BINTI NA KATIBA.
Live Jumamosi kupitia TikTok kuanzia saa Mbili kamili Hadi saa Tatu kamili Usiku, mabinti watajadili masuala mbalimbali yanayohusu katiba.
Usipange Kukosa.
https://t.co/K1wQrZ6Y8b
@BavichaQueens
BINTI NA KATIBA.
Live Jumamosi kupitia TikTok kuanzia saa Mbili kamili Hadi saa Tatu kamili Usiku, mabinti watajadili masuala mbalimbali yanayohusu katiba.
Usipange Kukosa.
https://t.co/YG2YtWOxW3
@BavichaQueens
“Upinzani dhidi ya Ukandamizaji ni utiifu kwa Mungu”.
“(Resistance to Oppression is obedience to God)”
Kauli Mbiu inayoongoza Maisha ya Tundu Antipas Mughwai Lissu.
Mtumishi wa Mungu huyu.
Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mwanga na Mjumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA Taifa, Lembrus Mchome, ameibua maswali kuhusu tofauti ya hatua zinazochukuliwa dhidi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, na Makamu Mwenyekiti John Heche.
Mchome amesema CHADEMA inalenga kuiondoa CCM madarakani kupitia mifumo ya kikatiba, hivyo chama kinahitaji viongozi wenye uthubutu, weledi na dhamira ya dhati ya kutekeleza lengo hilo.
Amesema amefuatilia kauli zilizowahi kutolewa na Lissu na
Heche, akidai zinafanana kwa baadhi ya vipengele, huku Lissu akikabiliwa na kesi ya uhaini wakati Heche akiendelea kuwa nje.
Mchome amehoji sababu za tofauti hiyo, akirejea pia tukio la mwaka jana ambapo Heche alikamatwa Dodoma na baadaye kuachiwa. Amehoji kwa nini Lissu anaendelea kuwa ndani wakati Heche yuko nje.
Aidha, Mchome ametoa wito kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA kuendelea kusimamia mwenyekiti wao na kutafuta njia za kisheria kuhakikisha Lissu anapata haki, huku akitaka pia wanachama kujiuliza kuhusu msimamo na dhamira ya viongozi wao katika kuiondoa CCM madarakani.
I welcomed my son from Tanzania, Abdul Halim Hafidh Ameir and his delegation at State House Entebbe.
We discussed investment opportunities and how the private sector can continue contributing to the growth and development of our two countries.
@Sativa255 Kuosha fedha chafu
Nyumba anajenga mwenyewe nyuma ya pazia na ananunua mwenyewe kwa fedha nyingi za halali
Watu wanamagunia ya fedha ndani na hawajui waziingize vip katika mzunguko
Uko kwenye biashara ya madini ndo balaa watu wanauza madini hewa kwa mabilioni
Kwa wasio jua mtu huru alilambishwa tenda ya kutengeneza nguzo za zege za umeme nchi nzima
Siasa biashara imepita na damu za vijana wetu wengi sana na kwakweli leo tumekumbushwa machungu yasiyo elezeka
Ipo siku
Mzee @freemanmbowetz
Wanyama wa porini huua/kupigana kwa sababu zinazohusiana na mahitaji ya kuishi: chakula, kujilinda, kulinda watoto au eneo. Simba anawinda kwa ajili ya chakula siyo mateso, chuki, kisasi
Binadamu ni viumbe katili zaidi ya wanyama. Binadamu anaweza kumdhuru mwingine kwa sababu ya chuki, ubaguzi, tamaa, kulipiza kisasi, madaraka au kwa sababu anaona mwingine hafai kuishi
Kutoka Mikocheni kwenda ilipo Mahakama Kuu ya Tanzania ni umbali usiozidi 5KM. Kutoka Mikocheni kwenda Rufiji ulipo mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ni umbali wa 260KM
Unaweza kusafiri kwenda mkoa mwingine kwa zaidi ya saa tano kuhudhuria shughuli za Serikali katili ya CCM lakini huwezi kutumia dakika 10 kutoka kwako kwenda Mahakama Kuu katika kesi ya TAL?
Huwezi kwenda safari ya 5KM kumuona Mwenyekiti wako wa chama, aliyerithi kiti chako katika uchaguzi HURU na HAKI lakini unaweza kwenda 260KM kuungana na watesi wa Mwenyekiti wako?
Nini muhimu zaidi kwako? Ni wewe ulitueleza miradi ya maendeleo haiwezi kuwa mbadala wa haki za binadamu. Leo kuna watu wanatekwa na kupotezwa, wanashtakiwa kwa ugaidi na uhaini. Hujui?
Lakini umechagua nini? Nimekusikiliza ukisema “mradi wa JNHPP usichukuliwe kisiasa kwa kuwa ni mradi unaokwenda kusaidia uchumi”. Umesahau ulitueleza nini kuhusu miradi ya MAGUFULI?
Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe kwa sasa ni ‘mjumbe wa kudumu wa kamati kuu ya CHADEMA - ni kutokana na hiki kinachoitwa ‘ustaafu’ wa uenyekiti wa CHADEMA Taifa
Kwa maana kwamba, Freeman Mbowe yupo katika kundi sogozi la WhatsApp na mengine (kama yapo) ambayo wajumbe wa kamati kuu wanajadili kwa hisia zao tofauti masuala mbalimbali ya chama
Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu CHADEMA huwezi kwenda Mahakamani katika kesi ya kiongozi wa chama, lakini unaweza kwenda katika shughuli zinazoongozwa na mwenyekiti wa CCM
Freeman Mbowe umesahau, wakati ukishtakiwa kwa makosa ya uongo ya UGAIDI, Tundu Lissu alikuwa Belgium akijiuguza majera ya risasi. Aliomba kukutana na Rais alipokuwa Brussels
Pamoja na mambo mengine waliyokubaliana, alisema Mwenyekiti Freeman Mbowe aachiwe ndiyo tufungue ukurasa mpya. Tundu Lissu alitujulisha mwenyewe hayo alipozungumza na umma.
Tundu Lissu akiwa na siku 500 gerezani. Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe hujawahi kukanyaga Mahakamani kuanzia Kisutu hadi Mahakama Kuu hata kwa bahati mbaya.
Saa 24 baada ya Mahakama Kuu kusema Tundu Lissu ana kesi ya kujibu katika mashtaka ya UHAINI ya uongo na uzandiki, Freeman Mbowe unaibuka katika shughuli za Serikali ukiwa na MAWAZIRI.
Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CHADEMA umekataa kabisa kuhudhuria shughuli zozote za CHADEMA lakini unaweza kuhudhuria shughuli unazoalikwa na WATAWALA KATILI wa CCM.
Unahudhuria shughuli za Serikali umeongozana na mawaziri wa Serikali katili ya CCM wakati ambao wanachama na wafuasi wa CHADEMA kwa mamia wamekamatwa na kushtakiwa kwa UGAIDI?
Mzee Freeman Mbowe umesahau haraka. Kuna watu walifungwa gerezani, wengine sasa ni walemavu, wengine sasa ni marehemu kwa sababu ya kupigania jina lako ukiwa kiongozi wa chama chetu.
Umesahau, wakati unakamatwa na Serikali katili ya CCM, 2021, wanachama wa CHADEMA walikwenda kuonyesha ‘solidarity’ na wewe pale KISUTU. Walikamatwa, wakashtakiwa, wakafungwa
Najutia zile siku nilisimama nawe, kukutetea na kunadi jina lako kwa nia njema kabisa nikifikiri unapambania uhuru, haki na mabadiliko ya kweli. Haikuwa hivyo. Ulitudanganya tukishindwa.
Nasema kwa kuwa kwa hiari yangu, niliamua kusimama nawe, kukunadi katika mazingira ambayo ilionekana ni kama kuuza kitimoto Mecca. Lakini sikutarajia tukishindwa, tuisaliti CHADEMA
Wengine sasa tumeelewa kwa kuchelewa sana. Hii chuki haiwezi kuwa ya kushindwa uchaguzi. Lazima kuna mafekeche mengine. Kuna kingine kimeujaza chuki moyo wako. Je, kuna mrija, umekatwa?
Najutia kumpa mtoto wangu jina lako, Freeman.
"Jana Stephen Wassira alisema kwamba hatutamsamehe Mhe. @TunduALissu kesi itaendelea, hatutamsamehe kama tulivyomsamehe @freemanmbowetz, Wasira alikuwa wamewasiliana na hao majaji? tunataka atuambie hayo maneno ameyatoa wapi." Mhe. @HecheJohn
Mimi na ndugu yangu @Mwinshehe07 tulikuwa mahakamani kufuatilia mwenendo wa shauri la UHAINI linalomkabili Tundu Antipas Mugwai Lisu.
Shauri Bado linaendelea, Tundu Lisu anapinga Mapingamizi ya serikali juu ya mashahidi aliowataja.!!
Leo ni siku muhimu kwa Tanzania na wapenda haki Duniani.
Asanteni Wananchi na wanachama wa CHADEMA kanda ya Pwani kwa kujitokeza ktk kushuhudia siku hii ya kihistoria.
Mwenyezi Mungu amtangulie Tundu Antipas Lissu.