HABARI:
Wanaume watatu wamekutwa katika chumba kimoja eneo la Msasani, Kitongoji cha Oloresho, Kata ya Moivo, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, katika mazingira yaliyoibua mashaka miongoni mwa Wananchi.
Mmoja wa Wanaume hao, aliyefahamika kwa jina la Alex Kimario, anayedaiwa kuwa dereva wa bodaboda, alishikiliwa na wananchi baada ya vijana wawili waliokuwa naye kutoroka katika eneo hilo.
Baadhi ya mashuhuda wanadai kuwa Alex alikuwa akiwafanyia Vijana hao wawili kitendo cha ngono kinyume na maumbile, madai ambayo bado hayajathibitishwa na mamlaka.
Akizungumza, Alex ameeleza kuwa vijana hao walimuita ili awapeleke eneo la Kambi ya Fisi, akisema tayari alikuwa amewahi kuwapeleka sehemu mbalimbali zaidi ya mara tatu.
โHawa vijana wameniita kuwapeleka mtaa wa Kambi ya Fisi, nilivyokuja kumbe hawa vijana tabia zao sizijui. Nimeshakuja zaidi ya mara tatu nawachukua na kuwapeleka mahali wanataka,โ amesema Alex.
Kuhusu mafuta yaliyodaiwa kukutwa katika chumba hicho, Alex amesema ni mafuta ya kawaida ya kujipaka ambayo yanaweza kutumika katika sehemu mbalimbali za mwili.
Mke wa Alex aliyefika eneo la tukio baada ya kupata taarifa amesema ameshtushwa na tukio hilo, akieleza kuwa anamfahamu mume wake kama mtu wa dini na mwimbaji wa kwaya.
Balozi wa eneo hilo, Lydia Danieli, amesema analifahamu tukio hilo na kwamba baadhi ya mienendo ya vijana hao ilikuwa imewahi kuwafanya wananchi kuwa na mashaka.
Jeshi la Polisi lilifika katika eneo hilo na kumchukua Alex kwa ajili ya taratibu zaidi za kisheria.
This house does a lot with a simple idea, a roof that becomes the architecture. The deep overhangs, exposed structure and warm materials give it character without trying too hard.