@Kingvannytz_@lil_dee06 Kitaalamu unaweza kuwa umepigwa kama hukujamiana na mwenza wako😂 Lakini kama ulijamiana nae mtoto anaweza akawa wako. Hapo tunathibitisha kwa recessive na dominant allele. Na kwa maelezo yako hapo wewe baba ulikuwa ni Ab na mama ni Bb (heterozygous dominant) hizo bb ndogo ndo O
Baba Yetu uliye mbinguni. Jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo Mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu. Kama nasi tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi. Lakini utuopoe maovuni, Amina🙏
Leo Alhamisi, wabunge wa Bunge la Ulaya (MEPs) wamepitisha azimio linaloitaka Tume ya Ulaya kuondoa pendekezo lake la kutoa ufadhili kwa Tanzania katika mwaka 2026.
Katika azimio hilo, wabunge walikumbusha kuwa mwezi Novemba 2025 Tume ya Ulaya ilisimamisha mchakato wa kuidhinisha ufadhili huo kufuatia wasiwasi mkubwa uliotolewa na wabunge wa Ulaya kuhusu mwenendo wa uchaguzi wa Tanzania wa Oktoba 2025, ambao waliutaja kuwa wa udanganyifu, pamoja na hatua za serikali za kukandamiza kwa nguvu maandamano yaliyofuata baada ya uchaguzi huo.
Kwa mujibu wa azimio hilo, zaidi ya watu 400 waliuawa huku mamia wakikamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya uhaini kufuatia maandamano hayo.
Hata hivyo, wabunge hao walisema kuwa pamoja na wasiwasi huo pamoja na maazimio mengine yaliyowahi kutolewa kuhusu hali ya demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria nchini Tanzania, Tume ya Ulaya imeendelea na mpango wake wa kuidhinisha ufadhili huo wa mwaka 2026 bila kuzingatia kikamilifu hoja zilizotolewa.
MEPs pia walieleza wasiwasi wao kuhusu kuahirishwa mara kwa mara kwa ziara ya ujumbe wa Kamati Ndogo ya Haki za Binadamu ya Bunge la Ulaya nchini Tanzania. Kwa maoni yao, hatua hiyo ni sawa na kukataa ziara ambayo ilikusudiwa kujadili masuala ya haki za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria.
Kutokana na hali hiyo, wabunge hao wanaamini kuwa rasimu ya uamuzi wa Tume ya Ulaya inazidi mamlaka iliyopewa Tume katika eneo hilo na kwamba haiendani na sheria za Umoja wa Ulaya.
Kwa sababu hiyo, Bunge la Ulaya limeitaka Tume ya Ulaya kuondoa rasimu hiyo ya uamuzi inayohusisha msaada wa euro milioni 156 kwa Tanzania na kuwasilisha rasimu mpya. Aidha, limeitaka Tume kuhakikisha kuwa mabadiliko yoyote mapya hayataathiri utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi, ulinzi wa haki za binadamu, demokrasia wala msaada kwa mashirika ya kiraia.
Kwa mujibu wa Bunge la Ulaya, baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025 ambao ulielezwa kuwa wa udanganyifu, serikali ya Tanzania ilikabili maandamano ya wananchi kwa kutumia nguvu. Tume ya Taifa ya Uchunguzi iliyochunguza matukio hayo ilitangaza Aprili 23, 2026 kuwa angalau watu 518 walifariki dunia wakati wa vurugu zilizotokea kuzunguka uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, lakini haikuwataja waliohusika wala kuweka wazi ripoti yake kwa umma.
Aidha, Mei 8, 2026, Bunge la Ulaya lilipitisha azimio kuhusu kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu. Azimio hilo lililaani kukamatwa kwake na kuonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu mashtaka yanayodaiwa kuwa ya kisiasa dhidi yake, ambayo yanaweza kusababisha adhabu ya kifo. Bunge hilo lilitaka serikali ya Tanzania imuachie huru mara moja bila masharti, ihakikishe usalama wake na kuheshimu haki yake ya kupata kesi ya haki pamoja na uwakilishi wa kisheria.
Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo leo Juni 11, 2026 amepanda ulingoni Abidjan Nchini Ivory Coast kuwania mkanda wa IBO katika pambano la round 12 dhidi ya Bondia Michel Soro raia wa Ivory Coast na Ufaransa.
Mwakinyo katika pambano hilo la round 12 la uzito wa middleweight, amepoteza kwa kupigwa kwa TKO round ya 9 na kufanya pambano hilo kuwa pambano lake la tatu kuwahi kupoteza kwa KO.
Hili linakuwa pambano la 4 kwa Hassan Mwakinyo, Moja akipigwa kwa point na matatu kwa KO.
Michel Soro leo amepigana pambano lake la 45, amefanikiwa kushinda kwa KO kwa mara ya 28, akipoteza mara 4 na ametoka sare mara 2.
#MillardAyoUPDATES