KWAKUWA NI HALALI KWA WAZANZIBARI KULINDA HAKI ZA WAZANZIBARI HAIWEZI KUWA HARAMU KWA WATANGANYIKA KULINDA HAKI ZA WATANGANYIKA.
Kwa yanayoendelea kujitokeza katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuhusu kujitanabaisha kwa misingi ya Uzanzibari na kulinda maslahi ya Zanzibar, je, si wakati sasa kwa Watanganyika nao kuzungumza kwa uwazi, kuhoji kwa uhalali na kujadili kwa kina masuala yanayohusu haki, hadhi na maslahi ya Tanganyika?
Je, Watanganyika hawana haki ya kuhoji na kulinda:
1. Bandari zilizopo ndani ya Tanganyika.
2. Misitu na rasilimali za mazingira za Tanganyika.
3. Rasilimali za asili zilizopo katika eneo la Tanganyika.
4. Hadhi, haki na umiliki wa ardhi ya Tanganyika.
5. Nafasi, haki na uwepo wa watu wasio Watanganyika katika idara na taasisi ambazo si za Muungano.
6. Uhalali wa viongozi wasio Watanganyika kuingia au kusaini mikataba inayohusu rasilimali za Tanganyika, hususan pale ambapo baadhi ya masuala hayo tayari yameondolewa katika eneo la Muungano kwa upande wa Zanzibar.
7.Kuhoji mchango wa Zanzibar katika kugharimia gharama za uendeshaji wa shughuli za Muungano na Ulipwaji wa Deni la Taifa.
Ikiwa ni halali kwa Wazanzibari kujadili, kuhoji na kulinda maslahi ya Zanzibar kwa misingi ya utambulisho wao wa kisiasa na kikatiba, kwa mantiki hiyo hiyo haipaswi kuwa kosa kwa Watanganyika kuhoji, kujadili na kutetea maslahi ya Tanganyika.
Katika mfumo wowote wa haki, usawa na kuheshimiana ndani ya Muungano, haki ya kulinda maslahi ya Zanzibar haiwezi kutenganishwa na haki ya Watanganyika kulinda maslahi ya Tanganyika.
Haki hizo zinapaswa kutambuliwa kwa usawa, bila upendeleo na bila kuonekana kuwa ni tishio kwa Muungano, bali kama sehemu ya kujenga Muungano wenye misingi ya haki, uwazi na kuheshimiana.
UKWELI,HAKI NA UWAJIBIKAJI ndiyo Msingi bora wa kuliongoza Taifa kutoka katika vitendo vya Ukatili dhidi ya ubinadamu,ukiukwaji wa Haki za Raia na,Mauwaji na Utekaji vilivyofanyika kanla,wakati na Baada ya Tarehe 29 Oktoba 2026.
BAK MWABUKUSI.
Huyu Saada Mkuya Salum amekua mbunge na waziri wa fedha huku bara..
Maneno muhimu kutoka kwako:
Unaelekeza mtu akienda hospital akitoa kitambulisho cha Taifa asitibiwe mpaka atoe cha Mzanzibari!!!! Ni mtu gani anaweza kuwa na kitambulisho cha Mtanzania lakini hana cha Mzanzibari?
Bila shaka ni mtu kutoka Tanganyika.
Umesema hatuna uwezo wa kutibu watu milioni 60 ambayo hiyo ni idadi ya Watanzania ambao wengi ni Watanganyika.
Je kuna siku wote wamevuka kuja kutafuta matibabu huko?
1. Saada unaweza kuwambia watu deni la Taifa ambalo kila mwezi tunalipa karibia trilioni moja na kadhaa ni kiasi gani kinatoka kwenye makusanyo ya Zanzibar?
2. Serikali za mitaa sio suala la muungano kwa katiba yetu,
Je unajua kuna wakurugenzi wa halmashauri za miji na majiji wameteueliwa kutoka Zanzibar huku Tanganyika?
Unajua kuna MADC wengi tu wameteueliwa kutoka Zanzibar wako huku bara?
Umefuatilia kwenye idara za madini, utaliii na wizara nyingi ambazo sio za Muungano kuna wakuu wa idara wangapi, wakurugenzi wa idara na maafisa wangapi kutoka Zanzibar?
Unataka Watanganyika wanaoishi huko wabaguliwe na wasipewe matibabu kwasababu ya kukosa kitambulisho cha Mzanzibari hata kama ana matibabu kadi ambayo ni sawa na bima ya afya….
Je Wazanzibari wanaoishi huku Tanganyika na wana bima za afya za NHIF nao wanyimwe matibabu?
Huyu ni waziri wa pili ndani ya mda mfupi kutoa kauli za kibaguzi dhidi ya Watanzania wengine na hakuna kauli yet kutoka kwa aliewateua… Kwahiyo huu ndio msimamo wa ccm na ndio msimamo wa wateuzi wao.
Nani anaewatuma hawa kusema haya? Maana sio bahati mbaya… nani anaewatuma kuwabagua Watanganyika?
Pamoja na kuwa Tanzania ina haki ya kuwa na mahusiano ya kirafiki na nchi yoyote duniani kwa kadri inavyowezekana, kwa maoni yangu safari ya kuelekea Moscow imefanyika katika wakati ambao si muafaka kisiasa na kidiplomasia.
Katika kipindi ambacho Marekani na Umoja wa Ulaya tayari wameonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa kisiasa nchini Tanzania, hususan baada ya matukio ya Oktoba 2025, malalamiko ya ukiukwaji wa haki za binadamu, na kuendelea kushikiliwa kwa viongozi wa upinzani, jambo la mwisho ambalo Tanzania ilihitaji ni kutuma ujumbe unaoweza kutafsiriwa kama kuhamisha mwelekeo wake wa kimkakati kutoka kwa washirika wake wakuu wa maendeleo kwenda Moscow.
Tatizo si kwenda Moscow.
Tatizo ni kwenda Moscow wakati Washington na Brussels wanaanza kuhoji mwelekeo wa kisiasa wa Tanzania.
Diplomasia sio suala la hisia; ni suala la muda, mazingira na maslahi ya taifa.
Ukweli ambao hatupaswi kuuficha ni kwamba kwa sasa Russia haiwezi kuchukua nafasi ya Marekani na Umoja wa Ulaya katika maendeleo ya Tanzania.
Takwimu zinaonyesha wazi:
Marekani imechangia zaidi ya dola bilioni 3 katika kipindi cha 2020–2025.
Umoja wa Ulaya umechangia takribani dola bilioni 3.2.
Russia imechangia karibu sifuri katika Official Development Assistance (ODA).
Haya si maoni. Hizi ni takwimu.
Wakati mwingine katika siasa tunajidanganya kwamba washirika wanaweza kubadilishwa kwa urahisi. Historia inaonyesha sivyo.
Marekani na Umoja wa Ulaya hawatoi fedha pekee.
Wamekuwa nguzo muhimu katika:
mapambano dhidi ya UKIMWI na malaria,
chanjo na mifumo ya afya,
elimu,
maji safi,
kilimo,
uwekezaji wa sekta binafsi,
teknolojia,
mafunzo ya wataalamu,
na upatikanaji wa masoko ya kimataifa.
Pengo litakalotokana na kupungua kwa ushirikiano huo haliwezi kuzibwa kwa picha za viongozi kukutana au mikataba michache ya kisiasa.
Mataifa hayajengwi kwa alama za kidiplomasia; yanajengwa kwa maslahi halisi ya wananchi.
Swali ambalo viongozi wanapaswa kujiuliza si kama tunaweza kuwa marafiki wa Russia.
Swali ni:
Je, Russia inaweza kuchukua mzigo wa afya, elimu, uwekezaji, biashara na maendeleo ambao Marekani na Umoja wa Ulaya wameubeba kwa miongo kadhaa?
Mpaka sasa, jibu la ukweli ni hapana.
Hatari kubwa zaidi si kupoteza misaada.
Hatari kubwa ni kupoteza imani.
Mataifa yanaweza kuishi bila misaada kwa muda fulani.
Lakini ni vigumu kuishi bila imani ya wawekezaji, masoko ya kimataifa, taasisi za kifedha na washirika wa maendeleo.
Fedha za dunia zina tabia moja:
Hukimbilia kwenye utulivu, uwazi wa kisiasa na taasisi zinazoaminika.
Ndiyo maana nchi yenye busara haiharibu madaraja kabla haijajenga mengine.
Na hata kama imeamua kujenga daraja jipya kuelekea Moscow, ni hatari kubomoa madaraja yaliyoiunganisha na Washington na Brussels kwa zaidi ya nusu karne.
Kwa sababu katika siasa za kimataifa, si kila rafiki mpya ana uwezo wa kuchukua nafasi ya rafiki wa zamani.
Na katika wakati ambao Tanzania inahitaji uwekezaji zaidi, ajira zaidi, teknolojia zaidi na masoko zaidi, taifa linapaswa kuwa makini sana lisije likachanganya uhuru wa kidiplomasia na kujitenga kidiplomasia.
Uzalendo wa kweli si kupiga picha na mataifa makubwa; uzalendo wa kweli ni kuhakikisha maamuzi ya leo hayaleti gharama ambazo wananchi wa kawaida watazilipa kesho.
BEIA YA MAFUTA IMESHUKA katika soko la Dunia sasa wakati wa Kupanda inapanda ghaflayaani ikipanda asubuhi mchana lazima huku tupewe kipenyo lakini cha ajabu sasa Imeshuka wameanza longo longo eti wanaangalizia kushuka zaidi yaani imeshuka kwa Asilimia 20?! halafu bei zisibadilike? Hii ni maajabu
Ni kweli wengine hatukusoma hesabu na ukokotoaji wa hesabu nisuala la kitaaluma tulikimbilia somo la Siasa but the number is not adding hapa tunapigwa.
Hivi hata hili Wabunge pale Dodoma nalo mnashindwa kuwalinda wananchi?
BAK MWABUKUSI.
Africa holds 60% of the world’s uncultivated arable land, 30% of global mineral reserves, 12% of global oil reserves
And yet the continent imports food.
This is not natural poverty. This is structural poverty,
Nimewasikiliza ma-bro na dada zetu huko mjengoni juu ya hili suala la kufutiwa VISA na USA. Nimetafakari sana bila majibu na kubaki najiuliza, kwanini walilie haki ya kutembelea nchi za Mabeberu wenye wivu na maendeleo yetu?😀
A country where graduates drive motorbikes to survive while politicians’ children secure powerful jobs through connections is not lacking talent, it is lacking fairness.
Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman wa Chama cha #ACTWazalendo, amesema hayo wakati akizungumza na Mwandishi wa BBC, Sammy Awami, Mei 21, 2026.
Fuatilia zaidi https://t.co/5zFRgsrL2O
#JamiiForums#Demokrasia#Siasa
ARUSHA: Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi ameyasema hayo Mei 21, 2026, kwenye Mkutano Mkuu wa 13 wa Kitaaluma wa Chama cha Waandishi Waendesha Ofisi (TAPSEA).
Upi mtazamo wako?
Fuatilia zaidi https://t.co/K1XIfDBdRO
#JamiiForums#Uwajibikaji#HumanRights
DAR: Mchora Katuni ambaye amewahi kuwa Mtangazaji wa Redio na TV, Masoud Kipanya ameyasema hayo Mei 15, 2026 kupitia chaneli ya Kipanya Tell A Vision akielezea mtazamo wake kuhusu tabia ya Watu wanaotoa maoni kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.
Zaidi tembelea https://t.co/ScLMyWwtKC
#JamiiForums #Uwajibikaji #Siasa #DigitalRights #FreedomOfExpression
Mtu aliyejitambulisha kama Mbunge wa jimbo la Ikungi Magharibi, ameishauri Serikali katili ya CCM kuanzisha tozo kuchangia Bima ya Afya kupitia miamala ya simu. Kila Mtanzania atachangia fedha kwa kila muamala.
Tanzania, kodi na tozo katika miamala ya simu zimegawanyika katika sehemu kuu tatu: Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), Ushuru wa Bidhaa (Excise Duty), naTozo za Serikali (Government Levies).
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT); Hii ni kodi ya (18%) inayotozwa kwenye huduma zote za kibiashara. Kodi hii inakatwa kutoka katika ada ya huduma (service fee) anayolipa mteja kwa kampuni ya simu.
Ushuru wa Bidhaa (Excise Duty); Ni kodi (17%) ambayo inatozwa katika huduma za mawasiliano na uhamishaji fedha. Kodi hii inatozwa kwenye ada ya huduma ya kampuni ya simu kwa ajili ya kutuma au kutoa fedha.
Tozo ya Serikali (Government Levy). Hii waliipa jina la Tozo ya Uzalendo. Tozo bado ipo kwenye kutoa fedha taslimu (kwa wakala). Unapofanya muamala (mfano: kutoa 10,000 TZS), unacholipa kinajumuisha:
Ukimtumia Mtu Fedha kiasi cha TZS 50,000, unacholipa ni Ada ya Mtoa Huduma (ndani yake ina VAT na Excise Duty). Hii ni TZS 800 mpaka TZS 1,000. Tozo ya Serikali ni TZS 0 (Imefutwa kwa miamala ya simu kwa simu).
Ada ya Mtoa Huduma & Wakala ni TZS 1,200. Tozo ya Serikali (Kutoa) TZS 500. Jumla utakatwa TZS 1,700 kutoa TZS 50,000. Unapotoa fedha taslimu, hapo ndipo Tozo ya Serikali ya kutoa inapofanya kazi yake.
Nimetuma TZS 100,000 kutoka CRDB kwenda M-PESA. Nimekatwa TZS 3,500. Hiyo pesa 100,000, ukitoa kwa wakala. Gharama ya kutoa kwa wakala (ikijumuisha ada ya mtandao na tozo ya serikali ya kutoa) ni TZS 3,300.
Sekta ya afya inahudumiwa na vyanzo mbalimbali vya mapato. Wameweka utaratibu wa kutoza kodi na tozo (levies) katika bidhaa au huduma ambazo asilimia ya mapato huelekezwa kwenye miradi au huduma za afya.
Serikali inatoza fedha katika miamala ya kutuma na kutoa fedha kwa njia ya simu. Hii imeelekezwa katika ujenzi wa vituo vya afya na zahanati, kata na vijiji na kuimarisha huduma za dharura na ununuzi wa dawa.
Kodi ya Bidhaa (Excise Duty); hii inatozwa katika bidhaa zinazosababisha magonjwa yasiyoambukiza kama vile sigara na bidhaa za tumbaku, vinywaji vikali na pombe, vinywaji vyenye sukari (sugar-sweetened beverages)
Tozo ya Mafuta (Fuel Levy); Kodi kama ongezeko la thamani (VAT), kodi ya mapato (Corporate Tax), na ushuru wa forodha (Excise Duty) huingia moja kwa moja katika Mfuko Mkuu wa Serikali (Consolidated Fund)
Kutokea hapo, Serikali hupanga bajeti na kugawa fedha kwenda sekta mbalimbali kulingana na vipaumbele vya taifa. Katika sekta ya Afya, fedha inakwenda kwtika Ujenzi wa hospitali, vituo vya afya, na ununuzi wa dawa.
Michango ya Bima ya Afya (NHIF na iCHF); Hii ni tozo (lazima) kwa watumishi wa umma. Ambapo, kila mtumishi wa umma anakatwa 6% ya mshahara ghafi (gross salary) na hiari kwa watumishi sekta binafsi.
Tozo za Huduma za Hospitali (User Fees); Mwananchi hulipa anapofika hospitali kupata huduma (kama hana bima). Zinabaki vituo vya huduma ili kusaidia ununuzi wa dawa za haraka na vifaa vidogo vidogo vya maabara.
TZ ni kati ya nchi zenye maeneo makubwa yaliyotengwa kwa hifadhi duniani (zaidi ya 25% ya ardhi). Hifadhi za Taifa (National Parks), Mapori ya Akiba (Game Reserves), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA)
Tanzania ina Hifadhi Wanyamapori. Madini ya Thamani na Viwandani. Gesi Asilia. Vyanzo vya Maji. Ardhi na Misitu. Nishati ya Maji, Jua na Upepo. Milima. Bado Mnaendelea kumjazia mwananchi kodi na tozo?
Kwanini hizo pesa zisitoke katika mishahara na posho zenu? Mbunge hakatwi kodi na anapata mshahara na posho unaokadiriwa kufikia TZS 18 milioni kwa mwezi. Kwanini tusipunguze mishahara yenu MAFISADI?
AKILI zenu zimeishia katika kufikiria kuongeza tozo na kodi tu? Halafu, hizo pesa za kodi zikipatikana, mnakwenda kukimbiza moto tu. Nyingine mnanunua magari ya kifahari. MBOGAMBOGA HAMJITAMBUI.
“Kumekuwa na majaribio na vitisho kutoka kwa watawala kunizuia nisiongee. Kuna wakati niliambiwa nizime simu yangu, nisiitumie mpaka (wao) watakapo niambia. Nikawauliza, kwa sheria gani? Kuna wakati nilikaribishwa mahali fulani, nikapigiwa simu na watawala, wakasemam mzee usiendee kwenye huo mkutano. Kwanini? Hauna manufaa. Nikawauliza, nani anaamua hayo manufaa? Nikakataa. Wakawafuata watu walio karibu na mimi ili wanishawishi nisiende, nikakataa pia. Mnakumbuka nilifanya mahojiano hapa na Jamhuri? Wakatoa summary, wakasema watachapisha mahojiano yote, neno kwa neno. Baadae Jamhuri wakanieleza wamezuiwa wasitoe yale mahojiano. Kuna viongozi wanaogopa kuzungumza na mimi, wanatuma ujumbe kupitia mbali huko. Marafiki zangu wanaogopa wakisema nitatekwa au kupewa sumu. Nawaeleza mimi ni mali ya Mungu, ndiye atakayeamua lini ananihitaji.”
— Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Tanzania.