@ErickKamihanda Hata China town ipo katika mji wa Manhattan ambako ndio one of the oldest ever since 1850's. Hapo ukifika Canal, Mott, Bayard streets utakuta chinese restaurants na wachina kibao kama upo China tu. Same as Italians. America haina mwenyewe.
@PinguRahim@kasesco_tz Nimesoma Mlimani toka nursery, primary na nimekulia mitaa ya silent inn miaka ya 80's pale kulikuwa na mikorosho kibao ilikuwa short cut ya kwenda shule. Ukipita kama hujulikani wanakuvua viatu maana jamaa walikuwa wanakula ganja beo wangu walimvuaga raba mtoni 😂
Mizaha sana, watu hawajui El nino sio mvua pekee kuna baa la njaa baada ya El Nino sababu baadhi ya maeneo hayatapata mvua na baadhi yatapata mafuriko hivyo hakuna chakula kitakuwepo aftermarth.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Reuben Kwagilwa amewataka Watanzania kuacha kubeza tahadhari zinazotolewa na wataalamu wa hali ya hewa kuhusu mvua kubwa za El Niño, akisema baadhi ya Wananchi wamefikia hatua ya kuidai Serikali mvua hizo badala ya kuchukua tahadhari dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza.
Akizungumza wakati wa ziara ya Makamu wa Rais mkoani Iringa, Kwagilwa amesema Serikali imekuwa ikitoa elimu na tahadhari katika mikoa 14, lakini baadhi ya Wananchi wamekuwa wakizichukulia taarifa hizo kama ahadi ya mvua zinazopaswa kunyesha.
“Makamu wa Rais, baada ya kuwa tumezunguka mikoa yote 14 kutoa tahadhari hii, sasa hivi tukipita Watanzania wanatudai mvua ya El Niño,” amesema Kwagilwa.
Aidha, amewataka wananchi kuendelea kufanya usafi wa mazingira, kuzibua mitaro na kuhakikisha njia za kupitisha maji hazizibwi na taka, ili kupunguza hatari ya mafuriko na madhara mengine yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa.
#MillardAyoUPDATES