#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 26
Tumerejea baada ya Mapumnziko ya nusu saa.
Anaanza Wakili wa waleta maombi Adv. Emmanuel Ukashu kumuhoji Maswali Mkuu wa Gereza la Ukonga Ntamamiro (Bwana Jela)
Adv. Ukashu: shahidi umewahi kuisikia TLS?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio naifahamu.
Adv. Ukashu: Ili mtu aingie Gerezani inahitajika wewe ndio umruhusu aingie?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sahihi
Adv. Ukashu: Ni sahihi ukipewa maelekezo yoyote lazima utekeleze na Kamishna General?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni sahihi
Adv. Ukashu: Maelekezo kutoka juu maana yake nini?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni maagizo ya kiutendaji unayopaswa kutekeleza.
Adv. Ukashu: Usipoyatekeleza unaweza kufukuzwa kazi?
Ntamamiro (Bwana Jela) : kwa mujibu wa sheria.
Adv. Ukashu: Unaweza kumbishia Boss wako?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Siwezi kufanya hivyo.
Adv. Ukashu: Soma SUPP 4 tar. 12/03/2026 entry no. 8 hebu isome hapo.
Ntamamiro (Bwana Jela): Huruma Tehejas mfungwa aliyekuja kumtembelea ni mfungwa na shida ya kisheria. Maoni hapakujazwa. Na sahihi hamna.
Adv. Ukashu: Sasa alienda wapi huyu Wakili kama hakuna uliposaini na maoni hukuweka.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Nilisahau kujaza na naamini hakukataliwa pia.
Watu wanacheka. 😂😂😂😂
Adv. Ukashu: Kwanini usifukuzwe kazi kwa uzembe wa aina hii? Maana haijulikani alikuja kufanya nini?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Nifukuzwe tu kazi kama unaweza kunifukuza. Fanya hivyo ila mimi nimesema nilijisahau.
Adv. Ukashu: Unafahamu kazi ya uwakili ina maadili yake?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kila kazi ina maadili.
Adv. Ukashu: Maadili ya magereza tumeshayaona hapa hujajaza nyaraka na hujui wakili alipoingia alielekea wapi? Sasa tuzungumze maadili ya mawakili.
Ntamamiro (Bwana Jela) : siyajui mi sio wakili.
Adv. Ukashu: Unaijua Mandela Principle?
Ntamamiro (Bwana Jela): yes
Adv. Ukashu: soma hapa inasemaje?
Ntamamiro (Bwana Jela): Mfungwa atazungumza na wakili wake kuwa atazungumza bila kikwazo.
Adv. Ukashu: Umeitekeleza?
Ntamamiro (Bwana Jela): Inasema nizingatie sheria za ndani pia?
Adv. Ukashu: Sasa tuambie ni kifungu gani cha sheria ya ndani ambacho kiko kinyume na Mandela Principle.
Ntamamiro (Bwana Jela): Hakipo.
Adv. Ukashu: Nimemaliza. Naomba Wakili Neema aendelee.
Anasimama Wakili Neema Saruni.
Adv. Neema Saruni: Nitakuwa sahihi nikisema mtu anayekuja kumuona mfungwa anapaswa kuwa na sababu ya msingi?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni sahihi kwa mujibu wa Sheria.
Adv. Neema Saruni : Ulisema mjibu maombi wa nne alikuwa na orodha yake hivyo basi alipotokea hayupo mlimrudisha?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio tulifanya hivyo.
Adv. Neema Saruni : Nitakuwa sahihi nikisema hamkumpatia haki yake ya kusikiliza.
Ntamamiro (Bwana Jela): Sahihi.
Adv. Neema Saruni: Nilipokuja mimi kumuona Lissu nilikuwa kwenye orodha yake?
Ntamamiro (Bwana Jela): Haukuwepo.
Adv. Neema Saruni : Nilipofika ikawaje?
Ntamamiro (Bwana Jela): tulienda kumuuliza lissu.
Adv. Neema Saruni : akasemaje?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Akaruhusu ukamuone.
Adv. Neema Saruni: Kwanini huyo mwingine mlimrudisha bila kwenda kuuliza Lissu anasemaje?
Ntamamiro (Bwana Jela): Hapo sasa ndio kuna utata.
Watu wanacheka 😂😂😂
Adv. Neema Saruni: Nimemaliza.
Haya wanasimama mawakili wa Serikali, anaanza Wakili wa Serikali anaitwa Wisdom
Wakili wa Serikali Wisdom: Ulitekeleza majukumu yako kwa mujibu wa nini?
Ntamamiro (Bwana Jela): masharti yapo kwenye sheria ikiwemo PSO.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji naomba asitaje kabisa PSO maana jana haikuwepo na hatukumuuliza. Asiulize. Sect. 156(3) ya Evidence Act iko wazi kuhusu Re- examination.
Jaji: Sasa Wakili wa Serikali Wisdom uko tayari kuendelea na njia hiyo ili tumruhusu Lissu nae aanze kuuliza kwenye PSO.
Wakili wa Serikali Wisdom: Naomba tu niishie hapo. Sitaendelea mbele.
Watu wanacheka 😂😂😂😂
Part 27 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 25
Wakili wa Waleta maombi Edson Kilatu anaendelea kumdodosa Shaidi ambae ni Mkuu wa Gereza la Ukonga Ntamamiro (Bwana Jela)
Adv. Kilatu: Ni sahihi ili tujue maduhu ni muongo anasema alifika Ukonga lakini hakufika kumbe ulipaswa kuleta kitabu cha watu wanaohudhuria ukonga wakifika pale getini wanaandika.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sahihi
Adv. Kilatu: Umeleta?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijaleta.
Adv. Kilatu: unakumbuka kuhusu huwa hamsomi nyaraka anazopelekewa Lissu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : ndio
Adv. Kilatu: umeleta kiapo chochote cha unaowatuma kusimamia kuwa wanasema hatujawahi kusoma nyaraka za Lissu tukitekeleza majukumu yetu.
Ntamamiro (Bwana Jela): nimeleta mimi kwa niaba yao.
Adv. Kilatu: Lissu alipeleka orodha ya mawakili wa kumtembelea?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sahihi.
Adv. Kilatu: Kuruhusu watu kumuona sio lazima wawepo kwenye orodha?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio kuna mazingira alikuwa anaomba Lissu mwenyewe.
Adv. Kilatu: Umeyasema mazingira hayo kwenye kiapo chako au kuna siku Lissu aliomba mtu ambae hayupo kwenye orodha ili amuapishe aingie.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijasema kwa kiapo changu.
Adv. Kilatu: unajua maana ya retainership ya mawakili kwa mteja uliyoisema kwenye kiapo chako.
Ntamamiro (Bwana Jela): Sijui ila uliza swali tu.
Adv. Kilatu: Basi tutarudi hapo kama hujui.
Soma paragraph nyingine hapo umesema shauri hili lilipaswa kuwa judicial review sio la kikatiba?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sahihi.
Adv. Kilatu: Una uelewa wowote kuhusu Judicial Review?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sina uelewa wa hili.
Adv. Kilatu: Basi sitakuuliza kwenye hilo nikuache.
Sasa nenda kwenye originating summons soma ibara za Katiba zilizotajwa humo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : zipo ibara ya 13 na zingine.
Adv. Kilatu: Asome ibara ya 30 aielewe halafu nimuulize swali.
Jaji: Asome au ajisomee?
Adv. Kilatu: Ajisomeee mwenyewe aelewe halafu nimuulize swali.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Tayari
Adv. Kilatu: Je ibara hiyo inasema mtu anaweza kuja kwa judicial review mahakamani kupitia ibara hiyo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hapana.
Adv. Kilatu: Soma para 4 ya kiapo chako kuwa ulimkataaa Kisabo kwasababu sio wakili wa Lissu?
Ntamamiro (Bwana Jela): lakini baadae lissu alileta ombi maalamu.
Adv. Kilatu: Sasa muambie Jaji hiyo paragraph nyingine uliyosema kulikuwa na ombi maalumu ni paragraph ya ngapi?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Haipo.
Adv. Kilatu: Sasa ili wakili aingie gerezani ni lazima kuwepo na orodha ya mawakili iliyoandikwa na mfungwa.
Ntamamiro (Bwana Jela): Utaratibu ni kukagua kitambulisho na kumruhusu.
Adv. Kilatu: Sasa kwenye kiapo chako ukimjibu Maduhu unasema kulikuwa hakuna proof of retainership? Hiyo ndio requirement ya sheria?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Nafikiri sifahamu.
Adv. Kilatu. Nimemaliza. Mh. Jaji.
Jaji twende mapumnziko kwa nusu saa.
Tukutane hapa baada ya dakika 30.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 24
Anaendelea John Seka
Seka Anamuongelesha anasema unanisikia au hunisikii. Anatumia sauti ndogo sana. Umenisikia?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nakusikia
John Seka: Pale ofisi ya Admission si kuna Meza?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Ukubwa wa meza zilizopo hapo admission ukoje?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sikumbuki.
John Seka: Katika maisha yako uliwahi kumuona wakili na mteja wake gerezani wanaongea?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Huwa wanakaaje?
Ntamamiro (Bwana jela) : Wanakaa kutazamana katikati yake kuna meza?
John Seka: Sasa narudi hapo. Kabla ya kesi hii uliwahi mfahamu Nashon Nkungu, Paul Kisabo?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nimewahi kukutana nao.
John Seka: Ulikutana nao wapi? Katika mazingira yapi?
Ntamamiro (Bwana jela) : Akija kuongea na mteja wake gerezani.
John Seka: Ulituambia stage za wakili akifika. Anaandika jina nje, kitabu kinaletwa kwako. Unaruhusu. Sasa tuambie unamuona wakati gani?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ofisi zote ni zangu.
Jaji: Jibu ni wapi hapo Gerezani?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nilikutana nae Kwa Recha.
John Seka: Kumbe hata Kisabo ulimfahamuje?
Ntamamiro (Bwana jela) : hivyo hivyo kumuona akizungumza na mteja.
John Seka: Umewahi kuwaona wakifanya mahojiano?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio
John Seka: Umekumbuka wakati Lissu anafanya mahojiano nani na nani anakuwa ndani?
Ntamamiro (Bwana jela) : Wanakuwa nje wote. Lakini wanachungulia kwa mlangoni.
John Seka: Unakumbuka tarehe ipi na ipi ulikuwepo na ipi haukuwepo?
Ntamamiro (Bwana jela) : Siwezi kukumbuka.
John Seka: Sasa nitakupitisha tarehe moja hadi nyingine?
Jaji: Amesema hakumbuki nafikiri huko muache acha libaki hivyo.
John Seka: Nitakuwa sahihi nikisema wewe hujawahi hudhuria majadiliano kati ya Lissu na mawakili wake?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio
John Seka: Mengi yaliyotokana na hayo wewe hukuwa unahusika moja kwa moja zaidi ya mrejesho.
Ntamamiro (Bwana jela): sio lazima feedback
John Seka: wewe hujawahi hudhuria mazungumzo ya Lissu na wanasheria wake. Huwa unapita tu. Unayoyaona.
Ntamamiro (Bwana jela) : nakagua napita.
Jaji: Hebu sikia kati ya wewe na hao akina Recha, Mumbii anaeweza kuelezea?
Ntamamiro (Bwana jela): Ni sahihi.
John Seka: Sasa tutajie majina yake.
Ntamamiro (Bwana jela): Siwakumbuki.
John Seka: Wakati wote maelekezo yako yalikuwa yanafuatwa ukiwaagiza kwenda kusimamia?
Ntamamiro (Bwana jela) : Mimi ni Mkuu wa Gereza sio lazima niambiwe feedback naweza kujua kwa namna nyingine.
John Seka: Kumbe ulijua kuwa mahojiano na Lissu na mawakili wake yamefuata taratibu kupitia mbinu zako zingine.
Ntamamiro (Bwana jela) : ndio
John Seka: Hao waliokufikishia hizo taarifa au hizo mbinu zako zingine umezielezea kwenye kiapo chako?
Ntamamiro (Bwana jela) : Hapana.
John Seka: Paul Kisabo na Nashon Nkungu. Wakiwa kwenye mahojiano kunakuwa na askari wanakaaa kulia na kushoto kwa Lissu na Kwa Nashon na kisabo nyakati zote.
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli.
John Seka: Ulikuwepo muda wote mahojiano yanapofanyika?
Ntamamiro (Bwana jela) : Napata taarifa kupitia vyanzo yangu.
John Seka: Nimemaliza Majaji. Aendeleee Edson Kilatu.
Anasimama Wakili Edson Kilatu
Adv Kilatu: Ukifika ukonga getini kuna kitabu cha ku register magari?
Ntamamiro (Bwana jela): Sahihi
Adv Kilatu: Anayeshughulikia registration zote sio wewe kwenye vitabu vya kuingia vya magari, raia wa kawaida na kitabu cha mawakili?
Ntamamiro (Bwana jela): Ni sahihi
Adv. Kilatu: Ni sahihi hakuna kiapo cha mtu anayesimamia hizo registration pale Ukonga? Hakijaja hapa mahakamani.
Ntamamiro (Bwana jela) : Hakipo.
Adv. Kilatu: Hii Register book uliyoileta hapa Mahakamani SUPP 1,2,3 ni nyaraka ya magereza hakuna sahihi za mawakili mle. Ni nyaraka yenu tu.
Ntamamiro (Bwana jela): sahihi
Part 25 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 20.
Mhe. Lissu anaendelea kumshona Shaidi ambae ni Mkuu wa Gereza, Ntamamiro (Bwana Jela)
Mhe. Lissu: Wakati wote mawakili wakija gerezani, simamia, wapekuliwe na wamepekuliwa. Swali ni kwamba ni je wewe Bwana jela wa Ukonga unawashuku na una wasiwasi na mawakili 37 waliokuja kuona wateja Ukonga? Kumbuka kanuni inasena ili uwasearch ni lazima uwe na wasiwasi nao.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sitegemei kanuni.
Mhe. Lissu: Sasa twende kwenye sheria yenyewe kwenye Prisons Act kuwa unaweza kusearch mgeni kama hautakuwa na wasiwasi nae? Kifungu gani hicho?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Waheshimiwa Majaji mtu yeyote anayeingia Gerezani awe mfungwa au mahabusu lazima apekuliwe.
Mhe. Lissu: Lazima apekuliwe?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Yuko kimya.
Mhe. Lissu: Kama kweli ni lazima. Twende kwa Mawakili wa Serikali waliokuja Ukonga kama uliamuru wapekuliwe. Twende kwa hao sasa. Wah. Majaji SUPP 4 tarehe 19/11/2025 nenda haraka tumalize hii ngoma. Na Tarahe 21/01 mwaka huu.
Ntamamiro (Bwana Jela): Kila anayeingia lazima akaguliwe.
Mhe. Lissu: SUPP 4 inasemaje kuhusu Tarehe 19/11 walikuja mawakili wafuatao Debora Mushi kutoka NPS, Caroline Nana kutoka NPS pia, Cleoface Leonce ambae ni investigator na alikuja Justo Dimba au Simba kutoka kwa ZCO. na mwingine kutoka DCEA. Wote hawa shida walioijia gerezani walikuja kuongea na mahabusu. Maoni yako ukasema nini? Wasomeee majaji.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Wasikilizwe kwa utaratibu.
Mhe. Lissu: Wakija mawakili wengine simamia mazungumzo yao, wapekuliwe, wapekue, Simamia kwa ukaribu. Lakini wa serikali wakija wasikilizwe kwa utaratibu.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Mawakili 37 wote nipe mfano mmoja tu w wakili uliyesema asikilizwe kwa utaratibu.
Ntamamiro (Bwana Jela): Naomba Tar. 20/01 wakili hapo nimesema SIMAMIA.
Mhe.!Lissu: Ahsante sana. Sasa kwa mawakili wa serikali wapi hata mara moja umeandika SIMAMIA?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio lazima niandike.
Mhe. Lissu: Wabelgiji nilipokaa wanasema Papiere yaani Paper. Tunaenda na maandishi. Onesha maandishi acha rongorongo maneno mengi unatumalizia.
Sasa angalia majina yanayofuata. Hapo kuhusu mawakili wa serikali.
Ntamamiro (Bwana Jela): Niliandika Waletwe.
Mhe. Lissu: Maafisa wa Madawa ya kulevya na Mawakili wao waliokuja 28/11 kazi yao ni kutukamata na kutupeleka Mahakamani ndio unaosema wasikilizwe?
Ntamamiro (Bwana Jela): Hatoi jibu.
Mhe. Lissu: Hawa watu ni watumishi wa serikali kama wewe?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli
Mhe. Lissu: Wanalipwa mshahara wa serikali kama wewe?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio lakini.
Mhe. Lissu: Lakini utawapa mawakili wa serikali.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hawa mawakili wa serikali huwa wanakuja kuongea na wote?
Mhe. Lissu: tuambie ni wapi umeandika kuwa walikuja kuongea na wote.
Ntamamiro (Bwana Jela) : sijaandika.
Mhe. Lissu: Ni sahihi kuwa kuna wakati nyaraka zinakataliwa na zinazokubaliwa lazima mseme zote. Kweli sio kweli mnafanya hivyo kwa mawakili wangu.
Ntamamiro (Bwana Jela) : sio kweli zinasomwa. Ila zinakaguliwa.
Mhe. Lissu: la kwamba zinakataliwa pia?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Katika nyaraka ambazo zinaletwa kwangu ni pamoja na hotuba ya Chande ya matukio ya tar. 29/10?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Lissu: Shahidi Paul Kisabo amesema wiki iliyopita Tar. 14/07 alikuletea waraka unaotoka common wealth kuwa niachiliwe ndani ya siku 30 na mliposoma mkakataaa.
Bwana Jela: Sio kweli.
Part 21 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 19
Mahakama Imerejea.
Majaji wameingia.
Wakili wa Serikali amesimama kujitambulisha anaitwa Narindwa Sekimanga.
Shaidi Mkuu wa Gereza nae yuko pale kizimbani yeye muda wote amekaa tu pale kizimbani.
Hajajihangaisha kusimama labda kwa vile ni mrefu na hicho kitambi anachoka kusimama pengine.😂
Jaji Mruma: Shaidi nakukumbusha bado uko chini ya kiapo.
Mhe Lissu: Sasa turudi kwa viongozi wangu wa Chama uliowakatalia wasije kuniona kule Gerezani. Angalia majibu yangu na uangalie kiapo kinzani kuhusiana na kiapo kinzani nilichomjibu Kisabo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ametoa macho. Hafanyi lolote.
Mhe. Lissu: Mawakili wa Serikali mnafanya nini si mumsaidie shahidi wenu azione hizo nyaraka naona ananiangalia tu.
Wakili wa Serikali anaenda.
Mhe. Lissu: Hizo aya kwenye kwenye kiapo changu kinzani zinaonesha namna ulivyowazuia viongozi na wanachama ikiwemo mashahidi na mawakili watatu ambao ni Dickson Matata, Deogratias Mahinyila na Gaston Garubindi. Swali langu waeleze majaji kama umewahi kupinga haya maelezo yangu yaliyopo kwenye kiapo changu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Waheshimiwa Majaji nimeshalijibu hilo.
Jaji: Umeelewa swali lake kweli.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sina jibu.
Mhe. Lissu: Nalo ni jibu pia. Haya kwenye aya ya nne wewe umefanya kampeni ya muda mrefu ya wewe na mlalamikiwa wa pili kamishna mkuu mmehakikisha nashindwa kujitetea wala kuandaa utetezi wangu na matukio nimeyasema kwenye para H na Y. kwamba umewazuia mawakili wangu watatu ambao Ni Mahinyila, Matata na Garubindi kama umewahi kujibu hili.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli nimewazuia.
Mhe. Lissu: Je umeleta supplimentary affidavit? Au majibu yoyote kwenye jambo hilo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : anatoa macho. Anashika makaratasi na kuyaacha.
Jaji: Umeelewa swali?
Mhe. Lissu: Ulileta counter affidavit mara ya kwanza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio
Mhe. Lissu: Baadae ukaleta suplimentary affidavit?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
Mhe. Lissu: Sasa kwenye hizo nyaraka zako mbili kuna mahali kokote ulijibu tuhuma za kuwa umewazuia mawakili wangu na viongozi wa Chama?
Ntamamiro (Bwana Jela) : sijajibu.
Mhe. Lissu: Tuhuma dhidi yako na maafisa wako kusearch mawakili na nyaraka zao kisheria. Jibu swali kwamba waleta maombi wote watatu wamesema wanasearchiwa, wanakaguliwa na kusomwa hizo nyaraka.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Reg. 17(2) ya kanuni za Magereza inasemaje?
Anatafuta hiyo kanuni.
Mhe. Lissu: Ni kweli mgeni anayekuja Gerezani kutembelea mfungwa atasachiwa endapo atakuwa na wasiwasi na huyo mgeni?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Haya isome sasa
Ntamamiro (Bwana Jela) : A prison officer when has any ground suspiciously may direct to search that visitor. Anasoma kingereza kibaya sana.
Mhe. Lissu: Any ground for suspicion may search or cause to search. Kumbe ataamuru asachiwe kama atakuwa na sababu za kumshuku?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Mgeni ataambiwa aondoke akikataa kusachiwa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kwa mujibu wa kanuni hii ni kweli.
Mhe. Lissu: Anayemfukuza atatakiwa kuandika sababu za kumfukuza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : yuko kimya tena. Hebu rudia swali.
Mhe. Lissu anarudia swali. Si ni lazima uandike sababu za kumfukuza.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Siku mjibu maombi wa Kwanza alipokataliwa kuingia gerezani tar. 28/11 alipokataliwa kuingia gerezani iliandikwa sababu kuwa amekataa kusachiwa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kwa kanuni hii.
Mhe. Lissu: Tutajie kanuni hizo zingine tuzione? Kwenye kanuni kuna sababu yoyote nyingine kwa mujibu wa kanuni?
Bwana Jela: Sijaipitia kanuni yote.
Mhe. Lissu: Sasa mimi niliyepitia kanuni zote na hakuna sababu nyingine unasemaje?
Bwana Jela: Sina jibu.
Part 20 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
‼️🚨BASHITE NA UTAPELI NI PETE NA KIDOLE‼️
Huyu jamaa hajawahi kufanya jambo la maana zaidi ya kuua na kuteka! Sasa baada ya kushiriki njama zote ovu anasimama na kutangaza kambi ya tiba Arusha na kumsingizia Mungu huku akiwa wamechangia watu kuwa wajane na wamama kupoteza vijana wao kwa utekaji na mauaji yake
Lakini sasa mdau amedokeza kuwa kuna madawa pia yame expire kutoka pharmacy za marafiki zake!
Ni hatari sana mambo haya! Ila #TutaelewanaTu mbona?
"Hili zigo tunalibebesha kwa Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es salaam na Mkoa wa Kipolisi wa Ilala na wilaya zake zinazohusika na eneo hilo la Mahakama hizi mbili, za Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa." Mhe. @jjmnyika
‼️MPANGO WA JESHI LA POLISI DHIDI YA CHADEMA‼️
Kama mtakumbuka siku kadhaa zilizopita ilisambaa taarifa kuhusu Jeshi la Polisi kuvamia nyumbani kwa Yoramu Mbyela (Huyu kwenye picha) ambae ni mfanyabiashara anaeuza vifaa vya CHADEMA ikiwemo matisheti, bendera, madera, kombati, n.k
Polisi wakiwa na gari aina ya FUSO walivamia nyumbani kwake, wakamlazimisha mke wa Mbyela afungue duka, kisha wakabeba na kuondoka na mzigo wote wa vifaa vya CHADEMA ambao waliukuta dukani kwake.
Mke wa Mbyela pamoja na Wakili wao wamefuatilia huo mzigo wao, Polisi wakarudisha baadhi ya vitu lakin mzigo mkubwa wakakataa kurudisha mpaka leo bado wamebaki nao.
Sasa nimejulishwa kwamba Jeshi la Polisi wamebaki na huo mzigo kwasababu wanampango wa kuutumia kufanikisha mpango wao dhidi ya CHADEMA hii ni kutokana na hofu waliyonayo kuhusu Maandamano ya 7/7 yani Julai 7, 2026.
Wamepanga kuwavalisha nguo za CHADEMA watu wao ambao ni Green guard, UVCCM na baadhi ya migambo kisha watawapeleka huko porini ambapo badae Polisi watajifanya kwamba wamevamia eneo hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa Wananchi kwamba waliona kuna kundi la watu ambao hawajui ni akina nan.
Baada ya Polisi kuvamia eneo hilo watautangazia umma kwamba Vijana wa CHADEMA wamekamatwa huko porini wakiwa wanapewa mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya Maandamano ya Julai 7 ili Msajili apate sababu ya kuingilia kati aseme kwamba CHADEMA imevuja sheria ya vyama vya Siasa maana Sheria ya Vyama vya Siasa ilipiga marufuku vikundi vya ulinzi na mafunzo ya kijeshi mwisho wa siku CHAMA kinaweza kufutwa.
Lakin pia Jeshi la Polisi litakuwa linawavalisha UVCCM hizo nguo za CHADEMA kisha wanawatuma kwenye mikutano ya hadhara ya CHADEMA kufanya fujo ili ionekane CHADEMA wanagombana wao kwa wao.
Sasa ni muhimu sana Wanachama wenzangu mnapoenda kwenda Mikutano, hakikisha unamtambua mtu ambae umekaaa nae jirani ukiona kuna mtu/watu huwaelewi toa taarifa kwa Viongozi wa CHAMA, hawa wahuni wakivamia mikutano yetu inatakiwa muwape HAKI YAO YA KIKATIBA.
Nimepokea taarifa ya kukamatwa kwa SAILENCE MWAKASALA Mwenyekiti wa CHADEMA Student Organization mkoa wa Mwanza mchana huu, Polisi 5 mmoja tu ndiye aliyevalia sare wakiwa na mitutu ya bunduki wamevamia nyumbani kwake na kumchukua kwa nguvu. Tunaendelea kufuatilia kila hatua.
‼️ALERT‼️
Thobias Mwesiga kamtumia mtu ujumbe eti aje kuniambia kwamba niache kuandika madudu yake eti nikiendelea yeye “atamwachia Mungu” so nisije kumlaumu.
Mie naelewa hapo anaposema kwamba atamwachia Mungu hamaanishi Mungu huyu wa Mbinguni maana tangu yeye na wenzake ambao huwa anawatumia kuteka walipoanza kuteka, kupoteza na kuuwa watu kuna namna wanajihisi kwamba na wao ni miungu watu so ni wazi kwamba kuna jambo baya anapanga dhidi yangu ndo maana anasema kwamba nisijekumlaumu.
Sasa mkisikia nimepatwa na jambo lolote baya iwe kutekwa/kupotezwa au kuuwawa basi muhusika wa atakuwa ni huyu Thobias Mwesiga, na ujumbe wake nimeutunza lakin pia nimewapa Mawakili wangu wautunze incase ikitokea chochote.
Mliokaribu nae mwambieni hasira na stress zake za kuporwa mabilioni ya pesa ambayo watu wa Gavoo haram waliyakuta ndani kwake baada kumsearch alivopiga mabilioni ikiwemo za project ya CHAUMA atafute wa kumpelekea.
Halafu watu wa Goba naomba mnitumie picha za yale maAppartment ya Mwesiga ambayo alianza kujenga baada ya kuwaliza CHAUMA bilioni 15 ambazo Serikali haram ilitenga kwa ajili ya project ya kuhamisha “watu wa Mbowe” kutoka CHADEMA kwenda CHAUMA.
Ni muhimu watu wajue ili hata wakiamua kupanga wajue kabisa kwamba wamepanga nyumba za muuaji.
BUNGE LA ULAYA limepiga Kura ya ndio-kunyima Misaada kuja Tanzania.
Wanatoa misaada kwa Tanzania wakiamini ni nchi ya kidemokrasia na zinakuja kukuza mahusiano mazuri kati ya wananchi na SERIKALI.
Wamekuja kugundua PESA ZAO na KODI za wanachi wao hazifanyi yale ambayo wanatarajia, zaidi zinakuja kutumika kama FIMBO kuadhibu watanzania.
Hivyo kwasasa PESA za ULAYA kuja bongo SAHAU. Ndio maana mnaona DIKTETA JIKE limeenda kwa Putin kupata angalau pakupumulia.
Nakukumbusha tuu DIKTETA JIKE bado ndio kunakucha. MAREKANI anafuata kupiga NDOIGE ya shingo jiandae hatujamaliza.
Huwezi kuuwa ndugu zetu ukatutawala kwa amani NEVER. Lazima ulipie maovu uliyofanya kwa watanzania.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Muswada hu unaipa Marekani mamlaka ya kuchunguza na kutengeneza orodha ya viongozi wa Tanzania wanaotuhumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu, na mara nyingi hatua kama hizi zinaweza kupelekea vikwazo kama: Kufungiwa visa
Kufungiwa mali
Kuzuiwa kufanya biashara au safari Marekani
Sijashangaa jana CHALAMILA kumtetea MAFWELE kwenye utekaji-hawa wote walihusika kwenye UTEKAJI WANGU.
Mnaokumbuka story yangu ya KUTEKWA hawa wote niliwataja na leo mmoja katoka hadharani kumtetea mwenzake.
CHALAMILA, MURILO , MAFWELE , GEORGE hawa ndio KUNDI kuu la utekaji Dar