Hongera Sana Serikali ya Tanzania kwa kuchukua hatua muhimu za kuimarisha maisha ya mtoto ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu, upatikanaji wa watoa huduma za afya wenye ujuzi, kuboresha utoaji wa dawa muhimu na upanuzi wa huduma za afya za jamii kwa mama na watoto.
👏🏾👏🏾👏🏾
Nafurahi kuwa uamuzi wetu wa kununua dawa, vifaa na vifaaTiba moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji badala ya mawakala umesaidia kupunguza bei za bidhaa hizi kwa wastani wa asilimia 40. Mfano Shuka 1 la Hospitali… https://t.co/x6nR7NeO80
Nimekubali mwaliko wa @thisistemidayo na @RahmaMwita kwenye @sundayxtra keshokuwa Jumapili. Tusikilize kupitia @timesfmz 100.5 Dar & 95.3 Mbeya kuanzia saa 12 jioni. Tutaongelea Katazo la Mifuko ya Plastiki na masuala mengine mbalimbali, ikiwemo ya uongozi kwa vijana.
Upumzike kwa amani ndugu yangu Charles ulikuwa kijana mdogo mwenye upendo mkubwa sana na ari kubwa ya kazi. Asante sana kwa support kubwa uliotupatia Kisarawe enzi za uhai wako ukiwa na timu ya @azamtvtz
Natoa pole kwa ndugu na uongozi mzima wa @azamtvtz kwa msiba huu mzito 🙏🏽
Mwaka huu tumetimiza miaka 40 tangu vita kati yetu na Uganda vimalizike rasmi. Mzee wangu alipigana vita hiyo akiwa mstari wa mbele na jana tulipiga story ndefu. Hapa mama yangu anamalizia story kwa kuelezea yaliyomkuta yeye na mimi. Nikipata muda nitaweka link ya mazungumzo yote
Leo nimefanya ziara mkoani Dar es salaam, ilalamanispaa ili kukagua utekelezaji wa maelekezo niliyotoa kwa Mikoa/Halmashauri ya kupambana na ugonjwa wa Dengue nchini.
...
kwa ufupi nimeridhishwa na hatua… https://t.co/JsnBkMCiFf
I’ve been in touch with the team and coach twice this afternoon, and my good friends in Kampala have made contacts with the team. I’m confident they will get the needed help. Will update, if necessary.
Pia nilitembelea kiwanda cha Twyford uzalishaji ulianza 2018 pamoja na Goodwill vinafanya uzalishaji mkubwa wa marumaru Afrika Mashariki na Kati vilivyopo ndani ya mkoa wetu wa Pwani, Tanzania. wote walifika ofisini kwa mazungumzo na niliahidi kuwatembelea #TanzaniaYaViwanda
Viwanda vyote hivi vinatoa malighafi zake za uzalishaji kwa asilimia 95 hapa hapa nchini na kwetu wilaya ya Kisarawe wanapata malighafi ya muhimu katika utengenezaji wa marumaru/tiles hizi udongo/madini ya kaolin ambapo kwa ubora kaolin ya Kisarawe inaongoza. #TanzaniaYaViwanda
Hawa ni wadau muhimu wa maendeleo Kisarawe. Mapato yetu ya ndani kwa 65-70% inatokana na malighafi mbalimbali ya ujenzi na viwandani. Tunajenga mahusiano ikiwa ni pamoja na kuvumbua fursa mpya baada ya ziara hii viwanda vitaanza pia kuchukua udongo wa chokaa kutoka Kisarawe.