Masikini yupo tayari alinde Sh.2000, lakini apoteze masaaa mawili zaidi.
Kuna namna ni muhimu kulinda muda wako kuliko pesa.
Muda unaweza kukurudishia pesa zako, lakini haziwezi kukurudishia muda wako.
Tumia pesa zako kununua muda wako.
Buy back your time.
Siku Moja Amka Asubuhi…,
Fungua Account Mpya Mitandao Yote Ya Kijamii,
Anza Kupost Biashara Yako Japo 10Posts/Day..
Baada Ya Muendelezo Wa Siku 90 Njoo Hapa Utuambie Umekosa Mteja Hata Mmoja!
Ntakurudishia Gharama Za Bando Lako🫵
Si unaona unavohangaika peke yako hakuna wa kukutia moyo wala wa kukuvusha usiogope pambana sana ili hata siku ukitoboa asitokee mpuuzi mmoja wa kusema bila yeye usingefika hapo, Mwamini Mungu Tu📍📌
Ukituliza akili vizuri, utagundua kwamba una mengi ya kumshukuru Mungu kuliko yale unayoyataka. Mara nyingi tunahesabu tunachokikosa, tukasahau kuhesabu tulichobarikiwa nacho.
Muda mwengine mambo yako hayaendi sababu wewe ni mtu wa matangazo, umeitwa interview ushatangaza, umepata nafasi fulani ushatangaza, umepata kazi ushatangaza yani huwezi kukaa na jambo. Unadhani kila mtu anafurahia mafanikio yako ?. Jitahidi kuwa msiri wa achievements zako.
Tuombe:
Bwana, ninakabidhi wiki hii mikononi mwako.
Nipe nguvu mpya, mawazo mapya, fursa mpya na hekima mpya.
Nisaidie nisiogope mwanzo mpya, bali niupokee kwa imani.
Uniongoze kwenye kila hatua na ufanye kazi ya mikono yangu izae matunda. Amina.🙏🏼