Siku kama ya LEO 24.06.2024 ndio mwanangu alianza kunisaka mtaa kwa mtaa, mitandaoni kushirikiana na watanzania bila kuchoka.
Familia ilibidi isafiri kutoka MBEYA kuja Kuweka kambi Dar kwaajili ya misako ya usiku na mchana, bila kusahau maombi ya KUFUNGA NA KUOMBA kwa pamoja.
Wazazi na watanzania mlijua kunipambania, leo ni miaka miwili na haya yote yapo bado kichwani mwangu na sitamani yajirudie, ndiomaana nakuwa mkali sana kuhusi UTEKAJI maana najua familia zinateseka kwa kiasi gani.
Leo vijana tumeamua kufanya hili dogo kwa wazazi, kama kuwapa FARAJA za mapambano yote waliyoyafanya kwetu.
Zamani hizi zilikuwa NDOTO, leo ni maisha ya kweli tunayoyaishi—ASANTE MUNGU hata kwa hii nafasi.
S/o kwa mwanangu JAMES (Taivina) kwa kuendelea kuwepo kwenye maisha yangu, wewe ni tafsiri ya NDUGU.
TUISHI.🫡
@Sincerelyrahma7 Hii story imekaa kiuongo uongo lkn pia huyo mwanamke seems lke anatako kubwa, na mwanaume ni fala bila shaka anatokea pwani zone huyo.