TURUDISHE TABASAMU LA CATHERINE NA FAMILIA YAKE. Tuma mchango namba 0740264760 Voda Jina:
Catherine johaness protace
Catherine johaness protace ni mwanafunzi wa mwaka wa 3 Chuo cha CBE Dare es salaam.
Anaishi Mtaa wa Mashine ya Maji Kata ya Buza Wilaya ya Temeke Dar.
Catherine amekosa matumaini ya kuendelea na Chuo baada ya kaka yake Baraka Chacha Mwita aliekuwa anamsomesha kuvunjwa miguu yote miwili na kupewa kesi ya Uhaini, mpaka sasa yupo gerezani.
Mahitaji muhimu ya Catherine na Familia yake.
1.Ada ya Chuo Million 1
2.Bima ya Afya
3.Kodi ya Nyumba
4.Mahitaji ya kila siku
5.Matumizi ya Kaka yake magereza.
Tumchangie kiasi cha Million 5, namba yake ni 0740264760
Catherine johaness protace
GEORGE ANAHITAJI MSAADA WAKO ILI AWEZE KUTEMBEA TENA.
Huyu anaitwa George Wayanga aliwahi kuwa Katibu wa BAVICHA Wilaya ya Chunya kipindi cha 2014-2019 na amekuwa Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Chunya 2019-2024.
Siku za hivi karibuni alipata ajali iliyopekea kukatwa mguu wake kwasasa anatumia magongo ili aweze kutembea.
George anahitaji msaada wa hali na mali ili aweze kupata mguu bandia ambao gharama yake ni TSH 2,200,000/=
Hivyo tunaomba mchango wako kiasi chochote ulichojaliwa na Mungu ili George aweze kupata mguu bandia ambao utamuwezesha kutembea na kuendelea na shughuli zake za kila siku.
Mchango wako unaweza tumwa kwenye hii namba
M-PESA 0760638604
Jina: George Wayanga.
Natanguliza shukrani za dhati.๐๐ป
UKIONA HII REPOST
Nimetoka kuongea na Ofsa Kiduku hapa kwa urefu kidogo.
Kwanza mwana anashukuru sana kwa Love Mliyoonyesha kwa kupaza Sauti, lakini pia kasema niwaambie kuhusu Afya yuko sawa na amedai kuna watu walikuwa wanaendelea ku show Love mpaka huko kituoni mwana anasema alikuwa anakula vizuri tu kwasababu ya U Familia wenu. ๐
Jambo lingine ambalo hakuniomba nililete ila mi nalileta kwenu baada ya mimi kumuomba akubali nililete ni hili.
Mwana ametoka kwenye matatizo hana Simu na kwa bahati mbaya ilikuwa ni muda wa kodi umekaribia na hajafanya kazi wiki akatuomba kama wana tufanye linalowezekana apate kodi na simu.
Ila tunajua kiume mwana ana changamoto zaidi ya hizo ila hawezi sema nikaona kidogo tutachochangia na wana tumchangie chochote kile maana kodi 600k na simu kwa biashara yake hawezi tumia kitochi lazima apate tambo.
Mimi na Sativa tutachangia 300K iliyobaki wengine tunaweza changia kwenye hii namba ya Mtu wake wa karibu maana yeye hana laini wala simu.
Namba ๐๐๐
0657523001
YAHSINTA CHUWA
REPOST REPOST
Mtoto Vincent Ibrahim (09) wa Manyoni, Singida amepigana vita dhidi ya kifo kwa miaka 8 sasa na amefikia hatua ya kukata tamaa. Akiwa na umri wa mwaka mmoja aligundulika kuwa na tundu kwenye moyo โ Ventricular Septal Defect (VSD) ambalo linasababisha damu safi na chafu kuingiliana.
Afya yake ilianza kuzorota, kushindwa kupumua vizuri, kuchoka, kupungua uzito, kutoka jasho sana na kukakamaa kama mtu mwenye degedege. Awali familia haikujua tatizo na hivyo mama yake akawa anampeleka kwenye maombi akiamini amelogwa. Lakini hali ilizidi kuwa mbaya na ndipo akampeleka hospitali ya St. Gaspar Itigi.
Baada ya vipimo alipewa rufaa kwenda Benjamin Mkapa, Dodoma alipogundulika kuwa na tundu kwenye moyo. Alipewa rufaa kwenda taasisi ya moyo JKCI, lakini wazazi hawakuwa na fedha hivyo walimrudisha nyumbani ili kujipanga kwanza.
Mwaka 2019 baba aliaga kwenda kutafuta kibarua mgodini ili apate pesa za matibabu ya mwanae, lakini haijulikani kama alifia huko au yupo hai, kwa sababu hajawahi kurudi wala kuwasiliana na familia. Hivyo basi mama akajikuta anapambana na mwanae peke yake.
Mwaka jana Vincent alizidiwa na kulazwa hospitali ya St. Gaspar Itigi. Jumuiya ya Kanisa ikamchangia fedha kidogo zilizomuwezesha kufika JKCI. Baada ya vipimo aliandikiwa upasuaji kwa gharama ya TZS 6M. Lakini baada ya kujielezea hali yake, alipewa msamaha na kutakiwa kulipia 3.6M tu.
Hata hivyo alishindwa kumudu gharama hizo, akaomba arudi nyumbani kujipanga. Kutokana na kukosa matibabu, hali ya Vincent imezidi kuwa mbaya. Kwa sasa amedhoofika, anashindwa kupumua vizuri, na ameshindwa kuendelea na masomo katika Shule ya Msingi Sayuni, Manyoni anaposoma darasa la 3.
Kumbuka Vincent aligundulika na tatizo la moyo akiwa na umri wa mwaka mmoja. Kwa sasa ana miaka 9. Amepigania maisha yake kwa miaka 8 bila matumaini. Miaka 8 ya mateso kwa kukosa 3.6M tu.
Mimi na wewe tuna nafasi ya kurudisha tabasamu kwa Vincent na kumsaidia kufanyiwa upasuaji. Sadaka yako ya leo ielekeze kuokoa maisha ya Vincent. M-PESA #0752581983, Tigopesa #0719744954, CRDB #0150633516500, NMB #24110012109 Gifted Hearts Foundation
#RudishaTabasamu #LetLoveLead