Ukiongea na Bodaboda wenye miaka 35 na kuendelea kuhusu mustakabali wa badae; unajifunza kitu. Mosi, wamejikongoja kupeleka watoto shule za โprivateโ; wakiwa na ndoto watoto wao na wasije kuwa โbodaboda kama mimiโ. Pili, wana hofu kuhusu Usalama wa kazi yenyewe, hivyo hawaendeshi โhovyoโ kama Gen-Z. Lakini, wanawaza Kustaafu tayari; kwa maana wamejipanga kubadili kazi; au kuajiri vijana wenzao. Aidha, baadhi wanaanza kuona umuhimu wa โkuacha pombeโ na โuselaโ! Ni hadithi ya umri na mabadiliko ya tabia pamoja na umuhimu wa kuwa na ndoto zinazotekelezeka.
Hatulindi mahusiano kwa kuzikana hisia zetu. Hatulindi mahusiano kwa kunyamaza tunapoumizwa wala kuigiza nyuso za amani.
Kelele ni busara za mwenye uchungu.
Unachoita โmatusiโ kwa aliyeumia ni tiba.
Kimya hufunga uchungu.
Kimya sio amani ni sumu.
Ukitumia nguvu kubwa kuficha uchungu, unaweza kuleta utulivu unaochachusha kidonda cha hisia. Kadri muda unavyoenda utulivu hugeuka mbolea ya chuki, hasira, visasi na mgogoro mgumu kuutatua baadae.
Kwa nini vidonda vya tumbo (Peptic Ulcer Disease โ PUD) vinaongezeka sana siku hizi?
Kwanza ni matumizi ya dawa za maumivu kupita kiasi na bila ushauri wa daktari (Painkillers / NSAIDs). Dawa kama diclofenac, ibuprofen, aspirin n.k. zinapunguza ulinzi wa asili wa ukuta wa tumbo na kufanya ile acid ikimwagika inachoma ukuta wa tumbo na kusababisha vidonda.
Pili ni maambukizi ya bakteria anaitwa Helicobacter pylori (H. pylori). Huyu bakteria akimuingia mtu, anaishi tumboni na huzalisha kemikali zinazoharibu ukuta wa tumbo.
Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa sehemu kubwa ya Watanzania wana H. pylori bila kujua, kwa sababu wengi hawapimi (H. pylori test).
Tatu ni msongo wa mawazo (Stress)
Msongo wa mawazo unaongeza uzalishaji wa tindikali (acid production) tumboni ambayo huchoma tumbo na kusababisha vidonda.
Nne ni ulaji usio sahihi (Poor eating habits). Watu wengi hawali kwa wakati, wanakula vyakula vya kukaanga, mafuta mengi, pilipili, kahawa nyingi, soda, au energy drinks. Tumbo linazidi kutoa tindikali bila chakula cha kuipooza maana vyote hivi juu vinatengeneza tindikali (asidi), matokeo yake, maumivu na vidonda huongezeka.
Mwisho ni Kutotibu kwa usahihi (Incomplete treatment). Wengi wakiumwa wanakimbilia dawa kama omeprazole au magnesia bila kupima.
Dawa hizo hupunguza maumivu kwa muda, lakini hazimalizi tatizo.
Kama chanzo ni H. pylori, lazima itibiwe kwa dawa maalum za antibiotics
Iko hivi,
Kukakola moja yenye mls 350 ina takriban gramu 39 za sukari, sawa na vijiko 10 vidogo vya chai vya sukari.
Funta Chungwa yenye mls 350 ina takriban gramu 44 za sukari, sawa na vijiko 11 vidogo vya chai vya sukari.
Pipsi yenye mls 350 ina takriban gramu 41 za sukari, sawa na vijiko 10โ11 vidogo vya chai vya sukari.
Upande mwingine, chai unayoweka vijiko vidogo, kawaida vijiko vidogo 1 mpaka 3, vina takriban gramu 8โ9 za sukari tu.
Mpaka hapa utaona chai ni bora zaidi kuliko soda, kwa sababu ina sukari kidogo sana na haina madhara makubwa ikiwa inakunywa kwa kiasi.
Sasa utamu upo hapa, hizi sukari zinatofautiana, hapa ndipo madhara ya soda yanaonekana.
Sukari iliyopo kwenye soda inaitwa high-fructose corn syrup (HFCS) au sucrose, hii inatengenezwa kutoka kwenye mahindi, ni mchakato mrefu, mahindi yanachemshwa, unga wake unachakatwa na kemikali na ule wanga unabadilishwa kuwa glucose kisha sehemu yake inabadilishwa kuwa fructose, huu utamu wake balaa, ndio sukari ya soda, kifupi soda ule utamu ni kemikali zimechanganywa.
Sasa mwilini hii sukari ya soda huchakatwa na ini, na ukinywa nyingi, yaani zaidi ya unavyohitaji (nguvu unazotunia au mazoezi) ndipo ini hubadilisha kuwa mafuta ili itunze kenye stoo za mwili (nyuma matakoni na tumboni), mtu ananenepa, mafuta yanaongezeka mwilini + sukari na hapo ndipo anasogelewa na magonjwa ya kisukari na moyo.
Sukari ya chai hii tunakoroga yenyewe ni sucrose ya kawaida, yaani table sugar, kwanza tofauti na ile ya soda inayotokana na mahindi hii inatokana na miwa au beetroot, pili hii unakunywa gramu chache tu (8-9) na tatu mwili huitumia sukari hii moja kwa moja kama nishati na hatari ya kubadilishwa mafuta ni ndogo kama unatumia kiasi hiki kidogo.
Kama Bado Hujamwaga Moto kwa Elon Repost, Post Tag arudishe Account
Tag @elonmusk@Support to reinstate @sativa255 (143K followers). He is a human rights defender & victim of political persecution. Silencing him = silencing truth.
@nikitabier share Please
#UnsuspendSativa255 #FreedomOfSpeech
Kama Bado Hujamwaga Moto kwa Elon Repost, Post Tag arudishe Account
Tag @elonmusk@Support to reinstate @sativa255 (143K followers). He is a human rights defender & victim of political persecution. Silencing him = silencing truth.
@nikitabier share Please
#UnsuspendSativa255 #FreedomOfSpeech
@fatma_karume Haya ni maneno makali kutoka kwa mtu ninayemheshimu sana. Rais akitokea Tanganyika sio malaika & hukosea. Na akikosea hukosolewa vikali. Ndivyo nilivyofanya kwa Mkapa aliyenipa kesi ya jinai; Kikwete aliyenipa kesi 3, & Magufuli aliyenipa kesi 6 na risasi 16. Sijaanzia kwa Samia.