekea mafanikio.