Kiongozi wa chama cha upinzani cha Afrika Kusini EFF Julius Malema amevishukia vyama tawala barani Afrika vilivyohusika na vuguvugu la uhuru ikiwemo CCM, ZANU-PF, SWAPO, FRELIMO na ANC kuwa kitakachowamaliza ni kifo cha asili ambacho hakikwepeki kwani havitaweza kujivua gamba ili kuendeleza ajenda ya ukombozi.
#TANZANIA: HECHE ASEMA NCHIMBI AMETOA SIRI ANAEKWAMISHA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA, "FREE LISSU"
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche leo Julai 29, 2026 amesema alichokiongea Makamu wa Rais, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuhusu kupambania katiba mpya ni fumbo linalotafsirika kirahisi kwamba anaekwamisha mchakato huo ni Rais mwenyewe.
Aidha, Heche amezungumzia katiba iliyopo kwamba inamapungufu makubwa hivyo inapaswa kufanyika mchakato wa kupata katiba mpya.
Pia, ameisihi serikali ya serikali kumuachilia huru Mwenyekiti wao wa Taifa, Tundu Lissu.
Zaidi: https://t.co/yz0pY4tah0
"Tunafuatiliwa, mimi nina taarifa za ndani kabisa kwamba nataka kukamatwa. Mimi siogopi, mimi sio mtu wa kutishiwa. I was born once, I live once and I will die once. Narudia hili kila siku wajue, mimi ni mtu huru, nafanya kazi iliyoruhusiwa na Nchi hii na hakuna wa kunitisha. Kama unataka kumtisha Heche unagonga pabaya na jipange upya."
"Katika hilo leo asubuhi kuna gari imekuja nyumbani kwangu Toyota hardtop nyeupe, tumeipiga picha na tumefuatilia, zile namba sio za gari hiyo, wamekuja wanauliza kwa Heche ni wapi. Hizo namba zimesajiliwa kwa Cartepillar, haya yanayolima barabara. Sasa kama ni watu wema, waje mchana, kama wana shida ya kunikamata waniite lakini shida ya kutishana, kutekana mimi haya sifanyi na watanzania msikubali. Wakinichukua kwenye mazingira ambayo hayaeleweki msikubali. Hatuwezi kuishi kwa kunyimana amani. Ukitunyima amani tutakunyima amani"- John Heche, Makamu Mwenyekiti wa Chadema bara, akizungumza na wananchi wa Nyamagana Mkoani Mwanza leo Jumatano Julai 29, 2026.
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara John Heche sasa amekuwa akizunguka kwenye vijiwe na maeneo mbalimbali kwaajili ya kuwashawishi na kuwahamasisha wananchi kuchangia 'TONE TONE' ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Baraza Kuu la chama hicho linalotarajiwa kufanyika Septemba 2026
"Kwa yeyote anayefikiri kuumiza Taasisi hii, kwa namna ambavyo watu wake wanapambana usiku na mchana ebu fikiri upya. Uwe serikalini ama kwingine, hutaweza kwasababu Taasisi hii imevuka viwango vya kuuwawa na mtu. Niwashukuru pia, Mimi nipo imara."- John Heche, Makamu Mwenyekiti wa Chadema akizungumza na wananchi wa Nyamagana, Mwanza leo Jumatano Julai 29, 2026.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amesema awamu ya pili ya kampeni ya uhamasishaji wa Tonetone imeendelea leo kwa kufanya ziara ya mtaa kwa mtaa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukamilisha lengo la kukusanya shilingi milioni 334.
Kwa mujibu wa Heche, mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa, huku wengi wakijitokeza kuchangia papo kwa hapo katika maeneo yaliyofikiwa na viongozi wa chama.
Akizungumza kupitia ujumbe wake aliouchapisha leo Jumanne, Julai 28, 2026, Heche alisema:
"Awamu ya pili ya kuhamasisha Tonetone leo tumeingia mtaa kwa mtaa kuhamasisha uchangiaji ili kukamilisha milioni 334. Kila tulikopita wananchi wametupokea kwa furaha na kuchangia papo kwa hapo." Amesema.
Aidha, amewahimiza wanachama, wafuasi na wananchi kuendelea kuchangia Chadema kupitia njia mbalimbali za malipo.
"Tuendelee kuchangia chama kwa namba M-Pesa: Namba 0744446969, Jina: CHADEMA HQ. NMB Bank, Namba ya Akaunti: 22606600140, Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo."
CHADEMA inaendelea na kampeni hiyo ya Tonetone ikiwa ni sehemu ya jitihada za kukusanya fedha za kuendesha shughuli za chama kupitia michango ya wanachama, wafuasi na wadau wake.
CHANGIA BARAZA KUU LA UMMA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Magaidi LISSU anasema peleka Moto peleka Moto 🔥🔥🔥🔥
Mpaka sasa tumefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 232.6, hivyo tumebakiza TSh. Milioni 1.4 pekee kufikisha Milioni 234.
Tuvuke hatua hii muhimu, kisha tuanze safari ya kukusanya Milioni 100 zilizobaki ili kutimiza lengo letu la TSh. Milioni 334 kwa ajili ya Baraza Kuu la Umma.
CHANGIA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
VIDEO:
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Dkt. Rugemeleza Nshala amesema chama hicho kimekuwa kikipitia MAPIGO makali ambayo kwa namna moja au nyingine MAPIGO hayo yanalenga kuwatoa kwenye reli viongozi wake, hata hivyo viongozi wa chama hicho wameapa kusimama imara na katu hawatakuwa tayari kuwasaliti Watanzania mara zote
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo, Jumatatu Julai 27.2026, Dkt. Nshala ametaja baadhi ya MAPIGO hayo kuwa ni pamoja na mfululizo wa kesi kubwa kama vile uhaini na ugaidi zinazowakabili viongozi na makada wake, karibu kila kona ya Tanzania
Amegusia pia uwepo wa mfululizo wa kesi zinazohusu chama zilizopo Mahakamani, sambamba na vizingiti vilivyopo kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
VIDEO:
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Dkt. Rugemeleza Nshala ametoa tahadhari juu ya kesi ya ugaidi ya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) Melkisedeki Kaijage akieleza kuwa inachafua taswira ya nchi.
Dkt. Nshala amesema hayo leo Julai 27, 2026 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam huku akieleza kuwa chama hicho kitatoa wanasheria kwa ajili ya kuwasaidia wote walioshtakiwa kwa mashtaka mbalimbali ikiwemo ya ugaidi.
Pamoja na hayo ameeleza kuwa wanasheria watahoji juu ya ukatiba wa mashauri mbalimbali yaliyofunguliwa.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa onyo dhidi ya kile kilichokiita kitendo cha serikali na vyombo vya dola kugeuza shughuli halali za kisiasa kuwa makosa ya jinai na ugaidi, kikisema mwenendo huo unaisukuma nchi siko na kuwatishia raia haki zao za kikatiba.
Rai hiyo imetolewa leo Jumatatu, Julai 27, 2026, jijini Dar es Salaam na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Rugemeleza Nshala, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya kisiasa na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini.
Dkt. Nshala ameeleza kuwa vitendo vya kuwakamata viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani wanapokusanyika au kupanga maandamano ambavyo ni haki za kikatiba na kuwabambikizia kesi za jinai na ugaidi, vinavunja msingi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Kugeuza shughuli halali za kisiasa kuwa jinai au ugaidi ni hatari sana kwa nchi wetu. Ibara za 3, 15, 18, 20, 26 na 29 za Katiba zinatamka wazi kuwa Watanzania wanayo haki ya kufanya siasa, kukusanyika, na kuwa huru. Ukigeuza raia huru kuwa watwana katika nchi yao, unaipeleka nchi mahali pabaya," amesisiitiza Dkt. Nshala.
Akiangazia athari za kisheria na kiuchumi kwa waathirika, Mwanasheria huyo Mkuu ameainisha kuwa chama hicho hakiwezi kuendelea kuangalia wanachama wake na viongozi wakiteseka magerezana kwa miaka kadhaa wakipambana na kesi zenye viashiria vya chuki na lengo la kukomoa, huku jamii ikiambiwa "sheria ichukue mkondo wake."
Kufuatia hali hiyo, CHADEMA kimetangaza kuchukua hatua za kimkakati za kisheria ili kuhoji ukatiba wa hatua hizo mahakamani.
Dkt. Nshala alieleza kuwa kama mawakili na maafisa wa mahakama, wamekaa chini na kufikia maamuzi ya kufungua mashitaka madhubuti yatakayolazimisha Mhimili wa Mahakama kutoa tafsiri sahihi ya Katiba na kuweka kumbukumbu ya kihistoria kuhusu ulinzi wa haki za raia.
"Tumevumilia sana. Mwenyekiti wetu na wanachama wengi wamepitishwa kwenye mbinu mbalimbali za mahakamani. Sasa hivi kuna haja ya msingi ya kuangalia ukatiba wa vitendo hivi ili Mahakama yetu iingie kwenye kumbukumbu za kihistoria kuhusu msimamo na tafsiri yake katika nyakati kama hizi," amehitimisha.
Mpaka sasa tumefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 226.1, hatua kubwa inayotusogeza karibu zaidi na lengo la TSh. Milioni 334.
CHANGIA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
"Nchimbi anasema Samia anataka Katiba lakini wakati huohuo anatuambia tukomae tupate katiba, sasa maana yake ni nini? Kama hakuna anayezuia si inatakiwa iwe yenyewe tu bila kukomaa!" ~ Heche
#TANZANIA: HECHE AWATAKA WANANCHI WOTE KUPIGANIA HAKI, "WANAFUNZI NA MWALIMU WAPEWA KESI YA UGAIDI, KILA MTU ATAFIKIWA"
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche leo Julai 25, 2026 akizungimza na Waandishi wa Habari jijini Mwanza amewataka Wananchi wote kupigania haki kwa sababu kila mmoja atafikiwa kwa wakati wake akitolea mfano wa Wanafunzi pamoja na Mwalimu 'waliobambikiwa' kesi ya ugaidi, amedai wakati Lissu anakamatwa na kupewa kesi ya uhaini walinyama.
Aidha, Heche ametoa wito kwa serikali kuacha 'kubambikia' watu kesi badala yake wawaachie ili waendelee na maisha yako kwa sababu kupigania haki si ugaidi.
Zaidi: https://t.co/AQX5r1i3H0
Kiongozi wetu na Mwenyekiti wetu alikamatwa akiwa mzima,
Taarifa Kama hizi za kuhusu kujaribu kucheza na maisha yake hazitakubalika.
Serikali hii dhalimu inapaswa kumuachia Lissu haraka.
Sisi Tunafuatilia kila kitu na hakuna taarifa hata moja tunaipuuza.
#freetundulissunow
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara, John Heche, amewaagiza Mawakili wa chama hicho pamoja na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA kuandaa timu maalumu itakayohakikisha viongozi wa chama hicho na wanachama wengine wanaoshikiliwa maeneo mbalimbali nchini wanarudi katika shughuli zao.
Heche ameeleza hayo Jumamosi, Julai 25, 2026, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza. Amewasihi wanachama wa CHADEMA nchini kote kuonana na ndugu wa watu waliokamatwa kama sehemu ya faraja.
"Natumia nafasi hii kuwaagiza viongozi wetu wa chama, mawakili wetu, viongozi wote wa chama na mawakili wengine wote waandae timu maalumu ya kuendelea kupambana kuhakikisha viongozi wetu wanaachiliwa wanarudi kwenye shughuli zao" amesema Heche.
Maagizo ya Heche yanakuja kutokana na viongozi mbalimbali na wanachama wa chama hicho kufikishwa katika mahakama mbalimbali nchini wakikabiliwa na mashitaka yanayohusu ugaidi ambayo hayana dhamana.